ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 9, 2015

KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA, MTATURU AONYA WATENDAJI NA WATUMISHI WA SERIKALI ILEMELA KUINGILIA SIASA.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, kimewaonya watendaji na watumishi wa serikali kutoingilia kati ‘mchezo’ wa siasa kwani hauwahusu wasubiri Chama kitakashoshinda na kuunda serikali ambayo wao watafanyakazi zake.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alipokuwa akizungumza juzi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela mkoani hapa kilichohusisha watendaji wa Halimashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilemela.
 
Katibu huyo amewaonya watendaji na watumishi wa serikali, na kusema kuwa, wakiache Chama hicho kichuane na vyama vya wapinzani ikiwemo vya Muungano wa UKAWA, serikali iliyoko madarakani ni sawa ni mkandarasi wa Chama hicho tawala.
 
Mtaturu, alisema kwamba  wajibu wa watendaji na watumishi wa serikali iliyopo madarakani ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyochaguliwa na wananchi kwa miaka mitano na kuwatumikia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vya kisiasa, makabila, dini zao na rangi bali kuwaletea maendeleo.
 
“Baadhi mmeacha kutekeleza majukumu yenu na kujiingiza kwenye siasa, mchezo wa siasa hauwahusu fanyeni kazi mliyotumwa na serikali iliyoko madarakani, msiingilie yetu na wenzetu (wapinzani) mtakiuka maadili yenu, ole wao watakaogundulika hatutowaacha tutaomba wachukuliwe hatua kali za kimaadili,” alionya Mtaturu.
 
Alidai, Katibu huyo alisema kuwa ,kumekuwepo na baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa watendaji wengine wamekalia siasa na kuacha wajibu wao wa kuwahudumia jambo ambalo linakiuka maadili yao ya utumishi, CCM haiwezi kuendelea kulaumiwa kwa sababu ya watendaji wa aina hiyo, itawafagia.
 
“ Sisi wakati tunamenyana na vyama vya upinzani baadhi mlivisaidia, wengine mlikuwa mnachungulia madirishani mkiuliza nani kashinda, wengine mlikuwa mnasema atakayeshinda ni huyohuyo mtafanya nae kazi,” alieleza Katibu huyo na kuwapasha.
 
Aliongeza kuwa CCM ilishinda hivyo msiingilie ngona isiyowahusu, tekelezeni Kandarasi ya Ilani ya CCM, waliyochagua wananchi, watakaoshindwa kuwajibika na kutumia ofisi za serikali kwa ufisadi, tutawang’oa waingie wengine, msichezee kazi wakati kuna watanzania kibao wanalilia kazi usiku na mchana.”
Wito wangu naombeni mwendelee kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa vitendo na muwatumikie wananchi bila kuwabagua pamoja na kuwepo itikadi za kisiasa za vyama vyao ili kuwaletea maendeleo na kuwapatia huduma zinazostahili katika sekta zote za kijamii na kiuchumi zilizopo nchini.

JINSI YA KUZUIA NA KULINDA TAARIFA ZAKO MTANDAONI SEHEMU YA II

Simu
Ili kulinda simu unazopiga na unazopokea, tumia application ya RedPhone.
https://lh5.ggpht.com/O2MTDEI9aoPNYBBc3Dd1uBTX6oaragGjz_4DeOB05In02eAMlAY0XUNlQO_OgnmeDvTU=w300
RedPhone imetengenezwa na kampuni ya Open Whisper System – kampuni ile ile iliyotegeneneza TextSecure. Faida zake ni kama za TextSecure:-
·         Ina encrypt mawasiliano yako wakati unaongea hivyo hauna anayeweza kusikiliza maongezi yako hapo katikati.
 Kwa watumiaji wa iPhone, Open Whisper System wametoa app inayoitwa Signal ambayo inaunganisha encyrption ya meseji na simu kwenye app moja. App hii inaweza kufanya kazi na TextSecure na RedPhone kwa Android unapotuma meseji au kupiga simu kutoka kwenye app moja kwenda nyingine.

Mtandao

image
Kujilinda kwenye mtandao kunahitaji umakini zaidi. Download Tor Browser kisha uendelee kufungua websites kama kawaida.

Inavyofanya Kazi
Unapotumia Tor, mawasiliano yako yanapitishwa kupitia mtandao wa Tor. baada ya hapo, mtanda wa Tor unapitisha mawasaliano yako kwenye vituo mbalimbali kutoka miji mbalimbali duniani kabla haijafika kwenye sehemu unayotaa kwenda (usijali, hii yote hufanyika chini ya sekunde moja) Hii inafanya hata ISP wako (Internet Service Provider) hawezi kujua unachokifanya.. Inazua hata websites zenyewe zisijue ulipo.

___________________MWISHO_________________________________
·         Kwa masomo na msaada wa maswala ya IT wasiliana nasi kwa anuani hizo chini.
______________________________________________________________________________
Support Team | RIGHT CLICK SOLUTIONS TANZANIA
P.O.Box 11503, Mwanza,Tanzania | Mob: +255 757 423421
Vijana Centre Building, Ground Floor | Room No.2 | Plot No. 11
Mlango mmoja street | Adjacent AAR Healthcare Hospital

for more options”

BODI YA UTT-PID NA MENEJIMENTI YAKE YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO CHINA

kwana Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.

Na Mwandishi Maalum
Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.
Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi wa maeneo hayo.

KAZI ZA UTT-PID
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
pili
Bodi ya UTT-PID pamoja na Menejimenti ikipata Maelezo kutoka wataalum wa uzalishaji nishati toka mji wa Chengdu.
saba
Pichani Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
sita
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
tano
Mkutano ukiendelea baina ya Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
tatuBodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elpina Mlaki (wa pili kushoto) pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo.
nne
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Zipingpu Hydropower mwenyeji wao, jinsi gani uzalishaji unavyofanyika na usambazaji wa nguvu za nishati. Mjumbe wa Bodi Mrs. J Mmari (kulia), akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dr. Gration Kamugisha mwenye shati jeupe na kushoto ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Bi. Tuzo Mpiluka.

NGUMI KUFANYIKA MEI 16 BAGAMOYO MJINI


Na Mwandishi Wetu 


MPAMBANO mkali wa masumbwi utafanyika Bagamoyo Mei 16 katika ukumbi wa  che kwa che uliopo Bagamoyo mjini mpambano uho utawakutanisha bondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo atakaezipiga na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam

Mpambano uho utachezwa baada ya kila bondia kujigamba kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie siku hiyo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali wenye upinzani mkali katika masumbwi

Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli 

mipambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo uho mjini Bagamoyo

kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikigawiwa na kocha  Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini.

Friday, May 8, 2015

SIKU MOJA KABLA YA SHOW YA JEMBEKA MADNESS JJ BAND WAACHIA NGOMA MPYA.

Wakipata selfie na baadhi ya watangazaji wa Jembe Fm + Jembe DjZ ni JJ Band wanaotumbuiza kila wikiendi pale Jembe Beach Mwanza, ambapo leo mchana ndani ya Hit Zone wametambulisha single yao 'NISHIKE' mpya ya kwanza waliyoirekodi ndani ya studio za Efex Studios chini ya producer Tiddy Hotter . 
 BOFYA HAPA KUSIKILIZA KILICHOJIRI PAMOJA NA SINGLE HIYO MPYA.

Kuelekea show kali ya Jembeka Madnes itakayopigwa kesho pale Jembe Beach jijini Mwanza tayari wasanii wote toka Kenya wakiwemo Granpa Family wote wamekwisha wasili, pichani mkali anayetamba na trax kama Banjuka na nyingine kali kibaoooo DNA (kushoto) akihojiwa na watangazaji wa Hit Zone, kutoka kulia ni VC aka The Voice Characters, Jackline Shuma na Bonz, mwishoni kuleeeeeee ni The Chris Dj toka Jembe Djz.
Miamba kutoka kushoto ni Bonz, VC, DNA, Oxy, Dj David, Fred na Dj Chris.
See you there.....at Jembe Beach.

KIWANDA CHA PAMBA AMBACHO PAMBA YAKE ILITEKETEA KWA MOTO MKOANI SHINYANGA CHAPATA BIMA YAKE TOKA UAP

Baadhi ya maafisa wa Kampuni uya Bima ya UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) wakitenbelea kiwanda hicho kujionea shughuli za utendaji ikiwa ni pamoja na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho mara baada ya kukipatia bima ya shilingi milioni themanini (80,000,000/=)  kufuatia kuunguliwa na pamba yake katika ghala la kuhifadhia lililopo kiwandani hapo.
Mwanzoni mwa mwaka huu 2015 pamba iliyokuwa imehifadhiwa kwenye moja ya maghala katika kiwanda cha pamba JIELONG Holdings Tanzania LTD iliungua na kuharibika kabisha mara baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu hali iliyosababisha pamba hiyo kuchemka na kuwaka moto.
Ghalani.
Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) akiwa na Meneja madai wa kampuni ya Bima ya UAP Bw. Michael Emmanuel .
Ili kuepuka udanganyifu toka kwa baadhi ya wateja wasio waaminifu wanaozusha majanga ili kunufaika na bima, kabla ya kulipa fidia ya bima kwa mteja Kampuni ya Bima ya UAP hufanya uchunguzi... ZAIDI BOFYA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA MENEJA MADAI.

Kampuni ya Bima ya UAP imeweka utaratibu wa kuwatembelea wateja wake kila msimu kwaajili ya kuona shughuli za utendaji na kutoa ushauri kwa wateja juu ya nyongeza mbalimbali za huduma zinazoongezeka. 
KAMPUNI ya Bima ya UAP iko mkoani Shinyanga kutembelea viwanda vya kusindika pamba, viwanda vya kutengeneza mafuta yanayotokana na mbegu za pamba na alizeti ikiwa ni pamoja na viwanda vya mashudu. 

UAP inawateja zaidi ya elfu arobaini nchini Tanzania. MSIKILIZE MENEJA MASOKO HAPA CHINI.

Sehemu ya majengo ya Kiwanda cha pamba cha JIELONG Holdings Tanzania LTD kilichopo mjini Shinyanga.
Nyuma ya majengo ya kiwanda.
Picha ya pamoja uongozi wa Kiwanda na maafisa wa UAP.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA

JE! FAINALI NI JUVENTUS VS BARCELONA UEFA??


Juventus vs Real Madrid 2015 1-2 Goles Resumen All Goals And Highlights Champions League.

LIGI ya Mabingwa Ulaya UEFA imeendelea katikati mwa juma hili mchezo wa kwanza ukipigwa nchini Italia ukizikutanisha Juventus dhidi ya Real Madrid ambapo Juve iliondoka na ushindi mwembamba wa mabao 2-1.

Ule mchuano mkali wa kutupia gozi nyavuni kati ya Lionel Messi dhidi ya Cristiano Ronaldo umeendelea, kwani baada ya mchezo wa awali ulioshuhudia Ronaldo akifunga bao la kwanza la kusawazisha kabla ya kuongezwa jingine na matokeo kuwa 2-1, Lionel Messi aliibuka shujaa katika mchezo wa pili akijibu mapigo kwa kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Bayern Munich.

A riveting subplot has developed in this season's UEFA Champions League. The two greatest forwards of the age have both surpassed Raúl González's total for goals in the competition and after the first legs of the semi-finals, Lionel Messi leads Cristiano Ronaldo 77-76 having briefly fallen behind on Tuesday night.

Licha ya kufungwa katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Real Madrid bado wana nafasi ya kusonga mbele hatimaye kutinga fainali wakihitaji ushindi wakuanzia bao 1-0 au bao 3-1 katika mchezo wa marudiano watakaocheza nyumbani kwao.

Upande wa pili Baryen Munich wanakibarua kigumu kubadili matokeo kwani kuifunga Barcelona iliyokamilika bao 4-0 kunahitaji miujiza.

Zaidi ya fainali Swali linabaki kuwa Je! nani atatengeneza historia kuwa mpachikaji mabao bora wa zama hizi? Ni Ronaldo au Messi? 


Barcelona vs Bayern Munich 3-0 2015 - All Goals 06-05-2015.

Thursday, May 7, 2015

KATIBU MKUU CCM TAIFA, KINANA, MWENYEKITI WA UDP TAIFA, CHEYO NA DK. MASHA WAMLILIA BOGOHE ALIYEPIGANIA AMANI.

 NA PETER FABIAN, BUCHOSA
MWENYEKITI wa Chama cha UDP taifa, John Cheyo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdullahman Kinana na Dk. Fotunatus Masha aliyewahi kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa UDP taifa wamlilia na kutuma salamu za rambirambi mazishi ya mwasisi wa Chama cha TANU na Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya Chama cha  UDP taifa, marehemu Mzee Lameck  Bogohe (93) , aliyezikwa juzi.

Marehemu Bogohe alizikwa juzi katika kijiji cha Kakobe Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, katika wasifu wa marehemu Bogohe henzi ya uhai wake alikuwa mmoja wa wajumbe 17 walikuwa waasisi wa TANU mwaka 1954 kabla ya kuungana na Afro Shiraz Part mwaka 1977 na kuzaliwa  CCM baadaye mwaka 1993 kuamua kujiunga na UDP.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP taifa, John Cheyo, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bariadi Mashariki, akitoa rambirambi za Chama hicho wakati wa misa ya mazishi ya marehemu mzee Lameck Bogohe aliyekuwa mmoja ya waasisi wa Chama cha TANU na  Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu UDP Taifa,  yaliyofanyika juzi kijijini kwao Kakobe Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Cheyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki mkoani Simiyu, akimuelezea marehemu huyo, alifariki Aprili 30 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa Mei 5 mwaka huu nyumbani kwake na mazishi hayo kuhudhuliwa na viongozi wa UDP na viongozi wa serikali, CCM na Mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kakobe.
 Awali akitoa salamu hizo za CCM kwa niaba ya Katibu Mkuu Kinana, Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu alisema CCM ilipokea kwa masikitika kifo cha mzee huyo aliyekuwa miongoni mwa wajumbe walioshirikiana na hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, kutafuta Uhuru wa Tanzania akiwa mwasisi wa Chama cha TANU.

“Katika mazishi haya namwakilisha Katibu Mkuu wa CCM taifa, Comred Kinana aliyenituma kwa niaba yake nimuwakilishe, nasema UDP mmetutendea haki kutualika kuja kumstili mzee wetu marehemu Bogohe, poleni wananchi wa Buchosa na wana UDP kuondokewa na mshauri na mpigania Amani,” alisema Mtaturu.
Huku akiongea na kuvuta hisia za waombolezaji na kuwafanya wampigie makofi (licha ya kuwa msibani) aliposema “Tuishi duniani kwa kutenda mema na kuhubiri amani kama marehemu alivyofanya akiwa hai, vyama vya siasa vipo tu wanachama wake ni watanzania, marehemu alianzia TANU, kafia UDP, siasa isiwe sababu ya kututenganisha, ituunganishe na tuvumiliane na kusisitiza amani na upendo,”alisisitiza.

Mtaturu alipongeza jitihada za marehemu kusimamia amani na umoja wa kitaifa wakati wa uhai wake, alieleza kuwa waasisi hao walitanguliza ‘Tanzania kwanza’ mtu na Chama akafuatia baadaye na kuhoji, amani ikikosekana kutokana na siasa za uchochezi na kusabisha mauaji, kukawa na  vurugu watu wauane wanasiasa kura wataomba kwa nani ?.

Katibu huyo alipigiwa makofi alipodai, historia ya marehemu Bogohe ni kubwa katika taifa hili kwani alipigania amani hivyo kumuenzi kwa maneno haitoshi bali tuwakatae watu wanaovuka mipaka ya demokrasia na kuchochea uvunjifu wa amani ili taifa limwage damu.
 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dk. Chrles Tizeba akitoa salam kwa waombolezaji na wafiwa, viongozi wa UDP na wananchi wa jimbo hilo, alisema marehemu alikuwa mzalendo wa kweli na mmoja wa wazee wake washauri, alimtia moyo katika shughuli za kisiasa na hakutaka kumuombea njaa adui yake.

“Nilipokea kwa masikitiko taarifa za msiba huu na haitoshi nimekuja kushiriki nanyi wananchi wenzangu, marehemu alikuwa mzalendo, hakuwa na usemi wa adui yako muombee njaa, alinipa ujasili katika changamoto za kisiasa kwa ushauri hivyo wana Buchosa tumeondokewa na hazina mhimu, tuienzi kwa vitendo,” alieleza Tizeba.

 Ibada ya mazishi ya Bogohe, iliongozwa na Mchunhaji Alphaxard Kabui wa AIC Kakobe, alisema mwili wa kufa na uharibikao utakapovaa kutokufa, neno lililoandikwa litatimia, mauti itamezwa kwa kushindwa kwani uchungu wa mauiti nidhambi na nguvu ya dhambi ni torati, watu wamshukuru Mungu, Yesu Kristo aliwapa nguvu ya kushinda dhambi, watashinda kila uovu wakimcha Mungu.
Katibu Mtaturu aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Katibu wa Mwenezi wa mkoa Simon Mangelepa, Mjumbe wa Baraza la UWT mkoa wa Mwanza, Kemilembe Julius na Katibu wa CCM wilayani Sengerema, Mohamed Shaaban Mohamed, CCM makao Makuu walitoa rambirambi ya sh 500,000.
Ndugu jamaa na marafiki msibani.
Eneo walilokaa watoto wa marehemu.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP taifa, John Cheyo (MB) kulia, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa UDP taifa, Dk. Fortunatus Masha (Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki) wa pili kutoka kulia, Mke wa Dk. Masha (wa tatu kutoka kulia) na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, aliyemwakilisha Katibu Mkuu CCM Taifa Abdullahaman Kinana, katika mazishi hayo ya aliyekuwa mmoja wa waasisi wa TANU na Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya UDP taifa, marehemu mzee Lameck Bogohe (93) aliyezikwa juzi kijijini kwake Kakobe- Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM taifa, Abdullahaman Kinana (kulia), kuaga mwili wa marehemu Lameck Bogohe (93) aliyekuwa mmoja wa waasisi wa TANU na Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya Chama cha UDP taifa aliyezika kijijini kwake Kakobe-Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wapili kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba wakitoa heshima za mwisho.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dk. Chrles Tizeba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Bogohe.









AIRTEL YATOA PUNHGUZO KABAMBE LA GHARAMA ZA MAWASILIANO

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati),  Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal, wakionyesha bango kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati),  Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal, wakionyesha bango kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Airtel yatoa punguzo kabambe la gharama za mawasiliano 
·         Kufurahia punguzo la hadi asilimia 99 za kupiga simu ndani ya nchi
·         Pungunzo kwa wateja wa Airtel Nchi nzima
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu nchini leo  imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya inayotoa  punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing) Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.

Huduma hii ya Airtel Zone imezinduliwa kwa mara ya kwanza na Airtel ili kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano ya simu za mkononi na kutoa fursa kwa wateja wake kuongea zaidi kwa gharama nafuu mara tu watakapo jiunga kwa kupiga namba 107 na kufuata maelekezo au kupiga *149*39#kisha kuchagua ‘0’.

Akiongea wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” uzinduzi wa punguzo la gharama za kupiga simu  ni uthibitisho wa dhamira ya kampuni ya Airtel kuwapatia watanzania dili lenye thamani halisia ya fedha zao na kuwawezesha watu wengi zaidi nchini kuwasiliana kirahisi. Lengo letu ni kuendelea kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu ili kukithi mahitaji ya watanzania wote. Wateja wetu watakaojiunga na huduma ya “Airtel Zone” kuanzia leo, sasa hivi wataweza kupiga simu na kupata punguzo la hadi asilimia 99 na punguzo hili litategemea mahali alipo mteja”

“Hii ni punguzo litakalosaidia sana wateja wa Airtel kupata unafuu wa kuwasiliana kibiashara, masomo au kwa kuwasiliana na ndugu jamaa au wapendwa wao bila kuwa na wasiwasi juu ya gharama zao za simu” alieleza bw, Nyakundi

Tunaamini huduma hii ya “Airtel Zone” imekuja kwa wakati muafaka wakati mawasiliano ya simu za mkononi ni nyenzo muhimu katika ukuzaji wa shughuli za kiuchumi na za kijamii aliongeza Nyakundi
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hii Mkurugenzi wa Mawasilaiano Bi Beatrice Singano Mallya, alisema” punguzo la gharama litategemea mahali mteja alipo na muda anaopiga simu, mteja atapata ujumbe utakaomuonyesha kiwango cha punguzo anachopata kwa mahali alipo, alikadhalika mteja anaweza  kupiga *149*39*0# ili kuangalia kiwango cha gharama ya kupiga simu. Huduma hii ya “Airtel Zone” ni kwa wateja wa malipo ya awali  na punguzo hili litatumika kupiga simu za ndani tu .

Sambamba na hilo mteja atakayekuwa na kifurushi cha muda wa maongezi kama vile Airtel yatosha na vifurushi vingine punguzo litaanza pale tu kifurushi chake cha muda wa maongezi kitakapoisha.

Kuujiunga ni rahisi, bure na mara moja tu, piga 107 ufate maelekezo au piga *149*39#” aliongeza, Singano Mallya