ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 26, 2019

KISIWANI UINJILISTI MTAA KWA MTAA.


Kutoka Kijiji cha Kaunda kisiwani Maisome wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Gsengo Tv inakutana uso kwa uso na mwinjilisti Ajilazaro anayesambaza injili mtaa kwa mtaa akitokea kanisa la EAGT kisiwani hapa.

RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,530


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530  ambapo wafungwa 722 wataachiliwa huru siku ya leo April 26, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Meja Jenerali Jacob G Kingu, imeeleza kwamba wafungwa 2808 watabaki gerezani kumalizia kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.

Katika kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Aprili 26, 2019, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa  msamaha kwa wafungwa ambapo kati ya waliopewa msamaha ni pamoja na wafungwa walioingia gerezani kabla ya machi 15, 2019.

Wafungwa wengine waliobahatika msamaha huo ni pamoja na wale wanaougua magonjwa kama Ukimwi, Kansa na Kifua kikuu ambapo watathibitishwa na Jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu Mkoa au Wilaya.






Thursday, April 25, 2019

SERA YA JPM 'SERIKALI YA VIWANDA' INAKWAMISHWA NA BAADHI YA WATAALAMU' MWEKEZAJI SENGEREMA AFICHUA.



TANGU aingie madarakani, tumemuona Rais John Magufuli akiwa na dhamira ya dhati ya kuanzisha viwanda ili kukuza uchumi wa nchi yetu, akisisitiza kuwa Tanzania ni kati ya nchi tajiri na kwamba hakuna sababu ya watu wake kuwa maskini.

Ni kutokana na dhamira yake hiyo, tumeona mambo kadhaa ambayo yanashabihiana na azma yake ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda yakifanyika kwa haraka na kwa ustadi mkubwa.

Kwanza, Rais ameimarisha miundombinu zikiwemo barabara,usafiri wa anga na sasa reli.

Pili ameimarisha kasi ya ukusanyaji wa mapato ya nchi, ambayo kwa sasa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania inakusanya karibu trillioni moja kwa mwezi kutoka makusanyo ya awali ya Sh bilioni 900 kwa mwezi.

Hili ni jambo jema, maana kama Taifa hatuwezi kuanza safari ya viwanda, kama hatuna uwezo wa kukusanya kodi kutoka hasa kwa wafanyabiashara wakubwa watakaokuwa kuja kuwekeza, katika hilo kama hatayumbishwa, Rais ameliweza na naamini hawezi kuwekwa mfukoni!

Lakini pamoja na juhudi zote hizo za Mheshimiwa Rais magufuli sanjari na nguvu za Mawaziri wake,  Je wataalamu wetu wameshiriki kikamilifu kuisaka serikali ya Viwanda?

Si ndiyo hawa hawa ambao baadhi yao kila kukicha wamekuwa wakilalamikiwa huku wengine wakitumbuliwa kwa ubadhirifu, urasimu na kuchelewesha miradi?

Katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella anadhuru wilayani Sengerema ambako anashuhudia mradi mkubwa samaki, ambapo mwekezaji wake mara baada ya kafanya utafiti kutoka nchini China juu ya ufugaji samaki, anafanya uwekezaji, lakini mwekezaji huyo anakutana na zungusha zungusha za mmoja wa wataalamu nazo zinamkatisha tamaa….....

Wednesday, April 24, 2019

MIMBA, UTORO NA WAZAZI KUWAOZA WANAFUNZI SUMU YA ELIMU KISIWANI MAISOME



ZAIDI ya wanafunzi 50 wa kidato cha 1 hadi cha 4 kwa shule za sekondari katika kisiwa cha Maisome Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameshindwa kuendelea na masomo ya muhula wa mwaka 2018 -2019, sababu kuu zikitajwa kuwa ni mimba za utotoni, kuozwa na wazazi wao pamoja na utoro.

Hayo yamebainika kupitia ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella wakati akifungua Jengo la Utawala kwa shule ya sekondari Maisome iliyopo katika kijiji cha Kisaba, kata ya Maisome wilayani humo, ambapo Shirika la Hifadhi nchini TANAPA limekabidhi nyumba ya kisasa ambapo zaidi ya shilingi milioni 100 zimegharamia ujenzi huo sanjari na thamani zilizomo ndani ya majengo.

Akionesha kusikitishwa na suala hilo Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amedhamiria kuunda kamati ya uchunguzi ili kuwabaini wahusika na kufuatilia baadhi ya kesi zilizofikishwa  mahakamani.

"Hivi umeshawahi kumuona polisi akishirikiana na kibaka kuvunja nyumba?" "Ole wako mzazi uliyekula mbuzi kumuoza mwanao  eti ili umalize kesi kimya kimya... Utamtapika" asema Mongella

Monday, April 22, 2019

MBAPPE AIPA PSG UBINGWA WA LIGUE 1


Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe akishangilia na mchezaji mwenzake, Dani Alves baada ya kuifungia mabao yote timu yake dakika za 15, 38 na 55 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Monaco kwenye mchezo wa Ligue 1, Ufaransa jana Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.

 Bao pekee la Monaco lilifungwa na Aleksandr Golovin dakika ya 38 na kwa ushindi huo PSG ilitangazwa rasmi kuwa bingwa wa Ligue 1 kutokana na kufikisha pointi 84 katika mchezo wa 33 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

"WATU WANANITAFSIRI VIBAYA NINAPOKUTA VITU VYA HOVYO" - MONGELLA


“LAKINI kubwa zaidi ni ubora wa ujenzi, Zahanati hii inaonekana ni ya viwango  vinavyofanana na hadhi ya jiji na ndiyo maana mara nyingine watu wananitafsiri vibaya ninapokuta vitu vya hovyo hovyo maeneo kama haya”

“Kuna maeneo unaweza kuwa na simile, lakini kwenye maeneo ya jiji lazima muishi kama watu wa kwenye jiji, hata vitu mnavyofanya lazima viwe na viwango”

“Iwe kwenye ujenzi wa barabara, madarasa, iwe ni zahanati, iwe ni kituo cha Afya, mjenge miundombinu yenye kuendana na hadhi na si ubabaishaji” 

Ni sehemu ya kauli za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John V.K Mongella wakati akifungua zahanati ya Mhandu iliyojengwa kwa fedha za wananchi na Serikali iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Sunday, April 21, 2019

c

MLIPUKO SRI LANKA: WATU 290 WAUAWA, 500 WAJERUHIWA BAADA YA MAKANISA NA HOTELI KULENGWA.

Idadi ya watu waliouawa kwenye mashambulio ya mabomu kwenye makanisa na hoteli nchin Sri Lanka imepaa na kufikia 290.
Milipuko nane iliripotiwa jana Jumapili katika mashambulio yaliyolenga makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka.
Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zilishambuliwa.
Watu wengine zaidi ya 500, wamejeruhiwa na kuna hofu idadi ya vifo ikaendelea kuongezeka.

KISWAHILI SASA CHAPAA - TUMEONGEA NA MTANZANIA ANAYEMLISHA KISHWAHILI



Mtangazaji wa kituo cha radio cha @jembefm kinachomililiwa na Dr Sebastian Ndege @jembenijembe Mr John Jackson jj amekuwa mwalimu mzuri wa lugha ya kiswahili kwa kijana mdogo na  mchambuzi wa soka la kimataifa anayeendelea kujizolea umaarufu nje na ndani ya Afrika Mashariki  

Kwa kuongea kiswahili hasa anapofanya uchambuzi wake wa soka @braydonbentpage amejizolea umaarufu baada ya vipande vyake vya video za uchambuzi wa soka  vikitumia baadhi ya maneno ya kiswahili.

Pamoja na kufanya uchambuzi wa soka amewashangaza wana Afrika Mashariki pale  kijana huyo aliposikika  akivitaja vivutio vya utalii vya nchini Tanzania kama Serengeti, Kilimanjaro na Ngorongoro, Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Waziri wa maliasili na Utalii Wazuri Dr Hamis Kingwangalla, amemuomba mchambuzi huyo wa soka wakimataifa awe balozi wa masuala ya Utalii na  kumpa ofa kijana huyo kuja kutembelea mbuga zetu za wanyama nchini Tanzania, Pongezi Kubwa kwa wizara maliasili na Utalii kwa kuliona hili na kulibeba.