ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 26, 2016

ADIDAS KUACHIA PISHI JIPYA SOKONI JUMAMOSI HII LAITWA “Triple White” NMD

adidas is stepping on fresh Air Max toes this Saturday with the release of a super-clean “Triple White” colorway of the adidas NMD Runner. Similar in color-blocking to the Monochrome Pack that dropped last week, this all-white Saturday release opts for basic white/white composition, only you won’t find Primeknit uppers on the shoe. These mesh-based versions of the all-white adidas NMDs are priced at $120 each and will drop at adidas retailers worldwide as well as adidas.com/NMD, so get a detailed look just below.



Friday, March 25, 2016

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA IJUMAA KUU

Waumini wa dini ya kikristo kote nchini waemeungana na wenzao duniani kote katika kuadhimisha mateso na kifo mwokozi wao Yesu Kristo.

MABADILIKO YA RATIBA SHUGHULI ZA KAMATI ZA BUNGE

TAARIFA KWA UMMA..

Kufuatia mabadiliko ya tarehe ya kupokea Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, Ofisi ya Bunge imefanya mabadiliko ya tarehe za shughuli za Kamati za Bunge kuelekea Mkutano wa tatu wa Bunge (Mkutano wa Bajeti) ili kuendana na masharti ya Kanuni za Bunge kuhusu shughuli hizo.

Kwa mabadiliko hayo , ratiba ya shughuli za Kamati itakuwa kama ifuatavyo:-

  1. Tarehe 29/3/2016 hadi tarehe 4/4/2016 Kamati za Kudumu za Kisekta zitatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi iliyotengewa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge. Hapo awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016.
  2. Tarehe 5/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 96 ya Kanuni za Bunge, Serikali itawasilisha Dondoo na Randama za Vitabu vya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 29/3/2016;
  3. Tarehe 6/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 97(1)-(2) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambapo Serikali itawasilisha Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 30/3/2016;
  4. Tarehe 7/4/2016 hadi 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Bunge, kwa kipindi cha siku tisa (9) Kamati za Kudumu za Kisekta zitachambua taarifa za utekelezaji wa Bajeti za Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo. Katika kipindi hicho, Kamati ya Bajeti itafanya uchambuzi wa Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2016/2017. Awali Kamati ya Bajeti ingefanya kazi hii kuanzia tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016;
  5. Tarehe 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98(3) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Kikao cha pamoja kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti ili kujadili mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara mbalimbali;
  6. Tarehe 16 na 17 Aprili, 2016 kama ilivyokuwa imepangwa awali Wabunge wataelekea Dodoma tayari kwa Shughuli za Mkutano wa Tatu wa Bunge ambao utaanza tarehe 19 Aprili, 2016.

MUTFI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA

Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery akiwa nyumbani kwake.
 Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
 Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
 Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

Na Dotto Mwaibale

MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote  Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery"  wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


SIKU SABA NGUMU KWA DR. SHEIN.

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu jana alimwapisha Dk Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar na hivyo kufungua siku saba ngumu kwa kiongozi kuunda Serikali itakayokidhi mahitaji ya Katiba.

Dk Shein aliyeapishwa baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa marudio, atalazimika kwa mujibu wa Ibara ya 39 (2) ndani ya siku saba kuanzia jana, kuteua makamu wa kwanza wa Rais na makamu wa pili wa rais.

Kwa mujibu wa Katiba hiyo ya mwaka 1984, Toleo la 2010, uteuzi huo unatakiwa kufanyika baada ya Rais huyo kushauriana na chama kilichoshika nafasi ya pili katika matokeo ya kura baada ya uchaguzi iwapo kitakuwa kimetimiza asilimia 10 ya kura zote za rais.

Hata hivyo, kwa kuwa hakuna chama kilichotimiza asilimia 10 ya kura zote, Dk Shein atalazimika kuteua makamu wa pili kutoka CCM na kuacha nafasi ya makamu wa kwanza kwa kuwa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi havina sifa za kupendekeza jina makamu huyo atakayeshika nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Maalim Seif Sharif Hamad.

Vilevile, kutokana na wapinzani kutotimiza vigezo hivyo, baada ya muda huo Rais huyo kwa mujibu wa Ibara ya 39 A (2) ya Katiba hiyo atalazimika kuwateua mawaziri na kuacha wazi nafasi za uteuzi wa chama au vyama vya upinzani.

Kibarua hicho kinamkuta Dk Shein huku ikiwapo ibara ya 9 (3) ya Katiba ya Zanzibar inayoeleza kuwa, “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia.”

Kiapo
Dk Shein alikula kiapo cha kulinda Katiba saa 4.59 asubuhi katika Uwanja cha Amaan, Unguja mbele ya jopo la majaji, viongozi wa dini, wazee na wanasheria.

Dk Shein alisema atalinda na kutetea katiba zote mbili ya Zanzibar na ile ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania pamoja na kuwa mwadilifu.

Baada ya Jaji Mkuu kumlisha kiapo, alimkabidhi Katiba ya Zanzibar na ya Muungano ambazo ni mwongozo wa utekelezaji na uendeshaji wa nchi.

Hotuba
Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa, Dk Shein aliahidi kushirikiana kwa kila hali na vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio kwa lengo la kuleta maendeleo visiwani humo na Tanzania kwa ujumla.

“Utayari wenu wa kushirikiana na Serikali umenipa moyo, nami nawaahidi kuwa nitakuwa tayari kushirikiana nanyi katika kuwatumikia wananchi kuijenga nchi bila ubaguzi wowote kwani mimi ni Rais wa Wazanzibari wote,” alisema Dk Shein.

Kiongozi huyo aliwataka wananchi kuweka kando masuala ya uchaguzi na kujikita kwenye shughuli za kujenga uchumi ili kuleta maendeleo.

Katika kufanikisha hilo, Dk Shein aliahidi kuunda Serikali itakayozingatia nidhamu na utendaji utakaokuwa na tija kwa wananchi.

“Nitahakikisha Serikali nitakayounda itaendelea kushirikiana na ile ya Dk John Magufuli ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na tunaendelea kushirikiana katika masuala yote ya maendeleo na kiuchumi,” alisema.

Dk Shein ambaye aliwasili katika uwanjani hapo saa 4.40 asubuhi alianza kwa kukagua gwaride na kisha kuelekea katika eneo maalumu la kiapo.

Alionya kuwa Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitamvumilia mtu au kikundi chochote kitakachoashiria kuleta uvunjifu wa amani nchini.

“Hatutomdhulumu mtu yeyote katika kutenda haki ila kubwa zaidi ninawanasihi wanasiasa pamoja na wanadini kuendelea kuitangaza amani iliyopo nchini ili isipotee kwa masilahi ya jamii na Taifa,” alisema.

Nderemo na shamrashamra zilitawala uwanjani hapo tangu asubuhi huku rangi za njano na kijani zikipamba kila kona.

Dakika 14, kabla ya Dk Shein kuwasili, Rais Magufuli aliingia uwanjani hapo ujio ulioamsha shangwe na vifijo kutoka kwa wanachama na mashabiki wa CCM.

Wimbo wa ‘Mpewa hapokonyeki aliyepewa kapewa’ uliopigwa na kikundi cha Cultural, ulionekana kuwa kivutio kwa watu wengi waliojitokeza katika sherehe hizo.

Mbali na Dk Magufuli, wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na marais wastaafu Amani Abeid Karume (Zanzibar) na Ali Hassan Mwinyi.

Imeandikwa na Haji Mtumwa, Hassan Ali, Kalunde Jamal na Elizabeth Edward    

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA MSD


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.

Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya wametembelea Makao makuu ya Bohari ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam.  Katika ziara yao kamati imeishauri serikali kutenga bajeti ya dawa na vifaa tiba kulingana na mahitaji. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema bado hakuna viwanda vya ndani vya kutengeneza dawa ,na vichache vilivyopo havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya MSD.

Katika hatua nyingine,wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge ya masuala ya UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa,huku wakihimiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie deni la serikali. Aidha, walisema kulipwa kwa deni kutasaidia MSD kununua dawa muhimu kwa wakati.

Kuhusu deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa kazi.

Hata hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari serikali imeshaahidi kupunguza deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa fedha.


MAGAZETI YA LEO> NYANI 61 WAWAPONZA VIGOGO WA MALIASILI. SHEIN NITAUNDA SERIKALI YA WAZANZIBAR WOTE


Ndege yanaswa KIA ikitorosha tumbiili 61,Shein nitaunda serikali ya wazanzibar wote na tumbua majipu yatua maliasili pata dondoo za magazeti hapa: 

Ndugai atajwa ufisadi shilingi million 133, kigogo idara ya wanyama pori akutwa na mambo magumu, pata dondoo za magazeti hapa: 

Siku saba ngumu kwa Dr.Shein Zanzibar,waziri wa Kenya azuiwa kuingia bandarini Tanga pata dondoo za magazeti hapa.
Na Albogast Benjamin Abo'g A plus B

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta amewaomba mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu ili kuwapa nguvu kwa kuwashangilia na kuonyesha uzalendo ili waweze kushinda mchezo huo.

Samatta akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere punde tu baada ya kutua na kikosi kizima cha Taifa Stars wakitokea Chad majira ya saa 9 usiku alifanya mahojiano na jembe fm akisisitiza kuwa jumatatu wapo tayari kucheza na kushinda, "Tumejipanga kwaajili ya mchezo na mchezo ndio maisha yetu" alisema Samatta.

Naye kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa alipata nafasi ya kuzungumza na Jembe fm na kubainisha kuwa kikosi chake kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao ni Mwinyi Kazimoto na Kelvin Yondan lakini hali zao zinaendelea vizuri hivyo anasubiri ripoti ya daktari ili kujua kama watacheza siku ya jumatatu.

Mashabiki wengi walijitokeza kuanzia mishale ya saa 5 za usiku wakiwasubiri Stars kwa hamu na kikundi maarufu cha ushangiliaji cha Tanzania Football Suporters Association kilikuwepo kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawia ambapo mwenyekiti wao aliwaomba watanzania kujiunga na kikundi hicho ili kutoa hamasa kwa wachezaji kujituma zaidi.

Tanzania ina pointi 4 kwenye kundi G ikiwa imecheza mechi 3 huku ikiomba mchezo wa ijumaa kati ya Nigeria na Misri umalizike kwa sare kisha wao washinde mechi ya jumatatu dhidi ya Chad ili kujiweka pazuri zaidi kwenye hatua hii ya kufuzu Afcon 2017.

Thursday, March 24, 2016

WAZIRI MAGHEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MSIMAMIZI WANYAMAPORI.

Waziri wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msimamizi wa Wanyamapori, Charles Mulokozi baada ya kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili kwenda Albania.

Sakata hilo limetokea baada ya Jeshi la Polisi kuwakamata raia 2 wa Uholanzi katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa na Tumbili 61 hai wakijaribu kuwasafirisha kwenda nchini Albania.

MAKAMUZI YA JJ BAND KATIKA USIKU WA BABA NA MWANA VILLA PARK JUMAMOSI HII TUNAHITIMISHA.

Abby Solo mmoja wa mavocalist wa JJ Band akifanya yake ndani ya Usiku wa Baba na Mwanza uliofanyika Villa park Mwanza jumamosi, basi unaambiwa weekend hii ndiyo mwisho, mpaka awamu nyingineeeeeeeE!!.
Kutoka kwa wadau wa Jembe family kushoto ni Mwaka D, Balozi waHeinkein na Bob White Pamba wakiwa red carpetini.
Heinkein man na mauaClassic.
Ma-Producer wanapokutana QThe Don, Oxy Okelleky na 
Abby Sollo na January Eleven wakishambulia jukwaa.
Pale shabiki anapopata mizuka na kutaka kuonyesha ufundi wake.
Chali....
Solo likikung'utwa.
Nyataaaaa!!.
Keybordist.
Drummer.
The view at ze area.
Mzuka.
Wakuitwa Popo Bawa.
Hisia ....
Mashabiki wanapokkolea mijisongi ya JJ Band.
Wakali wa town.
PICHA ZA AWAMU YA PILI NA SUPER KAMANYOLA ZAJA.