ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 1, 2010

MH!

USIKU

PILIKA ZA MCHANA.

ANGANI WANAKULA WANAISHI.

Friday, April 30, 2010

FRIENDZ AYEYAA!


MSHIKAJ ANAITWA CHIDY J. UKIPENDA RASHID JUMA HAPA DUNIANI ANAPIGA MZIGO KAMA IT, PLACE YA WORK NI PALE CORNER INTERNET CAFE INAYOPATIKANA KENYATA RD ROCK CITY. MCHESHI, MSTAARAB NA MCHAPAKAZI WA UKWELI.

APIGWA HADI KUFA

LEO HII MAJIRA YA SAA TANO ASUBUHI KIJANA MMOJA ANAYE SADIKIKA KUWA NI KIBAKA AMEPIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA HADI KUFA, MARA BAADA YA KUMTISHIA KWA KISU MAMA MMOJA ALIYEKUWA AKITOKA BENKI MOJA WAPO KATIKA BARABARA YA NYERERE JIJINI MWANZA.

TUKIO HILI LILILOTOKEA KATIKATI YA BARABARA LILISABABISHA MSONGAMANO WA MAGARI. KUTOKANA NA UMATI WA WATU ULIOZINGIRA MWILI WA KIJANA HUYO.

INASEMEKANA KIBAKA HUYU WAKATI ALIPOKUWA AKIMNYANG'ANYA KWA NGUVU MKOBA ALOKUWA AMEBEBA MAMA HUYO, ALIKUWA AKIMCHANA CHANA NA KISU HATA MAMA ASIUACHIE MKOBA, NDIPO KIBAKA ALIPOAMUA KUUKATA MKANDA WA MKOBA NA KUUVUTA KISHA KUKIMBILIA KUPANDA PIKIPIKI ILOKUWA NA DREVA AKIMSUBIRI.

MSIMULIAJI MMOJA KANINYETISHIA " MAMA YULE ALIPIGA KELELE ZA MWIZI! MWIZIIII! KIJANA MMOJA PEMBENI AKAMUWAHI ASIPANDE PIKIPIKI, AKAMPIGA NGWARA KIBAKA, PANGA KULE, MAMA AKACHUKUA POCHI YAKE NA KUKIMBILIA JIRANI NA HAPA PALEEE HOSPITALI YA IJUMAA KUPATA MATIBABU, HUKU NYUMA WANANCHI SIUNAJUA ZETU TUKAMALIZA"

JIWE LILILO MMALIZA KABISA KIJANA HUYO.

GARI LA POLISI LIKIONDOKA ENEO LA TUKIO NA MWILI.

Thursday, April 29, 2010

IKO HIVI....

BALAA LA MVUA SI POLE POLE, CHANZO KIKUBWA HAPA NI UFINYU WA MIUNDOMBINU. HATOKI MTU HAINGII MTU HAPA! KUMBI MBILI MAARUFU ZA BURUDANI JIJINI MWANZA VILLA PARK NA KISS CLUB.

OYAA...SIYO SAMAKI HAO!


SAMAKI HAWA WA BANDIA WALIO NING'INIZWA KAMA PAMBO PALE JIKONI MWA VILLA PARK WAMENONA KIASI CHA KUTUTIA HAMU. MWANZA NOW DAYS SANAMU ZA SAMAKI KILA KONA BUSTANINI HADI JIKONI....

ZOEZI LA AFYA....

HIVI KARIBUNI KUMEFANYIKA ZOEZI LA UKAGUZI WA HUDUMA ZA AFYA AMBAPO ZAHANATI, MAABARA NA MADUKA YA DAWA YAMEKAGULIWA NA MENGI YAMEFUNGWA KWA SABABU MBALIMBALI. UKAGUZI HUU NI WA KHERI KWANI UMEFANYIKA KWA MUJIBU WA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI ZILIZOWEKWA ILI KUHAKIKISHA HUDUMA ZINZFANYIKA KWA MISINGI ILIYOWEKWA.

KUPITIA ZOEZI HILI KUMEJITOKEZA TATIZO LA WATU KUKOSA MAHALA PA KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU, VIPIMO NA DAWA KWASABABU YA KUFUNGWA KWA VITUO HIVI KIMBILIO LA WANANCHI WENGI.

ZOEZI HILI NI CHANGAMOTO KWA WAMILIKI KUBORESHA HUDUMA ILI WAPATE KURUDI KUWAHUDUMIA WANANCHI.

SI AJABU INAPOTOKEA WAKAGUZI WAKACHUKUA MUDA MREFU BILA KUZIFANYIA UKAGUZI HUDUMA HIZI, WENGI HUJISAHAU NA KUANZA KUKIUKA MISINGI BORA YA UTOAJI HUDUMA KWA KULIPUA ILI WAPATE FAIDA. MAZINGIRA MABOVU YA UTOLEWAJI HUDUMA, UKOSEFU WA WAHUDUMU WENYE SIFA NA KUKOSA VIBALI VYA KUTOA HUDUMA NDIZO SABABU HASA. PLIZ WAHUSIKA FANYENI UKAGUZI MARA KWA MARA KUWAFANYA WAHUSIKA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA AFYA.

Wednesday, April 28, 2010

CCM KAMBARAGE SHINYANGA UWANJA AU SHAMBA LA NYASI?

NAKUMBUKA WAKATI TIMU YA SOKA BIASHARA SHINYANGA PINDI INASHUKA DARAJA WAKAZI WAKE WALISEMA UWANJA HUU HAUTOKUWA NA KAZI TENA ZAIDI YA KUCHEZEA NGOMA ZA MAKABILA NA KULIMA NYASI KULISHIA NG'OMBE. JE! MANENO HAYO YALIKUWA NA DHAMIRA NDANI YAKE?

MASHABIKI WAKIPITA NDANI, PEMBEZONI MWA PLAY GROUND KUELEKEA JUKWAANI.

ENEO LA NETBALL NDANI YA UWANJA HUO.

MIAKA YA NYUMA MOJA KATI YA VIWANJA VILIVYOKUWA NA HADHI YA KIPEKEE UWANJA HUU WENYE JINA LA HAYATI BABA WA TAIFA ULIKUWA MMOJA WAPO, KWANI MBALI NA MWONEKANO, VILEVILE ULIKUWA NA SIFA YA USAFI NDANI NA NJE. LAKINI LEO MMMMMH.

Tuesday, April 27, 2010

YA LEO LEO.

MCHIZI HUYU ALIPIGA MBONJI KTK BARABARA YA BALEWA. MPAKA ANAOTA..

BIDADA HAIJULIKANI USIKU WAKE ULIKUWAJE?! KWANI MAENEO HAYA YA KIRUMBA MZ. KUNA KUMBI MBILI ZA BURUDANI MAARUFU, LAKINI MWISHO WA SIKU YEYE ALIPACHAGU HAPA KAMA KITANDA, SHUKA NGUMI!


HATUKATAI USINGIZI POPOTE. JEH! KWA ENGO KAMA HII IMEKAA VIJE?

Monday, April 26, 2010

VILIO, HUZUNI NA SIMANZI VYATAWALA MSIBA WA BABA WA MISS TANZANIA. MKE, NDUGU WAZIRAI...

MWILI WA MAREHEMU GERALD UKIWASILI NYUMBANI KWAKE KWAAJILI YA TARATIBU ZA IBADA YA MAZISHI.

MKE WA MAREHEMU ALISHINDWA KUJIZUIA KWANI ALIZIMIA MARA TU BAADA YA KUONA JENEZA LA MUMEWE LIKIINGIA NYUMBANI KWAAJILI YA IBADA.

BAADA YA MUDA MAMA ALIREJEA KATIKA HALI YA KAWAIDA NA KUENDELEA NA IBADA.

FAMILIA YA MAREHEMU NA NDUGU ZAKE IBADANI.

MARAFIKI KATIKA HARAKATI ZA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO.

"AAH! BABA UMEKWENDA?" HAKIKA MIRIAM AMEPATA WAKATI MGUMU.

MTOTO WA MAREHEMU AMBAYE NI MISS TZ 2009-2010 MIRIAM GERALD AKITOA HESHIMA ZAKE MBELE YA MWILI WA BABA YAKE.

UMMA ULIOHUDHURIA MSIBA HUU ULIKUWA NA WAKATI MGUMU KUSIKILIZA MANENO YA KILIO CHA BINTI HUYU.... KILICHOBAKI KWA SISI TULIO BAKIA KUJIPA MOYO WA MATUMAINI NA KUJIVIKA UJASIRI.

MIRIAM ALISHINDWA KUJIZUIA HATA KUPEWA MSAADA.

MKE WA MAREHEMU BI.HELEN NAE AKITOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO.

SEHEMU YA UMATI ULIOJITOKEZA.

MWILI WA MAREHEMU HATUA KWA HATUA HADI KWENYE GARI TAYARI KUELEKEA NYUMBA YA MILELE.

SEHEMU YA UMATI ULIOFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU.

GARI LA MISS TZ.


MSAFARA KUTOKA BUGANDO KUELEKEA MAKABURINI ALIKOZIKWA ENEO LA IGOMA JIJINI MWANZA.

Sunday, April 25, 2010

MISS TANZANIA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

pichani marehemu na familia yake


MISS TANZANIA 2009 - 2010 MIRIAM GERALD AMEFIWA NA BABA YAKE MZAZI GERALD BOMANI ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA BASI LA ROBIN TOP LINE EXPRESS ILIYOTOKEA TAREHE 22 APRIL 2010 SAA TISA MCHANA KTK KATA YA TUKAMAHELA KIJIJI CHA KILIMATINDE MANYONI MASHARIKI NA KUUWA WATU WA3. KWA MUJIBU WA KAMANDA WA POLISI MKOANI SINGIDA CELINA KALUBA AMESEMA BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA MWANZA KUELEKEA DAR ES SALAAM LILIGONGANA NA ROLI. MWILI WA MAREHEMU UNAWASILI LEO USIKU JIJINI MWANZA KWAAJILI YA MPANGO WA MAZISHI. BABA HUYU NI MTOTO WA MARTHA BOMANI (DADA WA JAJI PAUL BOMANI) NITAENDELEA KUKUHABARISHA ......

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMEN