ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 21, 2017

KANDA YA ZIWA SASA KUMULIKWA USIKU NA MCHANA NA 'SUN KING' SANJARI NA KUWA NA MAZINGIRA SALAMA.

Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mbele), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza na wandishi wa habari kwa maswali ya ufafanuzi kupitia kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Wadau mbalimbali katika kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Mstari wa mbele kusanyiko la uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Kwa umakini kuzingatia yaliyomo.
Sun King.
Kwa umakiini zaidi.
Kusanyikoni.
Mbele ya mjengo uliopo Buzuruga Plaza Mwanza.
Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi,akifunguka juu ya faida na matumizi ya taa za sola.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia) akipokea maelezo kuhusu faida na uimara wa baadhi ya taa za Sun King kupitia jumba la ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa hii leo, kushoto mtoa maelezo ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.


















Wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya Sun King.



Meneja Masoko wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.



“Kila Kijiji nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.



Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana, amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira zaidi kwa vijana.


PROFESA LIPUMBA ATINGA MAHAKAMANI.

Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.

Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.

Maombi hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama wakiwa viongozi halali wa chama hicho, wanaomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kwa kuwa wana masilahi na shauri hilo.

Wakili wa CUF upande wa Katibu Mkuu, Juma Nassoro na Wakili wa Serikali, Hang Chang’a waliieleza mahakama kuwa bado hawajapewa hati za maombi hayo.

Jaji Wilfred Dyansobela aliamuru waombaji hao (kina Lipumba) kuwapatia nyaraka hizo na amepanga kusikiliza maombi hayo Juni 6, siku ambayo kesi ya msingi itatajwa.

KENYATTA AWAONYA WANAOFANYA NJAMA ZA KUVURUGA UCHAGUZI KENYA.


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewaonya watu aliosema wanafanya njama za kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.
Rais Kenyatta amewaambia waandishi wa habari kwamba, hatovumilia kitendo chochote cha kuchochea machafuko na kwamba sheria itamuadhibu vikali mtu yeyote atakayochochea machafuko na kujaribu kuvuruga uchaguzi huo.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 8 Agosti mwaka huu nchini Kenya. Ikumbukwe kuwa nchi hiyo ilishuhudia machafuko mabaya ya umwagaji wa damu baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 27 Disemba 2007. Mamia ya watu waliuawa na wengine wengine kupoteza makazi yao katika machafuko hayo.
Viongozi wa muungano wa NASA nchini Kenya.
Hivi sasa pia hali ya uchaguzi nchini Kenya ni ya wasiwasi kiasi kwamba machafuko yamekuwa yakiripotiwa katika chaguzi za michujo ya wagombea za vyama vya kisiasa nchini humo.
Aidha, hadi hivi sasa muungano wa upinzani wa NASA umeshindwa kutangaza mgombea wao kutokana na kila chama kutaka mkuu wake ateuliwe kugombea urais, suala ambalo linazidisha homa ya uchaguzi nchini humo. Karibu Wakenya milioni 19 wametimiza masharti ya kupiga kura.

MWAKYEMBE AFUKUWA MAKABURI YA ZMANI.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema yuko tayari kuuachia uwaziri ili aweze kulithibitishia Bunge kuwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa alihusika katika kashfa ya Richmond.

Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari na Mbunge wa Ubunge Ubungo (Chadema) Said Kubenea kumtuhumu juzi kuwa hakutenda haki mwaka 2008 wakati alipoongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond bila kumhoji Lowassa ambaye alituhumiwa.


Nassari juzi wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) alisema Dk. Mwakyembe ameikataa ripoti iliyomchunguza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds kwa madai kuwa haikumhoji mkuu huyo wa mkoa ili hali yeye aliendesha Kamati ya Teule ya Bunge ya Richimond na kumuondoa madarakani Lowassa, licha ya kutokumhoji.

Akijibu tuhuma hizo, Dk. Mwakyembe alisema ni kazi ngumu kwa sasa kumsafisha Lowassa kuhusu tuhuma zilizokuwa zinamkabili kuhusu Richmond.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.


Alisema kamati teule iliyoundwa na Bunge la Tisa kazi yake ilikuwa kuchunguza siyo kutoa maamuzi.

Alisema unapochunguza, suala la kusikiliza siyo lazima na ndiyo maana kamati ilikuja bungeni na kuiwasilisha ripoti ikiwa na mashahidi zaidi ya 40 "wakitusubiri nje.

“Aliyetakiwa kuhojiwa bungeni akajiuzulu, unamlaumu Mwakyembe kwa hilo, naomba msipotoshe umma kuwa hakuhojiwa, ahojiwe vipi?
"Unajua ni aibu, ni sawa na mtu anaenda mahakamani anasema unajua polisi hawakunipa haki ya kuhojiwa.

“Polisi? Uko mahakamani... ndiyo pa kuhojiwa hapo, kwa hiyo ndugu zangu mimi naomba tusipotoshe umma, sisi tulikuwa tumepata nyaraka za serikali 104, na tukahoji watu 75, tuliwauliza maswali 2,717 iko kwenye hansard.”

Alisema Kamati haikuona sababu yoyote ya kumuhoji Lowassa kwa kuwa ilikuwa na ushahidi wote.

“Mimi niombe, mheshimiwa mwenyekiti (Andrew Chenge) kama kuna mtu yeyote hapa, bado anakereketwa na kesi ya Richmond, aache maneno maneno hapa, leta hiyo kesi hapa kama hatujawanyoa nywele kwa kipande cha chupa.”

Wakati Dk. Mwakyembe akizungumza hayo, Kubenea aliomba utaratibu kwa Mwenyekiti akidai Dk. Mwakyembe analiongopea bunge.

Kubenea alisema Dk. Mwakyembe akiwa mwenyekiti wa kamati hiyo alieleza kuwa mtu anaweza kujiuzulu kwa mambo mawili, moja kwa kuwa yeye mwenyewe anahusika au mbili kwa kuwajibika kwa mambo yaliyofanywa na walio chini yake.

Alisema Kwa mujibu wa ‘hansard’ (kumbukumbu rasmi za bunge), Dk. Mwakyembe alisema Lowassa alijiuzulu kwa mambo yaliyofanywa na walio chini yake lakini leo anasema ana ushahidi wa asilimia 100 kwamba Lowassa alihusika na jambo hilo.

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kwa idhini yako unipe muda niwasilishe hansard hapa kwenye bunge hili kuthibitisha maneno ya Dk. Mwakyembe ya mwezi Februari mwaka 2008,” alisema Kubenea.

Mara baada ya Kubenea kueleza hayo, Dk. Mwakyembe alisema upinzani hawawezi kumsafisha Lowassa kama madoa ya lami kwa kutumia kamba ya katani au maji, bali warudishe bungeni suala hilo.

Dk. Mwakyembe alimwomba Kubenea kuleta hoja ya Richmond bungeni.

“Ileteni hapa, naomba kwa Mungu mkiileta hapa nitafurahi kwasababu mimi ninachosema hapa na ushahidi nilionao hapa... sisi tulimkuta huyu jamaa amehusika.

"Tupo hapa kuthibitisha hilo suala naomba sana kwa sababu mmekuwa na makubaliano ya kumsafisha, hamtaweza kumsafisha. Leteni kesi hapa.”

MAWAZIRI WAOGA
Dk. Mwakyembe pia alijibu hoja iliyotolewa juzi na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa kuwa mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano ni waoga katika kumshauri Rais Magufuli.BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Dk. Mwakyembe alisema hoja hiyo haina ukweli wowote na kwamba mawaziri wa serikali ya awamu ya tano wanafanya kazi bila wasiwasi.

“Ohoo Mawaziri ni waoga, hawana ujasiri, mimi nimekuwa najiuliza ni ujasiri wa aina gani? wa kumkaidi Waziri Mkuu, wa kumkaidi Rais, ujasiri upi?" Aliuliza.

“Umeona wapi ambapo mawaziri hawaongozwi na kanuni, ya kuwajibika kwa pamoja bungeni katika mfumo wa bunge?"

WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI, ATOA AMRI KULITAKA JESHI LA NCHI HIYO KUJIWEKA TAYARI KUKABILIANA NA PYONGYANG.


Waziri Mkuu wa Korea Kusini anayekaimu nafasi ya rais, amelitaka jeshi na vikosi vya nchi hiyo kujiweka tayari kutokana na kile alichokisema kuwa ni kushadidi kwa harakati za kijeshi za Pyongyang.
Hwang Kyo-ahn ameyasema hayo Alkhamis ya leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri la Korea Kusini kufuatia kuenea kwa habari zinazohusiana na uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio la sita la silaha ya nyuklia hivi karibuni. Kufuatia hali hiyo Hwang Kyo-ahn ametoa amri kwa jeshi la nchi yake kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na hatua yoyote ya kijeshi na harakati za Korea Kaskazini.

Jeshi la Korea Kusini
Kadhalika Waziri Mkuu wa Korea Kusini amelitaka jeshi la nchi hiyo kufuatilia kwa karibu mabadiliko na harakati zote za Pyongyang. Mgogoro katika eneo la Peninsula ya Korea ulishadidi baada ya Rais Donald Trum wa Marekani na makamu wake wa rais, Mike Pence kutoa matamshi ya vitisho kuilenga Pyongyang, vitisho ambavyo vilienda sambamba na kutumwa kwa meli tatu za kijeshi zinazobeba ndege za kivita karibu na pwani ya Korea Kaskazini.

Hwang Kyo-ahn, Waziri Mkuu wa Korea Kusini
Hatua hiyo ya Marekani ilitajwa na Korea Kaskazini kuwa, ya kichokozi na inayohatarisha usalama na amani ya peninsula hiyo. Mbali na hayo ni kwamba Korea Kaskazini imesisitiza mara kadhaa kwamba, madamu Marekani na waitifaki wake zitaendelea kutishia usalama wake, basi nayo itazidi kuimarisha uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na chokochoko za adui.

Thursday, April 20, 2017

MWILI WA MCHEZAJI MAARUFU WA NFL ALIYEJIUA GEREZANI WAKUTWA NA MSTARI WA BIBLIA ULIOANDIKWA KWENYE PAJI LA USO.

Mchezaji maarufu wa FNL Footballer  Aaron Hernandez, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mwaka 2015, amekutwa jana Jumatano (19 April) akiwa amekufa katika chumba chake cha gerezani ikisemekana kuwa amejinyonga kwa kutumia shuka lake za kulalia.

Hernandez aliyekuwa na umri wa miaka 27, hakuacha barua yoyote au kielelezo cha sababu za kujiua kwake, lakini inaripotiwa kuwa aliacha maandishi ya mstari wa biblia kwenye paji la uso wake yaliyoandikwa "John 3:16.

Mstari huo wa Biblia unasema "Kwa maana hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." 

The Washington Post wanaripoti kuwa katika tukio hilo lenye maswali mengi Biblia imepatikana ndani ya selo yake ikiripotiwa kuwa wazi katika ukurasa huo wenye mstari tajwa.
Hernandez alikutwa na kosa la mauaji kupitia tukio la moja la mauaji ya klabu ya usiku nchini marekani ambapo watu walikuwa wakipigana naye kuingilia kati na katika hali hiyo mmoja kati ya waliokuwa wakipigana alikufa kwa kupigwa risasi na ikasemekana Hernandez ndiye aliye fyatua risasi hiyo.

Kesi iliendeshwa kwa muda wa miezi takribani tisa hadi kumi na hatimaye wiki mbili zilizopita makosa mawili yaliondolewa akabaki na makosa matatu kati ya makosa matano aliyokuwa akikabiliana nayo hata hivyo akaendelea kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Jana tarehe 19 Hernandez kapatikana akiwa amejiua ndani ya selo yake, tukio ambalo limezua utata na maswali mengi kwani askari magereza kwa upande wao wanadai kuwa hakukuwa na dalili zozote kwa marehemu kuwa na mpango wa kujitoa uhai wala kufanya tukio lolote la ajabu.

Maafisa wa Souza-Baranowski Correction Center in Shirley walijaribu kuokoa maisha ya Hernandez kwa kumkimbiza UMass-Memorial Health Alliance Hospital iliyoko mjini  Leominster ambako ndiko ilithibitishwa na madaktari kuwa alikuwa amefariki dunia at 4.07am.

Maelezo mengine toka kwa wakuu wa gereza wanasema wamemkuta akiwa amejinyonga ile hali akiwa amejifungia kwa ndani.

Utata umezuka toka kwa ajenti wa Hernandez ambaye pia ni mwanasheria wake aitwaye Jose Baez, akidai kuwa kuna mchezo mchafu umechezwa hapo, kwa sababu kuna mambo mengi yanaonekana kuwa hayajakaa vizuri akihoji "Kwanini ajiuwe kwa muda huu ambapo wiki mbili zilizopita alipatikana kuondoshewa baadhi ya makosa?" Kisha akaongeza "Na kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba huwenda kifungo chake kingelegezwa hapa kuna mbinu mbaya"

"Familia na timu yake ya uangalizi imeshtushwa sana na kushangazwa na taarifa za kifo cha Aaron" 

"Kulikuwa hakuna mazungumzo yoyote aliyofanya na mkewe, mwanawe, dada yake au hata familia yake zilizo ashiria hiki kutokea. Mara zote Aaron alikuwa akizungumza lugha ya matumaini kwamba kuna nafasi nyingine, nafasi yake kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye hakuhusika na mauaji yale" alisema Baez na kuongeza zaidi  "Wote tuliompenda na kumjali tumevunjika mioyo lakini tunasema lazima ukweli ujulikane juu ya kifo chake. Ni imani yetu mamlaka husika zitakusanya taarifa za ukweli kupitia uchunguzi watakaoufanya" alimaliza mwanasheria huyo.

On Friday (14 April), a Boston jury found Hernandez not guilty of the 2012 deaths of two men, Daniel de Abreu and Safiro Furtado. Hernandez was serving a life sentence after being convicted in 2015 of the 2013 death of semi-pro football player Odin Lloyd.

According to the Boston Globe, Hernandez may have died an innocent man in the state of Massachusetts due to an archaic legal principle known as "abatement ab initio". Hernandez was appealing his conviction and because he died before exhausting his legal appeals, his case would revert to its status at the beginning.

Hernandez's appellate attorney, John M Thompson, told the Globe he would file to vacate the conviction. That move could be challenged by the Bristol County District Attorney Thomas M Quinn III's office or the Lloyd family.

STEVE NYERERE - BONGO MOVIE TUACHENI VISINGIZIO VISIVYO NA MAANA.


BAADA ya maandamano ya wasanii wa filamu nchini yaliyofanyika Jumatano hii katika mtaa wa Aggrey Kariakoo, msanii wa tasnia hiyo Steve Mengele Nyerere amefunguka kuhusu tukio hilo.

Akiongea na waandishi wa habari, Steve ameeleza kuwa sababu ya yeye kutokuungana na wasanii wenzake kuandamana ni kwa kuwa jambo hilo halioni kama lina tija kwake.

“Binafsi ninalipinga hili, wasanii tunataka kutumika ndivyo sivyo. Mimi siwezi tu kuambiwa kuwa kuna maandamano nikaenda.

“Tunavyosema filamu za nje zinazuia soko la ndani ni uongo, hizi filamu za nje tangu tunazaliwa zilikuwepo, tumewakuta akina Arnold Schwartzneger na Rambo, filamu zao zilikuwa zinauzwa Kariakoo. Tulizichukua majority tukatengeneza filamu zetu. Tuliwakuta wanigeria tukashindana nao tukaweza, hata filamu za Kihindi tuliweza kushindana nazo.

“Hatujawahi kumzuia Yemi Alade afanye muziki hapa nchini ijapokuwa tuna wanamuziki wetu akina Diamond na Ali Kiba.

“Ninachoweza kusema ni kwamba turudi tuangalie ni wapi tumeharibu, tuache kuingiza visingizio ambavyo havina mantiki. Wafanyabiashara Kariakoo wanauza filamu zinazouza na siyo uzalendo.

“Watanzania tumezoea kukaa mezzani na siyo maandamano. Utazuia Dar, je vipi kuhusu Arusha, Dodoma, Mwanza nk… hili janga sio la Dar es Salaam pekee ni la Tanzania nzima.

“Mpaka sasa msambazaji ni mmoja, aliyelemewa mzigo. Serikali iruhusu wasamazaji wengine wafanye kwenye biashara hii.”

“Tumeshindwa kutengeneza ladha ya Watanzania, tusiwaadhibu wafanyabiashara, tujiadhibu sisi wenyewe kwa kutengeneza filamu zisizouza.” Alisema Steve Nyerere.

VIDEO: JINSI JUVENTUS ILIVYO IONESHA BARCELONA MLANGO WA KUTOKEA



Juventus ambao mara ya mwisho walishinda Champions League mwaka 1996 wame watupa Barcelona nje ya Champions League. Barcelona wameshindwa kuushangaza tena ulimwengu wa soka kama walivyofanya katika hatua ya 16 bora pale walipoipiga Paris St-Germain bao 6-1 ingawa PSG ilikuwa na bao nne kibindoni.

DANNY ALVES AIBUSU LOGO YA BARCELONA MCHEZO WA KWANZA KURUDI NYUMBANI.
 

Sasa Juventus wanaungana na Real Madrid, Atletico Madrid na Monaco katika droo itakayotangazwa kesho.
 DANNY ALVES APATA KIBARUA KIZITO MUMTULIZA NEIMAR ASILIE.

Monaco nayo imeingia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004 baada ya jana kuwabamiza Borussia Dortmund bao tatu kwa moja

TIMU YA PAMOJA YACHANJA MBUGA

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

TIMU ya mpira ya Pamoja Sport Club imeingia mitini kwa kushindwa kuonekana kwenye mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 yanayoendelea kwenye uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana hao

Mashindano yaliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika soka hapo baadae
.
Akizungumza na Gsengo blog Mwenyekiti wa Mashindano hayo Selemani Makasi amesema timu hiyo imeshindwa kuhudhuria leo kwenye mechi hiyo baada ya kuwaondoa vijana watatu  hapo jana waliokuwa wamezidi umri hatua iliyopelekea kutoleta timu yao leo kwa ajili ya kuendelea na mashindano hayo.

“Changamoto tulionayo katika kuibua vipaji kwa watoto ni  umri wa miaka 15,timu nyingi zinazoshirki mashindano haya zinalenga ushindi tu lakini lengo letu ni kuibua vipaji,sasa kilichotokea kwa timu ya pamoja ni baada ya jana kuwaondoa vijana wao 3 waliozidi umri  wameamua kuzila mashindano”amesema Makasi.

Amesema Viongozi pamoja na makocha wa timu hizo wanatakiwa kuwa wa kweli kwani mashindano yanalenga kuibua vipaji na kuleta soka lenye ubora kwa watoto.

Timu ya Pamoja Sport Club  ilitakiwa kuchuana leo na Alliance kwenye uwanja huo hatua iliyowafanya wapinzani wao kujizolea pointi tatu baada ya kushindwa kuonekana.

Awali akizungumza na G sengo Mwenyekiti wa Mashindano timu ya Allince  Yusuph Budodi ameeleza kuwa huenda timu hiyo imehofia kufungwa, baada ya kushuhudia msululu wa magoli 18 kwenye mchezo wa pili kutoka alliance dhidi ya  ElCT S.A .

VIONGOZI WA UPINZANI ZIMBABWE KUUNGANA ILI KUPAMBANA NA RAIS MUGABE KATIKA UCHAGUZI 2018


Wapinzani wawili wakuu wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamesema wameamua kuungana ili kuhakikisha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 haendelei kubaki tena madarakani kwa muhula mwengine wa miaka mitano.
Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha MDC-T ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa serikali tete ya mseto iliyoongozwa na Rais Mugabe kuanzia mwaka 2009 hadi 2013 amesema yeye na Bi Joice Mujuru, ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Mugabe hadi alipotimuliwa mwaka 2014, watapigania kuunda serikali ya mseto ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.
"Huu ni mwanzo tu wa kuweka msingi kuelekea uundaji wa muungano mpana zaidi wa kupambana na ZANU PF kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao mwaka 2018", ameeleza Tsvangirai akikusudia chama tawala kinachoongozwa na kiongozi huyo mzee zaidi kiumri barani Afrika.
Rais Robert Mugabe
Chama hicho tawala nchini Zimbabwe ambacho kinaiongoza nchi hiyo tangu ipate uhuru wake mwaka 1980, mwezi Desemba mwaka jana kilimpitisha rasmi Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika katikakati ya mwaka ujao ambapo kiongozi huyo atakuwa ametimiza umri wa miaka 94.
 
Bi Majuru ambaye mwaka jana aliunda chama kipya cha Taifa cha Wananchi amesema vyama vyao viwili vya upinzani vimekuwa vikijadiliana kwa muda wa miezi sita ili kufikia makubaliano na kwamba sasa wanatarajia kuanza mazungumzo ya kina juu ya masuala maalumu ili kuimarisha muungano wao.
Wapinzani wanamlaumu Rais Mugabe kwa kuua uchumi wa Zimbabwe ambayo ni moja ya nchi za Kiafrika iliyokuwa na ustawi mkubwa; hata hivyo chama chake kinasema uchumi wa nchi hiyo umedhoofishwa na madola ya Magharibi

MAGAZETI YA LEO: MAGUFULI ATOA AJIRA KWA MADAKTARI 258, USALAMA WA TAIFAWAZUIWA BUNGENI, DALADALA YAGONGA TRENI DAR MMOJA AFARIKI.

Magufuli atoa ajira kwa madaktari 258, Usalama wa taifa wazuiwa Bungeni, Daladala yagonga treni Dar mmoja afariki, Mtei amfurahia rais Magufuli.
 
Spika Ndugai aagiza hotuba za upinzani Bungeni zifuatiliwe, Madaktari 258 Kenya waajiriwa Tanzania, Wabunge wahofia njaa. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa.

Wednesday, April 19, 2017

KUTOKA BUNGENI:- SWALI LA MBUNGE JOSEPH HAULE.

Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe. Joseph Haule akiuliza swali kuhusu uboreshaji miundombinu ya maji katika jimbo la Mikumi.

KUTOKA BUNGENI:- UBORESHAJI WA NYUMBA ZA NHC BUKOBA.

Ni lini serikali itakarabati nyumba za shirika la nyumba zilizo Bukoba? Hapa naibu waziri Angelina Mabula anatoa jibu.

WAVUVI WA LIBYA WAWAKUTA PWANI WAHAJIRI 28 WAKIWA WAMEKUFA


Wavuvi wa Libya wamepata miili ya wahajiri 28 katika pwani ya nchi hiyo ambao wanasadikiwa kuwa waliaga dunia kutokana na kiu na njaa, baada ya boti yao kupasuka katika pwani ya mji wa Sabratha. Hayo yameelezwa na afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya. 
Tangu Libya itumbukie machafukoni baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi apinduliwe mwaka 2011, nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika imekuwa kituo kikuu zinapoanzia safari za wahajiri wanaoelekea Ulaya kwa njia ya bahari. 

Wahajiri zaidi ya 150,000 wamefanikiwa kutumia njia hiyo ya bahari na kuingia Italia katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Eneo la pwani ya Sabratha ambako miili ya wahajiri hao imepatikana  
Ahmaida Khalifa Amsalam Kamanda wa Kitengo cha Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa baada ya kuzama jua wavuvi waliwakuta wahajiri hao 28 wakiwemo wanawake wanne wakiwa wameaga dunia katika pwani ya mji wa Sabratha. Ameongeza kuwa wahanga hao wamezikwa pamoja katika kaburi mahsusi la wahamiaji haramu.