ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 11, 2018

DKT TIZEBA AWAHAKIKISHIA WASINDIKAJI WA PAMBA KUJIAMINI SOKO LIPO LA KUTOSHA

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
Wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na waendeshaji wa soko la bidhaa nchini Tanzania Merchantile Exchange (TMX) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.

Na Mathias Canal, WK-Mwanza

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amewahakikishia wanunuzi na wasindikaji wa zao la Pamba kuendelea kununua na kusindika pamba kwa wingi kutoka kwa wakulima kwani soko la zao hilo kwa sasa limeimarika kwa kiasi kikubwa.

Waziri Tizeba ametoa kauli hiyo juzi tarehe 9 Agosti 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya  wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza.  

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwapatia uelewa wanunuzi wa zao la Pamba Mhe Tizeba alisema kuwa kuna njia mbadala zaidi ya waliyonayo sasa ya kuuza Pamba yao katika soko la bidhaa ambapo bidhaa hushindanishwa kutokana na ubora wake kwa wanunuzi walio wengi Duniani.

Alisema kuingia kwenye ushindani wa soko ni miongoni mwa njia muhimu na madhubuti kwao kwani itaongeza thamani ya zao hilo hivyo kuwa na kipato kikubwa kitakachoongeza tija na mafanikio ya kipato.

Tanzania Merchantile Exchange (TMX) inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa kwa pamoja na kwa wingi ili washindane katika bei jambo ambalo litawafanya wauzaji kuuza bidhaa zao kwa kiasi kizuri cha fedha na kupelekea kupata bei nzuri.

Katika mkutano huo Mhe Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba aliwataka wanunuzi hao kujifunza namna ambavyo soko la bidhaa Tanzania Merchantile Exchange (TMX) linafanya kazi Kwa kupeleka kiasi cha Pamba kilichozidi kutokana na mkataba walioingia na wanunuzi wao Nje ya nchi ili kujionea manufaa yaliyopo. 

Hata hivyo Mhe Tizeba aliwataka wanunuzi hao kuendelea kununua Pamba kwa wakulima bila wasiwasi wowote, kwani soko la bidhaa litaweza kutumika kwa manufaa makubwa kuuza Pamba yao na kumhakikishia mkulima soko.

Alisema kuwa Katika ngazi ya uzalishaji ni muhimu sana ubora wa pamba ukaimarishwa ili soko la bidhaa liweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha, Mhe Tizeba ameilekeza TMX kukutana na kampuni zinazonunua pamba mmoja mmoja ili kubaini kampuni ambazo zitaweza kuanza msimu huu kutumia soko la bidhaa.

MISHAHARA DUNI KWA MAASKARI WA BAADHI YA MAKAMPUNI BINAFSI CHANZO CHA UHALIFU NCHINI.




GSENGOtV

IMETAJWA kuwa huenda ongezeko la wahalifu wa uvunjaji na wizi wa maeneo kadhaa yenye mali nchini linachangiwa na ukwasi wa maisha wanayoishi baadhi ya walinzi wanaopewa dhamana ya kulinda maeneo mbalimbali ya huduma, majumbani na maeneo ya biashara.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amefunguka hayo wakati akishiriki hafla ya ufunguzi wa kampuni mpya ya ulinzi ya “Power Shield Security Services Ltd” yenye ofisi zake barabara ya Bugando jijini hapa.
"Matatizo ya ukosefu wa mafunzo, Mishahara midogo, Ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara, kutopata mahitaji muhimu na maslahi bora ni moja kati ya sababu zinazo wasukuma baadhi ya walinzi hao wanao pewa dhamana ya kulinda hasa maeneo nyeti yenye thamani na mali kujihusisha na vitendo vya uhalifu" alisema Mongella.

Wakati sekta ya ulinzi binafsi ikiendelea kukua katika miongo michache iliyopita, nayo mifumo iliyopo ya  kudhibiti wahalifu imeendelea kuboreshwa.

Ili kupambana na changamoto hizo  Uongozi wa kampuni mpya ya ulinzi ya “Power Shield Security Services Ltd” iliyozinduliwa Tarehe 10 Agasti 2018 Jijini Mwanza, umeahidi kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa kutumia askari wake wenye weledi wa hali ya juu pamoja na vifaa vya kisasa ikiwemo kamera.

Ujuzi wa walinzi wake katika kutoa huduma ya kwanza pamoja na huduma ya zimamoto iwapo majanga hayo yanapoweza kujitokeza ni moja kati ya sifa nyinyine za ziada walizonazo watoa huduma kutoka kampuni hilo.

Friday, August 10, 2018

RC MONGELA ATOA SIKU 14 KWA MHANDISI WA MAJI NA MKURUGENZI UKEREWE MAJI YAPATIKANE.



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mkuu wa mkoa Mwanza JOHN MONGELA, Ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe FRANK BAHATI na Mhandisi wake EMANUEL KAULANANGA kufikisha maji katika mradi mkubwa wa ujenzi wa Chuo Cha Uwalimu Murutunguru cha wilaya Ukerewe mkoani Mwanza.

SAMATTA AUNGANA NA WANAHABARI KULAANI POLISI WALIOSHUSHA KIPIGO KWA MWANDISHI.


WAKATI Watanzania mbalimbali wakitoa matamko ya kulaani kitendo cha Mwandishi wa habari wa Wapo Redio Silas Mbise kushambuliwa na Polisi katika mechi kati ya Simba na Asante Kotoko Siku ya Simba Day mchezaji wa kimataifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samata amesema kitendo hicho si cha kiungwana.

Samata ametoa kauli hiyo kutokana na kusambaa kwa video inayoonesha namna ambavyo mwandishi huyo akishambuliwa licha ya kujisamilisha.

Hivyo kutokana na video hiyo Samata kupita ukurasa wake wa Twitter ameelezea kusikitishwa na shambulio hilo.

Samata amesema hivi “Sio kitendo cha kiungwana askari kupiga mwandishi katika eneo la michezo , mpira ni mchezo unaoleta amani sio kuvunja amani.”.Wakati Samata akitoa kauli hiyo tayari leo mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linalaani vikali tukio hilo linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandishi huyo.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema tukio hilo limetokea Agosti 8 mwaka huu siku ya mechi kati ya Simba na Asante Kotoko ya nchini Ghana.Aidha amesema Polisi Kanda Maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa na kuonesha askari polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.

Mambosasa amesema hiyo inakwenda sambasamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe na kwamba mtu yoyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

JEMBE DJZ KAZINI DAKIKA 1 YA SAA 3 ZA MAANGAMIZI.



GSENGOtV
Just kipande cha dakika moja na sekunde zake katima show yenye saa 3 zake hewani HIT ZONE.

huyu hapa wakuitwa Dj Mike Beatz.

NAIBU WAZIRI WA MADINI ATOA HEKO KWA NFRA KWA ELIMU WANAYOITOA KUHUSU UHIFADHI WA MAHINDI BAADA YA KUVUNA


Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-NFRA)
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo akisikiliza maelezo kuhusu uhifadhi wa nafaka ya mahindi mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi baada ya kuvuna mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 8 Agosti 2018.

Na Mathias Canal, NFRA-Simiyu

Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo amepongeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa elimu wanayoitoa kuhusu njia bora za kuhifadhi nafaka ya mahindi mara baada ya kuvuna.

Nyongo ametoa pongezi hizo jana 8 Agosti 2018 wakati akizungumza na uongozi wa NFRA mara baada ya kutembelea banda la NFRA kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambapo Rais mstaafu wa srikali ya awamu ya tatu Mhe Benjamini Willium Mkapa ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo.

Pamoja na mambo mengine Mhe Naibu Waziri Nyongo amepongeza elimu inayotolewa kuhusu utunzaji huo wa mahindi mara baada ya kuvuna kwa kufuata taratibu zote za kuvuna wakati muafaka, ikiwa ni pamoja na Kukausha vizuri mahindi baada ya kuvuna.

Mhe Nyongo pia amepongeza elimu inayotolewa na NFRA kuhusu utambuzi wa mahindi kama yamekauka kwa kutumia njia za kienyeji ambazo ni rafiki kwa wakulima wa chini pamoja na njia za kisasa.

Pia alijionea na elimu kuhusu matumizi bora ya mifuko ya kuhifadhia mahindi ikiwa ni pamoja na mifuko ya PICS, Vihenge vya chuma sambamba na maghala ya tofali.

Alisema kuwa njia hizo zitaleta ufanisi iwapo mahindi yameandaliwa vizuri kabla ya kuhifadhi huku akiisihi NFRA kuongeza nguvu katika utoaji elimu ili wakulima waweze kunufaika kwani mkulima akielimika ipasavyo ni sehemu ya mafanikio ya mtu mmoja mmoja sambamba na  ukuzaji wa uchumi wa Taifa.

WASHINDI WENGINE WA JISHINDIE MAMILIONI NA PEPSI WAPATIKANA KATIKA SHEREHE ZA NANENANE MWANZA


GSENGOtV

Tizama jinsi shilingi 500/= tu inavyoweza kumtajirisha mtu.
 Focus Lusato (kulia) ambaye ni Meneja Rasilimali watu Kampuni ya SBC Tanzania Limited watengenezaji wa soda jamii ya Pepsi akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000/=) kwa Jofrey Benjamin mwenye umri wa miaka 17 aliyejishindia kitita hicho wakati akinywa soda katika banda la promosheni la kampuni hiyo viwanja vya Nane Nane Nyamhongolo jijini Mwanza. Shuhuda wa mwisho kushoto ni Gabriel Mkuele Msaidizi Meneja Uzalishaji SBC Mwanza.
  Abou Kassimu Marekani akionesha mkwanja wake fedha taslimu shilingi laki tano (500,000/=)  aliyejishindia kitita hicho wakati akinywa soda katika banda la promosheni la kampuni hiyo viwanja vya Nane Nane Nyamhongolo jijini Mwanza.  Focus Lusato (kulia) ambaye ni Meneja Rasilimali watu Kampuni ya SBC Tanzania Limited watengenezaji wa soda jamii ya Pepsi na kushoto ni Gabriel Mkuele ambaye ni  Meneja Msaidizi Uzalishaji SBC Mwanza.
  Focus Lusato (kulia) ambaye ni Meneja Rasilimali watu Kampuni ya SBC Tanzania Limited watengenezaji wa soda jamii ya Pepsi akikabidhi fedha taslimu shilingi laki tano (500,000/=) kwa Izengo S. Kadawi aliyejishindia kitita hicho wakati akinywa soda katika banda la promosheni la kampuni hiyo viwanja vya Nane Nane Nyamhongolo jijini Mwanza. Shuhuda wa mwisho kushoto ni Gabriel Mkuele Msaidizi Meneja Uzalishaji SBC Mwanza.
Washindi wakipata picha ya pamoja na Meneja mauzo SBC Tld Kanda ya Ziwa Bwana Hussein Mkwawa (kulia).

NI NANI KATI YA HAWA LIGI KUU YA NCHINI UINGEREZA?


Msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza (EPL), unatarajia kuanza kesho Ijumaa kwa mchezo mmoja wa ufunguzi kati ya Manchester United na mabingwa wa msimu wa 2015/16, Leicester City.

Kuelekea ufunguzi wa msimu mpya wa EPL, tunaangazia wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kuibuka wafungaji bora wa ligi hiyo msimu huu kutokana na rekodi zao za kufumania nyavu kwenye misimu kadhaa iliyopita.

Mohamed Salah, Alifunga jumla ya magoli 44 katika mashindano yote msimu uliopita ambapo 32 kati ya hayo ni ya EPL na kuibuka mshindi wa kiatu cha dhahabu, anaweza kurudia tena moto huo msimu huu kutokana na kiwango chake katika mechi za maandalizi ya msimu alizocheza mpaka sasa.

Harry Kane, Kijana huyo Muingereza alifunga magoli 30 ya EPL Msimu uliopita, mawili nyuma ya kinara, Mo Salah. Majeraha aliyoyapata katikati ya msimu uliopita yalimrudisha nyuma kasi yake ya kufunga, lakini sasa yuko vizuri, ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia iliyomalizika nchini Urusi na huenda msimu ujao akafanya makubwa na kushinda tuzo hiyo kama alivyofanya mara ya mwisho msimu wa 2016/17.

Sergio Aguero, Amekuwa thabiti katika ufungaji kwa misimu minne sasa, akifunga magoli si chini ya 20 kila msimu, msimu uliopita alifunga magoli 21 licha ya kubadilishana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na mchezaji chipukizi Gabriel Jesus. Aguero ataiongoza tena Man City msimu huu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa EPL kwa mara ya pili mfululizo.

Jamie Vardy, Amekuwa na misimu bora sana tangu alipopanda na Leicester City kwenye ligi kuu ya EPL msimu wa 2014/15, alifunga jumla ya magoli 20 msimu uliopita na endapo ataongeza ubora wa kasi yake na umakini wa kufunga kwenye msimu huu anaweza kuwa ni mshindani wa tuzo hiyo.

Romelo Lukaku, Alifunga magoli 16 pekee msimu uliopita huku kinara akiizidi mara mbili idadi yake, anayo nafasi kubwa ya kuibuka mshindi wa kiatu cha dhahabu msimu huu endapo atatumia vizuri nguvu na kasi alivyonavyo katika kutafuta magoli.

Pierre-Emerick Aubameyang, Alijiunga na Arsenal mwezi Januari mwaka huu na kufanikiwa kufunga magoli 10 katika mechi 13 za EPL alizocheza , akipata nafasi ya kucheza mechi nyingi msimu ujao anaweza kufungunga magoli mengi zaidi yatakayomsaidia kuibuka na ushindi wa tuzo hiyo.

KWAHERI KING MAJUTO.



Msanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia wakati akipokea matibabu kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Dar es Salaam Tanzania.
Mzee majuto leo safari yake ya kuelekea Kuhifadhiwa Huko Tanga ilianzia katika ukumibi wa Karimjee ambapo viongozi mbali mbali wakiwemo wastaafa na wakuu wengine wa nchi wakiongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA Mh Dkt John Pombe Magufuli wameshiri katika kuuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa nguli huyo wa sanaa ya uchekeshaji nchini na afrika mashariki.

MBUNGE MATIKO NA MWANAHABARI SITTA TUMA WAACHIWA KWA DHAMANA.

Ester Matiko.
Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, mwandishi wa habari Sitta Tuma na wafuasi wengine 14 wa Chadema waliokuwa wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano usio halali wameachiwa na kutakiwa kuripoti Polisi kesho.
Mwandishi wa habari Sitta Tuma.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 9 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya Henry Mwaibambe amesema polisi iliwataka wafuasi hao na viongozi watawanyike kwa kuwa mkutano huo siyo halali.

Matiko, Tuma na wafuasi hao walikamatwa na polisi jana wakati wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa chama hicho Kata ya Turwa.

“Nilipokea barua jana kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Turwa ya kusitishwa kwa kampeni za chaguzi za Chadema lakini chama hicho kilikaidi licha ya kupewa barua ya kusitisha mkutano”, amesema Kamanda.

Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa, “Polisi tulipewa barua ya zuio la mkutano ikionyesha kuwa Chadema wamekiuka kifungu cha 124 A cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi,kamati ya maadili ya uchaguzi Kata ya Turwa kupitia kikao kilichoketi Agosti 8,2018 kilichowashirikisha na viongozi wa siasa kilisitisha kampeni za Chadema,”.

Mwaibambe amedai mbunge Matiko alitakiwa kuondoka eneo hilo lakini aligoma na kuanza kutukana polisi na hakuna yeyote aliyepigwa wakati wanakamatwa na kupandishwa kwenye gari.

UTORO:- BABA AMPIGA MWANAYE HADI KIFO.

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi  jijini Mwanza, Mariamu Tabu (18) amefariki dunia kwa kile kilichodaiwa ni kupigwa na baba yake mzazi baada ya kutohudhuria shuleni.
Akizungumza na wanahabari leo Agosti 9, Kamanda wa Polisi jijini humo Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kituo cha Misungwi na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Kamanda Msangi amesema kuwa mama mzazi wa Mariam, Kija Mashauri amelieleza Jeshi la Polisi kuwa Agosti 6, mwanaye alikwenda shule lakini hakurudi nyumbani badala yake alirudi Agosti 7 jioni, ndipo baba yake aliuliza alipokuwa na kuanza kumpiga.

“Baba tayari tumemkamata kwa ushirikiano na wananchi, mara baada ya kutekeleza tukio la kumoiga mwanae alitaka kukimbia akazuiwa na wanakijiji, ambapo walimuwahisha mtoto katika zahanati ya kijiji kwakuwa alikuwa katika hali mbaya alifariki akiwa mapokezi”, amesema Msangi.

Juni 16, 2018 katika kilele cha siku ya Mtoto wa Afrika, ambayo kitaifa ilifanyika mkoani Arusha ambapo Tanzania ikitajwa kuongoza katika vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kuliko uovu unaofanywa kwenye ujambazi, takwimu zilizowasilishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dkt. Faustine Ndugulile, zinaeleza kuwa watoto 41,000 walifanyiwa ukatili katika kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi sasa, na kati yao 3,467 waliripotiwa kuanzia Januari hadi Disemba 2017.

Lakini pia, Idara ya Ustawi wa Jamii wizarani hapo, ilieleza kuwa asilimia 60 ya ukatili dhidi ya watoto unafanyika nyumbani, asilimia 33 ni shuleni na iliyobaki ni maeneo mengine.

Thursday, August 9, 2018

KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI TARIME : OJADACT YAOMBA WAANDISHI KUKUTANA NA SIRRO



GSENGOtV

OJADACT YASIKITISHWA   NA KITENDO CHA JESHI LA POLISI KUMSHIKILIA MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA SITTA TUMMA.

Chama Cha Waandishi wa Habari  wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania..(OJADACT), kimeshitushwa na taarifa ya kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari Sitta Tumma, anayeandikia Gazeti la Tanzania Daima.


Tumma alikamatwa kwenye mkutano wa siasa wa chama cha CHADEMA hapo Jana Agosti 8, alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kutafuta taarifa km ilivyoainishwa kwenye ibara ya 18 ya KJM na sheria ya haki ya kupata taarifa 2015.

OJADACT , inatambua kuwa, mkutano ya siasa ipo kisheria kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na kanuni zake za usajili wa vyama vya siasa, uwepo wa mwandishi kwenye tukio pia upo kisheria kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba, ambayo ndiyo sheria mama ya Nchi.

Mwandishi aliyekamatwa pia alikuwa na kitambulisho cha kumtambukisha kuwa, yeye ni Mwandishi wa habari.

Lakini licha ya kujieleza bado alishikiliwa na kulala kituo cha polisi, na kumsababishia usumbuvu usiokuwa na faida kwa jamii.

OJADACT, tumesikitishwa saba na tukio hilo linalokiuka misingi ya haki za binadamu na sheria za mbalimbali za Nchi na pia kuwa na sura ya kuminya Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.

Chombo cha habari kina dhima kubwa ya kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha na dhima ya kisasa ya kukosoa kwa upande chanya na hasi.

Tunaliomba Jeshi la polisi Nchini, kupitia kwa RPC wa Tarime na Rorya na IGP kuliingilia kati suala hilo na kuhakikisha Mwandishi Sitta Tumma anaachiwa huru, ili aendelee na majukumu yake ya kikazi.

Pia OJADACT inasisitiza vyombo vya habari kuwaandalia Waandishi wake vikoti maalumu press jackets zinazowatambukisha kwa urahisi Waandishi wawepo eneo hatarishi la kutafuta habari.

Tuna imani Sitta Tumma ataachiwa huru kwa kupewa dhamana, kwa kuwa,dhamana ni haki ya msingi km ilivyoaninishwa kwenye sheria ya makosa ya mwenendo wa jinai (CPA).

 EDWIN SOKO 
 MWENYEKITI 
 OJADACT
 9/8/2018

KWAHERI MUIBIZAJI MKONGWE KING MAJUTO.

Mkongwe wa tasnia ya vichekesho nchini Mzee King Majuto amefariki jana jioni ya tarehe 8/08/2018 akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokua amelazwa.


Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zimethibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyo wa sanaa ambaye amejizolea umaarufu kila pembe ya Nchi yetu.

Taarifa zaidi ya wapi ulipo msiba na taratibu zote za mazishi zitakujia baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.

Wednesday, August 8, 2018

WAKILI MWESIGWA: WAZEE CHUKUENI HATUA MNAPOONA UONGOZI WA CCM UNAYUMBA KATIKA MAENEO YENU


Na Mwandishi Wetu
Wazee wameshauriwa kutokaa kimya na badala yake kuchukua hatua madhutubi wanapoona uongozi unayumba katika kusimamia uhai na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo yao.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mwanasheria wa CCM, Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Zaidi wakati akizungumza kwenye kikao cha Wazee, katika Tawi la CCM la Muloganzira lililopo Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amewasihi Wazee hao kuhakikisha wanakemea tabia inayoanza kuota mizizi ndani ya CCM ya kumtegemea mtu badala ya Chama, tabia ambayo alisema ni hatari sana kwa uhai wa CCM kwa kuwa wengi wanaopenda kusujudiwa ndani ya Chama ni watoa rushwa na mafisadi.

Wakili Mwesigwa mewaomba wazee kuwashawishi watoto wao wenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi mbalimbali ndan ya CCM kujitokeza na wasiwe na hofu kwa sababu uongozi wa juu wa CCM uko imara kuhakikisha hakuna mtoa rushwa wala fisadi yeyote atakayenunua uongozi ndani ya CCM.

Amewataka kuziunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akissisitiza kuwa ndiyo njia salama ya mafanikio kwa watoto wao waliowasomesha  katika mazingira magumu. 

"Ndani ya CCM hakuna mtu maarufu wala nguvu zaidi ya CCM isipokuwa CCM yenyewe. Waliondoka wengi lakini CCM imezidi kuwa imara zaidi ilivyokuwa siku za nyuma", alisema Mwesigwa.

Akizungumzia kuhusu rushwa na ukiukwaji wa maadili ndani ya CCM Wakili Mwesigwa amesema CCM ina mkono mrefu na uchafu huo unashughulikiwa ipasavyo na na hivyo kuwasihi wazee hao wazidi kuwa na imani na CCM, Rais Maguli na serikali kwa jumla.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwa lengo la wazee kutadhmini uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM  katika tawi hilo la Mulonganzira, Wakili Mwesigwa alihudhuria kwa kwaliko wa wazee hao kuwa mgen rasmi na mtoa mada kuhusu itikadi ya Chama.

MOURINHO AKALIA KUTI KAVU MANCHESTER UNITED.



GSENGOtV
Hizi ni tetesi lakini zinaonekana zina ukubwa sana, Jose Mourinho ni moja ya makocha ambao wanapewa nafasi kubwa sana kutimuliwa msimu huu wa ligi kama hatafanya vizuri.

Na sio utani United hawataki kuburuzwa tena hawako tayari kuona timu kama Manchester City au Chelsea wanachukua tu kombe mbele yao kila kukicha huku wao United wanabaki kama wasindikizaji.

Lakini kitendo cha Manchester United kumtimua Jose Mourinho(kama wakifanya hivyo) baasi itawagharimu kiasi kikubwa sana cha fedha.

Manchester United watahitajika kulipa kiaso cha £12m kwa kocha huyo wa Kireno ambapo kiasi hicho ni sawa na mshahara wake wa mwaka mzima na haijalishi atatimuliwa mda gani bali pesa hiyo anapswa kupewa.

Jose Mourinho alisaini mkataba mpya na United utakaomuweka hadi mwaka 2020 lakini klabu hiyo ili kuogopa hasara waliamua kuweka kipengele katika mkataba wake ambacho hawatampa pesa yote ya mkataba wake kama utaishia katikati.

Tangu ajiunge na Manchester United Jose Mourinho ameshacheza mechi 120 huku kati ya hizo akishinda michezo 74 suluhu 25 na amefungwa michezo 21.

Manchester United ni klabu ambayo haitaki makombe madogo dogo na target kubwa ya klabu imekuwa makombe makubwa kama Championd League na Epl ambayo hawajawahi yapata toka Fergie aondoke huku pesa wanayotumia ya usajili ikiwa kubwa.

Orodha ya Makocha na pesa walizotumia tangu Ferguson aondoke.

David Moyes. Moyes ndiye alikuwa mrithi wa Fergie United na alipojiunga tu alipewa pesa akamnunua Marouane Fellaini kwa £27.5 kutokea Everton kisha Juan Mata kutoka Chelsea.

Louis Van Gaal. Baada ya Moyes mikoba ikaenda kwa Van Gaal ambaye aliwanunua Ander Herrera £32.4m kutoka A Bilbao, Luke Shaw £27m kutoka Southampton, Marcos Rojo £16m kutoka Sporting, Angel Di Maria £60m kutoka Real Madrid, Daley Blind £14m kutoka Ajax na kwa ujumla alitumbua £149m.

Msimu wa 2015/2016 akamnunua Depay kwa £25m(Psv Endhoven), Matteo Darmian £12.7m(Torino), Bastian Schweinsteiger £6.5m, Morgan Schnedelin £25m(Southampton), Anthony Martial £58m(Monaco).

Jose Mourinho. Baada ya LVG kutimuliwa ndipo Mourinho akachukua mikoba yake akaanza na Eric Bailly £30m(Villareal), Ibrahimovich free(PSG), Henrikh Mkhitaryan £27m(Borussia Dortmund), Paul Pogna £89m(Juventus) jumla £146m.

Msimu wa 2017/2018 akamnunua Romelu Lukaku £75m (Everton), Victor Lindelof £30(Benfica), Nemanja Matic £35m(Chelsea), jumla hapa akatumia £140m na hadi sasa ameshamnunua Fred

Kwa ujumla makocha hawa watatu wametumia kiasi cha zaidi ya £600m tangu Ferguson aondoke na hii inawafanya United kutokuwa na huruma pale kocha akishindwa kuwapa wanachotaka.

TANZIA: BINGWA WA DUNIA WA MBIO ZA MITA 400, NICHOLAS BETT AFARIKI DUNIA.


BINGWA wa Dunia wazamani wa mbio za mita 400, Nicholas Bett amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea hii leo siku ya Jumatano majira ya asubuhi huko Nandi.

Kamanda wa polisi wa County ya Nandi nchini Kenya, Patrick Wambani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo hii leo majira ya asubuhi.

Bett amekuwa mwanariadha wakwanza kutoka Kenya kushinda ubingwa wa Dunia kwakutumia muda wa dakika 47 na sekunde 79 kwenyemichuano ya iliyofanyika Beijing nchini China mwaka 2015.

Lakini pia mwanariadha huyo wa Kenya aliwahi kuvunja rekodi ya dunia katika kukimbiza upepo baada ya kutumia dakika 48 na sekunde 24.

Nicholas Bett akiwa amezaliwa Januari 27, 1990 ni mtoto wa pili kwenye familia yao yenye watoto watatu. Kaka yake Haron Koech akiwa kwenye timu ya taifa ya Kenya ya Olympics huku marehemu akiwa ameacha mke na watoto watatu.

'WANAUME KUOGOPA KUPIMA TEZI DUME KISA AIBU NI UJINGA' HAYA YABAINIKA UZINDUZI WA KLINIKI ZA JIONI BUGANDO

NA. GSENGOtV
Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku, Kushindwa kuzuia mkojo, yaani ukichelewa kidogo unaweza kukutoka bila breki, Maumivu wakati wa kukojoa, Kuishiwa nguvu za kiume, Kupungua kwa uwingi wa mbegu (low sperm count), Maumivu wakati unafika kileleni, Damu kutokea kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiume, Maumivu nyuma ya mgongo au hata nyonga nk basi uonapo dalili hizo unaweza kuanza kuhisi una saratani ya tezi dume.
Kupitia dalili hizo ni wazi kwamba afya ya mgonjwa itakuwa matatani kwenye mataabiko.
Wahenga walironga mficha maradhi kifo humuumbua. Kila kiungo cha mwanadamu kikipata tatizo ni jukumu la matabibu kufanya uchunguzi na kutoa huduma kwa eneo lililodhurika, Haiingii akilini kwamba uendelee kuteseka ile hali tiba ipo. Nao wataalamu wanasema uchunguzi wa kutumia kidole hauhitaji gharama kubwa kama ilivyo njia nyingine za kutumia vifaa maalum vya uchunguzi.
Ni tamaduni tu za watu wenye mawazo machafu ndizo zinazo wafanya wengi kudhani kipimo cha kidole ni udhalilishaji, lakini madaktari waliosomea fani hiyo wanasema kuwa ni njia ya kawaida sana.
Kwa kuliona hilo Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza imezindua hudumu za kliniki za muda wa jioni kwa siku za wikiendi na sikukuu, lengo likiwa ni kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi wote ambao watahitaji huduma za kibingwa muda wote.
Hasa wale ambao hawawezi kufika hospitali kutokana na kubanwa na kazi. Fuatilia kile kilichojiri katika uzinduzi ikiwa ni pamoja na mashuhuda wanaume wa Tezi dume.
Huduma za uchukuaji vipimo zikiendelea katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza 
Licha ya kuwa na idadi kubwa ya wahitaji wa kupima afya, idadi ya madaktari wahudumu wa afya iliendana na kasi.
Huduma rafiki.
Hakuna jambo lililojema kama kuijua afya yako.
Meza na meza vitengo kwa vitengo katika Uzinduzi wa Huduma za Kliniki za Jioni za Bure Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Bibi akipata vipimo.
Jeh urefu wako unalingana na uzito wa mwili wako?
Jeh urefu wako uanalingana na uzito wa mwili wako?
Afya muhimu.