KATIKA
KUELEKEA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA
ULINZI NA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA KUHAKIKISHA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA
ZINASHEHEREKEWA KWA AMANI NA UTULIVU. HIVYO TUWATOE HOFU WANANCHI NA WAGENI WATAKAOTEMBELEA
MKOA WETU KWAMBA ULINZI UMEIMARISHWA WA
WAO NA MALI ZAO.
AIDHA
TUTAHAKIKISHA NYUMBA ZOTE ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE ULINZI UNAIMARISHWA VYA KUTOSHA KWANI ASKARI
WATAKUWA KATIKA DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI, MBWA NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE YA
JIJI NA MKOA WA MWANZA, HIVYO WANANCHI
WASIWE NA HOFU YOYOTE PINDI WATAKAPOKUWA
KWENYE IBADA AU BURUDANI MBALIMBALI. PIA TUWATAKE WANANCHI WANAPOKWENDA KATIKA
MIKESHA YA SIKUKUU HIZI WASIACHE NYUMBA
ZAO BILA UANGALIZI AU KIZIACHA WAZI
KWANI KUNAWEZA KUSHAWISHI WEZI.
PIA
TUWAKUMBUSHE WAZAZI NA WALEZI KUWA PAMOJA NA KUSHEREKEA SIKUKUU HIZI WASISAHAU
MAJUKUMU YAO YA KUWA MAKINI NA WATOTO WAO KWA KUTOWAACHA PEKE YAO BARABARANI NA
KATIKA SEHEMU ZA MICHEZO MFANO MAENEO YA BEACH/MIALO, DISKO TOTO NA KWENYE
BEMBEA. PIA NI MARUFUKU KWA MAREVA WA
VYOMBO VYA MOTO KUENDESHA WAKIWA WAMELEWA AU MWENDO KASI, ENDAPO IKIBAINIKA
HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA
DHIDI YAO. HATA HIVYO KWA WALE WENYE TABIA YA KUCHOMA MATAIRI BARABARANI WAACHE
KWANI NI KOSA KISHERIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA
MWANZA LINAWATAKIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MWANZA NA WATANZANIA KWA UJUMLA
SIKUKUU NJEMA YA KRISMASI NA MWAKA MPYA. LAKINI PIA KUSHEHEREKEA SIKUKUU HIZO
KWA AMANI NA UTULIVU.
IMETOLEWA NA;
Muliro
J. MULIRO- ACP
KAMANDA
WA POLISI (M) MWANZA.
24 DESEMBA, 2019.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.