Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana (hawapo pichani) jana kuhusu mkutano wa wadau ili kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Kifua kikuu (TB),utakaofanyika Ijumaa jijini humu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana, kuhusu mkutano wao na viongozi wa dini ambapo mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jana.
Mjumbe wa kamati ya wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na na Ukimwi akielezea mikakati ya kamati hiyo ili katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo nchini ambapo Ijumaa wiki watakuna na viongozi wa dini zote nchini na Spika wa Bunge Job Ndugai atakuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
TB KUWAKUTANISHA WABUNGE, VIONGOZI WA DINI MWANZA
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
KAMATI ya Wabunge wanaojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi imesema changamoto ya inayowakabili watu wanaougua ugonjwa huo lakini hawafikiwi na huduma za tiba imeishawishi kukutana na viongozi wa dini zote nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo wabunge walio kwenye mapambano ya TB Oscar Mukasa ameyasema hayo jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano utakaowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini ili kusaidia kusambaza elimu kwenye jamii.
Mkutano huo utakaofanyika Ijumaa jijini Mwanza, mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenister Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Seleman Jafo watashiriki.
Alisema idadi ya watu nchini, wanaougua ugonjwa wa TB nchini ni kubwa huku changamoto yao kubwa ikiwa ni kutofikiwa na huduma za tiba.
“Ugonjwa wa TB ni tatizo kubwa la kiafya duniani,na hapa nchini watu zaidi ya 60,000 wanaougua hawafikiwi na huduma za tiba, hivyo kama hawapati matibabu jambo ambalo ni hatari kwa kuwa mtu mmoja anaweza kuambukiza watu 20,”alisema
Mukasa alisema wameamua kushirikisha viongozi wa dini kueneza elimu kuoitia nyumba za na endapo zitatumika vizuri zitasaidia kufikisha ujumbe na kuleta ufahamu kwa jamii juu ya tatizo na watakuwa wameunganisha nguvu pamoja na serikali yao.
“Kazi ya Bunge ni kuleta ushawishi, kuleta ustashi wa kisiasa na kuisimamia serikali na hivyo kutumia nyumba za ibada ni mkakati wa kuongeza elimu kwa jamii katika vita ya kupambana na TB kuhakikisha jamii haiathiriwi ,kwa sababu kabla ya kutumia dawa watajua unavyoambukiza,unatibiwaje lakini bila elimu itakuwa kazi bure,”alisema Mukasa.
Alieleza kuwa ushawishi huo wa viongozi wa dini utaifanya serikali kuendelea kuongeza nguvu kwenye vita hiyo kwa kuwa hayatengenishwi na mifumo ya dini na wakiamua wanaweza kufikia maeneo mengi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema maambukizi ya TB yako juu kwani takwimu za 2018 zinaonyesha wagonjwa wa TB 4,640 sawa na asilimia 6 wanatoka mkoani humu.
“Jambo hili ni kubwa lakini linazungumzwa juu juu, hivyo wataalamu wabobezi watatusaidia kupata elimu na taarifa sahihi kwenye mkutano huo wa wadau ili kupambana na tatizo hilo kwa umahiri na ufanisi mkubwa,”alisema Mongela.