ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 6, 2019

WAKULIMA WA PAMBA WA PAMBA KUANZA KUCHEKA KUANZIA JUMATATU YA SEPT 9


Hivi karibuni kumetokea hali ya sintofahamu kuhusiana na ununuzi wa zao Pamba baada ya kutangazwa kwa bei elekezi ya Sh1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) YAENDELEA KUFANYA VIZURI KIBIASHARA

Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Mh. Cleopa Msuya,(katikati) akifafanua jambo katika mkutano wa wanahisa,wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kulia)na Katibu wa bodi,Huruma Ntahena.
Licha ya changamoto za kibishara  zilizokuwepo katika kipindi cha mwaka uliopita, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, imeendelea kufanya vizuri kibiashara na kuchangia pato la serikali kupitia kodi sambamba na kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii.

Hayo yamebainishwa katika mkutano Mkuu wa 46 wa  wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo imeelezwa kuwa faida ya kampuni hiyo imeongezeka kwa asilimia 15 na kuwezesha wanahisa wake kupata gawio la shilingi 350 kwa kila hisa.

Baadhi ya wanahisa wakifuatilia ajenda za mkutano na kushiriki kutoa mapendekezo
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Cleopa Msuya na Mkurugenzi wa TBL, Philip Redman wakiongea na waandishi wa habari.

RAIS WA ZAMANI WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFARIKI DUNIA.

media
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati huo alitangaza kwamba hatapigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018.REUTERS/Siphiwe Sibeko
Rais wa zamani wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, 
Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Alikuwa amelazwa hospitalini nchini Singapore kwa miezi mitano.


Robert Mugabe ambaye alitawala Zimbabwe tangu uhuru wa nchi hiyo mnamo mwaka 1980, alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Novemba 2017 kwa shinikizo la jeshi na chama chake, ZANU-PF.
Nafasi yake ilichukuliwa na makamu wake wa zamani, Emmerson Mnangagwa, aliyechaguliwa tena kama rais wa Zimbabwe mnamo mwezi Julai 2018.
"Ni kwa huzuni mkubwa ninatangaza kifo cha baba wa taifa na muasisi wa uhuru wa Zimbabwe na rais wa zamani, kamanda Robert Mugabe," Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter.
“Mugabe alikuwa alama ya ukombozi. Mpigania uhuru wa Afrika aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya kuwainua watu. Mchango wake kwa Taifa hili na Bara hili hautasahaulika. Roho yake ipumzike kwa amani,” ameongeza.
Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo hayakuwahi kuwekwa wazi. Alikuwa akipatiwa matibabu nchini Singapore mara kadhaa, lakini alipatiwa matibabu mfululizo nchini humo tangu Aprili mwaka huu.
Hata hivyo Rais Emmerson Mnangagwa amebaini kwamba Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi pamoja na uzee..
Mugabe alilazimika kujiuzulu baada ya kupata shinikizo kutoka kwa jeshi na maafisa wakuu wa chama chake cha Zanu-PF, baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 37. Jeshi lilimtaka ajiuzulu baada ya kutokea malumbano kati yake na makamu wake ambaye ni rais wa sasa Emmerson Mnangagwa, aliefutwa kazi na kukimbilia uhamishoni, kabla ya kurejea nchini kuchukua nafasi ya mtangulizi wake. CHANZO/rfi
.

Wednesday, September 4, 2019

MWANZA YATAMBUA WADAU WA UCHANGIAJI DAMU

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Jophn Wanga, akipokea cheti cha uchangiaji wa damu kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio (kushoto) jana.
 Michael Mugerwa, Meneja mradi wa IMPACT wa Aga Khan Health Service akipokea cheti kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika uchangiaji damu jana.
 Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio (kushoto) akimtunuku cheti mdau mkubwa wa uhamasishaji wa uchangiaji damu, Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Alhaji Sibtain Meghjee, hafla iliyofanyika ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza jana.
 Meneja Masoko wa Isamilo Lodge Grace Kakwezi akipokea cheti cha kutambua mchango wa hoteli hiyo katika ushiriki wake wa kuchangia damu kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Christopher Kadio (kushoto) jana.
 Dk. Mabuba wa Hospitali ya SDA Pasiansi (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio jana baada ya hospitali hiyo kushiriki zoezi la uchangiaji damu.
 Mdau wa uhamasishaji wa uchagiaji dau aliyefahamika kwa jina moja la Peter akiaokea cheti cha kutambua mchango wake kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio jana.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Wanga,akipokea cheti cha uchangiaji damu kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji, Kiomoni Kibamba, jana.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio akizungumza na wadau na wataalamu wa afya kwenye kikao kazi muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti wadau wa uhamasishaji wa uchangiaji damju waliofanikisha zoezi hilo Juni mwaka huu kwa kukusanya chupa 10,669.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WADAU na Wataalamu wa afya wametakiwa kuweka mkakati wa kuelimisha na kuhamasisha jamii kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu.

Rai hiyo ilitolewa jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio, wakati akiwakabidhi vyeti wadau waliofanikisha uchangiaji damu kwenye maadhimisho ya siku ya damu yaliyofanyika mkoani Mwanza kitaifa , Juni mwaka huu.

Alisema ili kuokoa maisha ya wananchi wenye uhitaji wa damu wadau na wataalamu wa afya waweke mkakati endelevu wa kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha uchangiaji damu.

“Wataalamu wa afya mnatakiwa kulifanya zoezi la uchangiaji damu kuwa endelevu na hivyo mtafute jukwaa la kuelimisha jamii ili tufike mahali ijenge utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari na kuweza kutatua changamoto hiyo,”alisema Kadio.

Pia alishauri kutokana na hospitali nyingi kumilikiwa na taasisi za dini ni vyema viongozi wa madhehebu ya dini wakawahamasisha waumini wao kuona umuhimu wa kutoa damu kwa maslahi ya jamii.

Awali Mkuu wa Huduma Maabara Mkoa wa Mwanza, Julius Shigela alisema wadau hao wametunukiwa vyeti hivyo ili kutambua na kuthamini mchango wao kutokana na mafanikio ya ukusanyaji na uchangaji damu.

Alisema Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya damu duniani yaliyofanyika jijini humu Juni mwaka huu, ulifanikiwa kukusanya unit (chupa) 10,669 na kuvuka lengo la wizara kwa asilimia 203, kwa mkoa wakivuka kwa asilimia 101 la kukusanya chupa 4000.

Miongoni mwa wadau waliotunukiwa vyeti kwa niaba yaw engine  zaidi ya 30 ni pamoja na The Desk & Chair Foundation,halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, Isamilo Lodge,Aga Khan Foundation, hospitali za Pasiansi SDA,Hindu na CF.

Picha na Baltazar Mashaka

RAIS DKT MAGUFULI KUMPOKEA RAIS WA UGANDA MUSEVEN JIJINI DAR SEPT 5, 2019

Rais Dkt Magufuli akizungumza pembeni mwa Rais Yoweli Kaguta Mseven mara baada ya kuwasili mapema mwaka huu. (Maktaba).

Nchi yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Yoweri Kaguta Museven Rais wa Uganda, ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamisi ya Septemba 5/2019 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia  Septemba 5/2019 hadi 07/09/2019.

Mhe. Yoweri Kaguta Mseven atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 12.00 jioni.

Mhe. Rais Museveni anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Aidha, Mhe. Rais Museveni anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam Septemba 6, 2019.

Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 07/09/2019 na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Tunaomba radhi kwamba njia atakazopitia mgeni wetu zitakuwa zinafungwa kwa muda ili kupitisha misafara ya viongozi wetu wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Mwl. J. K. Nyerere kumpokea Mgeni wetu hususani barabara ya Nyerere mpaka Mgeni wetu atakapokuwa amewasili na siku ya kuondoka.

Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunamkaribisha mgeni wetu na ajisikie kuwa yuko nyumbani muda wote atakapokuwa hapa jijini.

UJIO WA YANGA KUINUFAISHA MWANZA KIUCHUMI

Mkuu Mkoa Mwanza John Mongela amesema ujio wa timu ya Yanga SC ni fursa ya kibiashara na uchumi kwa mkoa wake.

Mongella ameyanena hayo hii leo (Jumatano ya tarehe 4 September 2019) mapema asubuhi wakati wa kutoa taarifa za ujio wa timu hiyo jijini Mwanza kama sehemu ya maandalizi ya yake kuelekea mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zesco ya nchini Zambia.

HALI IMEKUWA VIPI BAADA YA YANGA KUTUA
Baada ya timu ya Yanga Afrika kuwasili leo majira ya saa 9:00 alasiri kwenye Mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza na maeneo ya jirani pilikapilika zilionekana kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutumia pikipiki na magari ya kukodi kuongozana kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuilaki hali iliyosababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara katika Mitaa huku wauzaji wa Jezi za timu hiyo wakitumia fursa hiyo kuuza ili mashabiki hao waweze kusherehesha mapokezi.


KCB YAINGIA MKATABA WA MWAKA MMOJA NA TFF KUIDHAMINI LIGI KUU.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Benki ya KCB leo Septemba 4,2019 wameingia Mkataba wa Mwaka mmoja wa Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Mkataba huo unathamani ya shilingi Milioni 495 pamoja na VAT.

Udhamini huo unakuja baada ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom kusaini Mkataba wa miaka mitatu ya  Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Mkataba huo unathamani ya shilingi bilioni 9 ambapo kila mwaka shilingi bilioni 3.

Tunaishukuru Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki - Dk. Ndumbaro

Mahakama Kuu ya Gauteng baada ya kuamuru kuachiwa kwa ndege ya Serikali ya Tanzania inayosimamiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa imezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini tangu Agosti 24, 2019. Hatimaye Serikali yaishukuru Mahakama.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro amesema nchini humo kuwa, Mahakama hiyo imekubali hoja zote za mawakili wa Tanzania hivyo Serikali imeshinda kesi na ndege imeruhusiwa kuondolewa uwanjani hapo.

"Kwa hiyo sisi tunaishukuru sana Mahakama ya Afrika Kusini kwa kutenda haki lakini tunawashukuru zaidi Watanzania ambao wameunga mkono juhudi zetu za kuinasua ndege hii kutoka huku Afrika Kusini," amesema Dk. Ndumbaro.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mahakama hiyo pia imeamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi.

Tuesday, September 3, 2019

TBL YATOA MSAADA WA PRINTER KWA TAASISI YA TULIA TRUST

Mkurugenzi wa taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman, wakibadilishana mawazo Katika hafla hiyo.

Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBEV, imetoa msaada wa Printer 9, kwa taasisi ya Tulia Trust, ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii hususani katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Hafla ya kukabidhi msaada msaada huo ilifanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman, na baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi hizo. Akiongea katika hafla hiyo,Dk.Tulia, alishukuru kampuni ya TBL kwa jitihada ambazo imekuwa ikifanya kusaidia kukabiliana na changamoto za kijamii. 

 Akiongelea msaada huo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi nyingine za maendeleo kushirikiana kupambana na changamoto mbalimbali kwenye jamii, hususani katika sekta ya elimu kama ambavyo inaendelea kutoa msaada wa Printer na vifaa vya kurahisisha elimu mashuleni.
Mkurugenzi wa Taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman Katika hafla ya kukabidhi printer 9 iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (katikati) akiangalia Printers zilizotolewa kwa Taasisi hiyo na TBL, (Kulia)ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman.

FURSA LUKUKI KWA WATANZANIA KATIKA KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA, UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita mapema Julai 2019. PICHA NA IKULU.

Na Mwandishi Wetu.
MTANZANIA mwenzangu, najua unajua kuwa siku za karibuni nchi za Tanzania na Uganda zinatarajia kufanya Kongamano la kibiashara la pamoja ambalo litakuwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini kwetu.
Kwa kukumbusha tu, kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Septemba 6 hadi Septemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo baina ya Tanzania na Uganda linatarajia kuwashirikisha wafanyabiashara wa nchi hizo.
Kongamano hilo kwa namna moja au nyingine itakuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara wa nchi hizo kubadilisha uzoefu wa kibiashara na namna nzuri ya kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya pande zote mbili.
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya utawala wa Rais mzalendo na mwenye upendo kwa nchi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine ameweka msingi imara katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata soko kwenye nchi nyingine zikiwemo za Afrika Mashariki.
Kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ambayo imekuwa ikihimizwa na Rais wetu imekuwa chachu kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa viwanda sambamba na utengenezaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zinaweza kushindana kwenye soko la Dunia, Afrika na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kabla ya kuendelea kuzungumzia umuhimu wa kongamano hilo la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda naomba kutumia walau dakika moja ama mbili kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Dk. Magufuli kwa namna ambavyo ameamua kufungua milango ya kuzikaribisha nchi mbalimbali kuja nchi kuwekeza.
Kwa upendo mkubwa kwa nchi yake, amehakikisha anaweka mkazo katika ujenzi wa miundombinu ya uwekezaji na kibiashara na matokeo yake muamko kwa watanzania katika kuwekeza na kufanyabishara umekuwa mkubwa na wenye tija. Hongera Rais wetu kwa kazi nzuri ambayo unaifanya kwa maendeleo ya nchi yetu.
Hata hivyo kupitia kongamano la biashara ambalo linahusisha nchi hizo mbili, ni wazi Tanzania itatumia nafasi hiyo kama fursa ya kutangaza bidhaa zake na wakati huo huo Uganda nayo itaonesha bidhaa zake.
Ni kongamano ambalo kwangu naliona limekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia chini ya Rais Magufuli nchi yetu imekuwa na mazingira mazuri ya kibiashara. Ni wakati muafaka kwa nchi zote mbili kutumia maonesho hayo kujengeana ujuzi katika utengenezaji wa bidhaa bora na utafutaji masoko.
Pamoja na mambo mengine kupitia kongamano hilo la kibiashara itakuwa sehemu sahihi ya kuweka mbinu na mikakati itakayofanikisha kuongeza thamani kwa bidhaa zinazotokana na mazao.Sina shaka na hilo hata kidogo na ukweli kwa Tanzania imedhamiria kuongeza thamani kwa bidhaa za mazao.
Katika maisha ya kawaida najua unaweza kujiuliza hivi , je Tanzania tunauza nini zaidi kwa nchi ya Uganda? Jibu vyovyote lakini hili ambalo nitakueleza ni muhimu
zaidi. Iko hivi mpaka sasa Tanzania inauza bidhaa za mazao na bidhaa za viwandani nchini Uganda.
Takwimu zilizopo zinaonesha kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita Tanzania imeweza kuuza bidhaa za mazao ya chakula na viwandani zenye thamani ya Sh. bilioni 300 kutoka Sh. bilioni 100. Hilo ni ongezeko mara mbili zaidi ya fedha zilizopatikana huko nyuma.
Ninaposema Rais Magufuli ameweka mazingira mazuri ya kibiashara naaminisha na takwimu zinaeleza wazi namna ambavyo nchi yetu ilivyoweka mazingira mazuri katika sekta ya biashara na viwanda.
Nikiri kwa namna ambavyo Tanzania unauza bidhaa zake nchini Uganda na kuingiza kiasi hicho cha fedha, kongamano litakalofanyika nchini litaongeza wigo zaidi wa kibiashara.
Hata hivyo kutokana na umuhimu wa kongamano hilo la kibiashara, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imejipanga vema kuhakikisha kongamano hilo linakuwa na tija na ushiriki wa Watanzania unakuwa mkubwa zaidi.
Nakumbuka wakati anazungumzia kongamano hilo Waziri wa Viwanda na Biashara Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema kongamano hilo litasaidia kuweka mazingira wezeshi ya kuongeza wigo wa kujenga viwanda zaidi nchini hasa vya usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani ya mazao hayo.
Naomba nitoe rai kwa wafanyabishara na wawekezaji na wote wanaojihusisha na sekta ya biashara waliopo nchini Tanzania kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kwa vitendo katika kongamano hilo. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imejikita katika msingi wa kufanya kazi kwa bidiii.
Hivyo kwa wafanyabiashara kupitia kongamano hilo wataendelea kunoa vichwa ili kujiimarisha zaidi kibiashara ana kiuwekezaji kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake kwa ujumla. Nihitimishe kwa kukumbusha tena kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda litafanyika Septemba 6 na Septemba 7 mwaka huu. Sote tushiriki bila kukosa.

PICHA VIONGOZI WA CCM WALIPOKAGUA MIRADI MKAKATI YA UKARABATI NA UJENZI WA MELI

 Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Eric Hamiss (kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi wa CCM wakiwemo watumishi wa kampuni hiyo kabla ya uongozi huo wa Chama kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa meli na ukabati wa meli za MV. Butiamana MV. Victoria kwenye bandari ya Mwanza Kusini.
 Meneja wa mradi wa ukabarati wa meli na ujenzi wa meli mpya,Meja, Mhandisi Abel Gwanafyo (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa uongozi wa CCM ulipokwenda kukagua miradi hiyo jana kwenye Bandari ya Mwanza Kusini.Kulia ni Mkujumbe wa NEC, Jamala Abdul Babu, wa pili ni Mwenyekiti wa Mkoa Dk. Anthony Diallo na wa tatu kutoka kushoto ni Katibu wa mkoa, Salum Kalli, aliyeinama ni Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamiss.
 Ujumbe wa CCM Mkoa wa Mwanza ukiongozwa na meneja wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa meli, Mhandisi Meja Abel Gwanafyo (wa kwanza kushoto) kukagua eneo linalojengwa chelezo ya meli mpya jana.Wa pili ni Mtendaji wa MSCL Eric Hamiss,wa tatu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Dk. Anthony Diallo.Kutoka kulia wa pili ni Katibu wa mkoa Salum Kalli na wa tatu ni Mjumbe wa NEC, Jamal Abdul Babu.
 Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza, wakipata maelezo mafupi ya mradi wa ukarabati wa meli za MV. Victoria na MV. Butiama kutoka kwa Mhandisi Abel Gwanfyo (wa tatu kutoka kulia) jana kabla ya kukagua ukarabati huo wa meli.Kulia ni Katibu wa Mkoa Salum Kalli, wa pili ni mwenyekiti wa mkoa, Dk. Anthony Diallo.
 Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Dk. anthony Diallo na Salum Kalli, wakiiingia ndani ya meli ya MV. Victoria inayokarabatiwa kwa gharfama ya sh bilioni 22 na kampuni ya Korea Kusini ya KMTI.
 Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza wakiangalia mafundi (hawapo pichani) wakikata vyuma vinavyotumika kwenye ukarabati wa meli ya MV. Victoria jana. Mbele ni Mwenyekiti wa CCM Dk. Anthony Diallo na kulia ni Katibu Salum Kalli.
 Mhandi wa MSCL Meja mstaafu Abel Gwanafyo, akiwapa maelezo ya mradi wa ukarabati wa meli ya MV. Victoria , viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo (kushoto) na Katibu wa mkoa Salum Kalli wakishuka kutoka kwenye meli y MV. Victoria baada ya kukagua na kujionea shughuli za ukarabati wa meli hiuo.Kushoto chini ni Mhandisi, Meja Abel Gwanfyo ambaye ni meneja wa mradi huo.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza. Salum Kalli akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuhimisha ziara ya ukaguzi wa mradi wa ukarabati wa meli na ujenzi wa meli mpya.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza. Salum Kalli akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuhimisha ziara ya ukaguzi wa mradi wa ukarabati wa meli na ujenzi wa meli mpya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anhtony Diallo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ukarabati na ujenzi wa meli katika Bandari ya Mwanza Kusini. 

PPRA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KUHUSU MFUMO WA TANePS

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqqaro, amefungua awamu ya nne ya mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Mtandao (TANePS) kwa wataalam wa manunuzi na Tehama kutoka taasisi nunuzi. 

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo wapatao 172 kutoka taasisi nunuzi 65, Mh. Daqqaro alipongeza jitihada za Serikali kwa kuanzisha mfumo huo mpya wa TANePS unaosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma - PPRA kwa kuwa utasaidia kupunguza malalamiko na kero zilizokuwa zinaelekezwa kwenye sekta ya manunuzi ya umma ikiwemo kukabiliana na vitendo vya rushwa,  kupunguza gharama na muda wa michakato ya manunuzi.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa Mfumo huo utaisaidia Serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zinaelekezwa kwenye sekta hiyo ya manunuzi, na kutoa wito kwa wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano wa dhati ili mfumo huo ufanye kazi.  
 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, kabla ya Ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo ya TANePS, jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo kuhusu Mfumo wa TANePS jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS

JISAJILI KUSHIRIKI MKUTANO WA KIBIASHA NA MAONESHO KATI YA TANZANIA NA UGANDA SEPT 6-7, 2019 JIJINI DAR ES SALAAM

• Sisi ni Zaidi ya Ujirani
• Sisi ni ndugu wa Damu
Tanzania na Uganda katika meza moja ili kukuza na kujenga Uchumi imara na madhubuti!
#TZUGBusinessForum19
#SisiNiTanzaniaMpyA+ ya Wazalendo, Waadilifu, Waaminifu, Wachapa Kazi!

Monday, September 2, 2019

ZAIDI YA WANANCHI 800 WA WILAYA YA KISARAWE WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA YA AFYA BURE

 Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani ambapo amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Wananchi wakiojitokeza kupatiwa huduma ya huduma ya afya bure iliyofanyika iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani  Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha (mwenye miwani) akigawia wananchi maji wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
 Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza (mwenye miwani) ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akisimamia utoaji wa huduma ya afya bure.
 Wananchi wakiwa katika dirisha la kupata dawa wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe Musa Gama (wa tatu toka  kulia msitari wa mbele) akiwa na  Timu ya Madaktari na wauguzi wa Wilaya ya Kisarawe na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Zaidi ya wananchi 800 wa wilaya ya Kisarawe, Pwani wamejitokeza katika zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyoandaliwa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).

Akizungumza wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha zoezi hili na limekuwa la mafanikio zaidi maana tulitarajia watu 400 ila tumepata watu mara mbili ya namba tuliyoiweka, yani tumepata watu zaidi ya 800 na wote tumeweza kuwahudumia japo sisi hatukuwa wengi," amesema.

Amesema kuwa ushirikiano na umoja walionao ndiyo nguzo pekee iliyoweza kufanikisha zoezi walilopanga kulifanya.

"Kiukweli timu yetu imekuwa na ushirikiano zaidi kuanzia Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakiwemo wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya, waandishi wa habari na wote tuliokuwa nao kipindi hicho," amesema Dkt Tungaraza.

Ameongeza kuwa magonjwa waliyokuwa wakichunguza ni yale ambayo si ya kuambukiza kama vile Shinikizo la damu, presha na idadi kubwa imeonyesha watu wengi wanaugua shinikizo la damu hasa akina mama.

"Tunashukuru waliojitokeza idadi kubwa ni akina mama kwa asilimia 60, akina baba asilimia 30 na watoto asilimia 10% na magonjwa yaliyoongoza baada ya uchunguzi ni Saratani ya Shingo ya Kizazi na Shinikizo la damu na kidogo Kisukari,' amesema.

Ametoa ushauri kwa jamii kuendelea kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuweza kujiimalisha kuliko kusubiri mpaka waugue ndiyo waweze kukimbilia kutibiwa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha amesema wameshukuru kwa ushirikiano walioweza kuupata kutoka katika serikali ya wilaya ya Kisarawe na pia ubalozi wa China nchini Tanzania ambao ndiyo waliowawezesha kufanikisha zoezi la utoaji huduma ya Afya Bure na pia amewaomba jamii na wadau wengine kuweza kuwaunga mkono ili kufanikisha waweze kufika maeneo mengi zaidi.

"Tumefurahi jinsi uongozi mzima ulivyoweza kutupa ushirikiano kuwezesha wakazi wa Kisarawe kupatiwa matibabu ya afya bure ila japo idadi iliyojitokeza imekuwa ni kubwa nje ya malengo yao waliyokuwa wamepanga," amesema.

Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Stanford John amewashukuru madaktari wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) kwa moyo wao wa kujitoa kuhudumia wananchi wa Kisarawe.