ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 26, 2019

WANAFUNZI WATALII KISIWA CHA SAANANE.

Mwongoza watalii qa Hifadhi ya Saanane Michael Pascal kuwapa maelezo wanafunzi na walimu wa Kilimani Sekondari walipotembelea hifadhi hiyo. 
Walimu wa Shule ya Kilimani  Sekondari  wakiwa wamevalia maboya kujiokolea kabla ya kupanda boti kuekelea Hifadhi ya Saanane jana.


 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani wakiwa wameruka juu ya mwamba eneo la Jumping Stone katika Hifadhi ya Saanane jana.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi  (kulia) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani wakionyesha umakini wa kuruka juu kwenye mwamba wa Jumping Stone katika Hifadhi ya Saanane. 
 Mwongoza watalii katika Hifadhi ya Saanane Michael Pascal akiwapa maelezo Wanafunzi na walimu wa Kilimani Sekondari ikiwemo Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi, kushoto mwenye kofia walipotembelea hifadhi hiyo jana.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi (mwenye kofia) akizungumza jambo wakati wa ziara ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani kutembelea Hifadhi ya Saanane jana .Mnandi ndiyo aliyefadhili ziara hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd,Mnandi Mrutu Mnandi wa nne kutoka kulia akishiriki pamoja na wanafunzi wa Shule ya Kilimani Sekondari, kuruka juu ya mwamba (Jumping Stone) katika Hifadhi ya Saanane. Wa tatu kutoka kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Gerana Majaliwa.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd, Mnandi Mrutu Mnandi aliyeketi kuahoto,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani Gerana Majaliwa  (kulia) walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza mwongoza watalii qa Hifadhi ya Saanane, Michael Pascal ,aliyesimama.
Boti za Hifadhi ya Saanane zikiwa zimewabeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani kwenda kutembelea Hifadhi ya Saanane jana  kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi.  Picha zote na Baltazar Mashaka 

KAMA UNATAKA KUFUGA NYATI MAJI 'MILANGO IKO WAZI NJOO UCHUKUWE MBEGU SERIKALINI'



Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza lilianzishwa mnamo mwaka 1966 baada ya Uhuru wa Tanganyika kwa ajili ya kuzalisha F1, hii ilikuja baada ya kugundua kuwa wafugaji wachache waliopewa ng’ombe wa kisasa kutoka Ulaya, wengi wao walishindwa kuwamudu wakafa ndipo wataalamu wa Mifugo waliokuwepo enzi hizo wakaona ni vyema kuzalisha ng’ombe wa maziwa wanaoweza kuhimili mazingira ya nyanda za nchi zenye joto ikiwemo Tanzania.

Shuhudia ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akizuru Shamba hilo la Mabuki kama sehemu ya mwendelezo wa Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji viumbe kwenye maji 2020 – 2025 ambapo pia amepata fursa ya kuwaona Nyati Maji wanaofugwa kituoni hapo, mbegu iliyoingizwa nchini enzi za utawala wa Rais wa Kwanza nchini Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere. Kwa wale wanaotaka kufuga Nyati hao, kitambo sana Serikali ilishafungua milango.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina.
Pia shamba la Mifugo la mabuki linafuga Mbuzi wa maziwa (hawapo pichani) aina ya Toggenburg wenye uwezo wa kutoa kati ya lita moja na nusu kwa mkamuo mmoja yaani lita 3 kwa siku, kiwango kinachozidi uwezo wa ngombe wa kienyeji anayekamuliwa lita 1 kwa mkamuo na lita 2 kwa siku.


Ng'ombe hasa madume yananunuliwa kwa wingi sana na wafugaji kwaajili ya mbegu.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akipata maelekezo toka kwa Meneja Msaidizi wa Shamba la mifugo la Mabuki ambaye pia ni Afisa Mifugo Daraja la Kwanza Pascal Godwin Bahemu (mwenye kofia).
Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, lina ukubwa wa Hekta 9,773, ambapo mpaka hivi sasa shamba linauwezo wa kuzalisha ng'ombe 580 kwa mwaka yaani wastani wa 320 majike na 260 madume.


TAFITI ZA AWALI. Kwa tafiti za URT za Mwaka 2015, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ikiwa na ng'ombe milioni 25, mbuzi milioni 16.7, kondoo milioni 8, nguruwe milioni 2.4, na kuku milioni 36. Kati ya ng'ombe milioni 25 ng'ombe wa asili ni 98%. Hivyo, ni 2% tu ya ng'ombe wote Tanzania wanaofugwa kwa mfumo wa ufugaji wa kisasa. Tafiti hizo zinaonesha kuwa ufugaji wa asili unachangia 7.4% ya pato la Taifa na ongezeko la ukuaji la 2.2% kila mwaka. Ufugaji wa asili umethibitika kiuchumi kuwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira. Ufugaji wa asili unategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kwa kuendesha maisha yao; iwe kwa chakula, mavazi, na maendeleo kwa mapana yake. Mchango wake katika uchumi rasmi na usio rasmi (informal and formal economies) ni dhahiri hasa kupitia kodi na tozo mbalimbali katika masoko ya mifugo, usafirishaji wa mifugo, ukaguzi wa mifugo, na upatikanaji wa malighafi kwa matumizi ya viwanda mbalimbali.

VIDEO MPYA TOKA KWA MZUNGU KICHAA.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Mzungu Kichaa amerudi na singo mpya.  You Got Me ni wimbo ya mapenzi inayogusia hitaji la kupendwa kwa kila mwanadamu.

Mashairi na upigaji stadi wa gitaa na bass kutoka kwa Mzungu kichaa vimebeba wimbo. You Got Me ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye album mpya ya Mzungu Kichaa inayoitwa “Huyu nani” itakayotoka mapema mwaka 2020.

We don’t have time (hatuna muda) / To take it slow (kuwa watulivu) / Cos the future (sababu kesho yetu) / We will never know (hatuijui)
Be open (uwe muwazi) / Be free (uwe huru) / Take a chance (itumie nafasi hii) /Jump on to the other side with me (ruka upande wa pili pamoja nami)

Khalid Kumbuka aka KK, ni kaka mdogo wa Adili mmoja wa waasisi wa kundi la kwanza la Hipihop Tanzania Kwanza Unit, ambaye alifariki katika ajali mbaya ya gari Dar es salaam mwaka 1992. Mzungu kichaa alipokuja Tanzania katikati ya miaka ya 90 mama yao Margarethe Kumbuka ndiye alimfundisha Kiswahili katika shule ya sekondari Dar es Salaam. Baada ya kuhamia London kusoma Chuo kikuu na mama Margarethe alihamishiwa chuo hicho hicho kufundisha Kiswahili na wote wakafanya masters pamoja. Baadae Mzungu kichaa alipogundua kipaji cha Khalid Kumbuka kwenye uandishi na kutumbuiza, ilikuwa rahisi kumualika studio na kufanya kazi pamoja.

Magitaa mawili yamechanganywa kwenye kiitikio na kutoa hisia ya kipee kutokana na upigaji wa gitaa wa Mzungu kichaa. Aina ya sauti ambayo amekuwa akiitengeneza tangu siku za awali kwenye Bongo Flava ambapo mtiririko wake wa gitaa ulisikika kwenye She Gatta Gwan wa Mangwaire na Mambo ya Pwani ya Solo Thang. Kwenye You Got Me, P Funk Majani alimjaribu Mzungu Kichaa kupiga gitaa la Bass na kuongezea ubunifu wake kwenye kuzalisha maadhi ya Trap hi-hat na kiki nzuri na snare. Pasipo shaka hii ni kazi bora iliyotokana na uzoefu wa muda mrefu.

CREDITS
Track: You Got Me
Featuring: KK, Grace Matata
Produced by: Mzungu Kichaa and P Funk Majani
Recorded at: Caravan Records and Bongo Records
Mixed by: P Funk Majani
Mastered by: Jacob Brondlund
Record Label: Caravan Records
Video Director: Jessica Maria Olsen
Video Editor: Carlo Kamin
Video Grading: Justin Campos

Ben Pol - Sikukuu (Official Music Video)


Ben Pol perfoming Sikukuu (Christmas) which was originally performed by George Kinyonga & Orchestra Jobiso. Enjoy! Video Directed by : Adam Juma (Tanzania)

Wednesday, December 25, 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA  KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA ULINZI  NA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA  KUHAKIKISHA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA ZINASHEHEREKEWA KWA AMANI NA UTULIVU. HIVYO TUWATOE HOFU WANANCHI NA WAGENI WATAKAOTEMBELEA MKOA WETU KWAMBA ULINZI UMEIMARISHWA  WA WAO NA MALI ZAO.

AIDHA TUTAHAKIKISHA NYUMBA ZOTE ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE  ULINZI UNAIMARISHWA VYA KUTOSHA KWANI ASKARI WATAKUWA KATIKA DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI, MBWA NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE YA JIJI NA  MKOA WA MWANZA, HIVYO WANANCHI WASIWE NA HOFU YOYOTE  PINDI WATAKAPOKUWA KWENYE IBADA AU BURUDANI MBALIMBALI. PIA TUWATAKE WANANCHI WANAPOKWENDA KATIKA MIKESHA YA SIKUKUU HIZI WASIACHE  NYUMBA ZAO BILA UANGALIZI  AU KIZIACHA WAZI KWANI KUNAWEZA KUSHAWISHI WEZI.

PIA TUWAKUMBUSHE WAZAZI NA WALEZI KUWA PAMOJA NA KUSHEREKEA SIKUKUU HIZI WASISAHAU MAJUKUMU YAO YA KUWA MAKINI NA WATOTO WAO KWA KUTOWAACHA PEKE YAO BARABARANI NA KATIKA SEHEMU ZA MICHEZO MFANO MAENEO YA BEACH/MIALO, DISKO TOTO NA KWENYE BEMBEA. PIA NI MARUFUKU KWA MAREVA  WA VYOMBO VYA MOTO KUENDESHA WAKIWA WAMELEWA AU MWENDO KASI, ENDAPO IKIBAINIKA HATUA STAHIKI  ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO. HATA HIVYO KWA WALE WENYE TABIA YA KUCHOMA MATAIRI BARABARANI WAACHE KWANI NI KOSA KISHERIA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MWANZA NA WATANZANIA KWA UJUMLA SIKUKUU NJEMA YA KRISMASI NA MWAKA MPYA. LAKINI PIA KUSHEHEREKEA SIKUKUU HIZO KWA AMANI NA UTULIVU.

IMETOLEWA NA;
Muliro J. MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
24 DESEMBA, 2019.

Tuesday, December 24, 2019

MAGUFULI AIBUA SHANGWE KRISMASI WAFANYAKAZI WAMTAKA WAZIRI MPINA KUFUNGA NATI UVUVI HARAMU


WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kuchakata mabondo cha HONGLIN INTERNATIONAL TRADE DEVELOPMENT cha jijini Mwanza wamepaza sauti zao na kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ilivyopambana na Uvuvi Haramu na kuwezesha kupatikana malighafi za kutosha zilizowezesha kupatikana kwa ajira ya uhakika viwandani.

Wameitaka Serikali kuendelea kufunga nati ili kuwabana wavuvi haramu ili rasilimali za uvuvi ziongezeke mara dufu na kuwezesha viwanda zaidi kwani sasa ajira zimeongezeka kutokana na ongezeko la samaki.

Waziri wa mifugu na uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia kuwa Serikali iko imara na itaendelea kulinda rasilimali hizo ili ziweze kutumika kwa manufaa ya Watanzania wote.

Monday, December 23, 2019

EH BAN Eeee... MWANZA KUSHEREHEKEA CHRISTMAS HAPA.


Kama ikatokea uko ndani ya Jiji la Mwanza Christmas hii ya 2019 basi hili ndilo eneo la kujimwaga na kujiachia ukila 'KITU BILI KWA JIWE MOJA'

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI, CP LIBERATUS SABAS, AMEFUNGA MAFUNZO YA ASKARI WA KIKOSI MAALUM CHA ULINZI MPAKA WA TANZANIA NA MSUMBIJI PAMOJA NA ULINZI WA AMANI KIMATAIFA KILELEPORI NA WEST KILIMANJARO.


 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na wakufunzi wa askari wa Kikosi Maalum kitakachosimamia Ulinzi wa Amani katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji huko mkoani Mtwara katika Mto Ruvuma ambapo kumekuwa kukitokea mauaji ya mara kwa mara kwa raia wema yaliosababishwa na wahalifu kutoka Nchini jirani ya Msumbiji. (Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akiongea na askari  wanaohitimu mafunzo ya usimamizi wa Ulinzi katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji yaliofanyika katika pori la West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.(Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akimkabidhi cheti cha ukufunzi bora Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP William Mwampagale wakati akifunga mafunzo ya askari wa Ulinzi wa Amani Kimataifa Kilelepori mkoani Kilimanjaro.(Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas wa tatu kutoka kushoto kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakufunzi wa ndani pamoja na wakufunzi wa umoja wa kimataifa baada ya kufunga mafunzo Kilelepori mkoani kilimanjaro. (Picha na Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na wakufunzi wa Askari wa Kikosi Maalum kinachotarajiwa kujiunga na vikosi vingine vya Ulinzi wa Amani Kimataifa kwaajili ya kusimamia amani katika nchi au mataifa yenye migogoro. (Picha na Jeshi la Polisi)