ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 3, 2015

VYAMA VITANO VIMEKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Viongozi wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015
Tamko hili ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.
2. Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.
3. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea.
4.Viongozi wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na sio madhabahu.
5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6. Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.
7. Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.

MWANZA LEO NDIYO LEO: PICHA ZA MWANAMUZIKI ROBERTO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


Yule Mwanamuziki mkali kutoka nchini Zambia, ambaye yu atamba na single yake Amarula inayopatikana ndani ya album yake yenye nyimbo nyingi kalikali Roberto, amepata fursa ya kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari jijini Mwanza nchini Tanzania.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa:- Anajisikiaje kuwa nchini Tanzania na pengine hii ni safari yake ya ngapi kudhuru hapa nchini? BOFYA PLAY KUSIKIA ALICHOSEMA.
Balozi wa Habari toka Jembe Media Group Mr. Albert G. Sengo (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria mazungumzo na mwanamuziki Roberto toka nchini Zambia (katikati) juu ya alivyojipanga kwa mashambulizi leo jumamosi ya tarehe 3October 2015 Jembe Beach Resort. Katikati ni Msemaji wa Groove Entertainment Dj HQ.
Jeh. Roberto ana wito gani kwa vijana kizazi cha katika kusaka maendeleo? BOFYA PLAY.

Yeye ni mwakilishi wa mamilioni ya wananchi wa Zambia hapa nchini kupitia nyanja ya sanaa, akipata nafasi ya kuizungumzia Tanzania mbele ya watu wa taifa lake kipi atasema? BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Pata kionjo cha wimbo Amarula... BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Talking ....
Sagga continue.


Meneja mauzo wa kampuni ya Tanzania Distillers  alikuwa na haya ya kusema. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.


Mpango mzima.

SKYLIGHT BAND KUSINDIKIZA TAMASHA LA FAHARI YA MWAFRIKA NDANI YA KIOTA CHA ESCAPE ONE LEO JUMAMOSI

Mmiliki wa Skylight Band Dk Sebastian Ndege(Jembe ni Jembe) akicheza moja ya nyimbo ya bendi Skylight. Njoo leo Jumamosi kwenye Show ya Fahari ya Mwafrika itakayofanyika kwenye kiwanja cha Escape One ambapo Skylight Band ikisindikizwa na Msanii machachari Barnaba Classic watadondosha moja ya show kali usisubirie kusimuliwa njoo wewe na yule.
Sam Mapenzi pamoja akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One Mikocheni.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa Skylight band waiimba na kucheza mbele ya mashabiki wao ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ndani ya kiota cha Escape One siku ya Jumapili iliyopita.
Burudani ikiendelea
Mwimbaji wa bendi ya Skylight Natasha akiwapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu na kutoa burudani ya nguvu kwa wapenzi wa bendi hiyo waliofika siku ya Jumapili ndani ya Kiota Cha Escape One.
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku wakiendelea kuzirudi nyimbo kali za Bendi hiyo
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Sony Masamba(kushoto) na Kasongo Junior(kulia).
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao
Sam Mapenzi pamoja(Kushoto) na Ashura Kitenge wakiimba kwa furaha huku wakikonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika kwenye kiwanja cha Escape One, Mikocheni
Kushoto Rapa mkongwe katika muziki wa Live Joniko Flower pamoja na mwenzake Sony Masamba wakisababisha mashabiki viuno vyao viweze kuzungushwa mithiri ya feni.
Ilikuwa noma sana siku ya Jumapili iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka
Wanaume wa shoka wakilisakata rhumba wakati wa kuwafurahisha mashabiki wa bendi ya Skylight
Bendi haiwezi kuwepo bila kuwa na hawa jamaa wakali wanaosababisha Bendi ya Skylight kupaa
Ule muda sasa ulifika wa kusugua maana ilikuwa ni noma sana
Wanaume wa shoka wakilisakata rhumba wakati wa kuwafurahisha mashabiki wa bendi ya Skylight
Mashabiki wa Bendi ya Skylight wakiendelea kukata mauno kutokana na muziki mkali wa bendi hiyo jumapili iliyopita.

MAWAZIRI WA ZAMANI NCHINI TANZANIA WAPUNGUZIWA KIFUNGO.

Mawaziri wa zamani Bazir Mramba, na Yona wapunguziwa adhabu ya kifungo kutoka miaka mitatu hadi miwili baada ya kukata rufaa.

Mawaziri hao walipatikana na hatia ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.5.

TCRA, JESHI LA POLISI KUKABILIAN NA WAHALIFU WA MTANDAONI.

TCRA, Jeshi La Polisi Kukabiliana Na Wahalifu Wa Mtandaoni.

MGOMBEA UBUNGE KIBAHA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUZILINDA ML.50 ZITAKAZOTOLEWA NA SERIKALI ZISIIBIWE NA WATENDAJI.

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka akiwawahutubia wananchi wa kata ya picha ya ndege katika mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini Maulid Bundala akiwa amemwinua mkono kwa ajili ya kumnadi mgombea ungunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kongowe.
Wananchi wakiwa wametulia wanafuatilia kwa umakini katika mkutano uliofanyika picha ya ndege.
Wananchi na wanachama wa CCM, wakiwa wanacheza wimbo wimbo unaofahamika kama CCM, mbele kwa mbela katika mkutano uliofanyika katika kata ya kongowe.
Mwonekano umati wa  wananchi waliofurika  kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara kushuhudia sera za mgombea huyo ubunge Silvestry Koka.
Mmoja kati wa wakeleketwa wa Chama cha mapinduzi ambaye amekiama chama cha Chadema hivi karibuni akiwa na wazee wakongwe wakiwa wanamsikiliza mgombea ubunge katika mkutano uliofanyika kata ya Kongowe.(Picha zote na Victor Masangu)
 NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kuputia tiketi tiketi ya (CCM)  Silvestry Koka  amewahakikishia wananchi wake endapo wakimchagua atahakikisha anazisimamia fedha zitakazotolewa na serikali kiasi cha shilingi milioni 50 katika kila mtaa zinatumika kwa ajili ya  kuleta  maendeleo kwa wananchi na sio zinaliwa na watu wachache kwa  maslahi yao binafsi.
 
Koka ameitoa kauli hiyo kwa wananchi  wakati wa mikutano ya hadhara  iliyofanyika katika kata ya picha ya ndege pamoja na kata ya Kongowe ambapo amesema kuwa suala hilo kamwe hawezi kulifumbia macho hata kidogo na badala yake ataweka mipango madhubuti ya kusimamia fedha hizo zisiweze kutumika tofauti na malengo yaliyowekwa.
 
Alisema kwamba serikali kupitia chama cha mapinduzi (ccm) imeona kuna umuhimu wa kuendelea kuleta chachu ya mabadiliko kuanzia ngazi za chini hivyo fedha hizo zitakazotolewa katika kila mtaa ni kutokana na mwongozo wa sera ambayo ipo katika ilani ya chama na wala sio ubabaishaji hivyo wananchi wasiwe na hofu.
 
“Sisi nia yetu ni kuona mabadiliko yanakuja kwa kasi kuanzia ngazi za chini na ndio maana Mgombea urais John Pombe Mgufuli amesisitiza kutoa kiaisi cha shilingi 50  katika kila mtaa, na hii ipo kwenye ilani ya chama sio imetoka hewani hivyo fedha hizo zitakuja na nina imani zitaweza kuleta mabadiliko,”alisema Koka.
 
Aidha Mgombea huyo alisisistiza kwamba anatambua kuna baadhi ya watendaji wamekuwa na tabia ya kufanya ubadhilifu katika fedha za serikali, hivyo pindi atakapowabaini wale wote ambao watahusika atawachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Akifafanua kuhusiana na suala  hilo la fedha za mitaa alisema kuwa endapo watendaji pamoja na wananchi kwa kushirikiana na yeyey mwenyewe wakizisimamia vizuri fedha hizo bila ya kuwa  na tama yoyote zitaweza kukuza uchumi kwani wanaweza kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo kupitia fedha hizo .
 
 Pia Mgombea huyo alisema kwamba licha  ya  serikali kutoa kiasi hicho cha fedha katika kila mtaa na yeye atajitahidi kwa hali na mali kuongezea fedha zingine na kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kukuza uchumi  kwa wananchi wa jimbo la kibaha mjini pamoja na maeneo mengine.

MAMA SULUHU HASSANI 'ATETEMESHA' JIMBO LA ITILIMA, SIMIYU.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Itilima kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Simiyu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi baada ya kumsimamisha Kata ya Lamadi alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoani Simiyu.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan  (hayupo pichani) baada ya kumsimamisha njiani Kata ya Lamadi alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoani Simiyu.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan  (hayupo pichani) baada ya kumsimamisha njiani Kata yaDutwa alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara kampeni za CCM Mkoani Simiyu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Titus Kamani (kulia) wakisaini vitabu vya wageni Jimbo la Busega kabla ya mgombea mwenza kuhutubia wananchi eneo hilo. 
Dk. Raphael Chegeni (hayupo pichani) wa Jimbo la Busega akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Busega kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Simiyu.
Dk. Raphael Chegeni wa Jimbo la Busega akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Busega kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Simiyu.
Vijana nao wakapanda mtini kumshuhudia Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia.


Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) wakizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Busega, George Mshomi katika Jimbo hilo.
Asumpta Mshama ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kampeni wanaoongozana na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Busega.
Asumpta Mshama (kulia) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kampeni wanaoongozana na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Busega, Dk. Chegeni.
Mgombea mwenza wa CCM tiketi ya urais, Mama Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Busega.
Salamu kwa wananchi njiani akielekea katika mikutano mikubwa.
Wagombea udiwani CCM, Jimbo la Bariadi wakijitambulisha kwa wananchi.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Titus Kamani (kulia) wakisaini vitabu vya wageni Jimbo la Busega kabla ya mgombea mwenza kuhutubia wananchi eneo hilo. 
'Tutakaa popote tumshuhudie Mama Samia Suluhu Hassan' ...Vijana wakiwa wamepanda juu ya bati Jimbo la Itilima ili kumshuhudia mgombea mwenza.

Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima, Njalu Daudi Silanga akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Itilima kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Simiyu.
Umati katika Jimbo la Itilima, Wilaya ya Itilima Simiyu.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima, Njalu Daudi Silanga akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Itilima kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Simiyu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com