ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 29, 2010

ZOEZI LA AFYA....

HIVI KARIBUNI KUMEFANYIKA ZOEZI LA UKAGUZI WA HUDUMA ZA AFYA AMBAPO ZAHANATI, MAABARA NA MADUKA YA DAWA YAMEKAGULIWA NA MENGI YAMEFUNGWA KWA SABABU MBALIMBALI. UKAGUZI HUU NI WA KHERI KWANI UMEFANYIKA KWA MUJIBU WA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI ZILIZOWEKWA ILI KUHAKIKISHA HUDUMA ZINZFANYIKA KWA MISINGI ILIYOWEKWA.

KUPITIA ZOEZI HILI KUMEJITOKEZA TATIZO LA WATU KUKOSA MAHALA PA KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU, VIPIMO NA DAWA KWASABABU YA KUFUNGWA KWA VITUO HIVI KIMBILIO LA WANANCHI WENGI.

ZOEZI HILI NI CHANGAMOTO KWA WAMILIKI KUBORESHA HUDUMA ILI WAPATE KURUDI KUWAHUDUMIA WANANCHI.

SI AJABU INAPOTOKEA WAKAGUZI WAKACHUKUA MUDA MREFU BILA KUZIFANYIA UKAGUZI HUDUMA HIZI, WENGI HUJISAHAU NA KUANZA KUKIUKA MISINGI BORA YA UTOAJI HUDUMA KWA KULIPUA ILI WAPATE FAIDA. MAZINGIRA MABOVU YA UTOLEWAJI HUDUMA, UKOSEFU WA WAHUDUMU WENYE SIFA NA KUKOSA VIBALI VYA KUTOA HUDUMA NDIZO SABABU HASA. PLIZ WAHUSIKA FANYENI UKAGUZI MARA KWA MARA KUWAFANYA WAHUSIKA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA AFYA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.