Wavuvi wa Libya wamepata miili ya wahajiri 28
katika pwani ya nchi hiyo ambao wanasadikiwa kuwa waliaga dunia
kutokana na kiu na njaa, baada ya boti yao kupasuka katika pwani ya mji
wa Sabratha. Hayo yameelezwa na afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Libya.
Tangu
Libya itumbukie machafukoni baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali
Muammar Gaddafi apinduliwe mwaka 2011, nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
imekuwa kituo kikuu zinapoanzia safari za wahajiri wanaoelekea Ulaya
kwa njia ya bahari.
Wahajiri zaidi ya 150,000 wamefanikiwa kutumia njia hiyo ya bahari na kuingia Italia katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Wahajiri zaidi ya 150,000 wamefanikiwa kutumia njia hiyo ya bahari na kuingia Italia katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Ahmaida Khalifa Amsalam Kamanda wa Kitengo cha Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa baada ya kuzama jua wavuvi waliwakuta wahajiri hao 28 wakiwemo wanawake wanne wakiwa wameaga dunia katika pwani ya mji wa Sabratha. Ameongeza kuwa wahanga hao wamezikwa pamoja katika kaburi mahsusi la wahamiaji haramu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.