MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka akiwawahutubia wananchi wa kata ya picha ya ndege katika mkutano wa hadhara. |
Wananchi wakiwa wametulia wanafuatilia kwa umakini katika mkutano uliofanyika picha ya ndege. |
Wananchi na wanachama wa CCM, wakiwa wanacheza wimbo wimbo unaofahamika kama CCM, mbele kwa mbela katika mkutano uliofanyika katika kata ya kongowe. |
Mwonekano umati wa wananchi waliofurika kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara kushuhudia sera za mgombea huyo ubunge Silvestry Koka. |
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kuputia tiketi tiketi ya (CCM) Silvestry Koka amewahakikishia wananchi wake endapo wakimchagua atahakikisha anazisimamia fedha zitakazotolewa na serikali kiasi cha shilingi milioni 50 katika kila mtaa zinatumika kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi na sio zinaliwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
Koka ameitoa kauli hiyo kwa wananchi wakati wa mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata ya picha ya ndege pamoja na kata ya Kongowe ambapo amesema kuwa suala hilo kamwe hawezi kulifumbia macho hata kidogo na badala yake ataweka mipango madhubuti ya kusimamia fedha hizo zisiweze kutumika tofauti na malengo yaliyowekwa.
Alisema kwamba serikali kupitia chama cha mapinduzi (ccm) imeona kuna umuhimu wa kuendelea kuleta chachu ya mabadiliko kuanzia ngazi za chini hivyo fedha hizo zitakazotolewa katika kila mtaa ni kutokana na mwongozo wa sera ambayo ipo katika ilani ya chama na wala sio ubabaishaji hivyo wananchi wasiwe na hofu.
“Sisi nia yetu ni kuona mabadiliko yanakuja kwa kasi kuanzia ngazi za chini na ndio maana Mgombea urais John Pombe Mgufuli amesisitiza kutoa kiaisi cha shilingi 50 katika kila mtaa, na hii ipo kwenye ilani ya chama sio imetoka hewani hivyo fedha hizo zitakuja na nina imani zitaweza kuleta mabadiliko,”alisema Koka.
Aidha Mgombea huyo alisisistiza kwamba anatambua kuna baadhi ya watendaji wamekuwa na tabia ya kufanya ubadhilifu katika fedha za serikali, hivyo pindi atakapowabaini wale wote ambao watahusika atawachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Akifafanua kuhusiana na suala hilo la fedha za mitaa alisema kuwa endapo watendaji pamoja na wananchi kwa kushirikiana na yeyey mwenyewe wakizisimamia vizuri fedha hizo bila ya kuwa na tama yoyote zitaweza kukuza uchumi kwani wanaweza kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo kupitia fedha hizo .
Pia Mgombea huyo alisema kwamba licha ya serikali kutoa kiasi hicho cha fedha katika kila mtaa na yeye atajitahidi kwa hali na mali kuongezea fedha zingine na kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi wa jimbo la kibaha mjini pamoja na maeneo mengine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.