ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 15, 2023

HII IMEENDA 'KUMBE NA RAIS SAMIA NAYE YANGA' MUSUKUMA ATETEMA KAMA MAYELE

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Wakati mashabiki na wanachama wa Yanga wakiwa na hofu juu ya hatma ya mshambuliaji wao hatari raia wa Congo DR, Fisto Mayele kama ataendelea kuwepo msimu ujao, mwanachama na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku 'Musukuma' amedokeza alichozungumza na Rais wa Klabu hiyo, Hersi Said juu ya hatma ya mkongomani huyo. Musukuma akizungumza leo katika uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi amesema amekuwa akifanya mazungumzo ya mara kwa mara na Rais Hersi ambaye amemuhakikishia kuwa wananchi wataendelea kupata burudani ya kutetema msimu ujao. Bila kutaja jina la Mayele, Musukuma ametumia lugha ya ishara akionyesha stairi ya ushangiliaji ya Mayele huku mashabiki na wanachama wa timu hiyo waliojitokeza katika uzinduzi huo uliofanyika Furahisha Wilayani Ilemela mkoani Mwanza wakimuunga mkono kwa kutetema.













YANGA YAFANYA KUFURU JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Wiki ya Mwananchi imezinduliwa rasmi leo jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha, kata ya Kirumba wilayani Ilemela, ikiambatana na zoezi la uchangiaji damu na kutoa misaada mbalimbali, huku kilele chake kikitarajiwa kuwa Julai 22, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Friday, July 14, 2023

MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI UJERUMANI WAWASILI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA BOMBO

  

Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman katikati akiwa na madaktari kutoka nchini Ujerumani waliowasili kwa ajili ya  kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman katikati akizungumza jambo na madaktari kutoka nchini Ujerumani waliowasili kwa ajili ya  kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).

Sehemu ya wananchi wakisubiri huduma 


Na Oscar Assenga, Tanga

MADAKTARI Bingwa kutoka nchini Ujerumani wamewasili katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga-Bombo kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).

Akizungumza leo mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo,Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman alisema kwamba madaktari hao wamekuwa wakishirikiana nao na kwa sasa ni mwaka wa 13 tokea wameanza ushirikianao huo

Alisema kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Naima Yusuf aliwashukuru Hospitali kwa matayarisho yaliyofanyika ikiwemo sapoti kwa uongozi kuanzia ngazi ya wizara kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wanashukuru .

Hata hivyo alisema kwamba wote waliofanya usajili wataonwa na kufanyiwa uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na madaktari waliopo hapa hospitali hiyo.

Awali akizungumza Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha maumbile (Plastic Surgery) katika Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata alisema kwamba baada ya kuwasili hospitalini hapo wameanza kufanya uchunguzi wa awali na baadae kupangiwa ratiba tayari kwa ajili ya upasuaji .

Dkt Karata alisema kwamba wanawashukuru wananchi kwa kuitikia wito na zaidi ya wagonjwa 250 wamejiandikisha na wataonwa leo na siku ya kesho kwa ajili ya kupangiwa siku ya zoezi la upasuaji

Thursday, July 13, 2023

MWANZA YAPOKEA MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA KWENYE MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 21

 NA ALBERT G. SENGO/𝗨𝗞𝗘𝗥𝗘𝗪𝗘

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla amesema, Mwenge wa Uhuru mkoani hapa unatarajiwa kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 17 yenye zaidi ya shilingi bilioni 13.7, kufungua miradi 9 ya zaidi ya shilingi bilioni 3.5, kuzindua miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 huku ukitarajiwa kutembelea miradi 10 iliyogharimu shilingi milioni 609.2 . Mwenge wa uhuru umepokelewa wilayani Ukerewe ukitokea mkoani Mara.

WAZIRI PROFESA MKENDA ASIFU UBUNIFU UNAOFANYWA NA TAASISI YA TOIO.

 

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akiendesha moja ya baiskeli ya magurudumu matatu iliyotengenezwa na kubuniwa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) wakati wa ziara yake


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akiendesha moja ya baiskeli ya magurudumu matatu iliyotengenezwa na  kubuniwa  na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) wakati wa ziara yake  kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein  kulia wakati wa ziara yake

Na Oscar Assenga,Tanga

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesifu ubunifu unaofanywa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) ya kubuni vifaa mbalimbali vya umeme ikiwemo Baiskeli na Pikipiki huku akihaidi kuunga mkono juhudi hizo.

Profesa Mkenda aliyasema hayo wakati alipoitembelea Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mradi wa pikipiki za umeme,baiskeli ambazo zinazoziunda wenye shule ya Sekondari Tanga Ufundi.

Akiwa katika eneo hilo Waziri Profesa Mkenda alizitaka taasisi zinazojihusisha na teknolojia na ubunifu kuwasaidia wabunifu nchini kuweza kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Alisema kwamba kupitia ubunifu ambao unafanywa na taasisi kama TOIO wanaweza kuona namna ya kupata bajeti ambayo wanaitumia kuweza kuitumia kwa ajili ya kununua hivi vitu ili kuwaunga mkono watanzania ambao wanabuni vitu mbalimbali vyenye manufaa.

“Kupitia bajeti hiyo tutaitumia kununua hivi vitu vinavyotengenezwa hapa kitu kimoja tutangeneza mfumo wa kuvifabrikate kwa scale ya haraka”Alisema

Waziri Mkenda alisema kwamba vipaumbele vyao kwa bajeti iliyopo ya serikali ni kuona namna ya kuwasaidia wabunifu hao kununua hivi vitu tayari na serikali itanunua.

Awali akizungumza Mwakilishi wa Botna Foundation  Dkt Hassan Mshinda alisema wao walipata ufadhii wa kujenga ujuzi huo sio kwa wanafunzi tu bali na jamii ya nje.

Alisema  wanachofikiria ile integration kwenye mafunzo kama hayo ni fursa nyengine nzuri wanaweza kuona namna ya kupatna pamoja

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema  wamekuwa wakitoa ujuzi jinsi ya kutengeneza na kurekebisha vifaa mbalimbali ikiwemo pikipiki za umeme na baiskeli nia ikiwa na ya kuwa mjasiriamali anaweza kutengeneza pia

BEDA ANDREW - KWA NGUVU ZA MUNGU

 Jembe Gospel ndani ya kanisa la Philadelphia Buswelu jijini Mwanza.

WABUNGE,WAKUU WA MIKOA WAOMBWA KULIFANYA SUALA LA UCHANGIA DAMU NI AGENDA YAO KWA JAMII

 

 

MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga  Sinde Mtobu

Na Oscar Assenga,TANGA.


MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga  Sinde Mtobu amewaomba viongozi mbalimbali wa kijamii wakiwemo Wakuu wa Mikoa,Wabunge na Madiwani kuhamasishaji wananchi kuchangia damu na kuifanya  kama sehemu ya agenda yao wanapokuwa katika matukio mbalimbali ya kijamii.

Pia amewasihi viongozi wa dini kutumia maeneo yao ya ibada kuhamasisha waumini kuchangia damu ikiwemo kuandaa matukio mbalimbali ya uchangiaji damu kwa sababu wananchi wanawaamini sana viongozi wao na hivyo itakuwa ni njia rahisi watoa huduma kupata damu ya kutosha kuwahudumia wahitaji.

Hatua hiyo inaweza kusaidia kwa asilimia kubwa wananchi kuwa na mwamko wa kuchangia damu na hivyo kuwezesha benki za damu kuwa na utoshelevu ambao utasaidia wahitaji wanapojitokeza.

Mtobu aliyasema hayo wakati akizungumza  kuhusu umuhimu wa wananchi kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania wengine ambapo alisema viongozi hao iwapo wakiitumia vizuri agenda hiyo ya kuandaa na kuwahamasisha katika mikutano na mikusanyiko mbalimbali wanayoifanya kwenye maeneo yao itasaidia jamii kuwa na mwamko wa kuchangia damu

Alisema wanawaomba viongozi wa dini wawasaidie maana wao wana watu wa kutosha wanaowaamini wakisimama kwenye maeneo yao na kuhamasisha wananchi kuchangia na wakati kuratibu matukio ya yatakayohusisha uchanguaji wa damu.

“Katika hili niwaombe viongozi wetu wa Kijamii, Serikali za Mitaa, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Mikoa kufanya matukio ya uchangiaji damu kuwa agenda yao ya jamii wanapokuwa na matukio ya watu kwa kuhamasisha  jamii katika kuchangia damu.” Pia aliongeza kuwa, jamii ina hofu juu ya ushiriki wa kuchangia damu, hivyo viongozi wetu wa kijamii wakiwa katika msitari wa mbele wa kuchangia kwa vitendo na kuhamasisha, hakika mwitikio na hamasa kubwa itakuwepo toka kwa wananchi, alisema ndugu Mtobu.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Idara alivitaka pia vyombo vya habari kuhamaisha na kuwaita wataalamu ambao watasaidia kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu kwa kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari mara nyingi iwezakanavyo.

“Ndugu zangu tendo la kuchangia damu ni la imani na thawabu mbinguni maana unakuwa umeokoa uhai wa mtu ni suala la kiimani hivyo niwaase wananchi wenzangu tuwe na mwamko wa kuchangia damu kuokoa maisha ya wenzetu wahitaji walau mara tatu kwa wanawake na mara nne kwa wanaume kwa mwaka” Alisema. 

Aidha pia aliitaka Jamii kuwa na mwamko wa kuchangia damu ili kuwa sehemu ya kuokoa uhai wa wengine ambao ni wahitaji

Mtobu alisema katika Hospitali hiyo, wanatoa huduma za kitabibu zinazohitaji matibabu tofauti tofauti kwa mfano huduma ya damu ni moja ya tiba muhimu kwa wagonjwa wenye uhitaji wa damu kama ilivyo tiba ya dawa.

Alisema hospitali ya Rufaa kwa mwezi inatumia damu wastani wa chupa 500 mpaka 600 za damu lakini uwezo wa kuchangisha damu kutoka kwa wananchi kwa hiari mara nyingi chupa 200 mpaka 300. Mtobu alisema upungufu huo unahitaji wananchi kujitokeza kwa wingi waweze kupata damu ya kutosha. Aliiasa jamii kuona umuhimu wa kuchangia damu. mara kwa mara kwa kuwa matumizi ya tiba damu yapo wakati wote katika kuwahudumia wagonjwa. 

Alisema watumiaji wa tiba damu wapo wa makundi mbalimbali  yakiwemo makundi ya akina mama wajawazito (kabla, wakati na baada ya kujifungua), kundi la majeruhi wa ajali mbalimbali, kundi la watoto, kundi la wagonjwa wa upasuaji na kundi la wagonjwa wa magonjwa wa kudumu kama vile seli mundo (sickle cell disease)  na kansa mbalimbali hasa kansa ya damu. Makundi haya ni moja ya makundi ya wagonjwa wanaotumia tiba damu kwa kiwango kikubwa, hivyo uwepo wa damu muda wote katika benki zetu za damu ni suala la lazima ili kuimarisha afya na kulinda uhai wa maisha yao.

“Hivyo niiase jamii ione umuhimu wa kuchangia damu mara kwa mara, kwa kuwa na moyo wa kufanya hivyo kutawezesha benki zetu za damu kuwa na damu ya kutosha kuwahudumia wahitaji wanapojitokeza wakati wowote ili kuepuka kupambana na changamoto za utafutaji wa damu kwa dharura katika kuwahudumia wagonjwa wahitaji wa tiba damu wakati wote” Alisema ndugu Mtobu.

Tuesday, July 11, 2023

Benki ya CRDB yatunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora na Taasisi ya Umoja wa Ulaya

 

 
Benki ya CRDB kwa mara nyingine imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora na Taasisi ya Umoja wa Ulaya ijulikanayo kama ESQR (European Society for Quality Research).  Tuzo hiyo imetolewa Jumapili, t Julai 9, 2023 jijini Brussels Ubeligiji, yalipo makao makuu ya Umoja wa Ulaya ambao hivi karibuni umetoa ufadhili wa Euro Milioni 179.35 kwa Serikali ya Tanzania kusaidia mabadiliko ya sera, ukuaji wa viwanda na maendeleo ya miuondombinu.


Taasisi ya ESQR inajulikana kutokana na juhudi zake za kuhamasisha uvumbuzi na ubora katika sekta mbalimbali duniani. Tuzo hii ni kielelezo cha jitihada za Benki ya CRDB katika kutoa huduma bora za fedha pamoja na mchango wake mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na maendeleo kwa ujumla.

" Tunajisikia faraja na heshima kubwa kupokea tuzo hii kutoka kwa ESQR (European Society for Quality Research)," alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB. Tuzo hii kubwa ni kielelezo tosha cha juhudi na kujitoa kwa wafanyakazi wetu ambao siku zote wana dhamira ya kuhakikisha wanatoa huduma za kipekee kwa wateja wetu. Tunapoendelea kutelekeleza mkakati wetu wa biashara wa muda wa kati, tumejidhatiti kuhakikisha tunaendelea kusimamia ubora na uvumbuzi katika kila tunachokifanya ili tuweze kuwa vinara katika masoko yote tunayoyahudumia.
Kupatikana kwa tuzo hii ya ubora kwa Benki ya CRDB ni hatua muhimu katika safari ya benki kuhakikisha inakua kinara wa ubora katika utoaji wa huduma za fedha, Lakini pia tuzo hii inaendelea kuiweka Benki ya CRDB katika nafasi bora ya kuwa taasisi ya fedha inayoaminika ambapo mnamo mwezi Machi 2023, Benki ilipokea kiasi cha Euro Milioni 150 kutoka kwa Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (European Investment Bank) kwa ajili ya kusaidia biashara changa, ndogo na za kati nchini Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Mheshimiwa Jestas Nyamanga, alihudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo ya ubora kwa Benki ya CRDB na kuonyesha furaha yake kwa Benki ya Tanzania kutunukiwa tuzo kubwa ya kimataifa ambapo alinukuliwa akisema, “Tunajivunia tuzo hii ya Benki ya CRDB kutoka kwa taasisi hii kubwa ya Ulaya. Tuzo hii inadhihirisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi ili iweze kufanya vizuri.”
Kwa upande wake, Mshauri Mtendaji Mkuu wa ESQR, Bw. Michael Harris ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuchukua tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya pili baada ya kutunukiwa tena tuzo hiyo mwaka 2021. " Naitakia Benki ya CRDB mafanikio zaidi ili iweze kuendelea kuleta utofauti katika masoko inayohudumia lakini zaidi iendelee kuongoza masoko hayo wa uadilifu, uwazi lakini kubwa zaidi ubinadamu kwa kugusa maisha ya watu inayowahudumia," alisema Michael.

Tangu Januari 2023, Benki ya CRDB imetunukiwa tuzo zaidi ya 13 ikiwemo tuzo ya Benki Bora Tanzania inayotolewa na Global Finance Magazine, Benki Bora Tanzania kwa kuhudumia biashara ndogo na za kati inayotolewa na Global Finance pamoja na Benki Bora ya Kanda inayotolewa na African Banker. Benki inaendelea na jitihada zake za kuchangia ukuaji wa uchumi na kuwezesha watu binafsi na biashara kufanikiwa. Vile vile, Benki itaendelea kujikita katika kutatua mahitaji ya wateja kwa kutoa huduma za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja yanayobadilika kila uchao pamoja na jamii inazozihudumia.

Monday, July 10, 2023

KOKA AFANYA KWELI AMWAGA MIFUKO 100 YA SARUJI UJENZI OFISI YA BAKWATA KIBAHA


Na  Victor Masangu,Kibaha 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ametimiza ahadi yake kwa vitendo baada ya kukamilisha zoezi la  kutoa mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya Bakwata iliyopo kata ya kongowe Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.


Koka ametekeleza kwa vitendo katika halfa fupi ambayo ilifanyika katika eneo la viwanja ambavyo ujenzi huo unafanyika na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini ya kiislamamu pamoja na chama cha mapinduzi  (CCM) na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Kibaha.


Katika halfa hiyo Mbunge huyo alibainisha kwamba ametekeleza ahadi hiyo kwa vitendo ikiwa ni moja ya sadaka yake kwa mwenyezi Mungu na kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa dini zote wa Jimbo la Kibaha bila ubaguzi wowote katika kuwatumikia katika nyanja zote.

"Leo nimekuja hapa kongowe mtakumbuka kwamba nilitoa ahadi yangu wakati wa Baraza la iddy na mm hii ni sadaka yangu kwa bakwata pamoja na Mungu pia na nitaendelea kutoa kadiri ya uwezo wangu kwani kila nikitoa na Mungu anazidi kunipa baraka,"alisema Mbunge Koka.


Alisema kuwa katika kuhakikisha kwamba ofisi ya bakwata Wilaya ya Kibaha inakamilika atahakikisha kwamba mbali na kutoa msaada huo wa saruji lakini pia ataendelea kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia katika kukamilisha ujenzi huo.


Koka alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo utakuwa na faida kubwa wa waumini wa kiislamu katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kuwahimiza kushikamana kwa pamoja katika kufanikisha ujenzi huo.


Kadhalika Koka aliwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu kuwa na upendo amani ikiwa pamoja na kuendelea kutoa sadaka kwa hali na mali ili kurudisha matendo mazuri kwa Mungu pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.


Kwa Upande wake Sheikh wa Wilaya ya Kibaha Said Mtonda ameshukuru kwa dhati Mbunge huyo kwa utekelezaji wake wa ahadi kwa vitendo kwa kutoa mifuko hiyo ya sarufi ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo ya Bakwata.


Aidha alisema Mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika siku zote za kuhakikisha anashirikiana bega kwa bega katika dini zote ili kuweza kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo bila ya kujali itikadi za kidini.


"kiukweli tumekuwa kwa kipindi kirefu tukishirikiana bega kwa bega na Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini katika mabaraza ya Iddy na amekuwa mstari wa mbele katika kutushika mkono na hii leo ametimiza ahadi yake katika kutoa mifuko 100 ya saruji nampongeza sana na Mungu ambariki sana,alisema.


Hivi karibuni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wakati wa Baraza la Iddy ambalo lilifanyika katika kata ya kongowe aliahidi kuchangia mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Bakwata Wilaya ya Kibaha na ameitekeleza kwa vitendo..

KAMPUNI YA ESAP MINING SERVICES LTD YAKARIBISHA WADAU WA MADINI KUTUMIA BIDHAA ZAKE BORA

 

 








DAR ES SALAAM

Kampuni ya ESAP Mining Services Ltd inayojihusisha na uuzaji wa vilipuzi, uchorongaji na ulipuaji wa miamba kwenye Sekta ya Madini imekaribisha wadau wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini na ujenzi nchini kutumia bidhaa bora, teknolojia ya kisasa na wataalam waliobobea katika masuala ya vilipuzi.


Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Afisa Mawasiliano na Utawala wa kampuni ya ESAP, Shaban Sadick, leo Julai 09, 2023 kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2022 imekuwa na rekodi ya kufanya kazi na kampuni kubwa nchini kama Buckreef Gold Mine, Busolwa Gold Mine, STAMICO, Kasco Mining Ltd na Nyanza Road Construction Ltd.


Akizungumzia huduma zinavyotolewa na kampuni ya ESAP, Shaban amefafanua kuwa huduma zinapatikana nchi nzima kupitia ofisi zake zilizopo katika maeneo ya Soko la Dhahabu Geita; Kahama, Shinyanga; Mbeya na Bariadi mkoani Simiyu.


Akielezea mipango ya kampuni ya ESAP kwenye uboreshaji wa huduma, Shaban amesisitiza kuwa kampuni ina mpango wa kufungua ofisi katika mikoa yote nchini yenye uhitaji pamoja na nchi za jirani za Afrika Mashariki na Kati .


Ameendelea kusema kuwa wanapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu 0677 800003 au 0782 800133 na email info@esap.co.tz.



“ _ESAP IS YOUR CHOICE FOR PARTNERSHIP WHICH MAY ADD THE VALUE OF YOUR OPERATING COMPANY IN TANZANIA”