ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 29, 2019

KWAHERI BI. CHEKA


Msanii mkongwe wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Cheka Hija Mzee, maarufu kwa jina la ‘Bi Cheka’ amefariki dunia mchana wa Alhamisi ya Novemba 28, 2019 katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

Kifo cha msanii huyo mkongwe kimethibitishwa na mtoto wake wa kiume, Adam Juma, ambaye amesema kuwa mama yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Bi Cheka atakumbukwa kwa umahiri wake wa ku-rap ambapo aliwahi kufanya kazi nyingi za muziki hasa akiwa na Kundi la TMK. Baadhi ya wasanii aliowahi kufanya nao ngoma ni Mheshimiwa Temba na marehemu Godzilla.


Jembe Fm inaungana na wale wote wailioguswa na msiba huu.

RIP Bi. Cheka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.