ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 24, 2016

ROCK CITY MARATHON KUTIMUA VUMBI KESHO JUMAPILI.


Rock City Marathon kutimua vumbi kesho (JUMAPILI)

Maandalizi ya Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

Mbio hizo zinazofanyika kwa mara  ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.


Alisema wanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.

“Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake,  mbio za Kilometa tano zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi  za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’

“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.

Kuhusu barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5 wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’

Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta  alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/-  kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.

“Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,  washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’

Akizungumzia usalama katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi  alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki mbio hizo.

CLINTON AMBULUZA TRUMP KURA ZA MAONI.

Hillary Clinton ameongoza kwa pointi 6 zaidi dhidi ya mpinzani wake Donald Trump wakati wakielekea kuchuana kwenye mdahalo wa kwanza Jumatatu ijayo.

Kura hizo za nchi nzima zimetolewa Ijumaa hii. Kura za McClatchy-Marist zilionesha kuwa Clinton ana 45% huku Trump akiwa na 39%.

Wiki hii kura za maoni za Wall Street Journal/NBC zilionesha Clinton anaongoza kwa 43% dhidi 37% za mpinzani wake. Clinton anaendelea kuwa na kura nyingi zaidi kutoka kwa wapiga kura weusi akiwa na asilimia 93% na Trumo 3%.

Clinton pia ana wapiga kura wengi walatino kwa asilimia 74% dhidi ya 16% za mpinzani wake.

MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB BANK DKT CHARLES KIMEI ATUNUKIWA TUZO NA AFRICAN LEADERSHIP, NEW YORK NCHINI MAREKANI

 
Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014  katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 Picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick  Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016.

 Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.


Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014

Friday, September 23, 2016

PICHA:MWANAMUZIKI WA JAMAICA LUCCI LACIANO ALIYEJICHORA TATOO YA RAIS MAGUFULI.

Mwanamziki wa Jamaica Las Laciano aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa , " ikiwemo its me against jah" amejichora tatoo ya rais kutokea Africa anayemkubali , ambaye ni rais wa Tanzania Mh. Dr John Magufuli.

Sababu ni kuwa ndo rais muwajibikaji, anayeona mbele hatishiwi na matatizo ya mpito ila anatishiwa na matatizo ya muda mrefu kama rushwa, urasimu na uzembe kazini.

SHULE YA KIBAHA INDEPENDENT (KIPS) YAWEKA MIKAKATI YA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI

Wanafunzi wa darasa la saba katika  shule  ya msingi ya Kibaha Independent (KIPS) wakionyesha uwezo wao wa kuimba na kucheza kwa furaha  katika mahafali ya 11 iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

 NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
KATIKA kuunga juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini uongozi wa shule ya msingi ya Kibaha Independent (KIPS) imesema kwamba inatarajia kujenga majengo mengine kwa lengo la kuweza kuanzisha shule ya sekondari ili kuweza kutoa fursa  elimu kulingana na mahitaji ya wanafunzi wanaohitimu shule za msingi.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Yusuph Mfinanga wakati wa mahafali ya 11 ya shule hiyo ambayo  ni ya binafsi ambapo ameahidi kushirikiana bega kwa began a wadau wengine wa maendeleo sambamba ana serikali katikam tutimiza lengo hilo la kujenga shule ya sekondari.
 
Mfinanga alisema kwamba anatambua katika elimu kuna changamoto nyingi ambazo zinahitajika kutatuliwa ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kuwapa elimu bora ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa katika siku zijazo, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.
 
“kumekuwepo na maombi mbali mbali kutoka kwa wazai kuhusina na kuwepo kwa shule ya sekondari katika Wilaya yetu ya Kibaha ambayo itaweza kuwapa fursa wanafunzi wanaomaliza katika shule za msingi kuweza kujiunga  na kidato cha kwanza wakiwa katika maeneo ya karibu ili kuweza kupata elimu bora zaidi hivyo sualla hili lipo katika mipango yetu,”alifafanua Mfinanga
 
 Katika hatua nyingine Mfinaga aliiomba Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa  wanadumisha zaidi miundombinu ya majengo katika shule mbali mbali sambamba na nyumba za walimu ili kuweza kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
 

Kwa upande wake mmoja wa wazazi akizungumza kwa niaba ya wenzake Selina Wilson walimu  wa shule wanapaswa kuwa waangalizi wa watoto shuleni kwa ukaribu zaidi kwa lengo la kuweza kuwafuatilia mienendo yao na kuepusha wimbi la watoto wanaokwenda kinyume na maadili.
 
 Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Herzon Musalale alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa 2002 kwasasa ina wanafunzi 650 ambapo kwasasa wana matarajio ya kuanzisha shule ya sekondari.

 Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa Halmashauri ya mji wa kibaha  Ramadhani Lawoga alisema serikali ipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbali mbali wa sekta ya elimu ili kuweza kuona ni namna gani wanaweza kusaidia kwa hali na mali katika kusapoti suala zima la elimu.

NGASSA AJIUNGA NA KLABU YA FANJA YA OMAN.

8e632975-6315-499d-989c-9406231d72d7Mchezaji wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC, Azam FC na Simba za Dar es Salaam, na kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Fanja ya Oman.


Ngassa anajiunga na wawakilishi hao wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, baada kama ya wiki tatu tangu avunje mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.

KAA TAYARI KWA 'DEBE NA JEMBE KIAFYA ZAIDI'



🆗... Kuelekea #DebeNAjembe Kiafya zaidi ambapo Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza imenuia kufanya upimaji afya ya moyo bure kwa wananchi tarehe 29 & 30 mwezi huu September kuanzia saa 3 nayo Jembe Fm ikilishika mkono zoezi hilo katika upashaji habari umma #KAZINANGOMA inakukutanisha na madaktari wa Hospitali hiyo kutoa muhutasari wa uhamasishaji ili kupata matokeo na watu kujitokeza kwa wingi siku hiyo. Saa hii studioni LIVE Tuko na Dr. Andrew Luhanga pamoja na Afisa Habari wa Hospitali husika......@chrissthedj @mwakad25 @mansourjumanne @gsengo @LucyMogele #VyumaVimekaza🔩🔧

MTOTO MWENYE MATATIZO YA AKILI AFUNGIWA NDANI KWA ZAIDI YA MIAKA 5 ENEO LA KIJITONYAMA ALIMAUA B DSM.

Mtoto mwenye matatizo ya akili afungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 5 eneo la Kijitonyama Alimaua B DSM.
Mtoto mwenye matatizo ya akili afungiwa ndani ya nyumba kwa zaidi ya miaka 5 eneo la mtaa wa Kijitonyama Alimaua B Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa na mzazi wake kuwa hana uwezo wa kumsaidia.

RAIS ASEMA DARAJA KUBWA KULIKO YOTE NCHINI LAJA.

Ujenzi wa daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo la Aga Khan kuanza kujengwa mwezi juni mwakani.

Thursday, September 22, 2016

LUIS ENRIQUE ALIA KUMKOSA MESSI DIMBANI.

 Kocha wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique, amesema kikosi chake kitabaki imara ingawa kitamsubiria Lionel Messi aliyepatwa majeruhi kwenye mchezo wa jana wa sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Messi alitoka nje kipindi cha pili cha mchezo huo, uliopigwa uwanja wao wa nyumbani baada ya kushtua misuli ya mguu, na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

Enrique amesema kumkosa Messi ni kukosa soka, lakini bado anayo safu ya ushambuliaji iliyo tayari kufanya kazi.

BAADA YA MWANZA KILIMANJARO QUEENS WATUA DAR NA MAPOKEZI YA NGUVU.

Kilimanjaro Queens imekanyaga ardhi ya Dar ikiwa na kombe la CECAFA Women’s Championship 2016 walilolitwaa nchini Uganda kwa kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets kwa magoli 2-1.
Timu hiyo imepeta mapokezi kutoka kwa viongozi wa serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo, viongozi wa TFF pamoja na mashabiki ambao walijitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mw. JK Nyerere.
 Safari ya Kilimanjaro Queens ilianza Septemba 9 ikiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma walikabidhiwa bendera ya taifa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tayari kuelekea Jinja nchini Uganda baada ya kuhitimisha kambi ya siku chache mjini Bukoba.
 Kabla ya kuelekea Jinja, Kilimanjaro ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.

Wanadada hao wa Tanzania bara waliwasili Uganda wakiwa tayari kukipiga kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania iliangukia kwenye Kundi B kundi lililokuwa na timu tatu (Tanzania, Rwanda na Ethiopia).

Ilianza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Rwanda kisha ikatoka suluhu na Ethiopia na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa matokeo ya kurushwa shilingi kufuatia kulingana pointi na Ethiopia.
 Kwenye husu fainali wakakutana na wenyeji wa mashindano hayo timu ya Uganga ambapo Kilimanjaro ikafuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Uganda kabla ya kuishinda Kenya na kutangazwa mabingwa wa CECAFA ya wanawake.

*MAGRUPU YA WASAP YA UONGOZI NA LEADERS YAKABIDHI MIL. 16 TETEMEKO*

*MAGRUPU YA WASAP YA UONGOZI NA LEADERS YAKABIDHI MIL. 16 TETEMEKO*
*Yadhihirika grupu za Wasap zaweza kuwa chachu ya Maendeleo*

Wanachama wa magrupu mawili ya wasap(whatsapp), leo (Septemba 22) wamemkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, jumla ya 16m/-, kwa ajili kusaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
Akiongea katika hafla hiyo,mmoja wa waratibu wa magrupu hayo Dk.Ave Marie Semakafu amesema fedha hizo ni michango ya wanachama wa magrupu hayo, yaitwayo ThebLeaders Forum na Jukwaa la Uongozi.
Amesema wanachama hao wameguswa na yaliyowakuta watanzania wenzao mkoani Kagera, hivyo,waliona njia pekee ya kuungana nao katika majonzi ya janga hilo ni kutoa kidogo wali nacho.
Dk Semakafu amewaasa watanzania wengine, hasa walioko kwenye vikundi mbalimbali hususani vya mitandaoni, kushiriki zoezi la kuwachangia waathirika hao kwa vyovyote wawezavyo, maana hali bado ni mbaya mkoani Kagera.
Alisema madhumuni ya magrupu hayo ni kujadili maendeleo ya taifa pamoja na kutoa ushauri mbinu mvadala kuifikia ndoto ya Tanzania tunayoiyaka.
Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10, ambapo watu 17 wamepoteza maisha,wengine zaidi ya 200 wameruhiwa,huku nyumba zaidi ya 800 zikiwa zimeharibika,zingine kuanguka.
Akiongea katika hafla hiyo Waziri Mkuu aliwashukuru wanachama wa majukwa hayo akisema wanapaswa hafla kuigwa na makundi mengine nchini. "Sisi kama serikali tunawashuru sana kwa moyo huo wa upendo kwa wenzetu wa Kagera,na hatutaishia hapa bali tutafanya hivyo kwa maandishi."
Aliwahakikishia wachangiaji waliokabidhi misaada yao leo yakiwemo makampuni mbalimbali na vikundi vingine vitano kuwa atahakikisha misaada yote itawafikia walengwa.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam. Wanachama wa majukwaa hayo ni watu wa kada mbalimbali hususani viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu,akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda.
Wengine ni Mwaziri,Wabunge, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi, wanataaluma wa vyuo vikuu,wanahabari, Wafanyabiashara na Viongozi wa vyama vya Siasa.
Waratibu wengine wa magrupu hayo ni Dereck Murusuli,Benjamin Thompson Kasenyenda,Leila Sheikh,Dr.Michael Francis,Maggid Mjengwa, Mustafa Ismail Kam

BODI YA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM YAJIUZULU

Christopher Ole Sendeka.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe 22 Septemba 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.

Bodi ya Uhuru Media Group ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia, kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti ya Makampuni hayo na kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa vyombo vya habari vya Chama.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe 22/09/2016.

AIRTEL YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 150 MAGOGONI FERI.

Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akikabidhi msaada wa miamvuli 150, kwa Mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu, kupitia mpango  wa Airtel Fursa, kwa ajili ya wafanyabiasha wadogo wadogo katika Soko la Samaki la Kimataifa la Magogoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (wa pili kulia), Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala, Eliakim Mnico na (wa tatu kulia) ni Naibu Katibu wa Kamati ya Wadau sokoni hapo, Abeid Bulla.
Mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu (katikati) na  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto kwake) wakimkabidhi mwamvuli mpaa samaki, Salum Ally (wa pili kushoto), baada ya Airtel kupitia mpango  wa Airtel Fursa, kukabidhi msaada wa miamvuli 150 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo katika Soko la Samaki la Kimataifa la Magogoni jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu  akimkabidhi mwenyekiti wa umoja wa wauza samaki DSM (UWASADA) bwn Charles Mussa miavuli baada ya Airtel kupitia mpango  wa Airtel Fursa, kukabidhi msaada wa miamvuli 150 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo katika Soko la Samaki la Kimataifa la Magogoni jijini Dar es Salaam jana.

Airtel yawafikia wafanyabiashara zaidi ya 150 Magogoni Feri

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA leo imewawezesha wafanya biashara zaidi ya 150 wa maeneno ya magogoni sokoni kuendesha biashara zao chini ya kuvuli baada ya kampuni hiyo kukabidhi miamvuli ya biashara kwa wafanya biashara wadogo wadogo kwa lengo la kuboresha maeneo yao ya biashara. 

Wafanyabiashara hawa wa bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na samaki, mboga za majani , soda,  maji, na nyingine nyingi wamekuwa wakipigwa na jua kali na baadhi ya bidhaa zao kuathiriwa na jua kali na mvua. Airtel kupitia Airtel FURSA imeona ni vyema kuwawezesha kwa kuwapatia miavuli ya biashara itakayokinga uharibifu wa  bidhaa zao na afya zao kwa ujumla

Vifaa hivyo vimekabithiwa na Airtel na kupokelewa na mbunge wa Ilala, Mh. Musa Zungu kwaniaba ya wakazi na wafanyabiashara wa maeneo hayo

Akiongea wakati wa  kukabidhi vifaa hivyo, mbunge wa Ilala, Mh. Musa Zungu alisema “nafurahi kuona Airtel wamejitoa kuwasaidia wafanyabiashara hawa kuendesha biashara zao, msaada huu unathibitisha dhamira ya Airtel ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kuendesha biashara zao ili kukuza kipato na kuinua maisha yao.
Miavuli inayotolewa na Airtel leo itawasaidia wafanyabishara hawa kujikinga na jua kali la Dar es salaam na wakati mwingine mvua”

Nachukua fursa hii kuwapongeza Airtel kwa juhudi zao mbalimbali katika kuwasaidia wafanyabiashara kupitia program yao ya Airtel FURSA. Na nNatoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huu , haijalishi kiasi gani tunatoa kwani kidogo kile tunachotoa kitasaidia sana kukuza biashara za wajasiriamali hawa wadogo wadogo.”


Kwa upande wake  Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema “ Airtel ni kampuni inayoamini katika kusaidia jamii katika maeneo  tunayoendesha biashara zetu .  Kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA kwa mara nyingine tunatoa msaada kwa wafanyabiashara wa wadogowadogo Kivukoni kwani tunaamini mtu  yeyote anaweza kufanya biashara pale atakapowezeshwa , kupewa motisha, na pindi yeye mwenye atakapokuwa na  nia dhabiti, kujituma na malengo sambamba na nidhamu katika kazi”.