IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KUFWATIA TSUNAMI KATIKA VISIWA VYA NCHINI INDONESIA IMEONGEZEKA HADI KUFIKIA WATU 282,MAAFISA WAMESEMA.
VIKOSI VYA UOKOAJI KATIKA VISIWA VYA MENTAWAI WAMESEMA MAMIA YA WATU BADO HAWAJULIKANI WALIPO, SIKU MBILI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI KUSABABISHA TSUNAMI MAGHARIBI MWA SUMATRA.
MAAFISA WANASEMA KULIKUWA NA MATATIZO KATIKA MTAMBO ULIOTENGENEZWA KWA LENGO LA KUTOA TAHADHARI KWA WAKAAZI JUU YA KUZIDI KWA MAWIMBI.
RAIS WA INDONESIA SUSILO BAMBANG YUDHOYONO AMEKATIZA ZIARA YAKE YA NCHINI VIETNAM ILI AWEZE KUTEMBELEA VISIWA HIVYO PAMOJA NA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA UOKOZI. RAIS HUYO ANATARAJIWA KUZURU ENEO HILO SIKU YA ALHAMISI KUTATHMINI JUHUDI ZA MISAADA.
PIA ATAELEZWA KUHUSU UOKOAJI KATIKA ENEO LA JAVA, AMBALO MLIPUKO WA VOLCANO UMESABABISHA MAAFA.
Simba yashindwa kufurukuta fainali
-
Simba ilijipa matumaini kwa bao la mapema la Joshua Mutale dakika ya 17,
lakini kasi ya upande wa Tanzania ilidhibitiwa baada ya beki Yusuf Kagoma
kutolewa...
KOICA Yajenga Maabara ya Kisasa ya 3D ATC
-
Na Woinde Shizza, Arusha
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Korea (KOICA), kimezindua rasmi maabara...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.