ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 4, 2017

SIMBA CHUPUCHUPU KUUMBUKA TAIFA.

CHANZO BIN ZUBEIR
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM SIMBA SC imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 55, baada ya kucheza mechi 24, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 52 za mechi 23 ambao kesho watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
  Mbeya City wao baada ya sare leo, wanafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 24. 
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, hadi mapumziko Mbeya City walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 37 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Raphael Daudi.
Shiza Kichuya ameifungia Simba bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 86
Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
  Beki wa kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alipiga shuti kali dakika ya 24, lakini kipa Mmalawi wa MCC, Owen Chaima akadaka na Nahodha Jonas Mkude naye alikaribia kuifungia Simba dakika ya 28 kama si shuti lake kwenda nje baada ya pasi ya winga Shiza Kichuya.
  Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Mrundi Laudit Mavugo alikaribia kufunga dakika ya 32 kama si beki wa Mbeya City, Rajab Zahir kuokoa.
  Kiungo Muzamil Yassin alipiga shuti zuri baada ya krosi ya Hamadi Juma dakika 34, lakini mpira ukapaa juu na dakika ya 40 mshambuliaji mwingine tegemeo wa Simba, Ibrahim Hajib nusura aipatie bao timu yake kama si shuti lake kudakwa na Chaima.  Zaidi ya bao lao, shambulizi lingine la maana Mbeya City walifanya dakika ya 25, Ditram Nchimbi akipiga shuti kali baada ya pasi ya Bryson Raphael, lakini mpira ukaenda nje.
  Hajib aliisawazishia Simba SC kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65, uliopigwa nje kidogo ya boksi la Mbeya Ciry baada ya Bryson Raphael kuunawa mpira.
  Baada ya bao hilo, Mbeya City wakafunguka na kuanza tena kusaka ushindi Uwanja wa ugenini na haikuwa ajabu walipofanikiwa kupata bao la pili dakika ya 79, mfungaji Nahodha wake, Kenny Ally.
  Hata hivyo, Simba SC wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya aliyefunga kwa penalti dakika ya 86 baada ya Tumba Lui kumuangusha beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye boksi.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, James Kotei, Abdi Banda, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Mwinyi Kazimoto dk80, Muzamil Yassin/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk54, Laudit Mavugo, Said Ndemla na Shiza Kichuya. 
  Mbeya City: Owen Chaima, Haruna Shamte, Majaliwa Shaaban, Tumba Lui, Rajab Zahir, Sankhani Mkandawile/John kabanda, Raphael Daudi, Kenny Ally, Ditram Nchimbi, Mrisho Ngassa/Ayoub Semtawa dk69 na Bryson Raphael/Zahor Pazi dk90. 

NGASSA ATAMBA KUIFUNGA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA.

KIUNGO mshambuliaji mwenye makeke wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, amejiapiza kuwa kamwe hawatakubali kufanywa daraja la kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba.
Mbeya City na Simba, zinakutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mechi ya ligi kuu huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo uliopita.

Katika mechi iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, mabao ya Simba yalifungwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ na Ibrahim Ajibu.

Ngassa alisema kwa maandalizi waliyoyafanya chini ya Kocha Kinnah Phiri, anaamini yanatosha kuwapa ushindi kwenye mchezo huo.

Ngassa alisema, hawataki kupoteza mchezo dhidi ya Simba kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo baada ya kupoteza 'Mbeya Derby' na Tanzania Prisons waliovaana nao katika Kombe la FA ambao walitolewa kwa mikwaju ya penalti.

“Sitaki kutoa ahadi ya mabao tutakayoshinda na badala yake mimi binafsi nitaipambania timu yangu kuhakikisha tunaibuka na ushindi ili tumalize ligi kuu tukiwa katika nafasi nzuri.

"Simba ni timu ya kawaida kama zilivyokuwa timu nyingine na kwa bahati nzuri timu hiyo niliwahi kuichezea, hivyo ninawafahamu nusu ya wachezaji niliokuwa nacheza nao pamoja,” alisema Ngassa.

CDEA YAENDESHA MAFUNZO YA IIDEA 2017 KWA WABUNIFU MAVAZI NA UREMBO WA AFRIKA MASHARIKI.

 
Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo

Washiriki na wataalamu wakibadilisha mawazo wakati wa semina magunzo hayo

Bi Amal Mohamed kutoka Kenya akitoa mafunzo ya namna ya kupata Ufadhili kupitia ubunifu kwa wabunifu wa Afrika Mashariki

Bi Bernadine Buzabo akiwasilisha mafunzo kwa washiriki kwa njia ya mtandao wa Skype kwa washiriki (Hawapo pichani)

Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo

Mmoja wa wanufaika wa ufadhili kupitia ubunifu kutoka Kenya Bwana James Otieno akitoa mafunzo kwa washiriki

Baadhi ya washiriki Ester Kiula na Whitnery Gnaj wakifuatilia mafunzo hayo

Mshiriki kutoka Uganda, John Okello akishona vazi alilobuni mwenyewe wakati wa mafunzo hayo

Kemi Kalikawe kutoka Tanzania akipitia mchoro wa mshiriki Clare Musila (Uganda) wakati wa mafunzo hayo

Mshiriki akimuonesha mkufunzi kazi yake namna ya inavyovaliwa

Mshiriki akipata maelekezo ya vipimo toka kwa mkufunzi

Kemi Kalikawe akimuelekeza Catherine Mood Board

Mshiriki Victoria Joseph akiwa kwenye ubunifu wake

Kebirugi Nina akishona vazi alilobuni

Whitney Gnaj akijaribu vazi alilolibuni

Kemi Kalikawe akipitia mchoro wa Clare Musila

Wakili masuala ya miradi na biashara Bi. Sia Mrema akifundisha kuhusu usajili wa biashara na makampuni kwa washiriki hao ili kujitangaza zaidi hasa kupitia majina yao ya ubunifu (brand).

Bibi Santa Anzo ambaye ni mbunifu mkongwe na mahiri nchini Uganda akitoa mafunzo ya namna ya wabunifu watakavyoweza kubuni ubunifu wao na kuuza bidhaa zao katika masoko ya nje.

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akipitia kazi ya mwanafunzi Clare Musila

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akitoa mafunzo kwa wabunifu hao (Hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya IIDEA 2017.

Mmoja wa walimu wakitoa mafunzo katika mafunzo hayo.

Vazi la mbunifu wa Tanzania Makeke Jocktan alilolibuni wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Wabunifu wakiendelea na ubunifu wao

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Kazi za wabunifu zilizofanywa na washiriki

Baadhi ya washiriki wabunifu na walimu wakipiga picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa.
Picha ya pamoja ya washiriki wote wakipiga baada ya kumaliza mafunzo hayo ya IIDEA 2017.
Na Mwandishi Wetu
Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki. Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka. Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika. Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo. Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda. Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu. Mwisho. CODES: CDEA yaendesha mafunzo ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara IIDEA 2017,mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki. Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka. Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika. Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo. Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda. Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu. Tazama hapa matukio mbalimbali ya picha ya mafunzo hayo:

LEMA AITIKISA ARUSHA, JAJI MAHAKAMA ILIINGILIWA, GWAJIMA MATATANI POLISI APEKULIWA TENA, JPM AZUIA PASIPOTI ZA WAKANDARASIMAGAZETI YA LEO:-


Gobless Lema aitikisa Arusha,  Kesi ya Lema: Jaji mahakama ilingiliwa, Gwajima matatani polisi, apekuliwa tena,  JPM azuia pasipoti za wakandarasi. 

Serikali yaagiza pombe kali ziwekwe kwenye chupa, aliyemkabidhi ardhi Makonda ahaha, Waziri Lukuvi ambana. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.

IGP MANGU AKEMEA DAWA ZA KULEVYA.

Mgeni rasmi Afande IGP Ernest Mangu akikagua vikosi mbalimbali vya jeshi la polisi mkoa wa Mwanza katika sherehe ya kukabidhi vyeti vya heshima kwa baadhi ya askari waliofanya vyema kipindi cha mwaka 2016-2017. Shughuli ikifanyika katika viwanja vya polisi mabatini.
Akizungumza na askari polisi jijini Mwanza wakati akiwatunuku askari 30 waliofanya vizuri kutoka katika wilaya 7 mkoani hapa Mkuu huyo wa jeshi hilo amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo bila kujali cheo chake.

“Mapambano ya dawa za kulevya si nguvu za soda ni mapambano endelevu tumetamka ,kwahiyo tu watupe ushirikiano na wale wanaobeza pengine ndiyo watumiaji wenyewewa dawa za kulevya au wanufaikaji, kwahiyo tunaomba waache hiyo biashara haramu,” alisema IGP Mangu.
 

VIDEO YA TUKIO.

SHILINGI MILIONI 10.8 ZAKUSANYWA KATIKA VITA YA UVUVI HARAMU GEITAMkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza dhana haramu  ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.

Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea.

Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo.

Katibu wa BMU mtandao wa kata ya Bukondo Methusela Samweli akisoma Risala ambayo ilikuwa inaelezea changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku wa kutokomeza uvuvi haramu.

Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi.

Afisa mfawidhi udhibiti  ubora wa samaki  na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita  Shafii Ramadhan Kiteri,akitoa taarifa ya zoezi la oparesheni Tokomeza uvuvi haramu.Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bi Janneth Mobe akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasalala.

Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akizungumza na wananchi wa kijiji cha nyasalala juu ya wao kutoa ushirikiano kwa serikali katika kupambana na uvuvi haramu.

Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akizungumza.

Afisa mfawidhi udhibiti  ubora wa samaki  na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita  Shafii Ramadhan Kiteri,akimwonesha mkuu wa Mkoa nyavu aina ya dududu ambazo zimekuwa zikitumika kuvulia samaki ambao wanakuwa bado awajafikia muda wa kuvuliwa.


Zoezi la uchomaji wa dhana hizo za uvuvi likiendelea.

                         IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE BLOG
WITO  umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo Mkoani Humo.

Rai hiyo imetolewa  na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu  Ezekiel Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi  kwenye  Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala  kata ya Bukondo   zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.

Aidha mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani  endapo uvuvi haramu ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika ziwa.

“Ndugu wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema Kyunga

Hata hivyo katibu wa BMU mwalo wa Daladala,Methusela   Samweli amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa ambayo wanapambana nazo katika zoezi la kutokomeza uvuvi haramu ni  kukosekana kwa vitendea kazi ikiwemo kukosekana kwa Boti kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha ambao utasaidia usalama wakati wa doria.

Karoli Makoba na Baraka Mkwazu ni wananchi ambao wapo kwenye mwalo huo wameiomba serikali na BMU kuweka uhusiano wa karibu kwa kushirikiano hili kutokomeza tatizo la uvuvi haramu ambalo limeendelea kushamiri kwa kasi kubwa hususani kwenye mialo ya Izumacheli  na Mganza.

Kwa mujibu wa maelezo ya afisa mfawidhi udhibiti  ubora wa samaki  na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita  Shafii Ramadhan Kiteri,ameelezea  kuwa Doria ambayo imefanyika kwa miezi miwili  imefanikisha kukamata jumla ya samaki wachanga  ambao  Kg 7,682,Mitumbwi 19,watuhumiwa 12,gari moja Hiace na Gari ya pili aina ya Fuso Tandam,pikipiki 3,Nyavu za makila 1,261,Makokoro ya kuvutwa nchi kavu 23,Dududu 41na Timba 17.

Kiteri ameongezea kuwa Katika  doria  hizo zote kiasi cha shilingi Milion,10,080,000 zimepatikana  ambazo zimetokana na faini mbali mbali ambazo walikuwa wakilipa watuhumiwa