Meneja Mahusiano wa
Benki ya CBA, Caroline Makatu (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa vitanda na
mashine kumsaidia mtoto anayezaliwa kabla ya muda, kwa Kaimu Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Delilah Moshi, katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka Benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja wadau waliofanikisha msaada huo
katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu
ya Jamii
TAASISI ya Doris Mollel
Foundation (DMF) kwa kushirikiana na Benki ya CBA wametoa msaada
vitanda viwili na mashine tatu za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
vyenye wa vitu vyenye thamani ya Sh.milioni mbili katika
Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana Jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi wa DMF, Doris Mollel, alisema kwa
kutambua umuhimu kwa sababu wanawakumbuka wanawake wanaojifungua kabla ya
wakati na kutoa msaada huo ni kutaka kuokoa uhai wa watoto hao .
“Kutambua thamani ya
watoto njiti tumeona katika kuokoa uhai na kuweza kufikia malengo tumeona
..mashine za kuwasaidia kufikia malengo yao kama walivyo watoto wengine…taasisi
itaendelea kutoa mchango kwa jamii,” alisema Doris.
Naye Meneja Mahusiano wa
Benki ya CBA ,Caroline Makatu amesema kuna changamoto nyingi
hospitali ikiwemo na uhaba wa vifaa kwa kutambua hilo wametoa msaada huo
ili kusaidia mama na mtoto.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo Dk. Delilah Moshi amesema wanashukuru kwa msaada huo uliotolewa
na taasisi hizo kwa kutambua uwepo wa wanawake na kuziwezesha hospitali.
Amesema kwa sasa shida
kubwa iliyopo kwa sasa ni uhaba wa majengo kutokana na nafasi chache za
kuhifadhia watoto njiti kwa sababu idadi ya watoto inaongezeka.
“Kutokana na kuwapo kwa
mashine za kuhifadhia watoto njiti idadi ya vifo vya watoto hao imepungua hivyo
naiomba serikali kuongeza madaktari wa watoto kwani hadi sasa wapo wawili tu,”
amesema Mushi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.