ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 11, 2015

MAHAKAMANI KWA KUGHUSHI TOVUTI FEKI NA KUTUMIA MAJINA YA TAASISI NA WANASIASA.


By Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam.  Watu wawili, Patrick Natala na Maxmillian Msacky  wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 10  yakiwamo ya kughushi, kutengeneza tovuti feki na mifumo ya mtandao  kwa kutumia majina ya  Taasisi, viongozi na wanasiasa.
Akiwasomea hati ya mashtaka leo Wakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa akishirikiana na Wakili Mwandamizi Mkuu wa TCRA, Johannes Kalungura walidai kuwa washtakiwa hao walitengeneza tovuti feki kwa kutumia majina ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Foundation (Ikulu), TCRA Foundation,  Akiba Saccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania na  Wekeza Fund.
Mutakyawa amedai kuwa  washtakiwa hao wametengeneza tovuti hizo feki kati ya Januari na Aprili  2014 jijini Dar es Salaam  kinyume  na kifungu cha 122 (b) cha sheria ya Kielektoliniki na Mawasiliano ya Posta  namba 3 ya 2010.
Mbali na mashtaka hayo, Mshtakiwa Msacky yeye anadaiwa kuwa kati ya 2006 na 2024 kwa njia ya udanganyifu alighushi cheti cha Sekondari  namba 0421130 chenye indexi namba S 0260-0001.
Iliendelea kudaiwa kuwa  kati ya 2005 na 2014 mshtakiwa huyo alighushi cheti kingine cha Sekondari  namba 0217951 chenye indexi namba S 0310-0532,akionyesha ni halali na kwamba vimetolewa na Baraza la Mitihani  Tanzania wakati akijua kuwa ni uongo.
Washtakiwa hao wamekana mashtaka na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika  na washtakiwa kupelekwa rumande hadi Septemba 28, 2015 itakapotajwa.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzage amesema kati ya Aprili na Juni  katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 walipata malalamiko toka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa makampuni feki yaliyokuwa yakidai kuwa yanatoa mikopo kwa muda mfupi.
Nzage amedai kuwa wahusika hao walitumia majina ya wanasiasa na pia kujifanya ni viongozi na wamiliki wa taasisi hizo na kwamba makumpuni hayo yanaandaa  shughuli za kuchangisha fedha. 
CHANZO: MWANANCHI

TAARIFA YA HABARI YA JEMBE FM SASA NI LIVE KUPITIA TV YAKO.

Taaarifa ya Habari ya jEMBe fM ya saa moja kamili jioni pamoja na kuwa husikika kupitia 93.7 Radioni pia utaipata LIVE #BarmedasTv kupitia king'amuzi cha Startimes channel no 115 @johnanatory @jembenijembe @makosewe #masokoTanzania @chokadj

MGUU KWA MGUU















PICHA ZA MKUTANO WA KAMPENI ZA MABULA IGOMA NYAMAGANA JANA

 NA PETER FABIAN, MWANZA.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula, afunika mikutano ya kampeni Kata za Nyegezi na Igoma, amtaka mgombea mwenzake ambaye ni mpinzani wake, Ezekiel Wenje (CHADEMA) kuacha porojo na uzushi bali kuwaeleza wananchi alichokifanya akiwa Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano iliyopita.

Mabula alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana wakati akihutubia wananchi wa Kata hizo waliokuwa wamefulika kumsikiliza wakati wa kuwaomba kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo kutokana na Mbunge Wenje aliyemaliza muda wake kuwa Mbunge wa matukio ya vurugu, migomo na kuhamasisha mapambano ya machinga na Polisi.

Akiwa Kata ya Nyegezi katika viwanja vya Magrasi kona Nyegezi aliwaeleza wananchi watakapomchagua atahakikisha anasimamia na kutetea yaliyoainishwa na Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015/2020 yanatekelezwa kwa vitendo na kuonekana kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma na tija katika ustawi wa maendeleo ya jimbo, mkoa na taifa kwa ujumla.
“Nimekuwa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa miaka mitatu baada ya kugawanywa na serikali na kuundwa Manispaa ya Ilemela mwaka 2013 nimesimamia utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 68 vya maabara za sekondari za Kata 12 kukamilika na kuwekewa thamani zake kwa Sh bilioni 3.5, kukamilisha ujenzi wa barabara za lami zilizo chini ya jiji kwa kiwango cha lami km 18.1.6 kwa zaidi Sh bilioni 15,” alisema.

Mabula alifafanua kwamba barabara za mawe zimejengwa Kata katika maeneo ya Idara ya maji eneo la Capil point (Nyamagana), Bugando-Igogo (Igogo), Nyabulogoya (Mkolani) Mkuyuni-Nyakurunduma (Mkuyuni) na Kitangili-Ibungilo (Nyamanoro) pia kusimamia ujenzi wa mradi wa maji safi Fumagila Kata ya Kishiri kufanikisha mashindano ya Meya Kombe la Meya Jiji la Mwanza kwa miaka mitatu mfululizo na kupunguza kero ya madawati shule za msingi na ujenzi wa vyoo.

Aidha aliwaomba wananchi wamchague Dk John Pombe Magufuli, yeye pamoja na madiwani wanaotokana na CCM kutoka Kata 18 zinazounda jijimbo hilo kwa sasa baada ya kuongwezwa kutoka 12, pili wamwamini kwa kuwa tayari aliisha ianza kazi hiyo ya kuwaletea maendeleo akiwa Meya na atahakikisha vipaumbele vyake katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Ujasiliamali/Uchumi, Michezo na Miundombinu ya barabara za lami na mawe.

Akihutubia mamia ya wananchi  wa Kata ya Igoma jana aliwahakikishia wafanyabiashara wadogo, machinga, mama lishe  na wauza mboga na matunda kuendelea kulitumia eneo pembezoni mwa barabara kuu ya Mwanza-Musoma na hakuna mtu wa kuwaondoa na ndiyo maana Halmashauri imewafungia taa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao hadi usiku.

“Wakataeni wanasiasa na wagombea wanaokuja na porojo na maneno ya kuwachonganisha ikiwemo kunichafua kuwa nilivunja mikokoteni yenu na kumwaga wali wenu, niwaombeni muwapuuzeni hao bali wakija waulizeni watawafanyia nini kwa miaka mitano ijayo na kama walikuwa wawakilishi wenu kwa miaka mitano wamefanya nini na wapi ili kujilidhisha kabla ya kuwachagua tena,”alisisitiza.
Kwa upande wake Katibu wa CCM, Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amewataka wananchi kuwachagua wagombea wa Chama hicho kutokana na kuwa wagombea bora kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani badala ya kuwachaguwa kwa ushabiki, hasira na kusikiliza porojo zao jambo ambalo walilolifanya mwaka 2010 na kupelekea baadhi ya mambo kukwama na kukosa maendeleo ikiwemo huduma za kijamii.

Mtaturu aliwakumbusha wananchi wa Kata hizo waliohudhuria katika mikutano hiyo ya kampeni kuhakikisha hawafanyi makosa kama ya mwaka 2010 ya kuchagua kwa ushabiki na hasira na matokeo yake kupata wawakirishi waliofanana watalii kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania na Baraza la Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kushindwa kutetea kero la matatizo ya wananchi waliowachaguwa ili wawatumikie.

"Muulizeni Wenje (CHADEMA) kwa miaka mitano ya Ubunge wake jimbo la Nyamagana amefanya nini na wapi lakini pia awaeleze fedha za mfuko wa jimbo zilifanya kazi ipi na katika maeneo yapi na katika Kata zipi ili mwende kujionea pia awaeleze mapato na matumizi ya fedha za Mfuko wa kusaidia Elimu aliouanzisha na kuchangiwa kiasi cha Sh milioni 75 katika harambee mbili ya Sahara na Gold Crest ili kujua pamoja na kushindwa kuwasaidia watoto wa masikini kulipiwa gharama za kusoma," haiwezekani aje na porojo kwenu. 

Wito wangu kwenu wananchi ni kuhakikisha tuchague wagombea bora wa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani ambao watapigania na kutetea masilahi ya wananchi na kuwatumikia bila kuwabagua lakini pia tuache kuwachagua wawakilishi wetu hawa kwa ushabiki na hasira kwa kusikiliza porojo na uchochezi kuwa CCM haijafanya kitu tangu kupatikana kwa uhuru wa taifa hili tumieni mikutano ya kampeni kuwasikiliza wagombea kisha mufanye uamuzi sahihi.









PICHA ZOTE NA PETER FABIAN/GSENGO BLOG 

NANI MWINGINE MWENYE ZARI KUYANASA MAMILIONI...!!?

Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya sita ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”, Rajabu Mwalapinga (kulia), mkazi wa Dar es Salaam, shillingi millioni tatu.
Afisa uhusiano na matukio, Bi Dangio Kaniki akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya saba ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Kigoma na Dar es Salaam walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne Septemba 1 2015.

WATEJA Wa Airtel wazidi kushida Mamilioni ya Pesa Dar es Salaam, Tanzania, Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imeendelea kuwafanya wateja wake mamilionea kupitia promosheni yake ya “Jiongeze na Mshiko”. 

Habibu Mwella Freuzi, mfanyabiashara kutoka Dar Es Salaam na Kitabu Ally, mkulima anayeishi Kigoma wamepatikana kuwa washindi wa million moja na million tatu baada ya droo ya kuchezesha droo ya nane katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.

Afisa Uhusiano na Matukio, Dangio Kaniki, alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi kushindaniwa kati ya sasa mpaka Novemba atakapopatikana mshindi wa mwisho wa droo hii, atakayeondoka na kitita cha shililingi milioni 50. 

Hivyo aliwahimiza watanzania kuchukua fursa hii waliopatiwa na Airtel kujiinua kiuchumi Hadi sasa, promosheni ya “Jiongeze na Mshiko” ya Airtel imewafanya watanzania 16 mamilionea. Mamilionea zaidi wanategemewa kutokea katika promosheni hii iliyoanzishwa wiki saba zilizopita. 

Vile vile Airtel imewazawadia fedha taslimu washidi wa droo ya saba, ambao ni, Geri William kutoka Dar es Salaam na Lui Saulo Karunda, mkazi wa Kigoma. Wateja wanaweza kujinga na promosheni hii bure kwa kutuma ujumbe wenye neno "BURE" kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

Mteja atakapomaliza kujibu maswali ya bure atapata ujumbe utakaomuuliza kama angependa kujiunga na ngazi ya premier, ili kuwezeshwa kufunguliwa maswali zaidi na kujikusanyia pointi nyingi kwa zawadi zenye thamani kubwa.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA NA KUWATAKA WAKIMBIZI HAO WADUMISHE AMANI NA UTULIVU

Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto) akizungumza na watumishi wa mashirika mbalimbali yaliyoko katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) aliyetembelea kambi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akizungumza na watumishi mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Daktari wa Hospitali ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Florence Mshana (aliyeshika karatasi), akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), alipotembelea hospitali hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Amah Assiama - Hillgartner( kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil (katikati), aliye tembelea hospitali hiyo wakati waziara yake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, MbarakAbdulwakil(katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner(kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kambini hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma inahifadhi wa kimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu waShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu katika makazi ya wakimbizi yaliyopo Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akimsikiliza mmoja wa maofisa waShirika la Chakula Duniani (WFP) alipotembelea ndani ya mahema wanakoishi wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

UZINDUZI WA MFULULIZO WA VIPINDI VYA MAMA MISITU KUHUSU UZALISHAJI WA MKAA ENDELEVU WAFANYIKA NEW AFRIKA HOTELI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo asubuhi.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland, William Nambiza.
Mshauri wa Ufundi Weizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Rahima Njaidi (kushoto), akielezea shughuli zinazofanywa na mtandao huo.
Mkuu wa Mradi ya Kilimo, Kipato na Ajira wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Ueli Mauderli (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
 Mkutano wa uzinduzi huo ukiendelea.
Mwezeshaji, Faustine Ninga kutoka Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), akitoa maelekezo mbalimbali.
Meneja Kampeni Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wasainii walioigiza namna ya utunzaji wa miti. Kulia ni Philemon Robari na Mohammed Titima.
Maofisa mbalimbali waliopo kwenye mradi huo wa Mama Misitu wakiwa katika uzinduzi huo.


MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.

Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Shirika la Kuendeleza Teknolojia  za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za vijijini na mijini.

Inakadiriwa kuwa mkaa na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012. Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.

Mkaa endelevu ni mkaa unaozalishwa kwa njia endelevu kutoka katika Misitu ya Hifadhi ya Jamii bila kuchangia ukataji miti na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, uzalishaji wa aina hii ya mkaa bado haujajulikana. Kampeni hii mpya ina lengo la kuleta mabadiliko kupitia ubunifu wa vipindi mfululizo vya runinga ambavyo vinazinduliwa leo.

Nishati zitokanazo na tongamotaka (biomas)  ni nishati muhimu sana nchini Tanzania itakayoendelea kutumika angalau zaidi ya miaka 20 ijayo. Kwa sasa, mkaa mwingi huzalishwa kinyume na utaratibu kutoka katika misitu ya hifadhi na misitu ya vijiji isiyo na mipango ya matumizi endelevu. Kutokana na usimamizi hafifu wa uzalishaji wa mkaa, imesababisha ukataji miti na uharibifu wa misitu kuongezeka nchini Tanzania.

Kampeni ya Mama Misitu na washirika wake (TFCG na MJUMITA) inalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya mkaa kutoka tatizo kuwa fursa kubwa muhimu. Hivyo, vipindi vya runinga vya Mama Misitu pamoja na jumbe muhimu za mawasiliano zitasambazwa nchini Tanzania ili kuibua mjadala wa pamoja juu ya kuboresha utawala bora wa rasilimali misitu na kuleta faida kwa watanzania.


Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano yenye lengo la kuboresha utawala bora wa misitu ya Tanzania na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali misitu zao.