Mbeya City na Simba, zinakutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mechi ya ligi kuu huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo uliopita.
Katika mechi iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, mabao ya Simba yalifungwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ na Ibrahim Ajibu.
Ngassa alisema kwa maandalizi waliyoyafanya chini ya Kocha Kinnah Phiri, anaamini yanatosha kuwapa ushindi kwenye mchezo huo.
Ngassa alisema, hawataki kupoteza mchezo dhidi ya Simba kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo baada ya kupoteza 'Mbeya Derby' na Tanzania Prisons waliovaana nao katika Kombe la FA ambao walitolewa kwa mikwaju ya penalti.
“Sitaki kutoa ahadi ya mabao tutakayoshinda na badala yake mimi binafsi nitaipambania timu yangu kuhakikisha tunaibuka na ushindi ili tumalize ligi kuu tukiwa katika nafasi nzuri.
"Simba ni timu ya kawaida kama zilivyokuwa timu nyingine na kwa bahati nzuri timu hiyo niliwahi kuichezea, hivyo ninawafahamu nusu ya wachezaji niliokuwa nacheza nao pamoja,” alisema Ngassa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.