ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 6, 2023

KITANDULA AKUMBUSHIA FIDIA ZA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI WA KIWANDA CHA SARUJI MKINGA

 

 


Na Mwandishi Wetu ,Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ameikumbusha Serikali fidia za wananchi Vijiji vya Kwale na Mtimbwani cha kiasi cha zaidi ya Milioni 570 kwa ajili ya kutoa ardhi kwa ajili ya uwkezaji wa kiwanda cha Saruji cha Hengya kilichokuwa kijengwe wilaya ya Mkinga mwaka 2017.

Kitandula aliyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge kinachoendelea  ambapo alisema mwaka 2017 alijitokeza Mwekezaji Hengya alionyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya Sariuji nchini na kiwanda kilikuwa kije kujengwe mkinga na mwaka 2019 Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ilimpa leseni aje awekekeze.

Alisema kwamba baada ya kupatiwa leseni mwaka 2020 akaanza kutoa fidia kwa ardhi aliyoitwaa kule mkinga wananchi wakaachia maeneo yao tokea wakati huo mpaka leo hakuna fidia stahiki iliyotolewa hivi na kwa sasa wako wananchi 143 wa Mkinga kutoka Kwale na Mtimbwani wanadaiwa Zaidi ya Milioni 570 hazijalipwa.

Alisema kwamba na serikali ilituma timu ikaja kukaa na uongozi wa mkoa na wilaya na mwekezaji wakakubaliana aifanyike kazi ya tathimini isiyo na shaka ili watu hao walipwe na kazi imekamilika na mwekezaji amepelekewa amegoma kulipa viwango stahiki vya kisheria.

Alisema kwamba na hao ni wananchi wamepoteza ardhi zao hawana ruhusa ya kuingia kwenye maeneo hayo mpaka leo hawalipwi kwa nini mwekezaji alipi kwa sababu ana machungu na aliwahi kusema jamani uwekezaji wa hengya ambao wakati ule kama ungefanyika mwekezaji angekuja kiwanda chenye thamani ya Trilioni 2.3 uzalishaji wa saruji alikuwa azalishe tani Milioni 7 kwa mwaka.

Aidha alisema amesikia taarifa ya wizara hapa kwamba leo viwanda 14 vinazalisha tani milioni 10 walikuwa na mwekezaji alikuwa tayari uwekezaji wa tani Trilioni 2.3 azalishe tani milioni 7 kwa mwaka wamemvuruga na alikuja kusema maneno hayo hapo kwamba kuna watendaji hawana nia njema wana wanamvuruga mwekezaji wapo ndani ya viwanda vya saruji.

Alisema wawekezaji hao hawamtaki mwekezaji huyo kutokana na kwamba ataleta ushindani leo wamepoteza uwekezaji huo watu wa Tanga wana machungu wanaiomba Serikali na Waziri Simamia watu wa Mkinga 143 walipwe stahiki zao.

Akizungumzia suala la uuzwaji wa hisa Tanga Cement alisema wao hawapingi lakini wanachokitaka ni kwamba taratibu zifuatwe watu wa Tanga leo hii kuna viwanda 8 baada ya kubinafsishwa vimegueka kuwa magodauni havifanyi kazi, magofu hivyo hawatakuwa tayari kuona Tanga Cementi inabinafishishwa inageuka kuwa godauni au magofui na mtu anakwenda kuchukua malighafi Tanga anakwenda kuzalisha Dar hilo hatutaki .

Mbunge huyo alisema kwamba viwanda 8 wamehangaika ndani ya serikali ili wawekezaji waheshimu mikataba yao wanapokuwa wakiuziwa hiyo ndio hofu yao watu wa Tanga wanaiomba Serikali taratibu za uwekezaji ufanyike wajenga confedence ya wawekezaji kwani hata wanapata shida kwenye sekta madini kila mwekezaji akija anagaganiza kukiwa na dispute waenda kuamuliwa maamuzi hayo nje ya Tanzania .

Alisema kwa sababu wanasema mahakama zetu haziaminika kama kuna jambo limeamulkiwa kisheria tusikiuke maamuzi hayo yaliyoamulkiwa kila mwekezaji anayekuja anakwenda kujisajili kampuni kwenye mikataba ya kimataifa hivyo wakiendelea kukiuka maamuzi.

Friday, May 5, 2023

MAMA KOKA AMWAGA MITAJI ML 22.8 KWA WANAWAKE WA UWT JIMBO LA KIBAHA MJI.

 Na Victor Masangu,Kibaha 


Mlezi wa jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Selina Koka katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kiuchumi ameamua kutoa kiasi cha shilingi milinioni 22.8 ili kuwawezesha katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwapatia mitaji na vitendea kazi.

Selina ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji amebainisha kwamba ameamua kuwasaidia wanawake wa UWT Kibaha mji hasa wale wajasiriamali  ili waweze kuanzisha biashara zao ndogo ndogo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi.

Mlezi huyo alisema anatambua katika jinbo la Kibaha mjini kuna idadi kubwa ya wanawake ambao ni wajasiriamali ndio maana akaamua kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa kata zote 14 ikiwa pamoja na kuwapatia fedhaa baadhi ya kata ili waweze kufungua akaunti zao zitakazowasaida kutunza fedha zao.

"Tulikuwa katika ziara ya UWT na  nimepata bahati ya kuzunguka katika kata zote 14 za jimbo la Kibaha nikiambatana na Mwenyekiti lakini nimeweza kutoa mitaji ya aina mbali mbali ikiwemo fedha pamoja vitendea kazi vingine ambavyo vitawasaidia katika kazi zao,"alisema Selina.

Kadhalika alioneza kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wanawake wa uwt pamoja na wengine katika kuweka mipango madhubuti ya kuwapatia mitaji mbali mbali ikiwemo sambamba na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali lengo ikiwa ni kujikomboa kiuchumi.
Pia sambamba na hilo aliwakumbuka wanawake wajane wa kwa kuwapatia mitaji ya mradi wa sabuni na kuwahimiza wafanye biashara hiyo kwa ajili ya kuleta matokeo chanya katika kujipatia kipato ambacho kitawasaidia kuendesha familia zao.

"Natamani kuona katika siku za usoni hii mitaji mbali mbali ambayo ninaitoa kwa wanawake inakuwa na tija na endelevu zaidi na kwamba fedha hizi mzitumie vizuri katika kuanzisha miradi ya tofauti na ndio maana hata wajane wa kata ya visiga nimewaanzishia mradi wa kuuza sabuni za kufulia.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha mji amempongeza Mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mji kwa juhudi zake  za  kuwapatia mitaji  ambayo itakuwa ni mkombozi katika maendeleo.

Nao baadhi ya wanawake wa UWT ambao wamepata fursa ya kunufainika na mitaji hiyo akiwemo Fatma Omary ametoa pongezi zake kwa mlezi wao Selina Koka pamoja na Mbunge wa jimbo la Kibaha mji kwa kuonyesha njia ya kuwakomboa wanawake katika kujikwamua kiuchumi.

HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA BOMBO KUNUNUA BASI LA WATUMISHI.

 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani katika akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani katika Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto Katibu wa Hospitali hiyo Abdiely Makange na kulia ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Peter Chambo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo
Katibu wa Tana Tawi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Mwanaisha Nyangasa akisoma risala 
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani wa pili kutoka kushoto akiwa na Katibu wa Hospitali hiyo Abdiely Makange wakitembelea mabanda mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani akizungumza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani katikati akipata maelezo  wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kulia ni Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abdiely Makange
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Juma Ramadhani kulia akiwa na watumishi wa Hospitali hiyo wakati wakiwasha mishumaa walipoingia wodini kwa ajili ya kugawa zawadi na kuwafariji wagonjwa
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani kulia akigawa zawadi kwa mgonjwa aliyelazwa kwenye Hospitali hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wauguzu Duniani 
Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe akigawa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani akiwa na Katibu wa Hospitali hiyo kulia Abdiely Makange wakielekea kwenye maadhimisho ya siku wa wauguzi baada ya kupokea maandamano

Maandamano ya wauguzi kutoka Kituo cha Toyota kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wauguzi duniani

Wauguzi wakiwa kwenye maandamano hayo

Wauguzi wakianza maandamano ikiwa  ni siku ya maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo William Masika akicheza wakati wa maandamano hayo ya siku ya wauguzi duniani yalipopokelewa
Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo William Masika akicheza wakati wa maandamano hayo ya siku ya wauguzi duniani yalipopokelewa
Sehemu ya wauguzi na wanafunzi wa chuo cha uunguzi wakifuatilia maadhimisho hayo
Sehemu ya wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo katika aliyesimama akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo



Na Oscar Assenga,TANGA 

KAIMU Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani leo amewaongoza wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwenye maaadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani ambapo kilele chake kitafanyika Mei 12 Jijini Mwanzasiku ya wauguzi Duniani. 

Maadhimisho hayo yalianza na maandamano kutoka eneo la Toyota mpaka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kulipofanyika kilele cha maadhimisho hayo

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo,Dkt Juma alisema kutokana na uwepo wa changamoto ya usafiri kwenye mkoa huo ambayo ilielezwa wakati wa risala ya wauguzi hao alieleza mipango ya uongozi wa hospitali hiyo kwenye bajeti zijazo na jitihada walizoweka kama taasisi wana mpango wa kununua basi ili kupunguza adha ya usafiri kwa watumishi. 

Dkt Juma alisema basi hilo kwa ajili ya Hospitali hiyo ambalo linaweza kupunguza changamoto ya uchelewaji kazini kutokana na hali hiyo na kwamba tayari wameshaliona na wameliweka kwenye mpango wao kuweza kulitatua 

“Hili la changamoto ya kuchelewa kazini kutokana na changamoto ya usafiri kwenye mkoa wetu hilo tumeliona kama uongozi wa Hospitali kwenye bajeti zijazo na jitihada tulizowekeza taasisi wana mpango wa kununua basi kwa ajili ya hospitali ambalo linaweza kupunguza changamoto ya uchelewaji kazini “Alisema Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Juma. 

Awali akisoma risala hiyo Katibu wa Tana Tawi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Mwanaisha Nyangasa alisema maadhimisho hayo ni kutafakari na kufauta nyayo za mwanzilishi wa huduma za uuguzi na ukunga Bi Florence Night Ngare. 

Alisema wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wamemuenzi kwa kutoa huduma mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo ikiwemo za uchunguzi wa saratani ya kizazi na matiti kwa wakina mama ,uchunguzi wa kisukari na macho,shinikizo la damu,kuhamasisha uchangia damu ,upimaji wa VVU kwa hiari na sambamba na utoaji elimu ya afya na lishe kwa wateja mbalimbali 

Aidha alisema pia katika maadhimisho hayo wametoa chanjo za Covid 19 ambapo wananchi waliohudumiwa tokea walipoanza maadhimisho hayo ni 154 ambao walihudumiwa kwa siku moja. 

Hata hivyo alisema kwamba Ukunga ni kada muhimu sana katika kufanikisha utoaji wa huduma nzuri za afya kwenye jamii na unapozungumzia afya bora muuguzi ni sehemu sahihi ya kufanikisha kila mtanzania anakuwa na afya bora. 

Alisema kwamba pamoja hayo kuna mafanikio makubwa ikiwemo mazingira ya kufanyia kazi yameboresha na miundombinu ya hospital na kuwezesha wanafanyakazi kufanya kazi kwenye mazingira mazuri. 

Aidha alisema kwamba pia ni wauguzi kupata nafasi ya kujiendeleza kimasomo,wauguzi kupata motisha mbalimbali,kuongezeka kwa hamasa kwa wauguzi . 

Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nayo alisema kwamba changamoto kubwa ni upungufu wa watumishi idara ya ukunga na uuguzi kulingana na mahitaji ya jamii kutokana na kuongezeka kwa vitengo na idara ambazo wauguzi wanahitajika. 

Alisema pia changamoto nyengine ni kuchelewa kufika kazini kwa watumishi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya usafiri kwenye mkoa wa Tanga hivyo upo umuhimu wa uwepo wa usafiri. 

BENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MTAJI WA BIASHARA

 


Siku mbili baada ya Benki ya CRDB kupata leseni ya kutoa huduma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amewahikikishia wanawake wajasiriamali nchini kupata mtaji wa kuanzisha au kukuza miradi yao.
 
Mwambapa ametoa uhakika huo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na wanawake wanachama wa Buta Vicoba kwenye mafunzo waliyokuwa wanapewa katika ukumbi wa Ngome uliopo Mwenge.

“Tukiwa Benki kiongozi na ya kizalendo, tumekuwa mstari wa mbele kuyawezesha kiuchumi makundi mbalimbali katika jamii yetu mkiwamo wanawake kupitia huduma, bidhaa na program bunifu. Benki inatoa mikopo maalum ya wanawake na mafunzo na hadi mwishoni mwa mwaka 2022 Benki ilikuwa imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 112 na kuwapa mafunzo wanawake wajasiriamali zaidi ya 14,774,” amesema Bi Mwambapa.
Pamoja na uwezeshaji wa huduma za fedha kwa wanawake, Mwambapa amesema Benki iliona bado kuna kundi kubwa la wanawake ambalo huduma zilizopo haziwezi kuwawezesha kujikwamua kiuchumi hasa wale ambao wana biashara au mawazo ya biashara lakini hawawezi kuingia katika mfumo rasmi wa huduma za fedha kutokana na kutokidhi baadhi ya vigezo hivyo wakaona wawahudumie kupitia sera yao ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI Policy) katika maeneo ya kipaumbele katika uwekezaji kwa jamii inaayotekelezwa na CRDB Bank Foundation kupitia program ya Imbeju.

Programu ya Imbeju inalenga kuwawezesha wanawake kukuza biashara zao ili kujikwamua kiuchumi wao na familia zao ili watoe mchango kwa Taifa kupitia kodi za biashara na kuwaajiri Watanzania wengine watakaojikwamua kupitia ajira hizo.

“Ili kuhakikisha programu hizi zinakuwa endelevu na zenye matokeo makubwa, CRDB Bank Foundation inajenga jukwaa shirikishi linalowaleta pamoja wadau wa maendeleo ndani na nje ya nchi. Ukiwa hapa una uhakika wa kupata elimu ya fedha Pamoja na mtaji wa kufanyia biashara yako,” amesema Bi Mwambapa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Buta Vicoba, Semeni Gama ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwapa mafuno zaidi ya wanachama wake 300 kutoka vikundi vinavyounda umoja wao waliojitokeza huku akiwasihi waache kubweteka badala yake wajielekeze katika kujijenga kiuchumi.

Mwanzoni mwa wiki hii Benki ya CRDB imepewa leseni ya kufanya biashara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kukamilisha hatua zote zinazohitajika hivyo kuwa benki ya kwanza ya kizalendo kuwahudumia Wacongo.

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Benki ya CRDB iliyoanzishwa mwaka 1996 inatoa huduma zake nchini Burundi pia.
 



Thursday, May 4, 2023

SINGINDA WAPOTEZA,YANGA UBINGWA WANUKIA

 

IKIWA Uwanja wa Liti, Singida Big Stars imeshuhudia pointi tatu zikisepa mazima kuelekea kwa wapinzani wao Yanga.

Ubao umesoma Singida Big Stars 0-2 Yanga huku kazi ikimalizwa kipindi cha kwanza.

Mabao ya Aziz KI na Clement Mzize yameipa Yanga pointi tatu na wanafikisha pointi 71 kibindoni wakielekea kutetea ubingwa wa ligi.

Mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji utatoa picha kamili kw mabingwa hao watetezi kusepa na taji hilo kwa mara nyingine tena.

Ni dakika ya 15 Aziz KI alipachika bao akiwa nje ya 18 na Mzize alipachika bao hilo dakika 20 akitumia pasi ya Jesus Moloko.

PASTOR T APENDEKEZA DCI IWASHIRIKISHE WACHUNGAJI WA KIROHO KUMHOJI MACKENZIE

 

Mchungaji Paul Mackenzie akiwa chini ya ulinzi.

Mhubiri maarufu Pastor T ameiomba serikali kuhusisha mtumishi wa kiroho katika kumhoji mchungaji wa dhehebu potovu Paul Mackenzie kwani huenda wanakabiliana na roho ya kishetani.

Katika video inayozunguka kwenye TikTok , mchungaji huyo amesema DCI haipaswi kuchukulia kirahisi semi za Mackenzie 'mnachopigana nacho hamkijui, kitawaramba'.

 Amesema kuwa kutokana na miili hiyo mingi kufukuliwa katika msitu wa Shakahola huenda ikawa imetolewa dhabihu na mchungaji huyo tata kumaanisha kuwa madhabahu ambayo DCI inajaribu kuzima inaweza isifanye kazi kwani inahusisha mambo ya kiroho.

"Hii haikuwa inahusu imani potovu. Ilikuwa ni ushirikina. Walikuwa wanatoa sadaka za binadamu. Kiongozi wao hakuaga. Na wanasema alikuwa amepangia kufunga mwisho.

Huyu mtu haifai kuhojiwa na DCI pekee, bali anapaswa kuhojiwa na watumishi wa kiroho kwa sababu anachofanya ni cha kiroho sana.

Ni kweli amevunja sheria za nchi, unaweza kumkamata mtu huyu lakini huwezi kumkamata roho yake.

Kwa sababu roho iliyofanya kazi ndani yake haitaweza kufungwa gerezani, bado itaendelea," alisema.

PIKIPIKI YALIPUKA NA KUTEKETEA JIJINI MWANZA.


 Pikipiki ambayo jina la mmiliki wala namba zake hajafahamika mara moja imelipuka na kuteketea kwa moto katika tukio lililotokea eneo la kituo cha mabasi madogo ya Posta jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya pikipiki hiyo ambayo hata dereva wake hakufahamika, Faustine Magiri, mmoja wa mashuhuda amesema kabla ya kulipuka moto, pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea njia ya Nyegezi kupitia barabara kuu ya Kenyatta ilikuwa ikivuja mafuta ambayo yaliacha michirizi barabarani.

“Pikipiki ile iliwaka moto na kuanza kuteketea likiwa bado linatembea ndipo dereva akalisimamisha na kuruka kuepuka kuungua,” amesema Faustini Magiri, anayemiliki duka la vifaa vya ujenzi karibu na eneo la tukio

Amesema pikipiki hiyo ilishika moto wakati dereva wake alipokuwa akielekea kwenye duka lake ndipo alipompigia kelele kumgutusha ashuke asiungue.

"Tulivyofuatilia, tuligundua pikipiki ile ilikuwa ikimwaga mafuta na kwa bahati mbaya dereva hakushtuka hadi ilipolipuka na kuteketea,” amesema Magiri

Amesema kukosa elimu na uelewa mpana wa namna ya kukabiliana na majanga ya moto ndio kumesababisha pikipiki hiyo kuteketea kwa sababu licha ya watu kujitokeza mapema, hakuna aliyeweza kusaidia kuzima moto huo.

“Mmoja wa wananchi alikuja nan doo ya maji na kumwagia pikipiki iliyokuwa ikiteketea; badala ya kuzimika, moto ukaongezeka mara dufu. Wananchi wangekuwa na elimu ya kutosha ya kukabiliana na majanga ya moto wangetumia mchanga au blanketi kufunika pikipiki ile kupunguza hewa ya Oksijeni ili moto uzimike,’’ amesema Hellene Zablon, mjasiriamali anayeuza mihogo ya kukaanga eneo la Posta

Juma Masanja, mmoja wa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga amewashauri wamiliki na madereva wa vyombo vya moto kujenga utamaduni wa kukagua vyombo vya kujiridhisha na ubora na usalama kabla na baada ya safari.

TIES KAMPUNI YA KWANZA YA KIZALENDO INAYOTENGENEZA VIFAA VYA KUCHENJUA DHAHABU NCHINI TANZANIA

 NA ALBERT G.SENGO

TIES ni kampuni ya inayojihusisha na kutoa huduma za kihandisi katika Nyanja mbalimbali za uhandisi ikiwemo uchimbaji wa madini. Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Jijini Dar-es-salaam ilianzishwa April 18 mwaka 2019. Kampuni hiyo imebuni na kutengeneza mtambo wa kuchenjulia madini ya dhahabu wa CIP katika mgodi wa mwamanga uliopo katika kijiji cha BURIGE halmashauri ya msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO TANGA WATOA HUDUMA ZA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI KWA WANANCHI



Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe akiwa kwenye eneo ambaalo huduma za upimaji kwa wananchi zinaendelea kwenye Hospitali hiyo ikiwa ni kuelekea siku ya maadhimisho ya Wauguzi Duniani

Wananchi wa Jiji la Tanga wakipatiwa huduma ya upimaji katikati Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe

Wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali

VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA KWA WELEDI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KILIMO NA UVUVI

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza, katika ufunguzi wa warsha ya Siku mbili  ya  utambulisho na uelewa  wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri. Dodoma Leo


Picha ikionesha baadhi ya watendaji wa Mikoa na Halmashauri, wakifuatilia wasilisho waliposhiriki katika, warsha ya Siku mbili ya utambulisho na uelewa wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri. Dodoma Leo
Sehemu ya washiriki wa warsha ya Siku mbili  ya  utambulisho na uelewa  wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri. Dodoma Leo



Na; Mwandishi Wetu – Dodoma 

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka watendaji wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia vizuri utekelezaji wa Programu ya Kilimo na Uvuvi katika maeneo yao kwani ni sekta muhimu katika uchangiaji wa uchumi na usalama wa chakula nchini. 

Ameyasema hayo mapema leo Jijini Dodoma, katika warsha ya utambulisho na uelewa wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri. 

Dkt. Yonazi amesema kuwa Serikali imeona kuna ulazima wa kuwepo kwa usalama wa mbegu katika kilimo hivyo kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini ASA imeweza kuwekeza mbegu kwa wingi ili kuyafikia maono ya serikali. 

“Serikali imeendelea kusimamia uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora ambapo hadi kufikia Aprili 2023, jumla ya tani 49,962.35 za mbegu bora zimepatikana sawa na asilimia 26.68 ya mahitaji ya tani 187,197 kwa mwaka,”Alisema Dkt. Yonazi. 



Aliongezea kuwa, serikali imejitahidi kuweka nguvu katika upatikanaji wa mbegu hizo ili kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula nchini, na kwa upande wa sekta ya uvuvi imehakikisha kunakuwa na manufaa ya rasilimali zilizopo katika sekta hiyo kwani bado hazijatumika vizuri. 

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ina mpango wa kununua meli zitakazotumika katika uvuvi wa kina kirefu cha bahari na hivyo kuweza kuongeza lishe na hatimaye nchi kunufaiika na rasilimali za uvuvi. 

Aliendelea kufafanua kuwa, Programu hii pia, itahusisha ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu mingine ikiwa ni pamoja na upanuzi wa vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki cha Kingolwira Morogoro. 

“Lazima tushirikishe wadau ili tupeleke elimu ya kuweza kuzalisha vifaranga na kujenga mabwawa, natoa msisitizo kwa viongozi wa mkoa kuwa kuna jukumu la usimamizi, tuhakikishe tunasimamia vizuri mradi huu, kushauri na kuutekeleza kwa wakati.” Alisisitiza Dkt. Yonazi 

Awali, akiongea wakati wa Ufunguzi wa Warsha hiyo Bw. Paul Sangawe Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, alisema lengo la programu hii kwa upande wa sekta ya uvuvi, ni kuendeleza ufugaji wa viumbe maji pamoja na kuanza uvuvi wa bahari kuu. 

“Tunatazamia katika program hii meli zitanunuliwa kwa matumizi ya pande zote mbili za Muungano na kuwezesha nchi yetu kwa mara ya kwanza kufanya uvuvi katika bahari kuu ili kuweza kutumia rasilimali tulizonazo kwa ufanisi, lakini vile vile uzalishaji wa mbegu pamoja na usambazaji, na kuhakikisha fedha ambazo za mkopo ambazo tumepewa kutoka shirika la IFAD takribani dola 58.8 milioni,zinatumika kwa ufanisi na kuleta tija katika utelezaji wa program hii.” Alisisitiza 

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchumi na Uzalishaji toka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Afisa Kilimo Mkuu Dkt. Rehema Mdendemi amesema programu hii ya maendeleo ya kilimo na uvuvi itaenda kuboresha maisha ya wakulima na wavuvi , na kujitosheleza kwa usalama wa chakula na kuleta ajira hivyo program hii ni ya muhimu kwa serikali na wanachi kwa ujumla.