ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 18, 2022

TIBA YAPATIKANA WATAKAO NYANYASA KIJINSIA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO

 HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO NA CHUO CHAKE CHA UDAKTARI WAZINDUA DAWATI NA SERA YA JINSIA

ILI kukabiliana na vitendo vya rushwa ya ngono na vitendo vya unyanyasaji kwa wanafunzi na waalimu wa vyuo nchini, chuo cha Udaktati Cha Hospitali ya Rufaa ya Bugando CUHAS na MWACHAS leo kimezindua Dawati la Jinsia na Sera ya Jinsia vitakavyo shughulika na kupokea taarifa za unyanyasaji wa kijinsia na kuzifanyia kazi kisheria. Unyanyasaji na Ukatili wa kijinsia vimekua tatizo kubwa sana katika jamii zetu kama ambavyo tafiti zilizotajwa hapo awali zinavyoainisha kwamba unyanyasaji na aina mbalimbali za ubaguzi ni masuala makuu yanayoathiri vibaya wanafunzi katika vyuo vya Afya duniani kote, katika taasisi zetu na jamii kwa ujumla. Ili Kukabiliana na tatizo hili serikali ya Tanzania imeelekeza na imewekeza nguvu nyingi katika kuhakikisha matatizo ya kijinsia yanashughulikiwa ipasavyo huku ikiagiza kila taasisi kuwa na jukwaa hili au dawati la jinsia.