Mwanamuziki matata wa nyimbo za Injili Chris Embarambaba amewaacha ndugu zake wengi na yai usoni baada ya kuachia video ya wimbo huo akiwa amevalia sidiria na rinda. Sammy Ondimu alikiri kuhisi kuaibishwa na Embarambamba. Mwimbaji huyo, maarufu kwa kuigiza kupiti kugaa gaa kwenye matope, alitoa wimbo huo Agosti 20, akionyesha Wakenya wamechoshwa na uchaguzi. Video hiyo ilianza kwa kumuonyesha akiwa amesimama katika shamba la migomba huku akimuunga mkono rais mteule William Ruto.
Embarambaba kisha akasema hakuna mrengo wowote wa kisiasa ambao utawalipia watu bili zao huku akitoa wito wa kukomeshwa kwa siasa hizo.
"Tuapishe Ruto, tumechoka na siasa. Hata ukipiga kelele ni lazima ukidhi mahitaji ya familia yako," aliimba. Kisha mwanamuziki huyo alitikisa tumbo lake kwa nguvu kabla ya kukimbia kuzunguka bustani kama ilivyo ada yake.
Sarakasi za Embarambaba zilimfanya afisa wa polisi ambaye hufanya kazi ya uhisani Sammy Ondimu kusema kwa utani kwamba hataki tena kuhusishwa na jamii ya Wakisii.
Ondimu alitania kwamba hata alikuwa amebadilisha jina lake la ukoo kwa sababu ya aibu iliyosababishwa na video ya Embarambaba. “Mimi kwangu ni Uasin Gishu. Mimi sio mkisii tena," alisema. "Jina langu ni Sammy Arap Kale.”
Haya ni baadhi ya maoni ya watu mitandaoni. Kemunto Kemunto: "Huyu sasa amevuka mipaka."
Anne Kerubo: "Huu sio mzaha tena, huyu sasa ni wazimu kabisa." Delvin Nyaboke: “Mimi najivunia kuwa Mkisii. Sitawahi kujitenga na damu yangu."
“Ninawezaje kuwaambia watu kwamba ninatoka katika jamii moja na mtu kamahuyu?” iliripoti kuwa Embarambamba alimtolea wimbo mpya mkewe, Pheny Osige. Alimthamini kwa kumfulia nguo zake zenye tope.
"Watu wengi huniuliza ni nani anayefua nguo zangu zenye matope. Ningependa kumshukuru mama wa watoto wangu," aliimba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.