Pikipiki ambayo jina la mmiliki wala namba zake hajafahamika mara moja imelipuka na kuteketea kwa moto katika tukio lililotokea eneo la kituo cha mabasi madogo ya Posta jijini Mwanza.
Akizungumza na Mwananchi muda
mfupi baada ya pikipiki hiyo ambayo hata dereva wake hakufahamika, Faustine
Magiri, mmoja wa mashuhuda amesema kabla ya kulipuka moto, pikipiki hiyo
iliyokuwa ikitokea njia ya Nyegezi kupitia barabara kuu ya Kenyatta ilikuwa
ikivuja mafuta ambayo yaliacha michirizi barabarani.
“Pikipiki ile iliwaka moto na kuanza
kuteketea likiwa bado linatembea ndipo dereva akalisimamisha na kuruka kuepuka
kuungua,” amesema Faustini Magiri, anayemiliki duka la vifaa vya ujenzi karibu
na eneo la tukio
Amesema pikipiki hiyo ilishika moto
wakati dereva wake alipokuwa akielekea kwenye duka lake ndipo alipompigia
kelele kumgutusha ashuke asiungue.
"Tulivyofuatilia, tuligundua
pikipiki ile ilikuwa ikimwaga mafuta na kwa bahati mbaya dereva hakushtuka hadi
ilipolipuka na kuteketea,” amesema Magiri
Amesema kukosa elimu na uelewa mpana
wa namna ya kukabiliana na majanga ya moto ndio kumesababisha pikipiki hiyo
kuteketea kwa sababu licha ya watu kujitokeza mapema, hakuna aliyeweza kusaidia
kuzima moto huo.
“Mmoja wa wananchi alikuja nan doo
ya maji na kumwagia pikipiki iliyokuwa ikiteketea; badala ya kuzimika, moto
ukaongezeka mara dufu. Wananchi wangekuwa na elimu ya kutosha ya kukabiliana na
majanga ya moto wangetumia mchanga au blanketi kufunika pikipiki ile kupunguza
hewa ya Oksijeni ili moto uzimike,’’ amesema Hellene Zablon, mjasiriamali
anayeuza mihogo ya kukaanga eneo la Posta
Juma Masanja, mmoja wa
wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga amewashauri wamiliki na
madereva wa vyombo vya moto kujenga utamaduni wa kukagua vyombo vya
kujiridhisha na ubora na usalama kabla na baada ya safari.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.