
Wale mabondia waliolalamikiwa na kocha wa mkoa wa Mwanza aliyetemwa kinyamela ajulikanaye kwa jina la Mgowa Haule, wanaotajwa kutoka katika kampuni ya ulinzi ya mmoja kati ya viongozi waandamizi wa timu hiyo na kuliwakilisha jiji la Mwanza kwenye michuano ya majiji iliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya hatimaye wamerejea nyumbani wakiwa na medali ikiwemo moja ya dhahabu ya ubingwa uzito wa juu.

Dittram Kaimbe aliyekichapa uzito wa Hevy Weight ndiye aliyeitoa kimasomaso Tanzania kwenye michuano hiyo kwa kutwaa medali ya Dhahabu huku mabondia Alex Mjakalanga wa uzito wa light welter na Daniel Wiliam wa welter wakirudi na medali za Shaba kila mmoja naye bondia wa kike Sara Andrew akirejea na medali ya Silver.

Kwenye mashindano hayo ushindi wa jumla ulichukuliwa na jiji la Nairobi, nafasi ya pili jiji la Kampala ile hali nafsi ya tatu ikitwaliwa na jiji la Mwanza.


Msafara wa timu hiyo uliondoka na jumla ya watu saba wakiwemo wachezaji watano, kocha na kiongozi mmoja ukiwa na kiasi cha shilingi milioni moja laki nne na elfu themanini tofauti na bajeti ya shilingi milioni 12 iliyokuwa ikihitajika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.