ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 6, 2013

LEO YANGA 1 KCC1, KURUDIANA KESHO NDANI YA UWANJA WA KAMBARAGE SHINYANGA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikabidhiwa na wanachama wa Yanga Kombe la Ubingwa lililonyakuliwa na timu hiyokatika msimu wa 2012-2013 kama ishara ya kombe hilo kuingia jijini Mwanza ni katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo kulikuwa na mechi ya kirafiki baina ya Mabingwa Yanga na Mabingwa KCC ya Uganda. Matokeo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. 

Yanga V/S KCC.

Mchezo ukiendelea.

Safu ya wageni meza kuu ikiongozwa na Mwigulu Nchemba.

kombe likitembezwa kwa mashabiki uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

VIP

Mahojiano na kepteni wa KCC ya Uganda.

Felix Minziro - Kocha msaidizi wa timu ya Yanga

Mahamudu Katerega- Kocha mkuu KCC ya Uganda.

Wanachama wa Yanga na makombe yao y Ubingwa na lile la timu yenye nidhamu.
Kesho timu hizo zitashuka tena dimbani kurejeana katika uwanja wa CCM Kambarage katika kusherehekea sikukuu ya sabasaba mkoani Shinyanga.

YANGA NA KCC YA UGANDA KUONYESHANA UNDAVA LEO JUMAMOSI UWANJA WA CCM KIRUMBA

Mabingwa wa soka wa Tanzania bara Dar es salaam Young African tayari wamekwishaingia jijini Mwanza na leo wanataraji kushuka dimba la CCM Kirumba kuvaana na KCC ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa. 

Sambamba na Yanga timu ya KCC ambao ni mabingwa wa ligi ya nchini Uganda nao tayari wamekwisha wasili salama mkoani hapa ambapo usiku wa kuamkia leo waliandaliwa chakula cha pamoja na waandaaji wa mpambano huo National Wide, iliyofanyika kwenye kiunga cha burudani Villa Park Mwanza.  
Sanjari na mchezo huo ambao unaonekana utakuwa na ushindani wa hali ya juu kwa wenyeji Yanga kutaka kuwakosha mashabiki wao vilevile KCC kutaka kudhihirisha kuwa wao ndiyo mabingwa wa Uganda taarifa toka ungozi wa timu zote zinasema kuwa timu hizo zitatumia mchezo huo kuonyesha zawadi na vikombe walivyotwaa kwenye ligi zao msimu uliomalizika.


Wakipiga stori za hapa na pale Villa Park Mwanza.


Benchi la Ufundi.


Ni mazungumzo zaidi.


Yanga.


Baadhi ya wachezaji wa KCC.


Eneo la tukio.


Chating huku wakila muziki.


Ufundi.



Akizungumza na blogu hii Mwenyekiti wa Taasisi ya Michezo ya National Wide Bw. John Kadutu, amesema kuwa mara baada ya mchezo wa leo dimba la CCM Kirumba mabingwa hao watarudiana tena tarehe 7/07/2013 kutoa zawadi ya  sikukuu ya Sabasaba kwa wakazi wa Shinyanga.

Amevitaja viingilio katika michezo hiyo kuwa ni shilingi 3,000/= mzunguko na shilingi 10,000/= jukwaa kuu.

Ratiba zaidi inaonyesha kuwa ziara hiyo ya mabingwa itahitimishwa mkoani Tabora kwa Yanga Africans kumenyana na Mtibwa Sugar. 

Yanga kwa mara ya mwisho walitimba mkoani Tabora enzi za wawakilishi  wa ligi kuu soka Tanzania bara, timu iliyoacha historia kwa kutandaza soka safi Mirambo ya Tabora.

Friday, July 5, 2013

LOWASSA AWATAKA WAFANYABIASHARA WAKUBWA KUWAWEZESHA MITAJI WAMACHINGA ILI WAJIKWAMUE KIUCHUMI AWACHANGIA MILIONI 20 KWENYE MFUKO WAO

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwa  ameambatana na makada wa chama, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini Mwanza, wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwaajili ya mkutano wa muda mfupi ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga wa jijini hapa.

Alipowasili alikaribishwa kishupavu na vijana.

Kisha akapanda mti eneo hilo ikiwa ni ishara ya kuthamini mazingira.

Naye diwani wa Nyamagana Bhiku Kotecha alifungua mkutano huo kwa maneno machache.

Wananchi kusanyikoni.

Risala ya wamachinga ikisomwa.
Wananchi wakitafakari wanayoelezwa.

Wadau wakisikiliza kwa makini shughuli zinazoendelea mtaa maarufu wa wafanyabiashara ndogondogo hapa jijini Mwanza.

Jiografia ya eneo la Makoroboi jijini Mwanza na umati wake.

Mhe. Lowassa akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wadogo kuliko wote wa timu ya Machinga Fc inayoshiriki ligi ya kuwania kombe la Meya's Cup jijini Mwanza.

Timu ya Machinga inayoshiriki ligi ya Meya's Cup nayo ilitambulishwa.

Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa amewataka wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo maarufu kwa MACHINGA ili kuwawezesha kupata mitaji ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na Machinga wa shirika la SHIUMA kwenye eneo la Makoroboi Jijini Mwanza leo mchana Mhe. Lowassa ambaye ni Mjumbe wa NEC  Wilaya ya Monduli na Mbunge wa Jimboni humo alisema njia pekee ya kuwawezesha wamachinga hao ni kuwachangia fedha ili kuwawezesha kujiendeleza kupitia biashara zao na kuwapatia maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao.

Maneno yaliyowagusa.
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza  na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.

Makoroboi jijini Mwanza.
Mjumbe huyo wa NEC alisema kwamba Ilani ya CCM inatambua na inaelekeza kwamba vijana wataandaliwa na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali (SACOS) na kusajiliwa ili kuwapatia fedha ikiwa ni mitaji ya kuwawezesha kujiendesha jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ukurasa wa 88 na 89 hivyo tunataitekeleza kwa vitendo kama ambavyo ninyi tayari mmeanza kuitikia na hilo ndilo limenileta hapa leo nikiwa kiongozi ndani ya CCM.

“Nitaka nirudie msimamo wangu kwenu kwani kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaniandika kwamba nimekuja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Mwiguru Mchemba (Mbunge wa Jimbo la Iramba)kuvunja ngome ya Chama furani hapa maeneo ya Jiji la Mwanza siyo kweli mimi niko na marafiki zangu nimekuja kutokana na wito wenu ili kuwasikiliza sasa puuzeni hayo”alisema.

Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga makofi). 
Bw. Lowassa alisema kwamba kutokana na marafiki zake ambao aliwataja Bw.Christopher Mwita Gachuma (MNEC- Tarime), Bw.Mathias Manga (MNEC-Arumeru), Bw.Raphael Chegeni (MNEC-Busega) Bw.Shanif Hiran Mansoor(Mbunge-Kwimba) na Bw.Altaf Mansoor (Mkurugenzi wa MOIL) ambao waliniomba na kunisisitiza kuwaona na kuwasikiliza nami nimewapa utaratibu wa kuandaa Harambee kubwa ya kuwachangia na marafiki zangu wengine.


“Leo hii siyo harambee bali nataka kuwachangia kianzio katika mfuko wenu na siku zote CCM inasema kwamba ni lazima kuwapatia mtaji vijana hivyo nawapatia Cheki ya milioni 10 na jioni ntwapatia shilingi milioni 10 jumla zitakuwa shilingi milioni 20 za kuanzia ili kujipanga na harambee kubwa


Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala.

Mkutano huo wa muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia. 

Thursday, July 4, 2013

UJIO WA LOWASSA LEO WATIKISA MWANZA KWA MAPOKEZI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha 

Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege leo.

Shekh Hassan Kabete wa JASUTA

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa

Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa

Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza naye alikuwepo kumpokea 

Mzee maarufu na Kada wa CCM wa siku nyingi Ally Zagamba akisalimiana na rafiki yake Mhe.Lowassa

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha wageni VIP baada ya kuwasili leo Jijini Mwanza.

Mwanahabari na Mdau wa Blog hii Peter K. Fabian akisalimiana na Mhe. Lowassa VIP

Umati wa wanawake wa dini ya kisilam waliokuwa wamejipanga nje ya VIP kusalimiana na Mhe.Lowassa

Mama maarufu wa Jijiji Mwanza Mama Magige akiteta jambo na Mhe. Lowassa baada ya kusalimiana naye.

Moja ya wanawake wa kisilam ambaye ni kiongozi akisalimiana  na Mhe. Lowassa 

Wanawake waliojitokeza kumpokea Mhe. Lowassa

Na Peter Fabian
MWANZA.

WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa leo amelitikisa Jiji la Mwanza baada ya mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha pikipiki (Bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini kati.

Mapokezi hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya dini,wamachinga ambao ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza kufunika mapokezi ya awali ya leo asubuhi ya  Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba unaofanyika jijini hapa.

Baadhi ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa serikali na Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini walifurika kwa mamia kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka uwanja wandege wakimshangilia huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba msafara huo.

Waziri mkuu mstaafu huyo leo  anataraji kushiriki harambee ya kuchangia kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili kusaidia kuongeza usikivu wa matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja wa Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika ukumbi wa New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.

Mheshimiwa Lowassa katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyabiashara, Taasisi na makampuni ili kufanikisha adhma na lengo lililokusudiwa kutokana na ushawishi alionao na kwa muonekano wa mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege imeonyesha Mhe. Lowassa ni kipenzi cha watu na bado ananguvu ya kukubalika kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo cha radio IQRA ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabete alisema maandalizi tayari yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa na kuwasili kwa mgeni rasmi Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.


“Tunayo matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji kukusanya kwenye harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400, ambapo tayari mfuko wetu umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni 190 hivyo tunataraji lengo litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh Kabete.