Saturday, December 3, 2022
MBUNGANI FC WAKABIDHIWA MILIONI MOJA NA DC MOYO.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikabidhi kiasi cha shilingi milion moja kwa viongozi wa timu ya mbugani FC
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipokea mipira kutoka kwa kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi
Wachezaji na wadau wa soka wa kata ya Mboliboli wakiwa kwenye hali ya furaha
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa sambamba na diwani wa kata ya Mboliboli na kaimu afisa tarafa ya Pawaga.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa
imekabidhidhiwa kitita Cha shilingi milioni milioni Moja iliyotolewa na wadau
wa soka wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya kama sehemu ya pongezi baada ya kutwaa
ubingwa katika mashindano ya Mbomipa Cup.
Kiasi hicho Cha Fedha kimetolewa kupitia harambee
iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ambapo amewahimiza
wadau wa soka Wilayani Iringa kuisaidia Timu hiyo Ili kuiwezesha kutatua
Changamoto zinazoikabili ikiwemo ukosefu wa vifaa vya Michezo na fedha Kwa
ajili ya uendeshaji wa Timu hiyo.
Moyo amesema Timu hiyo imeonesha ukomavu Kwa kutwaa
ubingwa wa kombe la MBOMIPAkupitia Michezo iliyojikita katika kuhamasisha
Utunzaji wa Mazingira na uhifadhi wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Sita
chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuchochea Ulinzi wa Wanyamapori
kwalengo la kuvutia watalii nchini
Katika Risala yake Kwa washiriki wa harambee hiyo wakiwemo
wachezaji wa Timu ya Mbugani Fc Mkuu wa Wilaya Iringa Mohamed Moyo amewataka
kuwa mabalozi wa uhifadhi Kwa kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu
wanafanya ujangiri katika hifadhi Ili kuwezeshabhatua za kisheria kuchukuliwa.
Katika hafla hiyo kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD
kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie ilichangua mipira miwili kwa ajili ya
kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya kiwilaya na
mkoa.
katika halfa hiyo ya kuwapongeza mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo alifanikisha kuchangisha kiasi cha shilingi milioni moja
kwenye harambee waliyoifanya siku ya kuwapongeza.
Timu ya
Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa inakabiriwa na changamoto
ya ukosefu wa vifaa vya mazoezi kama vile jezi,bipsi,viatu vya wachezaji,vifaa
vya golikipa,koni,nyavu na mipira hivyo wamewaomba wadau mbalimbali kuwachangia
ili waweze kufikia malengo wanayoyakusudia.
WAKULIMA IRINGA WANUFAIKA NA MRADI WA USAID LISHE ENDELEVU.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa makini kuwasikiliza viongoziNengilangen't Kivuyo-Meneja Mradi wa USAID Lishe Endelevu Mkoa wa Iringa akiwa kwenye moja la shamba la mfano.
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
MRADI wa
USAID Lishe Endelevu umeanzisha mashamba ya mfano 186 na kuwafikia na
kuwajengea uwezo wakulima 6,842 ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuusaidia
Mkoa wa Iringa kukabiliana na udumavu.
Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha katika kila watoto 100 wenye
miaka chini ya mitano mkoani humo, 47 sawa na asilimia 47 wamedumaa kutokana na
lishe duni.
Mratibu wa
USAID Lishe Endelevu (Kilimo Mifugo na Uvuvi), Samwel Kitila alisema hatua hiyo
imelenga kuiwezesha jamii kuongeza uzalishaji na ulaji wa vyakula vyenye
virutubishi vingi.
Aliongeza kwa kusema kuwa Mradi wa USAID Lishe Endelevu
kwa kushirikiana na Serikali ulianzisha Mabwawa 12 ya samaki (12000Vifaranga
vya samaki) 2021 lakini hivi tunavyoongea mkoa wa Iringa una mabwawa 52 ya
samaki(31840).
Kwa upande mazao Lishe (Mahindi Lishe,Maharage Lishe na Viazi) mwamko kwa wakulima umekuwa mkubwa sana mfano kuna kata inaitwa Nyanzwa-Kilolo
Ukilinganisha na awali ulaji wa mazao mchanganyiko na mazao mchanganyiko umeongezeka sana kwenye maeneo yote ya utekeleza wa Mradi.
Alisema mradi haukuishia kwa wakulima kwani ulifanya pia kazi ya kuvijengea uwezo Vikundi 99 vya kuweka na Kukopa(VSLA) ili viwe na sifa ya kupesheka na tayari 50 kati yake vimefanikiwa kupata mkopo wa Sh Milioni 83 ili kuendelea kukuza shughuli zao za kijasiriamali.
“Mradi pia umedhamiria kuongeza upatikanaji na utoaji wa huduma
bora za lishe katika ngazi ya vituo vya afya na jamii kwa kuimarisha uwezo wa
watoa huduma za afya,” alisema.
Katika kikao cha pamoja cha wadau kilicholenga kujua mafanikio
ya utekelezaji wa mradi huo, changamoto na utatuzi wake ili kuweka mikakati
endelevu,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi
Leonard Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa mkoa kushirikiana na wadau
ili kupunguza udumavu mkoani humo.
Mhandisi Masanja alisema;“Kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha
anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza athari za
utapiamlo na hasa udumavu miongoni mwa jamii yetu.”
Kwa kupitia msaada wa Watu wa Marekani, Masanja alisema mkoa wa
Iringa unatambua mchango mkubwa wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu wa mwaka 2018
hadi 2023 katika kutatua tatizo la lishe duni, utapiamlo.
Alisema mradi huo umechangia katika maeneo mengi yakiwemo; kuongeza hamasa ya mabadiliko ya tabia kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, watoto walio chini ya miaka mitano na vijana wa rika balehe kwa kupitia wanawake vinara, vikundi malezi na klabu za lishe.
Eng. Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa Mkoa wa Iringa wameshauriwa kushirikiana katika kuhakikisha udumavu unapungua ili kuwa na watoto wenye afya ya mwili na akili.
Alisema kuwa lishe ndiyo msingi wa maisha ya mwanadamu na
kuongeza kuwa afya ya mwanadamu ikiharikiwa kwa lishe duni katika siku elfu
moja (1,000)za mwanzo wa uhai, haziwezi kurekebishika kwamwe katika maisha yote
ya mwanadamu.
Eng. Masanja alisema kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha kuwa anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza athari za utapiamlo hasa udumavu
Pia aliwasihi viongozi kusimamia zoezi la mipango na bajeti za lishe kwa mwaka 2023/24 kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri ili kuhakikisha shughuli ambazo zimepangwa zinaendelea kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
“Vituo vyote vya kutolea huduma za afya,shule na serikali
mtambuka zipange shughuli za lishe zitakazosaidia kupunguza utapiamlo,”alisema
Masanja.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu
Tanzania Dk Joyceline Kaganda, Dk Benny Ngereza alisema mbali na Iringa, mradi
huo wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa ya Rukwa, Morogoro na Dodoma.
Dkt. Ngereza aliwataka maofisa mipango, wahasibu na maofisa lishe wa halmashauri kusimamia upangaji na utekelezaji wa shughuli za lishe ili kupunguza changamoto za lishe duni.
PWANI GENERATION QEENS YATOA MSAADA WA BAISKELI NA MAGONGO KWA WATOTO WALEMAVU.
Na Victor Masangu,Pwani
Imeelezwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa viungo katika mkoa wa Pwani bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa kutokuwa na mahitaji yao muhimu na kupelekea kuishi katika mazingira ambayo sio rafiki kwao.
Katika kuliona hilo Kikundi cha Pwani generation Qeen kimeamua kutumia fafrija ya utoaji wa tuzo kwa mwanamke sahihi fete kurudisha matendo ya huruma kwa kutoa msaada wa baiskeli zipatazo 15 kwa watoto wenye ulemavu pamoja na magongo ya kutembelea.
Kikundi hicho Cha Pwani generation Qeens 'Mwanamke wa shoka' kwa sasa kimetimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake na kimekuwa kikisaidia na kutoa michango mbali mbali kwa jamii pamoja na wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza katika tafrija za mwanamke sahihi fete zilizofanyika Wilayani Kibaha,Mwenyekiti wa Kikundi hicho Betty Msimbe alisema kwamba kwa mwaka huu wameweza kuboresha zaidi tuzo hizo ambazo zimeenda sambamba na kutoa msada wa baiskeli hizo 15 zenye thamani ya Shilingi zaidi ya milioni 6.
"Mwaka huu tumefanya maboresho katika tuzo zetu mbali mbali maana licha ya kutoa tuzo hizo kwa wanawake na wanaume tukaona kuna umuhimu wa kuisadia jamii hasa kwa watu wenye ulemavu kwani katika Mkoa wa Pwani wapo wengi,"alisema Msimbe.
Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba wao Kama Kikundi wamejiwekea yao katika siku za usoni kuwafikia watoto 100 ambao watawapatia msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo kuwapa baiskeli ambazo zitawasaidia hata kwenda shule kwa urahisi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika tafrija hiyo ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na vikundi ambavyo vimeweza kupatiwa vyeti vya pongezi pamoja na tuzo Bora kutokana na kazi zao pamoja na ushiriki wao katika shughuli za kijamii.
Katika hatua nyingine alimpongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatumikia wananchi na kuwaletea chachu ya maendeleo ikiwa sambamba na kutenga fedha ambazo zimeweza kusaidia katika shughuli za kijamii.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Pwani Recho Chacha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tafrija hiyo amekipongeza kikundi hicho kwa kuweza kuandaa tuzo hizo pamoja na kutoa msaada wa baiskeli 15 kwa watoto wenye ulemavu.
"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa dhati kikundi hiki cha Pwani generation Qeens kwa kuisaidia jamii kwa kutoa msaada wa baiskeli kwa watoto walemavu ikiwa sambamba na kutoa tuzo kwa wanawake na wanaume ambao wamefanya vizuri katika kazi zao,"alisema.
Aidha aliwaasa wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao na kuwapa malezi na maadili bora ambayo yataweza kuwasaidia kuepukana na mambo ambayo hayafai kufanywa katika jamii.
Pia aliitaja jamii kuachana kabisa na tabia ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wao na badala wake wahakikishe wanazuia na kupinga kabisa vitendo hivyo kwani ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.
Nao baadhi ya watoto hao walemavu ambao wamepatiwa msada wa baiskeli hizo wamekishukuru Kikundi hicho Cha Pwani generation Qeen kwa kufanya matendo ya huruma kwani kwa upande wao msada huo utakuwa ni mkombozi mkubwa.
Friday, December 2, 2022
MWILI WA ASKOFU KWANGU WAOKOTWA UKIELEA ZIWA VICTORIA.
NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu (61) amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa, marehemu aliaga familia yake na kuelekea wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi 2,500,000/= baada ya kuwa ameuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT- Sengerema. Hata hivyo hakuweza kulipwa kiasi hicho cha fedha kwa kuwa wanunuzi walimtaka awasilishe nyaraka ya umiliki wa eneo hilo hivyo, alirudi Mwanza mjini kwa ajili ya kushughulikia nyaraka hizo. Ilipofika jioni ya siku hiyo familia yake walipata wasiwasi kuhusu alipo Boniphace William Kwangu kwani hakuwa amerudi nyumbani pia alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya mkononi. Kutokana na hali hiyo ilibidi familia yake watoe taarifa Kituo cha Polisi Kirumba. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na familia na watu mbalimbali lilianza kufanya ufuatiliaji ili kubaini alipo askofu. ZAIDI VIDEO
AFRIKA YAKUTANA KUJADILI HATMA YA PUNDA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) na baadhi ya Viongozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Shirika la Umoja wa nchi za Afrika linaloshughulika na tafiti na haki za wanyama (AU-IBAR) wakifurahia jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano uliokuwa ukijadili hatma ya wanyama aina ya Punda uliofanyika leo (01.12.2022) jijini Dar-es-salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa kutetea haki za wanyama kutoka Kenya Bw. Josphat Ngonyo akiwaeleza Waziri wa Mifugo na Uzalishaji wa wanyama kutoka Chad Dkt. Abderahim Awat (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kushoto) namna wanyama aina ya Punda wanavyotumika nchini kwake muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano uliokuwa ukijadili hatma ya wanyama aina ya Punda uliofanyika leo (01.12.2022) jijini Dar-es-salaam. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameziongoza nchi zaidi ya 20 wanachama wa Umoja wa Afrika ambazo zimekutana leo (01.12.2022) jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya kujadili hata ya wanyama aina ya punda wanaodaiwa kuwa kwenye hatari ya kutoweka.
Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Ulega amewataka wataalam kutoka katika nchi hizo kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo ya kitafiti na kisayansi kuhusu njia zinazoweza kutumika kuwaokoa wanyama hao na kuziwasilisha ili zijumuishwe katika sera na kanuni kwa ajili ya utekelezaji.
“Kama tulivyofanikiwa katika kupiga vita biashara nyingine ambazo zilikuwa zikitupelekea kwenye kupoteza wanyama wetu basi mtafakari kama wataalam na kuja na tafiti za kisayansi zitakazotushawishi sisi watunga sera ili tuweke mkazo wa kupiga marufuku kama tulivyoweka kwa upande wa biashara ya meno ya Tembo” Amesisitiza Mhe. Ulega
Aidha Mhe Ulega amependekeza wanyama aina ya punda kujumuishwa kwenye kundi la viumbe waliopo hatarini kutoweka ili kuongeza nguvu ya jitihada zinazofanywa kwa ajili ya kuokoa hatma yao ambapo amesema kuwa hatua hiyo itafufua jitihada za kuongeza idadi ya wanyama hao.
“Lakini pia wakati mkijadili mnapaswa kujua kuwa pamoja na umuhimu wake kule vijijini wananchi wanashawishiwa kuuza punda wao kwa sababu ya umasikini hivyo wakati tunafikiria namna ya kudhibiti hali hii ya utowekaji wa Punda tufikirie namna ya kuwaelimisha na kuangalia njia mbadala kwa wanakijiji hao ili wasiwauze”Ameongeza Mhe. Ulega.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda amesema kuwa msisitizo mkubwa wa Tanzania katika mkutano huo ni kuueleza ulimwengu kuhusu hatua walizochukua katika kudhibiti hali ya kutoweka kwa punda ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku uuzwaji na uchinjwaji wa wanyama hao.
“Lakini jambo jingine tumeiambia dunia kuwa sisi kupitia mfumo wetu wa Sera tumeamua kulinda wanyama hawa kupitia eneo la ustawi wa wanyama lililopo kwenye mabadiliko ya sera ya Mifugo ya mwaka huu ambayo yanaendelea kufanyika” Amesema Nzunda.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa nchi za Afrika linaloshughulika na tafiti na haki za wanyama (AU-IBAR) Dkt. Nick Nwankpa amesema kuwa katika nchi zote za Afrika wanyama aina ya Punda wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kusaidia katika shughuli zote za kiuchumi.
“Lakini pamoja na msaada huo, Punda wamekuwa wakichukuliwa kama wanyama kazi tu ambao wamesahaulika hata kwenye sera na kanuni mbalimbali zinazolinda haki za wanyama na kadri idadi kubwa ya watu inavyoongezeka ndipo idadi ya punda inavyopungua” Amesema Dkt. Nwakpa.
Akielezea sababu za kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania Mwenyekiti wa Shirika linaloshughulikia haki za wanyama kazi (Brooke East Africa) Bw. Erick Kimani amesema kuwa hatua hiyo imetokana nchi hiyo kuwa ya kwanza kupiga marufuku biashara ya Punda ambapo amezitaka nchi nyingine za Afrika kuchukua hatua hiyo ili kuondoa hatari ya kutoweka kwa wanyama hao.
Mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar-es-salaam umelenga kujadili kwa kina umuhimu wa wanyama aina ya punda kiuchumi na kijamii na unatarajia kuwa na maazimio yatakayosaidia kuwaondoa wanyama hao kwenye hatari ya kutoweka.
HUYU NDIYE MRITHI WA DIALLO 'MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA'
NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Reuben Sixbert,ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mwanza,baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa kura 879.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika katika mkutano mkuu wa CCM mkoani Mwanza uliofanyika Novemba 21, 2022 uwanja wa CCM Kirumba, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Mwanza Gilbert Kalima alimtangaza Reuben Sixbert kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.
Ambapo katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa ilikuwa na wagombea watatu waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,ambao ni Ruben Sixbert,Nyirizu Makongoro na Nyanda Elias.
Kalima, ameeleza kuwa katika uchaguzi huo jumla ya wapiga kura walikuwa 1127,zilizoharibika ni 2 hivyo kura halali ni 1125, huku Ruben Sixbert akishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 879,akifuatiwa na Nyirizu Makongoro aliyepata kura 239 huku Nyanda Elias akiambulia kura 7.
Ameeleza kuwa zoezi hilo la uchaguzi lilikuwa gumu sana huku akitoa pongezi kwa wapiga kura sanjari na kuwataka wagombea wote ambao kura hazijatosha wajipange tena katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Reuben Sixbert, akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi aliwaomba Wenyeviti wa CCM Wilaya na Kata waungane kwa pamoja katika kusaidia utekelezaji wa ilani ya chama pamoja na kuwaunganisha wana CCM.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanaCCM kutopambana wao kwa wao bali wapambane na vyama vya upinzani, hivyo wajiandae vyema kwa ajili ya chaguzi za Serikali ya Mitaa mwaka 2024 na Mkuu mwaka 2025.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza aliemaliza muda wake Antony Diallo,amewahimiza viongozi hao wapya kuendeleza juhudi za ujenzi wa ofisi mpya za CCM katika majimbo ya Sumve na Buchosa.
DKT. NDUMBARO ATAKA MRADI WA KITUO JUMUISHI CHA TAASISI YA KISHERIA MWANZA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA.
NA ALBERT G.SENGO/ MWANZA
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt, Damas Ndumbaro ametaka mradi wa kituo jumuishi cha taasisi ya sheria kinachojengwa Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya fedha yenye tija na maslahi Kwa Nchi.
Hayo ameyabainisha wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi na kueleza kuwa ujenzi wa jengo hilo linapaswa kuwa kichocheo Kwa ujenzi wa majengo mengine Kama hayo katika sehemu nyingine za Nchi. Dkt, Ndumbaro ameeleza kuwa ili kuweza kufikia malengo ni lazima wahakikishe wanatembea katika dira na dhima ya wizara na kuendelea kuimarisha miundmbinu katika kuhakikisha uapatikanaji wa haki unakuwa kiurahisi Kwa Kila mtu. "Kutokana na hili nipende kutoa shukrani Kwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa fedha Kwa mahakama ambapo miradi mbalimbali imeendelea kujengwa ikiwemo ujenzi wa vituo jumuishi katika Mikoa mbalimbali" Alisema Ndubaro. Aidha ametoa wito Kwa mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha Kwa wakati jengo Hilo na Kwa ubora kwani fedha zinazotumika ni za wananchi. Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi ameeleza kuwa ujenzi wa vituo jumuishi utasaidia kuwezesha taasisi za kisheria za serikali, Wizara pamoja na wadau muhimu Kwa pamoja kuongeza tija katika kutoa huduma. Feleshi amesema kuwa mpango huo utafanikisha kazi zinazofanywa na mahakama mtandaoni pamoja na kuondoa zinazowakabili katika maeneo yenye mahakimu wengi kuliko mawakili wa serikali. Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri kutoka Wakala Majengo Tanzania (TBA), Wencelaus Kizaba amesema jengo hilo litagharimu zaidi ya Sh Bil, 3,181,548,096.83 hadi kukamilika kwa ujenzi huo. Kizaba amesema kuwa ujenzi wa jengo hili ulianza aprili 26 mwaka huu na unatarajia kukamilika oktoba 25 mwaka 2023 kwani mpaka hivi sasa upo asilimia 35 ya ujenzi wa kazi zote za mkataba. Ameeleza kuwa mradi huo umetoa ajira mbalimbali kwa wataalamu na wafanyabiashara wadogo wadogo ,umetoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya nchini "Vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi huu vinatoka kwenye viwanda vyetu vya ndani ikiwemo Saruji,Rangi,Mabomba na baadhi vitatoka kwenye viwanda vya nje,"amesema Kizaba. Kwa upande wake mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nyamagana,Florah Magabe ameipongeza Serikali kwa kuanzisha vituo jumuishi vitakavyosaidia kukabiliana na vishoka.TUZO BORA ZA MWANAMKE SAHIHI FETE MKOA WA PWANI 2022 KUFANYIKA LEO KIBAHA.
Na Victor Masangu ,Pwani
Thursday, December 1, 2022
MWANZA YATANGAZA VIWANJA VYA BEI RAHISI 'NUNUA LEO PATA HATI YAKO LEO'
HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA LANDSPECS DEVELOPERS LTD INAWAKARIBISHA WANANCHI WOTE KUJIPATIA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO:
· MAKAZI - UKUBWA WA MITA ZA MRABA KATI YA 535 MPAKA 1500 KWA SHILINGI 6,500/= KWA SQUARE MITA · BIASHARA/MAKAZI - UKUBWA WA MITA ZA MRABA KATI YA 522 MPAKA 6156 KWA SHILINGI 7,500/= KWA SQUARE MITA · HUDUMA ZA JAMII - UKUBWA WA MITA ZA MRABA 2035 MPAKA 7472 KWA SHILINGI 5,000/= KWA SQUARE MITA · NA SHILINGI 12,000/= KWA VIWANDA NA BIASHARA . VIWANJA HIVI VIPO ENEO LA KISESA - ISANGIJO UMBALI WA TAKRIBANI KILOMETA 20 KUTOKA MWANZA MJINI, KANDOKANDO YA BARABARA KUU MWANZA - MUSOMA, KARIBU NA KUKU POA, KARIBU KABISA NA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO KAMA MRADI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA NA BINAFSI UNAOJENGWA NA WATUMISHI HOUSING COMPANY LIMITED, CHUO CHA MICHEZO, MAENEO YA VIWANDA VIDOGO, SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI, VITUO VYA AFYA, KITUO KIKUU CHA MABASI KISESA. PIA MRADI HUU UPO TAKRIBANI KILOMETA TANO (5) KUTOKA STENDI KUU YA MABASI NYAHMONGOLO UTARATIBU WA MAUZO NI KAMA IFUATAVYO; · MNUNUZI ATAFIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU, IDARA YA ARDHI NA MALIASILI KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI KUNUNUA FOMU ZA MAOMBI KWA GHARAMA YA SHILINGI 20,000/= (FEDHA HIZI HAZITAREJESHWA) NA PIA KWENYE ONE STOP CENTER ITAKAYOKUWA KATIKA ENEO LA MAEGESHO YA MAGARI ROCK CITY MALL KUANZIA TAREHE 30/11/22 MPAKA 10/12/22 · MNUNUZI ATAKAPOTOA UTHIBITISHO WA MALIPO, ATAPEWA NYARAKA ZITAKAZOHUSIANA NA KIWANJA CHAKE NA KUANDALIWA HATI MILIKI YA KIWANJA CHAKE PAPO KWA PAPO · PIA TUNAWAKARIBISHA WATEJA WETU WANAODAIWA KUKAMILISHA MALIPO YAO ILI WAWEZE KUANDALIWA HATI MILIKI ZAO KWA UTARATIBU HUU WA PAPOP KWA PAPO · KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI FIKA KWENYE OFISI YA ARDHI NA MALIASILI MAGU AU KWENYE ONE STOP CENTER YETU (ROCK CITY MALL) KATIKA TAREHE ZILIZOTAJWA HAPO JUU. · WASILIANA NASI KWENYE NAMBA 0783233333 NA 0755540916 IMETOLEWA NA; FIDELIKA G. MYOVELLA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU.KYLIAN MBAPPE: YAIBUKA SABABU ZA STAR HUYO WA PSG KUKATAA KUCHEZA CAMEROON KWENYE KOMBE LA DUNIA
'FROM ZERO TO HERO' Kylian Mbappe yuko katika kiwango kizuri akiwa na Ufaransa kwenye Kombe la Dunia, lakini angechezea Cameroon.
BABA yake mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe amesimulia yaliyojiri, na kumlazimu mwanawe kuwachezea wabingwa watetezi badala ya Cameroon.
Mbappe alizaliwa mjini Paris na baba raia wa Cameroon Wilfried, na mama mzawa wa Algeria, lakini alifanya jitihada za kucheza soka la timu ya taifa hilo la Bara Afrika ya Kati ambako baba yake alizaliwa.
Kutoka kushoto ni Mama wa Mbape, Mbape, Mdogo wake Mbape na Baba yake Mbape. |
Mnamo 2018, Wilfried alidai kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Cameroon alimuitisha pesa kabla ya kumjumuisha mwanawe katika kikosi cha Indomitable Lions.
"Mwanzoni, nilitaka mwanangu achezee Cameroon lakini, mtu fulani katika Shirikisho la Soka la Cameroon alitoza kiasi cha pesa ambazo sikuwa nazo ili kumfanya acheze.
Kutoka kushoto ni Mbape, Baba yake na Mdogo wake. |
Wafaransa hawakutoza chochote." Mnamo 2018, Mbappe alikuwa katika kiwango cha kuvutia kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi huku akifunga mabao manne, likiwemo moja katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Croatia kwenye fainali.
Aliweka historia ya kuwa kinda wa pili kufunga katika fainali ya Kombe la Dunia baada ya gwiji wa Brazil Pele.
Ripoti za kuaminika zinaonyesha kuwa rushwa imekithiri katika timu za taifa za barani Afrika, ambapo ubora wa wachezaji hauzingatiwi.
Ni nafasi ya kipekee kuchezea timu ya taifa, na Kylian anaamini kwamba wachezaji hawapaswi kulipwa ili kutumikia nchi yao. Kylian Mbappe aling'aa katika ushindi wa Ufaransa wa 2-1 dhidi ya Denmark katika mchezo wao wa pili wa Kundi D kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022.
AJALI YA ROLI LA MATOFALI YAUWA WATATU, YUMO DALALI MAARUFU WA JIJI LA MWANZA
NA ALBERT G. SENGO / MWANZA
WATU watatu wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea mapema hii leo mkoani Mwanza maeneo ya Mataa Nyakato - sokoni. Tukio lililohusisha lori lililokuwa limebeba matofali kufeli breki katika mteremko wa kuelekea Nyakato National na hivyo kwenda kuyagonga magari yaliyokuwa yakisubiri ruhusa ya taa za kuongozea magari.
Magari matatu ya abiria (Hiace) na gari moja private yamehusika katika ajali hiyo. Dalali maarufu hapa Mwanza anaefahamika kwa jina la Mzee Shaaban Kumba ndiye mwenye gari private iliyogongwa ambaye amefariki papo hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa anashuka na taarifa zaidi kwa kina.
ANAYESADIKIKA KUMNYONGA KWA MTANDIO MHADHIRI CHUO CHA SAUT AKAMATWA STENDI YA MABASI
NA ALBERT G.SENGO / MWANZA
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza, Hamida Mussa (64).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja miongoni mwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Sara Mwendeshasahani (15) aliyekuwa mfanyakazi wa ndani wa marehemu.
Mwili wa mhadhiri huyo ulikutwa Jumanne Novemba 29, 2022 nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni huku mfanyakazi wa ndani wa mhadhiri huyo akidaiwa kutokomea kusikojulikana.
NEKTA YAZIFUNGIA SHULE 24 UDANGANYIFU MTIHANI LA SABA
Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya shule za msingi kwa mwaka 2022, jijini Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.
Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.
Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.
Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam).
Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).
Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).
“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.
Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.