Na Oscar Assenga,Tanga
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesifu ubunifu unaofanywa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) ya kubuni vifaa mbalimbali vya umeme ikiwemo Baiskeli na Pikipiki huku akihaidi kuunga mkono juhudi hizo.
Profesa Mkenda aliyasema hayo wakati alipoitembelea Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mradi wa pikipiki za umeme,baiskeli ambazo zinazoziunda wenye shule ya Sekondari Tanga Ufundi.
Akiwa katika eneo hilo Waziri Profesa Mkenda alizitaka taasisi zinazojihusisha na teknolojia na ubunifu kuwasaidia wabunifu nchini kuweza kuzalisha bidhaa zenye ubora.
Alisema kwamba kupitia ubunifu ambao unafanywa na taasisi kama TOIO wanaweza kuona namna ya kupata bajeti ambayo wanaitumia kuweza kuitumia kwa ajili ya kununua hivi vitu ili kuwaunga mkono watanzania ambao wanabuni vitu mbalimbali vyenye manufaa.
“Kupitia bajeti hiyo tutaitumia kununua hivi vitu vinavyotengenezwa hapa kitu kimoja tutangeneza mfumo wa kuvifabrikate kwa scale ya haraka”Alisema
Waziri Mkenda alisema kwamba vipaumbele vyao kwa bajeti iliyopo ya serikali ni kuona namna ya kuwasaidia wabunifu hao kununua hivi vitu tayari na serikali itanunua.
Awali akizungumza Mwakilishi wa Botna Foundation Dkt Hassan Mshinda alisema wao walipata ufadhii wa kujenga ujuzi huo sio kwa wanafunzi tu bali na jamii ya nje.
Alisema wanachofikiria ile integration kwenye mafunzo kama hayo ni fursa nyengine nzuri wanaweza kuona namna ya kupatna pamoja
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema wamekuwa wakitoa ujuzi jinsi ya kutengeneza na kurekebisha vifaa mbalimbali ikiwemo pikipiki za umeme na baiskeli nia ikiwa na ya kuwa mjasiriamali anaweza kutengeneza pia
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.