ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 29, 2019

RAIS WA ZAMANI WA VISIWA VYA MALDIVES AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA.


Rais wa zamani wa visiwa vya Maldives Abdulla Yameen amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela baada ya kukutwa na hatia ya utakatishaji wa fedha.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya uchunguzi ktika utawala wa kiimla wa kiongozi huyo, katika visiwa hivyo vinavyopendwa na watalii.

Yameen aliitawala Maldives kwa mkono wa chuma hadi mwaka 2018 aliposhindwa uchaguzi kwa hali ya kushtukiza.

Anashutumiwa kuhamisha kinyume cha sheria dola milioni moja kutoka akaunti yake ya benki, wakati uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

Abdalla Yameen mwenye umri wa miaka 60 alikamatwa mwezi Februari, na kufunguiwa mashitaka ya kuwahonga mashahidi wakati kesi dhidi yake ikiendelea.

Mwishoni mwa mwaka jana serikali ya visiwa hivyo vya bahari ya Hindi iliishikilia akaunti yake yenye kiasi cha dola milioni 6.5, ikimtuhumu kupokea malipo yasio halali.

Waendeshamashtaka wanaamini kuwa kiongozi huyo wa zamani ameficha mamilioni mengine ya dola nje ya nchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.