ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 5, 2013

LOWASSA AWATAKA WAFANYABIASHARA WAKUBWA KUWAWEZESHA MITAJI WAMACHINGA ILI WAJIKWAMUE KIUCHUMI AWACHANGIA MILIONI 20 KWENYE MFUKO WAO

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwa  ameambatana na makada wa chama, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini Mwanza, wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwaajili ya mkutano wa muda mfupi ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga wa jijini hapa.

Alipowasili alikaribishwa kishupavu na vijana.

Kisha akapanda mti eneo hilo ikiwa ni ishara ya kuthamini mazingira.

Naye diwani wa Nyamagana Bhiku Kotecha alifungua mkutano huo kwa maneno machache.

Wananchi kusanyikoni.

Risala ya wamachinga ikisomwa.
Wananchi wakitafakari wanayoelezwa.

Wadau wakisikiliza kwa makini shughuli zinazoendelea mtaa maarufu wa wafanyabiashara ndogondogo hapa jijini Mwanza.

Jiografia ya eneo la Makoroboi jijini Mwanza na umati wake.

Mhe. Lowassa akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wadogo kuliko wote wa timu ya Machinga Fc inayoshiriki ligi ya kuwania kombe la Meya's Cup jijini Mwanza.

Timu ya Machinga inayoshiriki ligi ya Meya's Cup nayo ilitambulishwa.

Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa amewataka wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo maarufu kwa MACHINGA ili kuwawezesha kupata mitaji ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na Machinga wa shirika la SHIUMA kwenye eneo la Makoroboi Jijini Mwanza leo mchana Mhe. Lowassa ambaye ni Mjumbe wa NEC  Wilaya ya Monduli na Mbunge wa Jimboni humo alisema njia pekee ya kuwawezesha wamachinga hao ni kuwachangia fedha ili kuwawezesha kujiendeleza kupitia biashara zao na kuwapatia maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao.

Maneno yaliyowagusa.
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza  na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.

Makoroboi jijini Mwanza.
Mjumbe huyo wa NEC alisema kwamba Ilani ya CCM inatambua na inaelekeza kwamba vijana wataandaliwa na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali (SACOS) na kusajiliwa ili kuwapatia fedha ikiwa ni mitaji ya kuwawezesha kujiendesha jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ukurasa wa 88 na 89 hivyo tunataitekeleza kwa vitendo kama ambavyo ninyi tayari mmeanza kuitikia na hilo ndilo limenileta hapa leo nikiwa kiongozi ndani ya CCM.

“Nitaka nirudie msimamo wangu kwenu kwani kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaniandika kwamba nimekuja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Mwiguru Mchemba (Mbunge wa Jimbo la Iramba)kuvunja ngome ya Chama furani hapa maeneo ya Jiji la Mwanza siyo kweli mimi niko na marafiki zangu nimekuja kutokana na wito wenu ili kuwasikiliza sasa puuzeni hayo”alisema.

Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga makofi). 
Bw. Lowassa alisema kwamba kutokana na marafiki zake ambao aliwataja Bw.Christopher Mwita Gachuma (MNEC- Tarime), Bw.Mathias Manga (MNEC-Arumeru), Bw.Raphael Chegeni (MNEC-Busega) Bw.Shanif Hiran Mansoor(Mbunge-Kwimba) na Bw.Altaf Mansoor (Mkurugenzi wa MOIL) ambao waliniomba na kunisisitiza kuwaona na kuwasikiliza nami nimewapa utaratibu wa kuandaa Harambee kubwa ya kuwachangia na marafiki zangu wengine.


“Leo hii siyo harambee bali nataka kuwachangia kianzio katika mfuko wenu na siku zote CCM inasema kwamba ni lazima kuwapatia mtaji vijana hivyo nawapatia Cheki ya milioni 10 na jioni ntwapatia shilingi milioni 10 jumla zitakuwa shilingi milioni 20 za kuanzia ili kujipanga na harambee kubwa


Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala.

Mkutano huo wa muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.