ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 3, 2022

ILEMELA FC MABINGWA ANGELINE JIMBO CUP 2022

 NA ALBERT GSENGO

FT Ilemela 3-1 Nyakato Fainali ya Angeline Jimbo Cup 2022 ndani ya dimba la CCM Kirumba. Awali katika mchezo wa utangulizi Machinga Fc wamewacharaza wavuja jasho wenzao Bodaboda Fc bao 2-1

Thursday, September 1, 2022

POLISI WA KIKE ALIYEJIFANYA KAHABA AMVIZIA KIONGOZI KIONGOZI WA GENGE HATARI NA KUMTIA MTEGONI.

 


Polisi katika kaunti ya Muranga wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge hatari linalowahangaisha wakazi. 

John Ngugi Maina aliviziwa kutoka kwa maficho yake ana afisa aliyejifanya kahaba. 

 Afisa wa polisi wa kike kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) ambaye alijifanya kahaba, alimvizia John Ngugi Maina kutoka kwa maficho yake baada ya kukubaliana kufanya biashara usiku huo. 

Ngugi anatuhumiwa kuongoza genge la Jeshi ya Gaica ambalo huendesha oparesheni yake mjini Maragua viunga vyake. Mshukiwa huyo aliwahi kukamatwa mnamo Aprili 21, na kuachiliwa kwa bondi ya KSh 30,000 na Mahakama ya Kigumo. 

Alikuwa amekamatwa kwa kutengeneza na kuuza pombe haramu. 

Ripoti za polisi zilionyesha kuwa genge hilo la uhalifu hutengeneza na kuuza chang'a na dawa zingine za kulevya. 

Nation Africa inaripoti kwamba watu watatu wa genge hilo walikamatwa mnamo Agosti 18 mjini Thika walipofumaniwa baada ya kuwaibia madereva na wasafiri wa miguu wakiwa wamejihami na bastola. 

Hati ya kukamatwa ilitolewa dhidi ya Ngugi kwa kukosa kufika kortini kesi yake ilipokuwa ikitajwa mnamo Julai 26, baada ya kupewa dhamana. "Kwa muda wa mwezi mmoja, mwanamume huyu amekuwa akitoroka, maafisa wetu wakapata taarifa za kijasusi kwamba alikuwa akionekana katika nyumba za madanguro mjini lakini kila tulipokuwa tukijitokeza, hakuwepo," Kamanda wa Polisi wa Murang’a Kusini Alexander Shikondi alidai. 

Mahakama ya Kigumo iliipa kituo cha polisi cha Maragua makataa ya kumkamata mshukiwa huyo kabla ya Septemba 5. 

 Shikondi alisema ilikuwa vigumu kumkamata kiongozi huyo wa genge la uhalifu kwa sababu alikuwa akihamahama sana. Kamanda huyo wa polisi alifichua kuwa Ngugi angeingia kwenye nyumba za madanguro akitumia pikipiki, na kumpeleka kahaba mmoja kwenye maficho yake na kumrudisha. "Tuliamua kutumia udhaifu wake wa kuwatumia makahaba ili kumnasa," polisi huyo alisema. 

Shikondi alisema walimwekea mtego kumnasa baada ya kupata nambari yake ya simu. Afisa wa kike anayehudumu katika makao makuu ya DCI huko Kiambu alitumia nambari hiyo kumpigia mshukiwa na kujitambulisha kama mwanamke ambaye alikutana naye mjini Kenol. 

"Tulikuwa tukifuatilia mazungumzo na ingawa alisita kwanza udhaifu wa mwanamke ulimfanya aache kujificha na kukubali kufika mjini kwa mkutano, akionya kwamba hatakaa muda mrefu," Shikondi alisimulia. Mhalifu huyo alijitokeza, akaegesha pikipiki yake na kujitolea kumnunulia vinywaji afisa huyo mpelelezi. 

"Alisahau kwamba alikuwa mtoro ... alimwongoza mwanamke 'wake' kwenye baa iliyokuwa karibu na kuitisha vinywaji ... Walikuwa wakijiburudisha na kinywaji chao cha pili kila mmoja wakati maafisa watatu walijitokeza na kumfunga pingu. Sasa yuko rumande na ataanza tena kujitetea katika marejeleo yake ya kesi ya jinai 388/22 katika mahakama ya Kigumo,” akasema. 

ZAIDI YA WATOTO LAKI 263 KUPATIWA CHANJO YA POLIO PWANI.

 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Gunini Kamba wa kulia akiwa na mratibu wa chanjo Mkoa wa Pwani Abasi Hincha wa kushoto akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Pwani wakiwa katika mkutano huo kuhusiana na kampeni hiyo ya chanjo ya polio

 Na Victor Masangu,Pwani 


Mkoa wa Pwani unatarajia kuchanja zaidi ya watoto zaidi ya laki 263 chanjo ya ugonjwa wa polio katika kipindi cha kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi Cha siku nne.

Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani Gunini Kamba wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni hiyo ya chanjo ya polio kwa watoto wadogo.


Kamba aliongeza kuwa kampeni hiyo itawahusisha watoto wote wa Mkoa wa Pwani wenye umri chini ya miaka mitano na kwamba Maandalizi yote yanakwenda vizuri katika zoezi hilo la kampeni ya chanjo.

"Tulifanya vizuri katika awamu ya pili kwa kuvuka lengo la uchanjaji kwa asilimia zipatazo 131ya walengwa wote na hivyo tunatarajia pia kufanya vizuri katika awamu ya tatu,"alisema Mganga mkuu.

Pia Kamba alisema kwamba katika kampeni ya kipindi cha nyuma waliweza kupata ushirikiano wa kutosha kwa wananchi pindi walipokuwa wakipita katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani.

Mganga huyo alibainisha kwamba kampeni hiyo itaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuwapatia watoto hao chanjo ambayo itaweza kuwalinda kupata maambukizi ya ugonjwa huo wa Polio.

"Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kwamba kampeni hii itakuwa kwa kipindi cha siku nne na kubwa tumeshafanya hamasa na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo kwa watoto wao,"alisema Kwamba.


Mratibu wa chanjo Mkoa wa Pwani Abasi Incha amebainisha kwamba lengo ni kuhakikisha katika kampeni hiyo ni kuwafikia watoto wote  ambao ni walengwa kuwapatia chanjo hiyo.


"Tuna Imani kwamba katika kampeni hii tutapita katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na kuhakikisha tunatoa matone ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio katika Mkoa wa Pwani na kwamba hii itasaidia watoto kujikinga,"alisema mratibu huyo.

Pia katika hatua nyingine alitoa wito kwa wazazi na walezi Mkoa wa Pwani kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu mbali mbali wa afya ambao watakuwa wakipita katika maeneo yao lengo ikiwa ni kukamilisha zoezi hilo.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo awamu ya tatu inasema kwamba kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza 'polio'

Nao baadhi ya wananchi Mkoa wa Pwani wameishukuru serikali ya Mkoa huo kwa kufanya uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwasaidia watoto kupata maambukizi ya ugonjwa wa Polio.

'MWANZA HOTEL YAUNGUA MOTO' - MKUU WA MKOA ANENA

 NA ALBERT G. SENGO

MWANZA Casino pamoja na klabu maarufu ya burudani ijulikanayo kwa jina la Club Dallas iliyoko katika jengo ya Mwanza Hotel jijini Mwanza vimeteketea kwa moto Jumatano ya tarehe 31 Agosti 2022 kuanzia majira ya saa 1 hadi majira ya saa 4 na dakika kadhaa usiku, huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana. Jicho la camera ya @jembefmtz limekuwashuhuda kwenye eneo hilo likishuhudia baadhi ya maofisa wa Jeshi la cha Zimamoto na Uokoaji wakihaha wakifanya jitihada za kuuzima moto huo ambao ulikuwa na tabia ya kuzimika na kuwaka.



Baadhi ya magari yaliyokuwa yamepaki karibu na eneo hilo la hoteli yaliamuliwa kuondolewa haraka, nalo jeshi la polisi likidhibiti wananchi kusogea karibu na eneo la tukio kwa sababu za kiusalama.
Adam Malima ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na hapa anazungumza..... Bado hakuna taarifa za madhara kwa binadamu zilizoripotiwa.

Tuesday, August 30, 2022

MAHAKAMA YAKATAA KUMWACHILIA MSICHANA ALIYEUA JAMAA ZAKE WANNE HUKU MIILI IKIPANGIWA KUFUKULIWA

 


Mahakama imeamuru kuendelea kuzuiliwa kwa msichana wa miaka 15 ambaye alikamatwa kwa mauaji ya ndugu zake watatu na binamu yake. 

Mahakama imeagiza msichana huyo aendelee kuzuiliwa ili polisi wakamilishe uchunguzi wao. 

Hakimu Mkuu Mkaazi wa Mahakama ya Kikuyu Catherine amekubali ombi la polisi la kumzuilia mshukiwa kwa siku 14 zaidi ili kukamilisha uchunguzi. 

Polisi pia wanapanga kumfanyia uchunguzi wa kiakili msichana huyo ambaye alikiri kutekeleza mauaji hayo. 

Gavana Mwangaza Afichua Alirushiwa Usoni Mayai Yaliyooza Mshukiwa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza atasalia rumande hadi Septemba 12 kesi hiyo itakapotajwa. 

Mshukiwa atekeleza mauaji ya jamaa zake wanne Msicha huyo kutoka Kaunti ya Kiambu alikiri kutekeleza mauaji hayo katika muda wa mwaka mmoja uliopita. 

Mshukiwa pia alikiri kuwa mwezi jana aliua binamu yake, mtoto wa umri wa miezi 20 kwa kumrusha katika kisimani nyumbani kwao katika kijiji cha Gathiga, kaunti ndogo ya Kabete.

 “Pia alikiri kumuua binamu yake a miezi 20 kwa kumrusha katika kisima nyumbani kwao mwzi jana. 

Leo babake alielekea katika kituo cha polisi cha Kikuyu na kuandikisha taarifa dhidi ya msichana huyo akimtuhumu kuua wanawe watatu,” taarifa ya DCI ilisema..

MSANII ALIYETAJWA NA HARMONIZE KUFANYA NAYE KOLABO AACHIA VIDEO AKIWA AMEVALIA SIDIRIA.




Mwanamuziki matata wa nyimbo za Injili Chris Embarambaba amewaacha ndugu zake wengi na yai usoni baada ya kuachia video ya wimbo huo akiwa amevalia sidiria na rinda. Sammy Ondimu alikiri kuhisi kuaibishwa na Embarambamba. 

 Mwimbaji huyo, maarufu kwa kuigiza kupiti kugaa gaa kwenye matope, alitoa wimbo huo Agosti 20, akionyesha Wakenya wamechoshwa na uchaguzi. 

Video hiyo ilianza kwa kumuonyesha akiwa amesimama katika shamba la migomba huku akimuunga mkono rais mteule William Ruto. 

Embarambaba kisha akasema hakuna mrengo wowote wa kisiasa ambao utawalipia watu bili zao huku akitoa wito wa kukomeshwa kwa siasa hizo. 

 "Tuapishe Ruto, tumechoka na siasa. Hata ukipiga kelele ni lazima ukidhi mahitaji ya familia yako," aliimba. Kisha mwanamuziki huyo alitikisa tumbo lake kwa nguvu kabla ya kukimbia kuzunguka bustani kama ilivyo ada yake. 

Sarakasi za Embarambaba zilimfanya afisa wa polisi ambaye hufanya kazi ya uhisani Sammy Ondimu kusema kwa utani kwamba hataki tena kuhusishwa na jamii ya Wakisii. 

Ondimu alitania kwamba hata alikuwa amebadilisha jina lake la ukoo kwa sababu ya aibu iliyosababishwa na video ya Embarambaba. “Mimi kwangu ni Uasin Gishu. Mimi sio mkisii tena," alisema. "Jina langu ni Sammy Arap Kale.” 

Haya ni baadhi ya maoni ya watu mitandaoni. Kemunto Kemunto: "Huyu sasa amevuka mipaka." 

Anne Kerubo: "Huu sio mzaha tena, huyu sasa ni wazimu kabisa." Delvin Nyaboke: “Mimi najivunia kuwa Mkisii. Sitawahi kujitenga na damu yangu." 

 “Ninawezaje kuwaambia watu kwamba ninatoka katika jamii moja na mtu kamahuyu?”  iliripoti kuwa Embarambamba alimtolea wimbo mpya mkewe, Pheny Osige. Alimthamini kwa kumfulia nguo zake zenye tope.

 "Watu wengi huniuliza ni nani anayefua nguo zangu zenye matope. Ningependa kumshukuru mama wa watoto wangu," aliimba.

SCOTT PARKER ATIMULIWA BAADA YA KICHAPO CHA LIVERPOOL 9-0

Klabu ya Bournemouth imempiga kalamu kocja mkuu Scott Parker mechi nne pekee ndani ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). 

Scott Parker amepigwa kalamu na Bournemouth baada ya mechi nne pekee ndani ya EPL. Chanzo: Getty Images Bournemouth imetimua Parker mwenye umri wa miaka 41 baada ya kutandikwa 9-0 na Liverpool mnamo Jumamosi huku mmiliki wa Maxim Demin akitoa wito wa umoja katika klabu hiyo. 

Japokuwa Parker aliongeza Bournemouth kurejea EPL katika msimu wake wa kwanza, uhusiano wake na uongozi ulikuwa umedorora baada ya klabu hiyo kufulia katika dirisha hili la uhamisho. “Ningependa kumshukuru Scott na kikosi chake kwa kujitolea kwake wakati akiwa na sisi. Kurejea kwetu EPL kutakumbukwa kama moja ya misimu bora zaidi katika historia yetu. 

Hata hivyo, ili kuendelea kupiga hatua kama timu na klabu kwa jumla, haina mjadala kwanza tukarabati mbinu zetu ili kuendesha klabu kwa njia tunayoweza kumudu,” Denim alisema kupitia kwa taarifa. 

Suala la ununuzi wa wachezaji wapya limeonekana kuwa kubwa, Parker akioneka kukosana na uongozi wa klabu hiyo kwa kumfeli. 

Hata hivyo mmiliki anasema kuwa klabu hiyo haitabadili jinsi ya kufanya mambo yake na kwamba mchakato wa kumsaka kocha mpya umeanza mara moja. “Lazima tuonyeshane imani na heshima. Hii ndio mbinu ambayo imeleta ufanisi katika klabu hii na hatutaibadili mbinu hii,” Denim aliongeza. 

UKICHUKULIA POA TATIZO LA MACHO ULILONALO HUENDA UKAWA KIPOFU KAMA HUYU.

 1. Wengi tunazaliwa na uono safi na maridadi kabisa, lakini kadri miaka inavyosonga uono wa awali unapotea na kutofautiana na wa zama hizi za ukubwani, huyu atasema sioni mbali naona karibu, yule atasema naona mbali sioni karibu, lakini chaajabu wengi huchukulia jambo hilo kama suala la kawaida tu.... Jeh unajua nini kinachotokea hapa?

2. Upi mwanga mzuri kwaajili ya kujisomea hasa majira ya usiku? 3. Zipi faida za kuwahi kupata tiba kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi? 4. Hivi presha ya macho iko vipi na inasababishwa na nini. Ungana na Dr. Emmanuel Ezekiel wa 'Ona Eye Care' ambaye tumepata kufanya mazungumzo naye katika maonesho ya Biashara yanayofanyika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza.

TANGA PRESS CLUB WAFANYA BONANZA LA KUHAMASISHA SENSA NA KUTAMBUA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI

 Vuta kamba' shindano liliendelea.MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa bonanza hilo kushoto ni Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akifuatiiwa na Bondia Mwakinyo na Afisa Michezo Mkoa wa Tanga Digna TeshaMKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kulia akiwa na Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George na Bondia Hassani Mwakinyo wakifuatilia bonanza hilo

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizungyumza wakati wa bonanza hilo

 Na Mwandishi Wetu,TANGA.

Bonanza la Mama Tumeikita lenye lengo la kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Tanga ikiwemo kutambua jitihaza za Rais Samia Suluhu katika maendeleo ya Taifa hapa .

Bonanza hilo ambalo liliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga *TPC*limefanyika mwishoni mwa wiki Jijini Tanga kwenye viwanja vya Disuza kwa kushirikisha viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo Mkuu wa Mkoa Mgumba alisema aliupongeza uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga chini ya Mwenyekiti wake Lulu George kwa kuanza na kuratibu bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake.

Alisema ubunifu ambao umefanywa na uongozi wa klabu hiyo unapaswa kuungwa mkono huku akisema bonanza hilo limefanikiwa sana  huku akiwataka viongozi hao kuhakikisha linakuwa endelevu mara kwa mara na kuwahaidi ushirikiano.

“Niwapongeze Tanga Press Club kwa ubunifu huu mkubwa mlioufanya kwa kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi na kutambua juhudi za Rais kuwaletea maendeleo wa Tanga limefanikiwa sana nimpongeza Mwenyekiti wa TPC na viongozi wengine kwa kufanikisha bonanza hilo ambalo limewakutanisha pamoja wanajamii wote wa Tanga,viongozi wa mkoa wilaya mpaka vitongoji na waandishi wa habari”Alisema

Alisema kwamba amefurahishwa kwamba na kupendwa na ujumbe uliobebwa kwenye bonanza hilo mama huku akisisitiza umuhimu wa jamii ya wana Tanga kuhakikisha wanaendelea kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi ikiwemo kuendelea kuwahabarisha wana Tanga.

Awali akizungumza wakati wa Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliushukuru uongozi wa Tanga Press Club kuweza kuliandaa bonanza hilo ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali kuishiriki katika michezo ambayo ni muhimu kiafya.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka waandishi wa habari mkoani humo waendelee kuboresha mahusiano baina yao kwa wao na taasisi mbalimbali za serikali na kupitia wao wanaweza kuwa na mabonanza mbalimbali huku akiwaomba waone umuhimu wa kufanya hivyo.

Monday, August 29, 2022

RC SERUKAMBA ATUA IKUNGI UKAGUZI SENSA

Mkuu wa mkoa wa singida Mhe. Peter Serukamba ameridhishwa na jinsi wilaya ya ikungi inayoendesha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 na kuitaka wilaya leo jumamosi tarehe 27/08/2022 wamalize zoezi lote la sensa ya watu na makazi 


Rc Serukamba amesema kama mpaka sasa wilaya imeshafikisha zaidi ya asilimia 85 kwa kuandikisha kaya zaidi ya elfu 51 kuna uwezokano mkubwa wakamaliza zoezi hilo mapema iwezekanavyo


Wakati huo huo Rc Serukamba amewataka wasimamizi na waratibu wa sensa ikungi kuwahamisha makarani waliomaliza katika maeneo yao na kuwapeleka kwenda kuongeza nguvu katika maeneo ambayo hayajafikiwa na yana idadi kubwa ya kaya uku zingine zikiwa kwenye umbali kufikiwa 


Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Ndugu Justice Kijazi amemuhakikishia Rc Serukamba kuwa zoezi litakwenda vizuri na litamalizika katika muda uliopangwa na kwa uadilifu mkubwa 











 Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi