ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 6, 2014

SHINDANO LA UONJAJI BIA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA LAFANA: AIDAN MUHANDO WA MWANANCHI AIBUKA MSHINDI 2014.

Umakini katika kutambua rangi akiuhusisha huyu ni mshindi wa kwanza wa shindano la Beer Tasting Competition kwa wanahabari (Muonjaji Bora wa Bia) Aidan Mhando wa Mwananchi Communications akizibainisha bia katika ungwe ya pili ya na ya mwisho ya shindano hilo.
Awali kabla ya shindano la uonjaji bia,  Mpishi mkuu wa Kampuni ya Bia TBL tawi la Mwanza Oscar Kilasi alitoa somo kwa waandishi hao juu ya kuzibaini tofauti za bia kupitia ladha, rangi, harufu na viwango vya alcohol.
Kupitia Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa ndani ya ukumbi wa mikutano TBL Mwanza.
Kupitia Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa ambapo hapa bia aina ya Castle Light ilikuwa ikitolewa maelezo ya vihusishi vilivyohusika hadi ukamilifu wake na maelezo ya viwango vyake.
Kupitia Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa ambapo hapa bia ya Safari Lager ilikuwa ikitolewa maelezo ya vihusishi vilivyohusika hadi ukamilifu wake na maelezo ya viwango vyake.
Bia mbalimbali zinazo tengenezwa na TBL Tawi la Mwanza.
Philbert Kabago (mbele) akiongoza Waandishi wenzake wa habari kutembelea vitengo mbalimbali vya uzalishaji bia kupitia kiwanda cha kutengeneza bia TBL kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Waandishi wa habari wakipata maelezo ya namna ya upikaji bia kupitia kiongozi wa kitengo cha maabara kiwanda cha kutengeneza bia TBL kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
"Hii ndiyo maabara ya TBL Mwanza"
Mtaalamu wa Ubora wa Bia kiwanda cha TBL Mwanza, David Keregeseni akitoa maelezo kwa waandishi wa habari William Bundara wa RFA (katikati) na Wilson Elisha wa Star Tv (kulia) ndani ya maabara ya kiwanda hicho kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza. 
Shughuli za uzalishaji zikiendelea ndani ya kiwanda cha kisasa cha kuzalisha bia TBL Mwanza.
Blogger Gsengo ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
Blogger William Bundala aka Kijukuu cha Bibi ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
Uzalishaji ukiendelea ndani ya mjengo.
Chupa zikiwa kwenye mstari kuelekea njia ya usafishaji ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
Wakiwa shughulini hawa ni wataalamu kitengo cha uwekaji lebo za bia ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
Philbert Kabago wa Passion Fm kikazi zaidi katika shindano la Muonjaji Bora wa Bia kiwandani TBL Mwanza.
Mashaka Bartazar anayeandikia magazeti ya Majira na Jambo leo akifanya yake.
Harufu na uonjari ni sehemu ya kubaini aina ya bia.
Biskuti maalum ni nyenzo kwaajili ya kufuta ladha ya bia uloionja awali kabla ya kuionja bia nyigine.
We Katulanda, unaonjaaaa au unakunywa? Tehe...teee!!
 Beer Tasting Competition.
Meneja Mawasiliano na Habari wa TBL Edith Mushi (kulia) akikusanya karatasi za mtihani wa shindano la Uonjaji bia kwa waandishi wa habari.
Meneja msaidizi katika uzalishaji kampuni ya bia TBL Mwanza, Jemedari Waziri akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la Beer Tasting Competition kwa wanahabari (Muonjaji Bora wa Bia) ambapo Aidan Mhando wa Mwananchi Communications ndiye aliyeitwaa nafasi hiyo kwa mwaka huu 2014-2015.
Carolyne Mhonoli ambaye ni Meneja ubora wa bia wa TBL Mwanza, akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili wa shindano la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Fredrick Katulanda ambaye ni Mhariri wa magazeti ya New habari Kanda ya Ziwa, katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo Ilemela mkoani Mwanza.
Afisa Habari na Matukio TBL Mwanza, Mr. Erick  akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa shindano la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Philbert Kabago wa Passion Fm Mwanza, katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo Ilemela mkoani Mwanza.
Kila mmoja alitoka na zawadi yake.
Mzigo umeuonaaaa!!? 
Bia tayari kwa kuingia sokoni. 
Tukipata U-PichaZ. 
Wanyama.
Picha ya pamoja ya waandishi wa habari na wadau wa TBL mara baada ya kumaliza matembezi katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited Mwanza.
MPANGO MZIMA KWA UFUPI.
MWEZI wa Sita wa kila mwaka kampuni ta Tanzania Breweries Limited (TBL) inaandaa mashindano kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kubaini vinywaji vya kampuni hiyo kwa kuonja ladha tofauti kisha kutambua ni bia gani. 

Jijini Mwanza mashindano hayo yamefanyika jana katika kiwanda cha TBL na kushirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari  zaidi ya Ishirini kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini mwanza. 


Katika mashindano hayo yaliyodumu takribani dakika thelathini yalimalizika kwa waandishi watatu kulingana point hali iliyopelekea mchuoano kurudiwa kwa watu watatu ili kumpata mshindi. 


Katika marudio hayo mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha Passion Fm Filbert Kabago aliibuka mshindi wa tatu hali iliyopelekea kutafuta mshindi wa kwanza na pili kati ya mwandishi wa gazeti la mwananchi Aidan Muhando na Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Fedrick Katulanda. 


Baada ya kupambana Aidan Mhando aliibuka mshindi wa kwanza na Fedrick Katulanda akakamata nafasi ya pili. Baada ya mashindano hayo waandishi walipata nafasi ya kutembelea eneo la maabara na eneo la uzalishaji ili kujionea namna bia za kampuni ya TBL zinavyozalishwa na kupata nafasi ya kuuliza Maswali ili kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii. 


Licha ya kubainisha kuwa ziara hiyo imesaidia kutambua masuala ya biashara takayo saidia kufikisha ujumbe kuhusu bidhaa zinazo zalishwa na kampuni hiyo, mmoja wa waandishi wa Clouds Fm jijini Mwanza ambaye pia ni mmiliki wa G.Sengo Blog, Albert Sengo amesema ziara hiyo ya wazi kwa waandishi wa habari ambao ni wadau wa kuibua taarifa na changamoto zilizopo ndani ya jamii, ni ushahidi tosha kwamba kiwanda hicho cha kutengeneza bia kinajiamini katika masuala yote ya teknolojia, afya, usafi na uzalishaji makini, kwani kungekuwa na magumashi (ubabaishaji) basi TBL wasinge thubutu kuwapa uhuru wadau hao kujiachia katika kuuliza maswali na kunasa matukio mbalimbali kiwandani humo.....

JULIAUS KISALAWE AMPIGA BONANS SAMWELI KWA POINTI KATIKA UKUMBI WA NDAME GYM.

Bondia bonans Samweli kushoto akimrushia konde Julius Kisalawe wakati wa mpambano wao uliofanyika katika GYM ya Ndame Dar es salaam jana Kisalawe alishinda kwa point mchezo huo.
Bondia Julius Kisalawe kushoto akimtupia konde Bonans Samweli wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Ndame GYM Manzese Dar es salaam jana Kisalawe alishinda kwa point mpambano huo. 
Bondia Julius Kisalawe akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake.
Mabondia Ally Yusuph kushoto akimtupia konde Sadam Manjepa bila mafanikio wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika GYM ya Ndame manzese Dar es salaam Yusuph alishinda kwa point. 
Mabondia Tasha Mjuaji kushoto akipambana na Hamisi Kicheba wakati wa mpambano wao uliofanyika katika GYM ya Ndame Manzese Midizini Dar es salaam jana Mjuaji alishinda kwa K,o ya raundi ya pili. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

KUNDI LA AL SHABAAB WAPATA PIGO.

Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya Marekani Pentagon zinasema kuwa mmoja wa wanzilishi wa kundi la Al Shabaab Ahmed Godane ameuawa.
Marekani imesema kuwa kuuawa kwa Godane ni hatua kubwa sana katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wamekuwa msumari mkali kwa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na hata kwa serikali ya Somalia yenyewe.
Katibu wa Pentagon Nchini Rear Admiral John Kirby ametangaza kuwa Ahmed Godane ameuawa katika oparesheni iliyofanywa nchini Somalia Jumatatu wiki hii.
Kwa Mujibu wa Admiral Kirby, kuuawa kwa Godane ni pigo kubwa zaidi kwa kundi hilo la Al shabaab na itasaidia kukabiliana na ugaidi unaofanywa na kundi hilo eneo la Afrika Mashariki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na washirika wake wakuu kukabili wapiganaji hao wa AL shabaab ambapo katika miaka ya hivi karibuni wamezidisha mashambulio sio tu nchini Somalia bali hadi nchi jirani.
Wiki iliyopita Kikosi cha kulinda amani chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika AMISOM kikishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia kilianzisha oparesheni kali kuwasaka wapiganaji hao wa AL shabaab. Na kufikia mwanzoni mwa wiki hii Marekani ikajiunga katika oparesheni hiyo ambapo walishambulia msafara ambao Ahmed Godane alishukiwa kuwa ndani.
Walioshuhudia waliambia BBC kuwa muda mfupi baada ya msafara huo kushambuliwa, ndege za kivita za helikopta zinazoaminiwa kuwa za Marekani zilishuka na kubeba maiti zote zilizo kuwepo. Kwa hiyo kwa muda hakukuwa na thibitisho lolote iwapo Godane mwenyewe aliuawa au la.
Upande wa AL shabaab nao walianza kukusanya watu katika kijiji karibu na eneo hilo la Shebeele ambako shambulio lilifanywa na kuwaua au kuwateka wengijne ambao hadi sasa hawajulikani waliko.
AL shabaab hawakuzungumzia iwapo Godane alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Leo asubuhi kulikuwa na picha zilizo sambazwa katika mtandao ambazo hazikuthibitishwa zilizodai kuwa ni Ahmed Godane bado alikuwa hai.
Al shabaab hawajasema lolote baada ya tangazo la Pentagon kuthibitisha kifo cha Godane
CHANZO:BBC SWAHILI

WALA WALA CUP YABAINI KWA VITENDO KUWA MICHEZO NI AJIRA.

Mratibu wa mashindano ya OG Walawala Cup,Omari George (kulia) akipokea jezi zitakazotumika katika mashindano hayo kutoka Meneja Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abas Ali Isere katika hafla fupi iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kuwania Kombe la Walawala wilayani Muheza linatarajia kuanza mapema mwezi huu katika uwanja wa Jitegemee.

Mratibu wa Mashindano hayo, Omari George (OG)akizungumza mjini Dar es Salaam jana alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika ambayo ni pamoja na kuandaa vifaa vya michezo.

Alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yamelenga kuibua vipaji vya wachezaji watakaochukua nafasi ya wachezaji waliowahi kuwika zamani na kujenga heshima ya wilaya Muheza kama vile Kasongo Athumani, ISsa Athumani Mgaya na James Kisaka.

OG alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kutoka mwaka 2010 kila timu shiriki hupatiwa jezi na washindi hupata zawadi mbalimbali kama vile vikombe, mipira na sare za michezo.

Alisema katika mashindano ya mwaka huu kila timu imepewa jezi seti moja, sare  kwa ajili ya makocha wa timu 18 zinazoshiriki mashindano hayo, sare kwa viongozi wa Chama cha Soka Wilayani (TFF) na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo.

Mratibu huyo alisema amekuwa akishirikiana na Kampuni ya Isere kuandaa vifaa vinabyotumika katika mashindano hayo Kutoka mashindano ya Walawala Cup yaanzishwe timu zilizowahi kutwaa ubingwa ni Polisi (2011), City Boys (2012) na Bambino (2013).

Friday, September 5, 2014

WATU ZAIDI YA 35 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI ILIYOTOKEA LEO MKOANI MARA


Picha na habari kwa hisani ya Ahmad Michuzi, Musoma.
Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa. 
 Ajali hiyo mbaya ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya matukio ya ajali ya barabarani yakihusisha mabasi kuwahi kutokea kwa mwaka huu, imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma wakati moja ya mabasi hayo yakiovateki gari lingine. 
Baadhi ya mashuuhuda wakitizama basi la J4 Express  lililogongana na basi la mwanza coach halipo pichani na wengine wakitoa  msaaada wa kuokoa majeruhi toka katika basi hilo
Gsengo blog inawapa pole wafiwa, tupo pamoja kwenye kipindi cha majaribu makubwa, tunamwomba Mwenyezi Mungu atupe nguvu na uvumilivu.