ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 30, 2022

SCOTT PARKER ATIMULIWA BAADA YA KICHAPO CHA LIVERPOOL 9-0

Klabu ya Bournemouth imempiga kalamu kocja mkuu Scott Parker mechi nne pekee ndani ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). 

Scott Parker amepigwa kalamu na Bournemouth baada ya mechi nne pekee ndani ya EPL. Chanzo: Getty Images Bournemouth imetimua Parker mwenye umri wa miaka 41 baada ya kutandikwa 9-0 na Liverpool mnamo Jumamosi huku mmiliki wa Maxim Demin akitoa wito wa umoja katika klabu hiyo. 

Japokuwa Parker aliongeza Bournemouth kurejea EPL katika msimu wake wa kwanza, uhusiano wake na uongozi ulikuwa umedorora baada ya klabu hiyo kufulia katika dirisha hili la uhamisho. “Ningependa kumshukuru Scott na kikosi chake kwa kujitolea kwake wakati akiwa na sisi. Kurejea kwetu EPL kutakumbukwa kama moja ya misimu bora zaidi katika historia yetu. 

Hata hivyo, ili kuendelea kupiga hatua kama timu na klabu kwa jumla, haina mjadala kwanza tukarabati mbinu zetu ili kuendesha klabu kwa njia tunayoweza kumudu,” Denim alisema kupitia kwa taarifa. 

Suala la ununuzi wa wachezaji wapya limeonekana kuwa kubwa, Parker akioneka kukosana na uongozi wa klabu hiyo kwa kumfeli. 

Hata hivyo mmiliki anasema kuwa klabu hiyo haitabadili jinsi ya kufanya mambo yake na kwamba mchakato wa kumsaka kocha mpya umeanza mara moja. “Lazima tuonyeshane imani na heshima. Hii ndio mbinu ambayo imeleta ufanisi katika klabu hii na hatutaibadili mbinu hii,” Denim aliongeza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.