USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 5 MOTO UMETOAKEA KTK SOKO LA KILIMAHEMA KWA MSUKA. MALI, NAFAKA NA BIDHAA MBALIMBALI ZIMETEKETEA NA MOTO HUO AMBAPO CHANZO CHAKE INA SEMEKANA KUWA MOTO HUO ULIANZIA KUTOKA MOJA YA MABANDA YA MAMA LISHE SOKONI HAPO AMBAYE ALIACHA MAJIVU YENYE MOTO KTK BANDA LAKE.
MAMA HUYU MOTO ULIPOTOKEA MAJIRA HAYO YA USIKU, MUME WAKE ALIWAHI SOKONI HAPA KUOKOA MALI, LICHA YA KUOKOA MALI HIZO TOKA BANDANI HAKUAMBULIA CHOCHOTE KWANI WAKATI YEYE AKIOKOA NA KUHIFADHI SEHEMU, VIBAKA NA WANANCHI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO WAKIDAI KUTOA MSAADA WANAPITIA, MWISHO WA SIKU AKAJIKUTA NA MIKUNGU MIWILI TU YA NDIZI. MTAJI WAKE WOTE WA SHILINGI LAKI TATU UMETEKETEA.
NGOJA NAMI NIOKOTE HIKI AAAH MBOGA MEZANI.
MABANDA YAMEANGUKA NJIA ZIMEZIBIKA.
MAMBO MPWITO MPWITO.
MDAU INGAWA MALI YAKE YOTE KWISHNI, JAPO BATI ZAKE.
KUFA KUFAANA NA SIO KUFANANA, WATOTO NA AKINA MAMA WAKIWA WAMEBEBA VIJIFUKO KUOKOTA MASALIA YA NAFAKA.....
TATIZO KUBWA HAPA NI KUTOKUWA NA MPANGILO KUTENGANISHA BIASHARA. BANDA LA KWANZA UTAKUTA NI LA MITUMBA, LINALOFUATA MAMA LISHE KISHA NYANYA NA MBOGAMBOGA, LINGINE NAFAKA, LINALOFUATA TENA MAMALISHE MBELE WACHUUZA SAMAKI. JE KUNA USALAMA HAPO?
TASAF YAJENGA STENDI YA MABASI LUNDUSI KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI KWA
WANANCHI
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songea
MRADI wa Ujenzi wa Stendi ya mabasi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) katika Kijiji cha Lundusi w...
1 hour ago