|
Tumain Makene ambaye ni Afisa Habari wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini CHADEMA AKITOA TAARIFA YA mikutano inayoendelea kufanyika jijini Mwanza. |
Chadema Dk. Slaa sio lolote si chochote
Nafasi yake kuzibwa na mtu makini
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo Chadema, kimesema kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, si lolote na si chochote ndani ya chama hicho na kwamba nafasi yake itazibwa na mtu makini zaidi yake.
Chadema ambacho kimejichimbia mkoani Mwanza, kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ya kumpata mrithi wa Dk. Slaa pamoja na kujiwekea mipango mahususi ya chama hicho katika kipindi cha mwaka 2016/2020.
Dk. Slaa alijiondoa Chadema na kutangaza kuachana na masuala ya kisiasa, baaada ya chama hicho kikuu cha upinzania kumteua aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa kugombea urais kupitia chama hicho na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa.
Hata hivyo, katika uchuguzi wa mwaka 2015 vyama hivyo vilionekana kuwa na nguvu kubwa, ikilinganishwa na kipindi cha nyuma mwamko wa Wananchi kwa vyama vya upinzani ulikuwa ni mdogo ikilinganishwa na hivi sasa.
Katika matokeo ya uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea Urais wa ukawa, Edward Lowasa alipata kura milioni 6 huku Rais wa Sasa, Dk. John Magufuli alipata kura milioni 8, kura ambazo hazijawahi kufikiwa na mgombea urais wa upinzani nchini.
|
Wakijdiliana kutoka kushoto ni Mbunge wa CHADEMA viti maalummkoa wa Mwanza, Bi Suzan Masele akifuatiwa na Afisa Habari Bw. Tumaini Makene (katikati) na kulia ni Tungaraza Jugu ambaye ni Afisa Oparesheni Kanda ya Ziwa Victoria. |
Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema kuwa ndani ya chama hicho wapo viongozi makini, wachapa kazi na watu wenye weledi mkubwa wa kukiongoza chama hicho.
Alisema kuwa pengo la Dk. Slaa bado halijaonekana mahala popote pale na kwamba wafuasi wa chadema na wanachama watarajie Katibu mkuu ambaye ni makini na mchapa kazi ndani ya saa 48 zilizobaki.
Makene alisema kuwa watu wengi wameanza kuzungumza mambo mengi ambayo hayana msingi wowote ndani ya chama ikiwemo kwamba ndani ya Chadema hakuna mtumwenye sifa ya kurithi mikoba ya Dk. Slaa.
Ndani ya Chadema kuna watu makini ambao ni zaidi ya Slaa. DK willbrod Slaa, nashangaa watu wanaodai kwamba hakuna mtu wa kuirithi mikoba yake, hii ni taasisi nitashangaa kuona watu wanasema mambo kama hayo.
Pia Makene alisema kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anatarajia kuwasilisha majina mawili aliyopendekeza kwenye Baraza kuu la chama hicho lenye zaidi ya wajumbe 400 ili kuchagua jina moja.
Mpaka sasa hakuna jina ambalo limeishafahamika litapelekwa baraza kuu, anaefahamu ni mwenyekiti mwenyewe Freeman Mbowe, kwa hiyo muda uliobaki tusubili tuone ni nani atakaechaguliwa.
|
Waandishi wa Habari kikazi zaidi. |
Majina ya ukatibu yanayotajwa
Mpaka sasa kuna majina mbalimbali yanayotajwa kushika nafasi ya ukatibu wa chama hicho yakiwamo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibari, Salum Mwalimu, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni KUB, Tindu Lissu.
Majina mengine yanayotajwa ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijini, John Heche.
Licha ya majina hayo kutajwa kila kukicha na baadhi ya Wananchi na viongozi mbalimbali wa kisiasa, chama hicho kinatarajiwa kutangaza Katibu Mkuu wa Chadema katika mkutano wa hadhara.
Juzi na jana ilikuwa ni vikao vya kamati kuu ya chama hicho taifa, kesho ni kikao cha Baraza Kuu, ambapo katika kikao hicho kitapokea mapendekezo ya majina mawili yatakayowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Kikao kingine ni Machi 13, ambacho ni cha Kamati Kuu kitakachoketi kwa siku moja na kisha jioni kutafanyika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela mjini hapa.
Wananchi wazungumza
Baadhi ya Wananchi waliozungumza, wakisema kuwa wanategemea kuona Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye ni makini na hodari wa kujenga hoja kwa mstakabili wa kukikuza chama hicho kilichoanzishwa mwaka 1992.
Walisema kuwa endapo Katibu huyo wa chama hicho atachaguliwa kwa kufuata misingi na sheria ya chama, matarajio yao ni kuona Chadema mpya ya miaka mitano ya 2016 na 2021 kwa ajili ya ukombozi wa watanzania.
Unajuwa Katibu Mkuu wa chama ndio kila kitu na kama Chadema watachagua mtu ambae sio makini, ujuwe sasa hata mipango yao ya kulikomboa taifa haitafanikiwa tunategemea kuona mtu makini, alisema Edward Nyoni ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa.