NA PETER FABIAN, MWANZA.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, kimewaonya watendaji na watumishi wa serikali kutoingilia kati ‘mchezo’ wa siasa kwani hauwahusu wasubiri Chama kitakashoshinda na kuunda serikali ambayo wao watafanyakazi zake.
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alipokuwa akizungumza juzi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ilemela mkoani hapa kilichohusisha watendaji wa Halimashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilemela.
Katibu huyo amewaonya watendaji na watumishi wa serikali, na kusema kuwa, wakiache Chama hicho kichuane na vyama vya wapinzani ikiwemo vya Muungano wa UKAWA, serikali iliyoko madarakani ni sawa ni mkandarasi wa Chama hicho tawala.
Mtaturu, alisema kwamba wajibu wa watendaji na watumishi wa serikali iliyopo madarakani ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyochaguliwa na wananchi kwa miaka mitano na kuwatumikia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vya kisiasa, makabila, dini zao na rangi bali kuwaletea maendeleo.
“Baadhi mmeacha kutekeleza majukumu yenu na kujiingiza kwenye siasa, mchezo wa siasa hauwahusu fanyeni kazi mliyotumwa na serikali iliyoko madarakani, msiingilie yetu na wenzetu (wapinzani) mtakiuka maadili yenu, ole wao watakaogundulika hatutowaacha tutaomba wachukuliwe hatua kali za kimaadili,” alionya Mtaturu.
Alidai, Katibu huyo alisema kuwa ,kumekuwepo na baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa watendaji wengine wamekalia siasa na kuacha wajibu wao wa kuwahudumia jambo ambalo linakiuka maadili yao ya utumishi, CCM haiwezi kuendelea kulaumiwa kwa sababu ya watendaji wa aina hiyo, itawafagia.
“ Sisi wakati tunamenyana na vyama vya upinzani baadhi mlivisaidia, wengine mlikuwa mnachungulia madirishani mkiuliza nani kashinda, wengine mlikuwa mnasema atakayeshinda ni huyohuyo mtafanya nae kazi,” alieleza Katibu huyo na kuwapasha.
Aliongeza kuwa CCM ilishinda hivyo msiingilie ngona isiyowahusu, tekelezeni Kandarasi ya Ilani ya CCM, waliyochagua wananchi, watakaoshindwa kuwajibika na kutumia ofisi za serikali kwa ufisadi, tutawang’oa waingie wengine, msichezee kazi wakati kuna watanzania kibao wanalilia kazi usiku na mchana.”
Wito wangu naombeni mwendelee kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa vitendo na muwatumikie wananchi bila kuwabagua pamoja na kuwepo itikadi za kisiasa za vyama vyao ili kuwaletea maendeleo na kuwapatia huduma zinazostahili katika sekta zote za kijamii na kiuchumi zilizopo nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.