ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 2, 2011

WADAU NAOMBA KUWASILISHA.

Hi, How are you today,

Nimetembelea duka lenu la Arusha leo na nikashangazwa kupita kiasi na mmiliki wa funiture center,, muindi mweusi anaevuta sigara mbele ya wateja,, kiustarabu nikamwambia samahani unaweza kuzima sigara yako,, kwa kweli majibu yake yalikuwa kama yafuatayo,, "hili ni duka langu,, huwezi kunipangia kama huwezi do not come to this shop"

Nimeshangaaa,, ninashangaaa na nitazidi kushangaa kwa kukutana na mtu huyu,, asiyejua thamani ya mteja,, naomba kujua kama amesomea marketing popote au customer care popote,, na kama anajua madhara ya sigara kwa mwili wa binadamu tena asiyetumia sigara,,

Funiture Center nimekuwa nikiiamini sana kwa service nzuri but today,, nimeona maajabu.

It is not important to me kununua kitu Funiture Center,, naweza kwenda popote na kununua,, hata kuagiza nje i can,, but tell the guy,, biashara haiendi hivyo,, kumpoteza mteja mmoja kwa business ni kupoteza wengine 49 na maelfu mbele ya safari...


Thank you and all the best.
Regards
Fran.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. tatizo ni ufuatiliaji wa sheria, nadhani kuna sheria mpya za uvutaji sigara lkn tatizo ni usimamizi kaka

    ReplyDelete
  2. ndugu Fran, kama ulivyopoteza nguvu na muda kutuandikia sononeko lako, nami naomba nipoteze muda kukupa ushauri ufuatao. Ni kweli kuna sheria (nasikia) kuhusu uvutaji wa sigara hadharani. sijui 'hadharani' inaanzia wapi na inaishia wapi. Lakini kwa kuwa hapo pahala, kama alivyosema mmiliki wake, ni sehemu ya biashara sidhani kama ulihitaji kukasirika na kuhamaki kiasi cha kutoa ndita kiasi ulichotoa. sehemu ya biashara inaaminika ni sehemu ya kumletea kipato huyo muhusika. anayepaswa kujua umuhimu wake ama upuuzi wa sehemu hiyo ni mfanyabiashara mwenyewe. nakuaomba zisikutoke ndita na kupoteza nguvu nyingi kuandika sononeko hili. biashara ni ni kitu huria. hapo pangekuwa hospitali, mahakamani au sehemu yoyote yenye ulazima wa kwenda ningekuunga mkono (pengine na mguu pia). when one shop is closed (because owners smoke), many more shops are open just around the corner. we jiagizie fenicha zako ulaya. achana na muhindi huyo

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.