Mchungaji Paul Mackenzie akiwa chini ya ulinzi. |
Mhubiri maarufu Pastor T ameiomba serikali kuhusisha mtumishi wa kiroho katika kumhoji mchungaji wa dhehebu potovu Paul Mackenzie kwani huenda wanakabiliana na roho ya kishetani.
Katika video inayozunguka kwenye TikTok ,
mchungaji huyo amesema DCI haipaswi kuchukulia kirahisi semi za Mackenzie
'mnachopigana nacho hamkijui, kitawaramba'.
Amesema
kuwa kutokana na miili hiyo mingi kufukuliwa katika msitu wa Shakahola huenda
ikawa imetolewa dhabihu na mchungaji huyo tata kumaanisha kuwa madhabahu ambayo
DCI inajaribu kuzima inaweza isifanye kazi kwani inahusisha mambo ya kiroho.
"Hii haikuwa inahusu imani potovu. Ilikuwa
ni ushirikina. Walikuwa wanatoa sadaka za binadamu. Kiongozi wao hakuaga. Na
wanasema alikuwa amepangia kufunga mwisho.
Huyu mtu haifai kuhojiwa na DCI pekee, bali
anapaswa kuhojiwa na watumishi wa kiroho kwa sababu anachofanya ni cha kiroho
sana.
Ni kweli amevunja sheria za nchi, unaweza
kumkamata mtu huyu lakini huwezi kumkamata roho yake.
Kwa sababu roho iliyofanya kazi ndani yake
haitaweza kufungwa gerezani, bado itaendelea," alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.