Mahudhurio langoni. |
Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba akizungumza jambo na kumkaribisha Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki jukwaani na kusalimiana na Wakazi wa Bukoba waliokuwa kwenye Tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2014 kwenye Uwanja wa Kaitaba. |
Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), Balozi Khamis Kagasheki(kushoto, ndie akuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la Serengeti fiesta 2014 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Tamasha lililofanyika leo Ijumaa 15.08.2014. Tamasha hili litaendelea tena kwenye miji mingine na sasa baada ya kufanyika hapa Bukoba linahamia kwenye Mji wa Kahama Jumapili kesho kutwa tarehe 17. |
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Pamoja na Wananchi mbalimbali walihudhulia kwa wingi katika Uwanja huo wa Kaitaba. katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoa Mheshimiwa Zipporah Pangani na kulia ni Bw. Denis. |
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki ambaye ndie alikuwa mgeni Rasmi kwa Furaha akizungumza jambo Jukwaani kwenye Tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika kwa mara ya kwanza hapa Bukoba |
.
Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba (kulia, akiwapongeza washindi wa BK Dancers waliojinyakulia Millioni moja. |
Katikati ni Super Nyota Divas, Joylen Aliyeshinda katika katika shindano la kumtafuta msanii wa kike kupitia Mikoa yote inayopita Fiesta, Shindano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Lina's Club.
Joylen aliwashinda wenzake kwa kila vigezo vilivyokuwa vikiangaliwa na Majaji. Joylen amekuwa akiimba nyimbo za Recho na Vumilia ikiwemo, Nashukuru umerudi, Upepo wako na zinginezo.
|
Msanii wa Muziki Ras Nod wa hapa Bukoba akiwajibika kuwaburudisha mashabiki wake jukwaani. |
Sehemu ya umati wa wakazi wa Mji wa Bukoba na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Tamasha la Serengeti fiesta 2014 katika Uwanja wa Kaitaba leo. |
Msanii wa Bukoba Nshomile akiimba mbele ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Kaitaba wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Fiesta 2014, Tamasha lililofanyika kwa mara ya kwanza katika Mkoa huu wa Kagera na kushuhudiwa na Wakazi wengi wa Mji huu na Vitongoji vyake. |
Wadau marafiki toka Mwanza waliosafiri hadi mjini hapa, pembeni na vinywaji vyao aina ya Serengeti wakifuatilia kwa karibu Tamasha hilo huku wakifurahia jambo kwenye Uwanja wa Kaitaba ambako ndipo Tamasha hilo limefanyikia leo ijumaa. |
Msanii mkongwe wa nyimbo za asili ya Kihaya Nchini mwenye sauti ya aina yake Saida Karoli akiwa na Kundi lake zima wakipagawisha Wakaazi wa Bukoba leo kwenye Tamasha la Fiesta 2014 Mjini Bukoba. |
Saida Karoli akicharaza ngoma tatu kwa mpigo na kuwashangaza Mashabiki wake. |
Ngoma ikishika kasi jukwaani!! |
Saida Karoli akikonga nyoyo za umati wa Wakazi wa Mji wa Bukoba waliojitokeza katika Uwanja wa Kaitaba katika tamasha la Serengeti fiesta 2014. |
Kundi zima la Saida Karoli likijiachia kwa nyimbo za Asili jukwaani |
Saida Karoli akifanya yake Jukwaani.. |
Nyomi... |
Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Recho akifanya yake jukwaani!! |
Msanii wa Bongoflava Jux nae aliwajibika kisawasawa jukwaani |
Simu nazo zikawa Viganjani juu kwa juu!! Kuamsha Fiesta!!! Upendo nao ukisambazwa kitaratiiibu!Hakika ilikuwa ni Sheeeeda!!! Hii ni Historia Bukobaaaa!!!Sambaza upendo na hamsha hamsha za hapa na pale!Mikono juu!! Linah na waimbaji wake wakifanya yao kwenye Usiku wa FiestaLinah akipawawisha Mashabiki wake Msanii wa Bongoflava BarnabasBarnaba akiendelea na Kuburudisha kwa nyimbo tofauti tofauti katika Tamasha hilo Mjini Bukoba.Dada alishindwa kuvumilia!! Furaha ilimteka kwa BarnabasMsanii wa bongofleva Mr. BlueBk Sande akishambulia Jukwaa!Msanii wa bongofleva wa Bukoba, BK Sande akiimba kuwabueudisha Wahaya wenzake kwa miondoko ya Kihaya zaidi...nyumbani ni Nyumbani!Msanii wa Bongoflava Ommy Dimpoz ulifika Muda wake..Kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Bukoba...salaam kutoka kwa wadau wake ilikuwa mhimu sana Ommy DimpozNipe tano..!Alikuwa na wenzake Jukwaani na walikuwa na staili ya aina yao kuichezaji!Ommy Dimpoz akicheza na Vijana wake kwa staili yao ya kipekee!Ommy Dimpoz akiendesha kamuzi la aina yake jukwaaniNey wa Mitego jukwaaniMsanii wa muziki wa kizazi kipya, Ney wa Mitego akiimba moja ya nyimbo zake katika Tamasha la Fiesta 2014 katika Uwanja wa Ksitaba.Dj Fetty na wewe Unaimba?? Dj Fetty nae ilikuwa siku yake ya kwanza kufika Bukoba...hivyo na yeye alijikusanyia mashabiki wake akiwa jukwaani....Furaha yake alijikuta anacheza na kuongea maneno machache na Wakaazi wa Bukoba akiwa jukwaani Wakati Tamasha la Fiesta likiendelea katika Uwanja wa Kaitaba..!Dj Fetty akiachia 1,2...jukwaani.Willy O. Rutta akiteta jambo na Ruge Mutahaba