ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 1, 2022

NEKTA YAZIFUNGIA SHULE 24 UDANGANYIFU MTIHANI LA SABA


 Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya shule za msingi kwa mwaka 2022, jijini Dar es Salaam.

 Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.


Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.


Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.


Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam).


Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).


Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).


“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.


Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.