ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 3, 2012

KOMEDI DAR WAMDUNGA MTU HOME 4-3

Tale wa timu ya wasanii wa Komedi toka Dar akionyesha... Hizooo... kuashiria...!!!

Ni burudani toka kwa Sharo Millionaire na wenzake Bongo Komedi toka jijini Dar wakitoa rubudani kwa stage CCM Kirumba Mwanza leo.

Kikosi cha Komedi toka Mwanza katika flash ya pamoja kabla ya mchezo.

Kikosi cha Bongo Komedi toka Dar es salaam katika flash ya pamoja kabla ya mchezo ambapo kikisi hiki kilitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 4-3.

"Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mh.Said Amanzi iliupate mikono ya wachezaji hawa wa nyumbani kwako lazima utupie ngawira kwenye chungu....!!!"

Mheshimiwa aliambiwa na msanii huyu ambaye ndiye alikuwa mganga wa timu ya Bongo Komedi na shahidi alikuwa kingwendu na wenziwe "Mheshimiwa umenishika mimi baaaaassss!!! tushashinda...."

Mganga wa Komedi Mwanza kushoto na shabiki...

Mtanga alipata shavu sana toka kwa watoto naye bila hiyana....flash!

Mshambuliaji Tale toka Bongo Komedi alikuwa mwiba kwa ngome ya Komedi Mwanza hapa ni kana anapiga vile .... anafinyaaa.....

Mara goliiiii....

Sharo Millionaire ni moja kati ya wachezaji walokuwa wasumbufu kwenye mchezo huo na of coz alitupi lake moja...

Nkabaaaa!! Hili ndilo bao la Sharo Millionaire ambapo mengine yalifungwa na Tale ambaye alifunga mawili na jamaa mwingine hivi.....

Mashabiki na macho yao kwenye stage mara baada ya dakika 90 kumalizika.

Man of the match Tale akiwapa wakazi wa Mwanza rubudani...

Mfuniko wa maraha.

BBC YAGONGA MIAKA 80 HEWANI

Shirika la BBC World Service linasherehekea miaka themanini ya matangazo yake ya kimataifa.

Siku ya kwanza ya matangazo ya himaya ya kiingereza BBC ilianza rasmi matangazo yake mwezi Disemba mwaka 1932 kwa redio ya masafa mafupi.

Hotuba ya Mfalme
Siku sita baada ya kufunguliwa rasmi kwa idhaa ya himaya ya kiingereza, ndio ulikuwa mwanzo wa utangazaji, huu ndio ulikuwa ujumbe wa Krismasi wa himaya ya Uingereza. Hotuba ilitolewa na Mfalme George wa tano, moja kwa moja kutoka katika nyumba ya familia ya kifalme ya mapumziko Norfolk mjini Sandringham. Maneno hayo yaliandikwa na mshahiri na mwandishi Rudyard Kipling na hivvi ndivyo hotuba ilivyoanza: " Nazungumza nanyi kutoka nyumbani kwangu maneno haya yakitoka rohoni mwangu." Hivi ndivyo mkurugenzi mkuu wa wa BBC John Reith aliandika katika kitabu chake cha kumbukumbu: " Huu ndio ulikuwa ufanisi mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya BBC. Mfalme alisikika kote duniani.

Vive le Gerale
Serikali ya UIfaransa ilisalimu amri kwa utawala wa Nazi wa Ujerumani mwezi Juni mwaka 1940. Kiongozi wa vuguvugu la 'Free French' Generali Charles De Gaulle, alipeperusha matangazo hadi nchini Ufaransa, kutoka chumba cha matangazo cha B2, katika Broadcasting House. Wafanyakazi waliambiwa kuwa generali ambaye hakutajwa, alikuwa anakuja Broadasting House. Hata hivyo hotuba yake haikurekodiwa na ilibidi kurejelewa, kitu kilichomkera generali huyo. Aliendelea kutangaza kwa dakika tano kila usiku kwa miaka minne. Kulingana na mwandishi mmoja wa idhaa ya kifaransa, hakuwahi kusikia generali huyo akikosea hata kidogo katika matangazo yake. Alikuwa mkarimu na kila baada ya matangazo alimshukuru fundi wa mitambo.

War of words
Ofisi za BBC ziliweza kupatikana Broadcasting House, Oxford Street na katika Senate House. Idhaa mpya ya kimataifa sasa iliweza kupata nguvu baada ya serikali ya Uingereza kugundua umuhimu wa utangazaji. Mwaka 1941, kulikuwa na zaidi ya wafanyakazi 1400. Mwaka huo mbunge wa eneo bunge la Derby, Phillip Noel_Baker, katika mjadala bungeni, alisema "sidhani waziri atatofautiana nami nikisema kuwa katika njia zote alizonazo za kuwafikia watu barani Ulaya, utangazaji ndio njia bora zaidi."


Kuhamia Bush House
Nafasi ya utangazaji kwa idhaa nyingi za BBC, ilikuwa inapungua kule Broadcasting House. Wakati bomu la kutegwa ardhini lililipuka nje ya Broadcasting House mwaka 1940, ilisababisha moto uliodumu saa kadhaa na kusababisha uharibifu mkubwa. Idhaa za Ulaya zikalazimika kuhamia Maida Vale kaskazini magharibi mwa London ambapo walitangazia kutoka kwa chumba kidogo. Mwaka 1941, idhaa hizo zilihamia Bush House, katika barabara ya Fleet Street kitovu cha viwanda vya kuchapishia magazeti wakati huo ikitozwa kodi ya pauni thelathini kila wiki.

Ishara za siri
Wakati wapiganaji waliokuwa wanapinga vikosi vya kigeni barani Uropa, walipojaribu kukabiliana na vikosi hivyo, idhaa hiyo iliwatangazia ujumbe wa siri. Ujumbe huo haukueleweka mfano ''Le lapin a bu un aperif'' ( kwamba sungura alikunywa kinywaji cha aperitif), au '' mademoiselle caresse le nez de son chien'' ( kwamba mademoiselle anapapasa pua la mbwa wake). Huu ujembe ulikuwa unaawambia wapiganaji kuwa ikiwa oparesheni ilikuwa iendelee au ikiwa imesitishwa au ikiwa watu ama stakabadhi zilikuwa zimefika.

Waandishi wa Bush House
Kutoka mwaka 1941 hadi mwaka 1943, George Orwell alifanya kazi kama mtayarishaji wa kipindi katika idhaa ya mashariki. Hakufurahia kazi yake na ilipofika mwaka 1944, aliandika "huenda nikarejelea maisha yangu, na kuweza kuandika kitu muhimu. kwa sasa mimi ni kama chungwa ambalo limekanyagwa na kiatu kichafu sana" Lakini kazi yake katika BBC ilimsaidia kuweza kuandika kitabu chake, mwaka 1984 ambacho inasemekana alitoa mawazo yake mengi kutoka maisha yake BBC.

BBC wakati wa vita baridi
Baada ya vita baridi, uhusiano na utawala wa Strelin ulianza kudorora huku ukuta wa chuma ukiwekwa kati yao. Februari mwaka 1946, wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza, iliitaka BBC kuanzisha idhaa ya kirusi na mwezi mmoja baadaye ikaanza kupeperusha matangazo yake. Mwanzoni wasikilizaji wa Urusi waliweza kusikiliza idhaa hiyo bila wasiwasi lakini punde vita baridi vilipokuwa vinaendelea, serikali ya Urusi ikaanza kudhibiti hali. Matangazo yalianza kuingiliwa, hitilafu za kila mara zikiripotiwa na hivyo BBC ikalazimika kuongeza nguvu za mitambo yake.

Kuhifadhi uwazi.
Wakati wa kutangaza mzozo wa Suez mwaka 1956,waziri mkuu wa Uingereza Anthony Eden, aliamini kuwa idhaa ya kiarabu, inapaswa kutangaza kwa kupendelea majeshi ya Uingereza. Idhaa hiyo nayo iliendelea kutangaza bila mapendeleo kwa usaidizi wa mkurugenzi mkuu Ian Jacob licha ya wizara ya mambo ya kigeni kusema kuwa itapunguza mamilioni ya dola ambazo BBC ilikuwa inapokea kama ufadhili. Katika wiki chache zilizofuata, licha ya vitisho vya waziri na wabunge, BBC ilisisitiza msimamo wake ya kutopendelea upande wowote.

Mageuzi ya Transista
Miaka ya tisini, ilikuwa miaka ya kueneza umiliki wa redio, hasa baada ya kuzinduliwa kwa betri ambazo zingewezesha transista kufanya kazi. Kati ya mwaka 1955 na 1965, umiliki wa redio ulipanda katika nchi za kikomunisti mashariki mwa Ulaya na kuongezeka hata maradufu mashariki ya kati, China , nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na nchini India. Mwezi Mei mwaka 1965, iligeuzwa na kuwa World Service kuweza kuonyesha umaarufu wake wa maswala ya dunia.

Kuhusu vitabu vya kijasusi mwaka 1978, mwandishi katika idhaa ya Bulgeria, Georgi Markov alipokuwa anaelekea kazini Bush House, akiwa katika eneo la Waterloo Bridge. Alihisi uchungu katika paja lake. Alipogeuka alimwona mtu akiokota mwavuli lakini Markov aliendelea na safari yake kwenda Bush House. Baadaye siku hiyo aliugua na kufariki siku tatu baadaye. Uchunguzi uliofanyiwa mwili wake uligundua kidude kidogo katika paja lake. Inaamika kidude hicho kilikuwa na sumu kali. Ilibainika baadaye kuwa polisi wa siri wa Urusi waliunda mwavuli ulioweza kumdunga mwathirika simu hiyo.

Elimumwendo ya Lugha
Katika historia yake, BBC imepeperusha matangazo yake katika lugha 68. Nyingi ya Lugha hizi zimekuwepo na kwenda ikiwemo, Maltese, Gujarati, Kijapani, na Welsh iliyotumika kwa ajili ya idhaa ya Potagonia. Kuanguka kwa ukuta wa Berlin, ilikuwa ishara ya enzi mpya Ulaya Mashariki na BBC ikawa sio muhimu sana kwa watu wa nchi hizo kama ilivyokuwa mwanzoni. Kwa hivyo nyingi ya idhaa za nchi hizo zikafungwa ili kuweza kufadhili vitengo vingine vya BBC ikizingatiwa bajeti yake ambayo ilikuwa inapungua. idhaa hizo zikafikishwa 28 zikipeperusha matangazo yao kupitia mtandao tu.

Habari za uetendeti
Wakati tawala za Kisovieti zillipoporomoka miaka ya tisini, kulikuwa na eneo jipya lililokuwa linatokota katika Ghuba. Tarehe 2 mwezi Agosti, mwaka 1990, majeshi ya dikteta wa Iraq, Sadam Hussein walivamia Kuwait. Wakati uvamizi ulipoanza, mwezi Januari mwaka 1991, World Service, iliondoa mpangilio wa vipindi ili kuweza kupeperusha habari na kuweza kuzungumzia maswala ya dunia kwa mara ya kwanza.

Sifa kutoka kwa Gorbachev
Wakati Mikhail Gorbachev aliposhikwa kwa siku tatu nchini Urusi, Agosti mwaka 1991, mawasiliano yake na dunia ilikuwa tu kupitia idhaa za kimataifa za redio. aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa World Service John Tusa, alikumbuka mkutano wa waandishi wa habari ambapo Gorbachev alisema kuwa BBC ilisikika kwa uzuri na ilishinda redio. zengine. Ina maana kuwa sifa zilitolewa kwa BBC kwa ujumla na kwa idhaa ya kirusi.

Jukumu lisilofaa la Redio
Redio ilikuwa na jukumu kubwa sana katika matukio nchini Rwanda mwaka 1994. Redio Mille Collines, redio ya Rwanda, ilichochea chuki na uhasama kati ya Watutsi na Wahutu. BBC ilisaidia, kutuliza hali kufuatia ombi la mashirika ya misaada. wasimamizi wa vipindi kutoka idhaa za Kifaransa na kiswahili, walisaidiana na shirika la msalaba mwekundu kuwasidia mamilioni ya watu walioachwa bila makao na vile vile kutoa taarifa kuhusu watu waliopotea. Idhaa hiyo baadaye iliweza kupanuliwa na kuwa idhaa ya maziwa makuu.

Hatua za haraka
Tarehe kumi na moja mwaka 2001, wakati mashambulizi yalitekelezwa dhidi ya jumba la World Trade Centre nchini Marekani, waandishi katika Bush House mara moja walipigwa na butwaa hali ikawa ya taharuki. Mhariri msaidizi Rachel Harvey alilazimika kusimama juu ya dawati lake ili kutuliza waandishi na punde kutoa mwelekeo wa namna ya kupeperusha habari hizo kwa siku nzima. 29 Februari, 2012 - Saa 12:28 GMT

Televisheni ya kimataifa
Idhaa ya kiarabu ilianza kupeperusha matangazo yake kupitia televisheni mwezi Machi mwaka 2008, na kufuatiwa na idhaa ya kifarsi mwaka uliofuata. Haikuwa mara ya kwanza World service kutangza kupitia televisheni. Matangazo ya televisheni ya kimataifa ya kiingereza yalianza mwaka 1991kupitia televisheni ambayo baadaye iliitwa World TV mwaka 1996 na kisha sasa inaitwa BBC World News

Utangazaji wa chanzo kwa watu
Wakati wa tetemeko la ardhi nchinin Haiti ishaa ya BBC ya visiwa vya Caribbean, ilitangaza kipindi cha dakika ishirini kila siku kwa lugha ya Haiti, kuweza kutoa taarifa muhimu kuwasaidia watu kuweza kupokea maji na chakula pamoja na dawa baada ya tetemeko hilo lililotokea tarahe kumi na mbili Januari mwaka 2010. Kando na kutoa taarifa za usaidizi kwa waathirika wa tetemeko hilo, kipindi kiliwasaidia watu kuweza kuwasiliana na jamaa zao waliokumbwa na tetemeko hilo. Pia kilitoa fursa kwa wanamuziki wa kigeni kuwafikia waathirika wa tetemeko .

Mtandao wa kijamii.
Wakati wa mapinduzi ya kiraia katika nchi za kiarabu, mwaka 2011, mitandao ya kijamii uligeuka na kuwa chanzo muhimu cha habari kwa waandsihi wa habari katika eneo hilo. Matukio mawili yalionekana kuwa muhimu sana. Mwanzo mitandao hiyo ilibainika kuwa chanzo kikubwa cha habari kwa waandishi wa habari, pili, kupeperusha habari hizo kulifanya wasikilizaji kuwa sehemu ya habari za BBC World Service na namna ambavyo BBC inakusanya na kupeperusha habari zake. 29 Februari, 2012 - Saa 12:28 GMT

A Jolly Good Show
Novemba mwaka 2010, kiongozi anayepigania demokrasia, nchini Syria, ung San Suu Kyi, aliachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Burma. Katika mahojiano baadaye, alisema kuwa alisikiliza BBC World Service, wakati wa kuzuiliwa kwake na kusema kuwa pamoja na vipindi vingine alipenda kusikiliza kipindi cha ombi la muziki cha A Jolly Good Show ambacho huendeshwa na DJ Dave Lee Travis. Alisema kuwa kusikiliza kwake kwa BBC kulimkamilishaia mtukio duniani.

Nyumba mpya
Mwaka 2012 BBC World Service, inahamia katika jumba la Broadcasting House ila tu wakti huu limefanyiwa ukarabati wa hali ya juu na kuwa jumba la kifahari la matangazo yake baada ya miaka sabini na moja katika Bush House. Waandishi wa habari wotw sasa watakuwa katika jumba moja na wafanyakazi wengine wa BBC mfano waandishi wa mtandao pamoja na wenzao wa Televisheni ili kuweza kuweka habari za kimataifa katika kitovu kimoja.

Habari zote kwa hisani ya bbc swahili.

Friday, March 2, 2012

TUNDU LISU AWASHA MOTO MWANZA KESI YA UBUNGE

Wakili maarufu nchini, Tundu Lisu jana aligeuka kuwa mbogo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza, Highness Kiwia (Chadema), ambapo katika kesi hiyo alimbana maswali magumu shahidi wa kwanza na mlalamikaji wa tatu wa kesi hiyo ya madai.Katika kesi hiyo namba 12/2010 iliyofikia hatua ya mashahidi, iliyosikilizwa na Jaji Mjemas kutoka Bukoba Mkoani Kagera, Lisu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kampi rasmi ya upinzani Bungeni, alitumia hati ya mashtaka ya walalamikaji kumbana shahidi huyo, Beatus Martin Madenge kuhusu maelezo ya hati hiyo, ambayo aliyakubali na baadaye akayakana mbele ya mahakama hiyo.

Katika mahojiano mbele ya mahakama hiyo, Wakili Lisu anayemtetea Mbunge Kiwia, alimtaka shahidi na mlalamikaji wa kesi hiyo ya madai, Madenge kuithibitishia mahakama Kuu iwapo maelezo na saini yake iliyomo kwenye hati ya mashtaka ni sahihi ama si sahihi, ambapo alikiri mbele ya mahakama kwamba maelezo yote yaliyomo kwenye hati hiyo ni sahihi na hakuna hata neno moja la uongo.

Baada ya shahidi huyo kukiri kupiga kura kihalali siku hiyo ya Oktoba 31 mwaka 2010, Lisu alimtaka pia shahidi huyo aieleze mahakama sababu za kutoa maelezo mahakamani hapo kwamba yeye alizuiliwa kupiga kura katika kituo alichopangiwa cha Mihama Shule ya Msingi Ilemela, baada ya kukamatwa na kundi la vijana waliokuwa wakiwazuia wafuasi wa CCM kwenda kupiga kura katika kituoni hicho.

Kufuatia maswali hayo magumu, shahidi huyo baadaye alikana mbele ya mahakama kwamba yeye siku hiyo ya uchaguzi hakufanikiwa kupiga kura, kwani alikamatwa majira ya saa 4 asubuhi wakati akienda kupiga kura, na kwamba walalamikaji wenzake ndiyo waliopiga kura siku hiyo, jambo ambalo lilisababisha watu waliokuwa wamejaa kusikiliza kesi hiyo kuangua kicheko cha chinichini.

"Mheshimiwa Jaji, yaliyoandikwa na kuyasaini mimi kwenye hati hii ni ya kabisa. Lakini mimi nasema sikupiga kura siku hiyo nilikamatwa. Sikupiga kura ila wenzangu ndiyo waliopiga kura", alisema shahidi huyo mbele ya mahakama, akikana maelezo yaliyomo kwenye hati yake ya mashtaka yanayoeleza kwamba siku hiyo ya uchaguzi yeye alipiga kura kihalali.

Kesi hiyo ya madai namba 12 ya mwaka 2010, imefunguliwa na walalamikaji watatu, ambapo wanaiomba mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itengue ushindi wa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Highness Kiwia (Chadema), kwa madai kwamba mbunge huyo hakushinda kihalali kwenye uchaguzi huo Mkuu wa mwaka 2010, na wanaoshtakiwa kwenye kesi hiyo ya madai ni Mbunge Kiwia, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Ilemela pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mbali na hayo, wakili Lisu alimhoji shahidi huyo akitaka aieleze mahakama ni kwa nini aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Ilemela, Anthony Diallo hajafungua kesi mahakamani, isipokuwa hao walalamikaji, na alimtaka pia shahidi huyo kueleza iwapo amepewa fedha au alikuwa mgombea mwenza wa Diallo katika uchaguzi huo Mkuu.

"Umeiambia mahakama kwamba Diallo ndiye aliyekuwa mgombea wa CCM Jimbo la Ilemela, sawasawa. Ni kwa nini Diallo hajalalamika popote wala kuleta kesi mahakamani?. Je wewe ulikuwa mgombea mwenza wa Diallo, au nani amekutuma kufungua kesi?", alihoji Lisu huku Jaji Mjemas akimsisitiza shahidi huyo kujibu maswali ya wakili huyo wa upande wa utetezi.

Kufuatia maswali na majibu hayo, wakili Lisu ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini huku akizunguka huku na kule mahakamani hapo, alimhoji shahidi huyo kwamba: "Kama Diallo hajalalamika mahala popote juu ya kushindwa kwake, wala hajaleta kesi mahakamani, unaufahamu usemi wa kwamba pilipili aile mwingine wewe ikuwashie nini?".

Akijibu swali hilo, shahidi Madenge alisema yeye hajatumwa na mtu wala hakuwa mgombea mwenza wa Diallo, na kwamba yeye na wenzake wamepata machungu baada ya mgombea wa CCM kuonekana ameshindwa pasipo kihalali na mbunge wa sasa wa jimbo hilo.

Katika kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi, iliyoendelea tena leo Ijumaa, walalamikaji wanadai kwamba watu ambao hawakupiga kura Ilemela siku hiyo ya Uchaguzi ni 114,085, kati ya watu 175,978 waliojiandikisha ambapo waliopiga kura ni 61,893 pekee, na kwamba anaamini idadi ya watu ambao hawakupiga kura ilitokana na kuzuiwa na vijana 200 anaoamini ni wafuasi wa Chadema.

Thursday, March 1, 2012

JOKA.....

JAMANIeeee!! HIVI Itakuwaje akiamua kuwawageukia wananzengo? Kasheshe ni kwa hao wenye hizo sari (nguo za akina mama wa kihindi) na wanaume walovaa misuli bila puntus' au japo bukta kwa inside.....? Picha na Irene Kirenga

KOMEDI WA MWANZA, DAR KUWASHA MOTO CCM KIRUMBA JUMAMOSI, KINGWENDU NDANI

HOMA ya pambano la soka la wasanii wa vichekesho vya luninga ‘komedi’ wa kutoka mkoani Dar es Salaam na jijini Mwanza ‘Rock City’, imepanda baada ya mastaa hao kutambiana kuwa kesho Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba patachimbika.
Kingwendu
Tayari wachekeshaji wa Dar es Salaam wamewasili Mwanza kwa mchezo huo maalumu wenye lengo la kutoa burudani, kumaliza ubishi wa nani zaidi kati yao na kujenga ushirikiano kwa wasanii hao.

Mechi hiyo imekuwa gumzo kubwa katika jiji la Mwanza na mikoa ya jirani ya Kanda ya Ziwa, baada ya wachekeshaji Kingwendu na Bambo kuwasili mkoani humo na kutamba kupitia vyombo vya habari kwamba, wamekwenda kutafuta ushindi katika mchezo huo.

Kwa mujibu wa mratibu wa mechi hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Brayance Promortes, Pearson Samwel, maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa siku ya mchezo ili kumaliza ubishi uliotawala wa komedi wa Dar es Salaam na Mwanza kina nani wanaweza kusakata soka.

“Tunashukuru tumekamilisha maandalizi yote na wasanii wote wamefanya mazoezi kwa ajili ya kucheza soka kwa dakika 90 na wanatazamia kutoa ushindani mkubwa kati yao,” alisema Samwel kutoka Mwanza.

Alisema kuwa viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh 2,000 mzunguko na sh. 5,000 katika jukwaa kuu na mpaka jana walikuwa wanakamilisha taratibu za mwisho kupata mgeni rasmi.

Wasanii kutoka Dar es Salaam watakaoshuka ndani ya CCM Kirumba siku hiyo ni Kingwendu, Sharo Milionea, Mboto, Senga, Pembe, Bambo, Mtanga, Mau, Ringo na Chilly, Defender, Zimwi, Muhogo Mchungu, Masele, Erick, Kiuno na Hawa.

Timu ya wachekeshaji wa Mkoa wa Mwanza inaundwa na Babu Mkombe,Sharobaro wa Kihaya, Mchele, Chugu, Ngosha, Brother K, Mama Brandina, Msimbe wa ukweli,Okech Okech, Kafuku Kaukananga, Mzee Dude, Itagata, Malapulapu, Choko na Tengambili.

Wasanii wengine watakuwepo siku hiyo ni Tatu Mkate wa Arusha, Avodia Tolu, Mrefu kwenda chini na Jully Tax, ambao wamepania kuwafunga wachekeshaji wenzao wa Dar es Salaam.

MCHAFU KOGA....

Jamaa anapiga mzigo kwenye moja ya daladala kama kondakta ambapo yeye kuoga ni inshu kiasi kwamba harufu ya mwili wake imekuwa ni kero kwa abiria na marafiki wanaomkaribia, si kwa mwili tu hata mavazi jamaa ana katabia ka kuvaa nguo mbili mbili hivyo kama daladala ni mbanano lazma utaondoka na shombo lake, hapa wadau wakaona si hasara wamfunge kamba akaoge kwa lazima.....

Tukio limetokea Nyakato Buzuruga karibu na kituo cha mabasi yaendayo njia ya Musoma, sasa hapa alibebwa mzobemzobe kuelekea mtoni kwa waosha magari na kuogeshwa kisha akapewa sabuni kufua nguo zake.

loh! mchafu koga....

Wednesday, February 29, 2012

SIZ KITAA YAMALIZA ZIARA YAKE ROCK CITY SASA SUBIRI MZIGO HEWANI.......

Castor Dickson aka Mwananchi wa kawaida ambaye ni presenter wa program ya SIZ KITAA inayorushwa na CLOUDS TV akifanya kipindi pembezoni mwa mti wa kumbukumbu ambao ulikuwa ukitumika kunyongea watu enzi za ukoloni.

Hapa SIZ KITAA ilikuwa na Mwenyekiti wa Mwanza Kwanza Philbert Kabago ambaye pia ni presenter wa Michano time katika Radio Passion Fm.

Topix...

Kuna mengi mazuri yameonekana na kuzungumzwa na SIZ KITAA toka wadau wa Rock City hadi safari ilipofika tamati, so kufaidi yote mazuri 'Tega jicho' kwa liprogram la SIZ KITAA kila siku saa moja na robo CLOUDS TV....Walaaaa!!!

Tuesday, February 28, 2012

LICHA YA KUPELEKA WALINZI, MABONDIA WA JIJI LA MWANZA WAWEKA HESHIMA WAREJEA NA MEDALI

Bingwa wa majiji Afrika mashariki katika Hevy Weight Dittrain Kaimbe akiwa na medali yake ya dhahabu sanjari na kombe nafasi ya tatu iliyotwaliwa na timu ya jiji la Mwanza.
Wale mabondia waliolalamikiwa na kocha wa mkoa wa Mwanza aliyetemwa kinyamela ajulikanaye kwa jina la Mgowa Haule, wanaotajwa kutoka katika kampuni ya ulinzi ya mmoja kati ya viongozi waandamizi wa timu hiyo na kuliwakilisha jiji la Mwanza kwenye michuano ya majiji iliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya hatimaye wamerejea nyumbani wakiwa na medali ikiwemo moja ya dhahabu ya ubingwa uzito wa juu.
Medali ya dhahabu.
Dittram Kaimbe aliyekichapa uzito wa Hevy Weight ndiye aliyeitoa kimasomaso Tanzania kwenye michuano hiyo kwa kutwaa medali ya Dhahabu huku mabondia Alex Mjakalanga wa uzito wa light welter na Daniel Wiliam wa welter wakirudi na medali za Shaba kila mmoja naye bondia wa kike Sara Andrew akirejea na medali ya Silver.

Daniel William uzito wa Welter (69) na kombe lake sambamba na medali yake ya bronz.
Kwenye mashindano hayo ushindi wa jumla ulichukuliwa na jiji la Nairobi, nafasi ya pili jiji la Kampala ile hali nafsi ya tatu ikitwaliwa na jiji la Mwanza.

Kocha wa timu ya jiji la Mwanza Omary Akida akizungumza na vyombo vya habari.

Kutoka kushoto waliosimama ni Meja Mstaafu Changarawe, bondia Alex Nyakalungu, kocha wa timu hiyo Omary Akida na Dittraim Kaimbe waliochuchumaa ni Daniel William na Sara Andrew.
Msafara wa timu hiyo uliondoka na jumla ya watu saba wakiwemo wachezaji watano, kocha na kiongozi mmoja ukiwa na kiasi cha shilingi milioni moja laki nne na elfu themanini tofauti na bajeti ya shilingi milioni 12 iliyokuwa ikihitajika.