“LAKINI kubwa zaidi ni ubora wa ujenzi, Zahanati hii inaonekana ni ya viwango vinavyofanana na hadhi ya jiji na ndiyo maana mara nyingine watu wananitafsiri vibaya ninapokuta vitu vya hovyo hovyo maeneo kama haya”
“Kuna maeneo unaweza kuwa na simile, lakini kwenye maeneo ya jiji lazima muishi kama watu wa kwenye jiji, hata vitu mnavyofanya lazima viwe na viwango”
“Iwe kwenye ujenzi wa barabara, madarasa, iwe ni zahanati, iwe ni kituo cha Afya, mjenge miundombinu yenye kuendana na hadhi na si ubabaishaji”
Ni sehemu ya kauli za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John V.K Mongella wakati akifungua zahanati ya Mhandu iliyojengwa kwa fedha za wananchi na Serikali iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.