MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula, afunika mikutano ya kampeni Kata za Nyegezi na Igoma, amtaka mgombea mwenzake ambaye ni mpinzani wake, Ezekiel Wenje (CHADEMA) kuacha porojo na uzushi bali kuwaeleza wananchi alichokifanya akiwa Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano iliyopita.
Mabula alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana wakati akihutubia wananchi wa Kata hizo waliokuwa wamefulika kumsikiliza wakati wa kuwaomba kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo kutokana na Mbunge Wenje aliyemaliza muda wake kuwa Mbunge wa matukio ya vurugu, migomo na kuhamasisha mapambano ya machinga na Polisi.
Akiwa Kata ya Nyegezi katika viwanja vya Magrasi kona Nyegezi aliwaeleza wananchi watakapomchagua atahakikisha anasimamia na kutetea yaliyoainishwa na Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015/2020 yanatekelezwa kwa vitendo na kuonekana kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma na tija katika ustawi wa maendeleo ya jimbo, mkoa na taifa kwa ujumla.
“Nimekuwa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa miaka mitatu baada ya kugawanywa na serikali na kuundwa Manispaa ya Ilemela mwaka 2013 nimesimamia utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 68 vya maabara za sekondari za Kata 12 kukamilika na kuwekewa thamani zake kwa Sh bilioni 3.5, kukamilisha ujenzi wa barabara za lami zilizo chini ya jiji kwa kiwango cha lami km 18.1.6 kwa zaidi Sh bilioni 15,” alisema.
Mabula alifafanua kwamba barabara za mawe zimejengwa Kata katika maeneo ya Idara ya maji eneo la Capil point (Nyamagana), Bugando-Igogo (Igogo), Nyabulogoya (Mkolani) Mkuyuni-Nyakurunduma (Mkuyuni) na Kitangili-Ibungilo (Nyamanoro) pia kusimamia ujenzi wa mradi wa maji safi Fumagila Kata ya Kishiri kufanikisha mashindano ya Meya Kombe la Meya Jiji la Mwanza kwa miaka mitatu mfululizo na kupunguza kero ya madawati shule za msingi na ujenzi wa vyoo.
Aidha aliwaomba wananchi wamchague Dk John Pombe Magufuli, yeye pamoja na madiwani wanaotokana na CCM kutoka Kata 18 zinazounda jijimbo hilo kwa sasa baada ya kuongwezwa kutoka 12, pili wamwamini kwa kuwa tayari aliisha ianza kazi hiyo ya kuwaletea maendeleo akiwa Meya na atahakikisha vipaumbele vyake katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Ujasiliamali/Uchumi, Michezo na Miundombinu ya barabara za lami na mawe.
Akihutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Igoma jana aliwahakikishia wafanyabiashara wadogo, machinga, mama lishe na wauza mboga na matunda kuendelea kulitumia eneo pembezoni mwa barabara kuu ya Mwanza-Musoma na hakuna mtu wa kuwaondoa na ndiyo maana Halmashauri imewafungia taa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao hadi usiku.
“Wakataeni wanasiasa na wagombea wanaokuja na porojo na maneno ya kuwachonganisha ikiwemo kunichafua kuwa nilivunja mikokoteni yenu na kumwaga wali wenu, niwaombeni muwapuuzeni hao bali wakija waulizeni watawafanyia nini kwa miaka mitano ijayo na kama walikuwa wawakilishi wenu kwa miaka mitano wamefanya nini na wapi ili kujilidhisha kabla ya kuwachagua tena,”alisisitiza.
Kwa upande wake Katibu wa CCM, Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amewataka wananchi kuwachagua wagombea wa Chama hicho kutokana na kuwa wagombea bora kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani badala ya kuwachaguwa kwa ushabiki, hasira na kusikiliza porojo zao jambo ambalo walilolifanya mwaka 2010 na kupelekea baadhi ya mambo kukwama na kukosa maendeleo ikiwemo huduma za kijamii.
Mtaturu aliwakumbusha wananchi wa Kata hizo waliohudhuria katika mikutano hiyo ya kampeni kuhakikisha hawafanyi makosa kama ya mwaka 2010 ya kuchagua kwa ushabiki na hasira na matokeo yake kupata wawakirishi waliofanana watalii kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania na Baraza la Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kushindwa kutetea kero la matatizo ya wananchi waliowachaguwa ili wawatumikie.
"Muulizeni Wenje (CHADEMA) kwa miaka mitano ya Ubunge wake jimbo la Nyamagana amefanya nini na wapi lakini pia awaeleze fedha za mfuko wa jimbo zilifanya kazi ipi na katika maeneo yapi na katika Kata zipi ili mwende kujionea pia awaeleze mapato na matumizi ya fedha za Mfuko wa kusaidia Elimu aliouanzisha na kuchangiwa kiasi cha Sh milioni 75 katika harambee mbili ya Sahara na Gold Crest ili kujua pamoja na kushindwa kuwasaidia watoto wa masikini kulipiwa gharama za kusoma," haiwezekani aje na porojo kwenu.
Wito wangu kwenu wananchi ni kuhakikisha tuchague wagombea bora wa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani ambao watapigania na kutetea masilahi ya wananchi na kuwatumikia bila kuwabagua lakini pia tuache kuwachagua wawakilishi wetu hawa kwa ushabiki na hasira kwa kusikiliza porojo na uchochezi kuwa CCM haijafanya kitu tangu kupatikana kwa uhuru wa taifa hili tumieni mikutano ya kampeni kuwasikiliza wagombea kisha mufanye uamuzi sahihi.
PICHA ZOTE NA PETER FABIAN/GSENGO BLOG
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.