ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 30, 2010

BREAKING NEWS: MZIRAY KATUTOKA.



"KWAHERI MZIRAY"

HABARI ZIMEINGIA ASUBUHI HII ZINASEMA SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA AKISUMBULIWA NA MALARIA.

SUPER COACH MZIRAY, ALIYEKUWA MWAJIRIWA WA CHUO KIKUU HURIA KAMA MHADHIRI, ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI SOKA KATIKA VILABU MBALIMBALI HADI TIMU YA TAIFA ILIYOSHINDA UBINGWA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. ALIFUNDISHA PIA PLISNER, SIMBA, YANGA, PAN AFRICAN NA KABLA YA MAUTI KUMKUTA ALIKUWA MWALIMU WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA WA KLABU YA SIMBA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA MSIBA HUU MZITO AMBAO NI PIGO KWA TASNIA YA MICHEZO NCHINI UKIZINGATIA KUWA TUNA MAKOCHA WACHACHE WALIOSOMEA FANI HIYO NA KUBOBEA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALA PEMA PEPONI
AMEN.

HEREEEEeee! JINA LANGU LIMO-MO FAZA!!!!

ILI KUWA MFANO KWA WATANZANIA WENZANGU, KUITUMIA HAKI YANGU YA MSINGI NA KUHAKIKISHA KWAMBA KILE NINACHOKISEMA NDICHO NINACHO KITENDA, ASUBUHI YA LEO MGUU KWA MGUU HADI OFISI ZA MTENDAJI KATA YA KIRUMBA KUHAKIKI KAMA JINA LANGU NALO LIMO KWENYE ORODHA YA WAPIGA KURA ILI KUEPUKA USUMBUFU HIYO KESHO.
SIKUFANIKIWA KATIKA KITUO HIKI KUONA JINA LANGU NDIPO NIKASHAURIWA NA WASAIDIZI KWENDA ENEO NILILO JIANDIKISHA KITAMBULISHO CHA KUPIGA KURA (SHULE YA M/S MWENGE).

MARA KABAaa! PALE KATI JINA LANGU LILILO ZUNGUSHIWA WINO.

WANANCHI WA KIRUMBA WILAYA YA ILEMELA JIJINI MWANZA WAKITIZAMA KWA MAKINI KUHAKIKI MAJINA YAO NA VITUO VYA KUPIGIA KURA.

WEKA HISTORIA PIGA KURA KWANI NI HAKI YAKO YA MSINGI.

Friday, October 29, 2010

WAPIGA KURA NENDENI MKAHAKIKI MAJINA YENU.

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU MBILI KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU, TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC), TAYARI IMEBANDIKA MAJINA YA WATU WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA KATIKA VITUO MBALIMBALI KOTE NCHINI ILI WAPIGA KURA HAO WAWEZE KUYAHAKIKI. LENGO HASA LA ZOEZI HILO MUHIMU NI KUHAKIKISHA KWAMBA IWAPO KUNA WATU AMBAO MAJINA YAO YAMESAHAULIKA KWA SABABU MOJA AMA NYINGINE WATOE TAARIFA NEC ILI IWEZE KUREKEBISHA KASORO HIYO KABLA YA SIKU YA KUPIGA KURA.

TUNASEMA ZOEZI HILO NI MUHIMU KWASABABU NYINGINE MBILI ZIFUATAZO: KWANZA, LINAMSAIDIA MPIGAKURA KUGUNDUA MAPEMA MAHALI ATAKAPOPIGIA KURA BADALA YA KUHANGAIKA KUTAFUTA KITUO HICHO MWISHO WA SIKU. PILI, ZOEZI HILO LINASAIDIA WAPIGAKURA KUBADILISHANA MAWAZO KUHUSU MAJINA WANAYOYATILIA SHAKA, HIVYO WAKIWA KAMA RAIA WEMA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI YAONDOLEWE KWENYE ORODHA YA WAPIGA KURA.
HIVI WALE MGAMBO WA JIJI WAKO LIKIZOoooo nini? AU...

NITAKUPA RIPOTI MARA BAADA YA UCHAGUZI.

NI NYERERE ROAD MWANZA 'MAKILAKINGA FRENGWA' UNAPATA (BIDHAA ZOTE).

Thursday, October 28, 2010

TSUNAMI INDONESIA : WALIOKUFA SASA NI 282

IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KUFWATIA TSUNAMI KATIKA VISIWA VYA NCHINI INDONESIA IMEONGEZEKA HADI KUFIKIA WATU 282,MAAFISA WAMESEMA.

VIKOSI VYA UOKOAJI KATIKA VISIWA VYA MENTAWAI WAMESEMA MAMIA YA WATU BADO HAWAJULIKANI WALIPO, SIKU MBILI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI KUSABABISHA TSUNAMI MAGHARIBI MWA SUMATRA.

MAAFISA WANASEMA KULIKUWA NA MATATIZO KATIKA MTAMBO ULIOTENGENEZWA KWA LENGO LA KUTOA TAHADHARI KWA WAKAAZI JUU YA KUZIDI KWA MAWIMBI.

RAIS WA INDONESIA SUSILO BAMBANG YUDHOYONO AMEKATIZA ZIARA YAKE YA NCHINI VIETNAM ILI AWEZE KUTEMBELEA VISIWA HIVYO PAMOJA NA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA UOKOZI. RAIS HUYO ANATARAJIWA KUZURU ENEO HILO SIKU YA ALHAMISI KUTATHMINI JUHUDI ZA MISAADA.



PIA ATAELEZWA KUHUSU UOKOAJI KATIKA ENEO LA JAVA, AMBALO MLIPUKO WA VOLCANO UMESABABISHA MAAFA.

HAPPY BIRTHDAY BROO.

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA bwashee' EDGAR J.MAPANDE WA ZANTEL DAR, BLOG HII INAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAISHA, MAZINGIRA NA MAENDELEO. MUNGU AKUONGEZEE MARAFIKI, AKUEPUSHE NA MAADUI.
UMEZALIWA SIKU MOJA NA RAIS WA SASA WA IRAN (WA 6) BWANA MAHAMOUD AHMADINEJAD MZAWA WA TAREHE 28.OCT.1956, PAMOJA NAE MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA PRINCE BAINA KAMUKULU.
HAIJAISHIA HAPO VILE VILE NI SIKU MOJA NA 'MZEE WA KUKU' BILL GATES. (picha ndogo kulia)

HAPPY BIRTHDAY BRAZAz.

Wednesday, October 27, 2010

TUKIO LA MAUAJI NA UPORAJI UKEREWE, JAMBAZI MOJA LAKAMATWA.

MNAMO TAREHE 24/10/2010 MAJIRA YA SAA 20:00 HUKO KATIKA KISIWA CHA NANSIO UKEREWE KATIKA ENEO LA KISIMA CHA MAFUTA KINACHOMILIKIWA NA MFANYABIASHARA CHACHA KANENE (43), KUNDI LA WATU WA 5 WAKIWA NA BUNDUKI MOJA AINA YA SMG NA MAPANGA WALIWAVAMIA WALINZI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO CHA MAFUTA NA KUWATEKA KISHA KUMUUA MAREHEMU JITIHADA IBRAHIM MWAIPOPO NA KUMJERUHI KWA KUMPIGA RISASI YA KISIGINO MGUU WA KULIA BW. CLEOPHAS HAMISI AMBAYE NI MTEJA DEREVA WA PIKIPIKI NO T811BGA.

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUWATEKA WALINZI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO NA KUPORA SH. 1,200,000/= ZIKIWA NI MAUZO YA SIKU KUANZIA SAA 10 JIONI HADI MUDA HUO SAA 2 USIKU.

MARA BAADA YA TUKIO HILO KUFIKA KITUO CHA POLISI UKEREWE, POLISI WALIANZA UFUATILIAJI NA MNAMO TAREHE 25/10/2010 IKIWA NI SIKU YA PILI MARA BAADA YA TUKIO WALIFANIKIWA KUMKAMATA FRANSIS BHOKE AKA MASELO (33) KABILA MKURYA MKAZI WA KIJIJI CHA MAGOLO TARIME MKOANI MARA AKIWA NA BUNDUKI AINA YA SMG YENYE NAMBA 56-390-10-27 IKIWA NA MAGAZINE YENYE RISASI 10 NDANI, MAKASHA MATATU YALIYOTUMIKA, MAPANGA MANNE, MAKOTI MATATU NA KOFIA TATU AINA YA SOX VYOTE HIVI VIKIWA NDANI YA BEGI.

MTUHUMIWA MARA BAADA YA KUKAMATWA NA KUHOJIWA ALIKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO IKIWA NI PAMOJA NA KUHUSIKA NA MATUKIO YA UJAMBAZI UKEREWE NA MIKOA YA SINGIDA, DODOMA NA ARUSHA.

JESHI LA MKOA WA MWANZA LINATOA PONGEZI KWA WANANCHI WA WILAYA YA UKEREWE KWA USHIRIKIANO WALIOUONYESHA.

HOFU YA AJALI FEKI YALIKUMBA JIJI LA MWANZA . WANANCHI WAHAHA KUSAKA NDUGU ZAO WASAFIRI.

MARA BAADA YA TAARIFA ZA KUANGUKA KWA NDEGE HALI TETE YA SINTOFAHAMU PAMOJA NA HOFU VIMELIKUMBA LEO JIJI LA MWANZA. TAARIFA HIZO ZILIZO CHAGIZWA NA PILIKA PILIKA ZA MAGARI YA WAGONJWA KUTOKA ENEO LA TUKIO ZILIMEUSHITUA MJI NA VITONGOJI VYAKE HALI ILIYOSABABISHA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUJAA WANANCHI KUTAZAMA EITHER NDUGU ZAO AU PENGINE KUPATA TAARIFA IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA NINI CHANZO CHA AJALI.

ILINIBIDI KUSITISHA SHUGHULI NILIYOKUWA NIKIIFANYA MARA BAADA YA KUPATA TAARIFA ZISIZO NA MWELEKEO, WATU WAKIDAI NDEGE IMEANGUKA AIR PORT WAKATI IKITUA, WENGINE WAKIDAI KWAMBA KAMBI YA JESHI ILIYOPO KARIBU NA VIWANJA HIVYO IMEUNGUA, WENGINE WAKIDAI KUWA NDEGE ILIYOKUWA IKIRUKA KUTOKA MWANZA IMEANGUKA MUDA MCHACHE WAKATI IKIONDOKA ALIMURADI KILA MMOJA ALIKUWA NA LAKE (SI UNAJUA TENA WABONGO KWA UWONGO!?)

NAMI KAMA MWANDISHI MWAKILISHI NIKATIMKA MOJA KWA MOJA HADI AIR PORT KWENDA KUCHUKUWA NYUZI.

IKIWA NA NA MWENDO KASI WA KAZI AMBULANCE HII IKIWA NA MIILI YA WATU WALIOIGIZA MAJERUHI, NILIKUTANA NAYO ENEO LA GHANA ILEMELA MWANZA.

MENEJA WA UWANJA WA MWANZA ESTER B. MADALE AKATOA TAARIFA KWAMBA NDEGE YA ABIRIA YENYE USAJILI NAMBA SH-INT INAYOMILIKIWA NA SHIRIKA LA NDEGE LA INTERIOR AIR ILIYOKUWA NA ABIRIA 51 IKITOKEA KIGOMA KUJA MWANZA MAJIRA YA SAA 4:59 IMENGUKA WAKATI IKITUA NA KUUWA WATU 25.

MAJERUHI WENYE HALI MBAYA 15 NA ABIRIA WALIONUSURIKA WENYE HALI YA AFADHALI 11, MENEJA HUYO WA UWANJA AKATAJA KUWA UCHUNGUZI WA AWALI ULIONYESHA KUWA NDEGE HIYO ILIKUWA NA MAFUTA YA KUTOSHA KUMUDU SAFARI YA MASAA MANNE NA HATIMAYE SABABU ZA NDEGE KUANGUKA KWA NDEGE HIYO ZIKATAJWA KUWA NI HITILAFU UPANDE WA INJINI.

MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA TAARIFA YAKE NDIPO MENEJA HUYO WA UWANJA AKATUPA PICTURE HALISI KWAMBA TUKIO HILO LA AJALI HALIKUWA AJALI BALI ILIKUWA NI SEHEMU YA MAZOEZI YA JESHI LA ANGA AIR PORT MWANZA KUPIMWA NI JINSI GANI MAMLAKA HIYO UPANDE WA MWANZA ILIVYOJIPANGA KATIKA UOKOAJI IWAPO AJALI YA NDEGE IKITOKEA NA ZOEZI LIMEKUJA MARA BAADA YA KUTUNUKIWA CHETI CHENYE HADHI YA JUU CHA USALAMA WA ANGA NGAZI YA KIMATAIFA.

PICHANI WAANDISHI WA HABARI. 'WAJANJA WA MUJINI WAINGIZWA MUJINI' TEHE TEHE!! LENGO LA ZOEZI HILO NI KUTAKA KUONA USHIRIKIANO ULIVYO KUTOKA IDARA MBALIMBALI KAMA JESHI LA POLISI, HOSPITALI, UONGOZI WAWILAYA, MKOA NA IDARA MBALIMBALI ZA SERIKALI. KATIKA MKOA WA MWANZA ZOEZI KAMA ILI MARA YA MWISHO LILIFANYIKA MWAKA 2008.

HALI ILIKUWA MBAYA ZAIDI KWA NDUGU WA RUBANI WA NDEGE HIYO HEZRON GOLDEN AMBAYE ALIPATA USUMBUFU KUTOKA KWA MARAFIKI, NDUGU, MAJIRANI NA JAMAA ZAKE WOTE WANAOMFAHAMU NA HATA WAKATI NIKITOKA VIWANJANI HAPO RUBANI HUYO ALIKUWA AKIPOKEA SIMU KWA WATU WANAOMFAHAMU KUJUA HALI YAKE. BAADAE MAMBO YALIKWENDA SAFI...KUMBE ILIKUWA MAZOEZI!

PWEZA MTABIRI PAUL AMEKUFA.

PWEZA ALIYEPATA UMAARUFU MKUBWA WAKATI WA MASHINDANO YA KUWANIA KOMBE LA DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI AMEKUFA. SAMAKI HUYO ALIBASHIRI MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA UJERUMANI NCHINI AFRIKA KUSINI NA BAADAE USHINDI WA HISPANIA. BAADA YA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA PWEZA PAUL ALITOKEA KWENYE VIDEO AKIIPIGIA DEBE UINGEREZA KUWA MWENYEJI KOMBE LA DUNIA 2018. KULINGANA NA HIFADHI YA OBERHAUSEN NCHINI UJERUMANI, KIFO CHA PWEZA HUYO ALIYEPEWA JINA LA PAUL NI CHA KAWAIDA.

PWEZA PAUL AMBAYE ALIKUA MAARUFU SANA KATIKA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA KWA KUTABIRI SAWASAWA MATOKEO YA MECHI ZA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI NCHINI AFRIKA KUSINI NA PIA MECHI YA FAINALI, KATIKA UTABIRI WAKE WA MWISHO ALIKUWA AKIONESHA ENGLAND ITAKUWA NA NAFASI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018.
WAKATI HUO HUO HABARI ZINASEMA, ALIYEKUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA DIEGO ARMANDO MARADONA AMEFURAHI SANA KUFA KWA PWEZA HUYO KWANI ALIITABILIA MABAYA ARGENTINA NA HIVYO KUCHEZEA KICHAPO CHA MABAO 4-0 DHIDI YA GERMANY KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2010 AFRIKA KUSINI.

Tuesday, October 26, 2010

JK ALIVYOISHAMBULIA KISAWA SAWA MWANZA LEO JIONI.

MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEWASIHI WANANCHI KUICHAGUA CCM ILI ILI KUTIMIZA SERA ZAKE MADHUBUTI. AKIWA NA FURAHA KWA MAPOKEZI MAZURI MGOMBEA HUYO WA URAIS CCM AMERINDIMA VILIVYO KATIKA VIWANJA VYA SAHARA, WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU TANZANIA ULIOBAKIZA SIKU 5 TU KUFANYIKA.

KATIKA HOTUBA YAKE JAKAYA KIKWETE AMESEMA CHAMA CHAKE HAKITANGAZI SERA ZA KUMWAGA DAMU, KUHUBIRI UDINI WALA KUTUMIANA SMS ZA UCHOCHEZI BALI SMS ZA KUTANGAZA SERA NA MIPANGO YA BAADAE KWA MAENDELEO YA NCHI.

KAMANDA UMETISHAAAAAA!!!! KJ AKITETE NA MGOMBEA WA CCM JIMBO LA NYAMAGANA (UBUNGE) LAU MASHA MARA TU BAADA YA KUTUA VIWANJANI HAPO.

JK AKIMTAMBULISHA KWA WANANCHI MGOMBEA UBUNGE CCM NYAMAGANA LAWRANCE K. MASHA.

HAPA JK AKIMTAMBULISHA KWA WANANCHI MGOMBEA UBUNGE CCM ILEMELA ANTHONY DIALO.

SHAVU LA KUTOSHA PALE ILIPOFIKA ZAMU YA DIWANI WA KATA HUSIKA.

"TUNALO TATIZO LA VIJANA KUTOPENDA SOMO LA SAYANSI, TUNAOMPANGO MADHUBUTI WA KUONGEZA MAABARA ZENYE VIFAA VYA KUTOSHA ILI WANAFUNZI WAJIFUNZE KWA VITENDO NA SI KWA NADHARIA, HIVYO KUREJESHA ARI YA KUPENDA SOMO HILO NA HATIMAYE TUZALISHE WATAALAM." by JK

WAKAGUZI WA KIMATAIFA NAO NDANI.

"WANAOSEMA JK ANAPENDA KUTEMBEA WAJIULIZE, JE! TUNGEPATA VIPI MISAADA YA VITABU KWA MASHULE, UMMEME VIJIJINI, VIPI KUHUSU ZAHANATI VIJIJINI, HATUJAISHIA HAPO UPO MPANGO WA KUBORESHA HUDUMA ZA HOSPITALI YA BUGANDO IWE HOSP YA DARAJA LA JUU"

JIONI IMEINGIA.

HAPA MH.JK AKISALIMIANA NA BABA WA MGOMBEA WA JIMBO LA NYAMAGANA MZEE KEGO MASHA. KABLA YA KUHUTUBIA MKUTANO HUO MKUBWA WA KAMPENI, MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA MHESHIMIWA LAWRENCE KEGO MASHA ALIWAHIMIZA WANANCHI HAO KUWA MAKINI NA VYAMA AMBAVYO HAVITAWALETEA MAENDELEO NA KUWASIHI WATU KUICHAGUA CCM.

TIGO YAZINDUA TAWI JINGINE MWANZA.

MKUU MPYA WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. SAID ALLI AMANZI AKIFUNGUA RASMI OFISI MPYA ZA TIGO JENGO LA CBE MWANZA.

MGENI RASMI ALITOA PONGEZI TIGO KWA KUTUNUKIWA TUZO YA BIDHAA BORA KWA KAMPUNI ZA MAWASILIANO NCHINI NA WATAALAM WA SUPERBRAND, PIA KWA KUTOA MAWASILIANO KWA GHARAMA NAFUU KWA WATANZANIA WOTE SAMBAMBA NA KUTOA AJIRA KWA VIJANA.

TIGO SASA IMETIMIZA JUMLA YA MATAWI 26 NCHI NZIMA, MWANZA IKIWA NA MATAWI MAWILI. PICHANI NI TECHNICAL MANAGER BW. BERNARD.

MGENI RASMI AKITEMBEZWA NDANI YA OFISI HIZO MPYA KUJIONEA BIDHAA MBALIMBALI ZA TIGO.

KATIKA TAWI HILI KUNA IDARA YA HUDAMA KWA WATEJA YENYE WAFANYAKAZI WAPATAO SITA. IDARA YA MASOKO NA USAMBAZAJI YENYE WAFANYAKAZI WAPATAO 12 PAMOJA NA TIMU YA MAUZO YA WATU 200.

ZAWADI KWA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA KUTOKA TAWI JIPYA LA TIGO LILILOPO JENGO LA CBE MWANZA.

KUTOKANA NA MVUTO WA SIMU MPYA TOKA TIGO AMBAZO ZIKO KWENYE PROMO HIVI SASA, MGENI RASMI ALIAMUA KUMNUNULIA MKEWE MOJA YA SIMU HIZO NA HAKUSITA KUTAMKA WAZIWAZI.

PICHA YA PAMOJA WAFANYAKAZI WA TIGO TAWI HILO JIPYA NA MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. SAIDI ALLI AMANZI.

WADAU WA TIGO NA VIPEPERUSHI VYA HUDUMA KWA WATEJA.

TIGO WANASEMA BURUDANI MUHIMU KUKOSHA MACHO.
TIGO IMEAHIDI KUENDELEZA KANUNI YAKE YA KURAHISISHA MAWASILIANO HUKU IKIMWAGA MAAJABU MTAANI.

HUDUMA ZITOLEWAZO NI PAMOJA NA KURUDISHIWA LAINI ILIYOPOTEA, USAJIRI WA NAMBA ZA SIMU, HUDUMA YA TIGO PESA, KUTENGENEZA LAINI MPYA, KUPATA HUDUMA YA INTANET, KUPATA HUDUMA YA NYIMBO KWENYE SIMU NA MENGINEYO.