ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 3, 2011

UZINDUZI WA MSIMU WA DHAHABU MWANZA ULIVYOFANA HII LEO JIJINI MWANZA.


Anaitwa Msamy ni msanii toka kundi la THT akionyesha utundu katika siku ambayo msimu wa Dhahabu umezinduliwa rasmi.



Ilianza kama mchezo hivi

Shughuli zimefanyika kwenye kipita shoto kikuu cha Mwanza kinachounganisha Barabara za Makongoro, Kenyata na Nyerere ambapo umati mkubwa umejumuika kushuhudia dakika hizo chache muhimu tamu za msimu wa Dhahabu.


Daah! hawa jamaa walitia fora pozi za ukweli steps za maaana.



Haina majotrooo!



Kamziki kanapo mdatisha mwananchi...



Barabara zilifungwa kwa muda kupisha tukio la kihistoria kuchukuwa nafasi, pichani barabara ya Kenyata.



Wewee...



AMPLIFAYA MAN Milard Ayo mbele ya wadau wa Uzinduzi wa msimu wa Dhahabu Mwanza hapa wakiwa mbele ya mjengo wetu.



Mara baada ya kazi kumalizika, tathimini kisha nikupongezana tu!

Kufanyika kwa Tamasha hili la Kumi la Kimataifa la Serengeti Fiesta 2011 nchini, hakika kutatoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kutokana na shughuli mbalimbali za kibiashara zitakazofanyika ndani ya msimu wa fiesta mwaka huu.


KIDOKEZO NI KUWAAAAaaaaaa...'' SAFARI HII MWANZA KUNA KITU YA 'HATARI' YAJA KUONDOA 'MAJOTROO. SWALI NI KWAMBA:- MWANZAAAAaaaaa mmejianda'ndaaje?

OLIVER & ALBERT NI SIKU KAMA YA LEO VILE

Albert $ Oliver 3june2006.
Ni picha za kumbukumbu ya Harusi yangu iliyofungwa siku kama ya leo katika kanisa la st. Joseph Anglican Arusha mjini.

Sahihi ya bi harusi mbele ya mchungaji Kajembe.

Sahihi ya bwana harusi.

Bi harusi akitoa ishara kutambulisha tukio la ukataji keki.

MATUNDA NDIYO HAYACuthbert Albert G.Sengo.

Cedrick Albert G.Sengo. (first born)

We...

Thursday, June 2, 2011

KOSHA MACHO:

Kaka akila bata' ni ndani ya hoteli moja maarufu pale Ngudu wilayani Kwimba.

Stephano Charles na Sahani Richard wakifuma mpira.
Ayaaaaa ananikumbusha mbaaali sana....Enzi zanguZZz!! Nakumbuka enzi hizo nilikuwa fundi mzuri kweli kweli - kufuma mipira ya chandimu yaani nyenzo zote mpira utadunda huo... nowmaa (Uliza kwa sana Shule ya Msingi Levolosi Ar, Hinduki Mlp na Uhuru Shy).

Barabara inayoingia katikati ya mji wa Ngudu hatimaye kituo cha mabasi Ngudu wilayani Kwimba.

Barabara ya Mwanza-Shinyanga inayoendelea kufanyiwa matengenezo mara baada ya kuchekesha.

Barabara ya Mwanza-Shinyanga inayoendelea kufanyiwa matengenezo mara baada ya kuchekesha ikitiwa maji.

Mwanza usiku na barabara ya mtaa wa posta.

KATULANDA AIOMBA JAMII KUMSAIDIA DADA HUYU

Nimetembelea Shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga ambayo hutunza watu wenye Ulemavu mbalimbali na kwa sasa imegeuzwa pia kuwa kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Hapo shuleni nimekutana na Kabula Nkalango (14) mmoja wa wahanga wa mauaji ya Albino ambaye alinusulika kuuawa na wauaji kutoweka na mkono wake.

Anaomba msaada wako kumuwezesha kupata mkono wa bandia au vifaa mbalimbali vya masomo. kama uko Tayari wasiliana nami nitakuunganisha na mkuu wa shule yake.


Nae Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Babu Sikare maarufu kwa jina la Albino Fulani ambae pia ni CEO wa Afrobino akiwa katika kituo hicho cha Malezi ya watu wenye Ulemavu wa ngozi mkoani Shinyanga ambako alitembelea na kutoa misaada ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Sunscreen), Kofia na Mianvuli. Aliweza kuzungumza na mwanafunzi Kabula Nkalango ambaye alinusurika kuuawa katika mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kukatwa mkono wake wa kulia na kumkabidhi msaada huo kwa niaba ya walemavu wengine.

Fredrick Katulanda
Mwandishi wa habari
Mwananchi Communication
Mwanza.

WADAU NAOMBA KUWASILISHA.

Hi, How are you today,

Nimetembelea duka lenu la Arusha leo na nikashangazwa kupita kiasi na mmiliki wa funiture center,, muindi mweusi anaevuta sigara mbele ya wateja,, kiustarabu nikamwambia samahani unaweza kuzima sigara yako,, kwa kweli majibu yake yalikuwa kama yafuatayo,, "hili ni duka langu,, huwezi kunipangia kama huwezi do not come to this shop"

Nimeshangaaa,, ninashangaaa na nitazidi kushangaa kwa kukutana na mtu huyu,, asiyejua thamani ya mteja,, naomba kujua kama amesomea marketing popote au customer care popote,, na kama anajua madhara ya sigara kwa mwili wa binadamu tena asiyetumia sigara,,

Funiture Center nimekuwa nikiiamini sana kwa service nzuri but today,, nimeona maajabu.

It is not important to me kununua kitu Funiture Center,, naweza kwenda popote na kununua,, hata kuagiza nje i can,, but tell the guy,, biashara haiendi hivyo,, kumpoteza mteja mmoja kwa business ni kupoteza wengine 49 na maelfu mbele ya safari...


Thank you and all the best.
Regards
Fran.

PICHA ZA MAJERUHI WA RISASI NA MABOMU SAKATA LA UTEKAJI WA KITUO CHA POLISI MUGUMU MKOANI MARA.

Majeruhi Wambura Itembe Kisera.
Majeruhi wa sakata la kuvamia kituo cha polisi MUGUMU lililotokea wiki hii wako taabani ifuatayo ndiyo hali halisi na hatua zilizo chukuliwa dhidi ya majeruhi hao wenye kesi ya kujibu.

Majeruhi Wambura Itembe Kisera akiwa hospitali akisubiri kupelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza, baada ya kubainika kuwa risasi alipigwa risasi kwenye nyonga na kuvunja mifupa, wakati wa vurugu za uvamizi wa kituo cha polisi, hata hivyo alisomewa mashitaka akiwa hospitalini hapo.

Pichani majeruhi Mkira Maswi mkazi wa Itununu katika hali tofauti aliyelazwa kitanda no.6 hospitali teule ya Nyerere ddh wilayani Serengeti kutokana na majeraha ya kupigwa mabomu ya moto na askari polisi katika tukio la kuvamia kituo cha polisi Mugumu ili watoe watuhumiwa wawili wa mauaji wawaue.

(picha zote na Anthony Mayunga)

‘MO’ ACHANGIA MASHINDANO YA RIADHA YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI…!!!

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya MeTL ambaye pia ni msaidizi wa Mh. Mohammed Dewji (Mb) Esther Dotto akikabidhi mchango katoni 42 za maji safi ya kunywa ‘ MAISHA’ yanayotengenezwa na Kampuni ya A-ONE Products and Bottlers ambayo ni moja ya makampuni ya MeTL kwa Mkurugenzi wa Radio One Deogratius Rweyunga kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 3-4 June, 2011.

Deogratius Rweyunga.
Mkurugenzi wa Radio One Stereo Deogratius Rweyunga akitoa shukrani kwa kampuni ya MeTL kwa kuona umuhimu wa kuchangia ili kufanikisha mashindano hayo na kuzitaka kampuni zingine kuiga mfano huo.

Msaada.
Katoni za maji safi ya kunywa aina ya MAISHA yanayotengenezwa na moja ya kampuni ya MeTL yaliyokabidhiwa kama mchango kwa ajili ya mashindano hayo.

Mh. Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini.
“Ni vyema sisi kama watanzania tukachangia kukuza maendeleo yetu wenyewe katika michezo, na si katika soka peke yake, bali kwa michezo yote kwa ujumla”

Wednesday, June 1, 2011

UZINDUZI WA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA YAFANYIKA LEO WILAYANI KWIMBA MKOANI MWANZA.

Huku wengine waki... hakika ilikuwa patashika nguo kuchanika kwa mheshimiwa huyu jukwaa kuu, pale ngoma ya nyoka toka Bujora ilipokuwa ikitoa burudani

Uzindizi wa kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa mkoa wa Mwanza umefanyika rasmi leo kwenye Uwanja wa KWIDECO katika Tarafa ya Ngudu Wilayani Kwimba ambapo masuala ya ukosefu wa maji, uhaba wa chakula, ukame, ulinzi na usalama ndiyo yalikuwa yameteka sehemu ya mkutano huo wa uzinduzi ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 9Desemba mwaka huu.

Kundi la Sungusungu Busule Likimwaga utamu wa burudani.
Shughuli za Uzinduzi zimefanyika sambamba na vikundi mbalimbali vya ulinzi shirikishi yaani Sungusungu kupita mbele ya meza kuu iliyokuwa imesheheni wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Mwanza na Sekta mbalimbali za serikali, vikitoa ujumbe kupitia nyimbo kuapa kushirikiana na serikali katika suala zima la ulinzi.

Kundi la Sungusungu Kimiza.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo za uzinduzi alikuwa Mkuu wa wilaya Geita Mh.Filemon Shelutete ambaye katika hotuba yake amewataka watanzania hususani vijana katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa nchi, kufuata misingi aliyotuachia Baba wa taifa Hayati MWALIMU JULIUS NYERERE ikiwemo kudumisha umoja kwani ndio njia pekee ya kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Aidha amesema mtaji mkubwa kwa taifa lisilo tajiri kama TANZANIA ni kuhakikisha umoja unalindwa kwa nguvu zote..

Wadau hawa wa ulinzi walijiandaa kweli kweli kutia nakshi sherehe hizo za ufunguzi kwa mikogo, mwendo wa madaha sambamba na nyimbo zao tamu za makabila ya kisukuma.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ngudu Lugulu.
Ni miaka 50 ya Uhuru inakwenda kutimizwa rasmi tarehe 9desemba2011 na wilaya ya kwimba haina maji, visima vya kupampu maji vilivyojengwa na ESAWA vyote ni vibovu vimeharibika.

Matanki tegemewa ya maji kwa wilaya nzima.
Wilaya nzima inamatanki mawili ya maji yaliyojengwa enzi za Ukoloni kwa hesabu ya kuwakimu watu Elfu tatu miaka hiyo ambapo sasa idadi imeongezeka. Malambo ya maji ambayo wananchi walikuwa wakiyategemea yamekauka mapema tena katika msimu wa mvua, Jeh kiangazi kikianza itakuwaje?

Kwaya ya Mawe Matatu ikitumbuiza katika sherehe hizo za uzinduzi.

Unaona Utaaaaamu!

Kasheshe ilizuka pale moja kati ya nyoka hao alipowekwa juu ya meza ya wagenirasmi, si waheshimiwa wakaingia mitini!!.

Filamu la kusisimua... Akiwa ameakti kama kagongwa na nyoka aka Snake.

Wanafunzi wa shule mbalimbali Wilayani Kwimba wakiimba wimbo wa 'Tanzania nakupenda kwa moyo wote'

Wadau wa Chama cha Mapinduzi ambao walijitokeza viwanjani hapo hapa wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa ulioongozwa na alaiki ya wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani Kwimba.

Halaiki ya wanafunzi.

Tuesday, May 31, 2011

MTEMI MILAMBO FESTIVAL NI JULY 8-10 TABORA.

TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Milambo linatarajiwa kurindima kuanzia Julai 8 hadi 10 kwenye Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.Meneja wa Bia ya Balimi Bi.Edth Bebwa na Amon Mkoga Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam leo (30/05/2011), Mkurugenzi wa taasisi ya Chief Promotions ambao ndio waandaaji, Amon Mkoga, alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Kitanzania, hususani makabila makubwa ya mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza, ambao ni Wanyamwezi na Wasukuma.

Mkoga alisema pia michezo na maonyesho ya bidhaa zenye asili ya Kitanzania pia vitakuwepo,kama vile mchezo wa bao na kurusha mishale. Alisema, Ijumaa ya Julai 8 shughuli itaanza saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni na kuendelea kwa muda huo huo hadi Jumapili Julai 10.


MTEMI MILAMBO pichani mnamo mwaka 1885-->

Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya ngoma zitakazokuwemo wakati wa tamasha hilo kuwa ni pamoja na Manyanga, Maswezi, Uyeye, Bagalu, Bagika, Bazuba, Radu na nyinginezo.
Naye Meneja wa Bia ya Balimi, ambao ni kati ya wadhamini wa tamasha hilo,Bi Edith Bebwa, alisema wameamua kujitosa kudhamini tamasha hilo kwa mara ya pili ili kuwaenzi wateja wa bia hiyo ambayo ni mahususi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. “Ngoma hizi za Wasukuma na Wanyamwezi huchezwa sana wakati wa mavuno, hivyo kwa kuwa Balimi ni bia ya mkulima tumeona tuungane kusherehea pamoja wakati wa mavuno huku tukienzi utamaduni wa Kitanzania,” alisema Bebwa.

Mgeni rasmi katika Tamasha hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Abeid Mwinyimusa.

Kauli mbiu ya Tamasha hili mwaka huu ni KUSHOKE KUKAYA yaani turudi nyumbani tafsiri ya Kiswahili toka kinyamwezi.

Mbali ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi, wadhamini wengine ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ubalozi wa Switzerland ,Kalunde General Supplies, UNESCO na Fly 540(Shirika la ndege),Geita Goldmines, Magic Fm, Channel Ten na TBC.


Aksanteni kwa kunisikiliza na karibuni Tabora

Amon Mkunga
Mkurugenzi Mtendaji
Chief Promotions
P.O.Box 78566
Simu: 0755 638 004/0655 638 004
Barua Pepe:dramontz2002@yahoo.com
Tovuti:www.chiefpromotions.or.tz
Dar es Salaam
Tanzania

Pn'C BARBER SHOP MWANZA 'DUH - NI PAUKWELI'

Ni sehemu ya huduma makini, Saluni iliyo kwenda skuli kwa masuala ya:- Hair Cuts, Mancure, Pedcure, Facial, Scrub, Massage, Foot Massage & Footrub, Black, Etc...

Sehemu muhimu kwa ajili ya 'kujiswafi' kwa watu wa rika zote (Nyumbani kwa mtoto mwoga aliaye mlizi wakati akinyolewa)

Pn'C Barber Shop tunajivunia utamaduni wetu wa ukarimu na usafi kupitia vifaa vyetu na mazingira yetu.

Pn'C Barber Shop tupo Nyakato Mecco Kwenye kona kurudi barabara kuu iendayo Igoma Mwanza Tanzania.

KARIBU TENA...