NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini uongozi wa shule ya msingi ya Kibaha Independent (KIPS) imesema kwamba inatarajia kujenga majengo mengine kwa lengo la kuweza kuanzisha shule ya sekondari ili kuweza kutoa fursa elimu kulingana na mahitaji ya wanafunzi wanaohitimu shule za msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Yusuph Mfinanga wakati wa mahafali ya 11 ya shule hiyo ambayo ni ya binafsi ambapo ameahidi kushirikiana bega kwa began a wadau wengine wa maendeleo sambamba ana serikali katikam tutimiza lengo hilo la kujenga shule ya sekondari.
Mfinanga alisema kwamba anatambua katika elimu kuna changamoto nyingi ambazo zinahitajika kutatuliwa ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kuwapa elimu bora ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa katika siku zijazo, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.
“kumekuwepo na maombi mbali mbali kutoka kwa wazai kuhusina na kuwepo kwa shule ya sekondari katika Wilaya yetu ya Kibaha ambayo itaweza kuwapa fursa wanafunzi wanaomaliza katika shule za msingi kuweza kujiunga na kidato cha kwanza wakiwa katika maeneo ya karibu ili kuweza kupata elimu bora zaidi hivyo sualla hili lipo katika mipango yetu,”alifafanua Mfinanga
Katika hatua nyingine Mfinaga aliiomba Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa wanadumisha zaidi miundombinu ya majengo katika shule mbali mbali sambamba na nyumba za walimu ili kuweza kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi akizungumza kwa niaba ya wenzake Selina Wilson walimu wa shule wanapaswa kuwa waangalizi wa watoto shuleni kwa ukaribu zaidi kwa lengo la kuweza kuwafuatilia mienendo yao na kuepusha wimbi la watoto wanaokwenda kinyume na maadili.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Herzon Musalale alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa 2002 kwasasa ina wanafunzi 650 ambapo kwasasa wana matarajio ya kuanzisha shule ya sekondari.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa Halmashauri ya mji wa kibaha Ramadhani Lawoga alisema serikali ipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbali mbali wa sekta ya elimu ili kuweza kuona ni namna gani wanaweza kusaidia kwa hali na mali katika kusapoti suala zima la elimu.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa Halmashauri ya mji wa kibaha Ramadhani Lawoga alisema serikali ipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbali mbali wa sekta ya elimu ili kuweza kuona ni namna gani wanaweza kusaidia kwa hali na mali katika kusapoti suala zima la elimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.