ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 10, 2018

MBUNGE MATIKO NA MWANAHABARI SITTA TUMA WAACHIWA KWA DHAMANA.

Ester Matiko.
Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, mwandishi wa habari Sitta Tuma na wafuasi wengine 14 wa Chadema waliokuwa wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano usio halali wameachiwa na kutakiwa kuripoti Polisi kesho.
Mwandishi wa habari Sitta Tuma.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 9 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya Henry Mwaibambe amesema polisi iliwataka wafuasi hao na viongozi watawanyike kwa kuwa mkutano huo siyo halali.

Matiko, Tuma na wafuasi hao walikamatwa na polisi jana wakati wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa chama hicho Kata ya Turwa.

“Nilipokea barua jana kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Turwa ya kusitishwa kwa kampeni za chaguzi za Chadema lakini chama hicho kilikaidi licha ya kupewa barua ya kusitisha mkutano”, amesema Kamanda.

Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa, “Polisi tulipewa barua ya zuio la mkutano ikionyesha kuwa Chadema wamekiuka kifungu cha 124 A cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi,kamati ya maadili ya uchaguzi Kata ya Turwa kupitia kikao kilichoketi Agosti 8,2018 kilichowashirikisha na viongozi wa siasa kilisitisha kampeni za Chadema,”.

Mwaibambe amedai mbunge Matiko alitakiwa kuondoka eneo hilo lakini aligoma na kuanza kutukana polisi na hakuna yeyote aliyepigwa wakati wanakamatwa na kupandishwa kwenye gari.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.