ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 28, 2016

HIZI HAPA BENDI MBILI ZINAZOMSUMBUA ASHA BARAKA HATA KUING'ANG'ANIA TWANGA PEPETA.

Mapema leo asubuhi #SATURDAYXPRESS ya 93.7 Jembe Fm ilitembelewa na Mkurugenzi wa ASET Media Group Mama Asha Omar Baraka... Mama kafunga bendi mbili zinazompa changamoto kumfanya aendelee kuisuka Twanga na katu asiiachie.... Je wazifahamu? Jeh kwanini alikubali FM Academia kihivyo au chuki...? Dumbukia #GSENGOBLOG ... Unajua nini nimekula shavu la u-Mc usiku wa Twanga Pepeta na uzinduzi wa Album yao mpya #UsiyaogopeMaisha 🎸Tukutane Villa Park Resort leo. @rama.maganga @mzairebokilo_93.7jembefm @aishabarakaironlady @mwakad25 📌
BOFYA PLAY KUSIKILIZA 
Mkurugenzi wa ASET Media Group Mama Asha Omar Baraka mara baada ya mhojiano na Jembe Fm Mwanza.
Mkurugenzi wa ASET Media Group Mama Asha Omar Baraka (kushoto) akiwa na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha #SATURDAYXPRESS ya radio Jembe Fm.
Full.
Mpango mzima wa leo ndani ya Villa Park Resort Mwanza.
🐯**Baba jioni ya leo** kutoka kushoto ni @mwakad25 @ashabarakaironlady @nattyebrandy na 🎧@djmike_beatz_ on air right now kupitia 93.7 #KIKWETU baadae tukutane VILLA PARK RESORT tukalicheze Twanga👑📌

Friday, May 27, 2016

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA TOKA JUU YA MNARA KISA SUKARI.

Kijana Mmoja Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka juu ya mnara wa simu wenye urefu wa takribani mita 30. 

Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae alipanda katika mnara huo tangu majira ya alfajiri na kukataa kata kata kushuka toka juu ya mnara huo hadi ilipofika majira ya saa sita mchana baada ya kughasiwa vya kutosha na kuamua kujirusha.

Jamaa huyo ambaye alikuwa akisikika kulaumu ugumu wa maisha pia kwenye kauli zake aliligusia suala la kupanda bei na kuadimika kwa sukari akimtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika mahala hapo kabla ajafanya maamuzi mabaya ya kujiachia.



Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayozunguka minara yao ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kufanya kweli.

Baada ya kijana huyo kujirusha chini, alipoteza fahamu huku baadhi ya maeneo ya mwili wake yakitoka damu kiasi na kukimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya zaidi.

APIGWA JIWE NA KUFA KISA KUMWAGA POMBE BAA.

TARIME.

Mkazi wa Kijiji cha Matongo, Kata ya Matongo-Nyamongo wilayani hapa, Mkoa wa Mara, Samwel Kesocho (35), amefariki dunia baada ya kupigwa jiwe kisogoni kwa madai ya kuanzisha fujo baa.


Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Sweetbert Njewike alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 23, saa tano usiku katika baa ya Magaigwa Bukima iliyopo Mtaa wa Makaranga.

Njewike alisema, inadaiwa Kesocho alipigwa na jiwe hilo lililorushwa na mtu mmoja.

Alisema majeruhi huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya KMT Shirati wilayani Rorya.

“Chanzo cha ugomvi huo kilisababishwa na Kesocho kuanzisha fujo na kumwaga vinywaji vya wateja,” alisema Njewike.

Kamanda alisema muuaji alikimbia baada ya tukio hilo na kwamba hadi sasa hajapatikana.

Kilo 200 za bangi zakamatwa

Wakati huohuo; Mkazi wa Kijiji cha Sirari wilayani Tarime, Clement Marwa (42) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa akisafirisha kilo 200 za bangi na 20 za mbegu za dawa hizo za kulevya kwenye gari aina ya Toyota Probox alilokuwa akiendesha.

Njewike alisema polisi pia walimkamata raia wa Kenya, Janeth Nyamhanga (49) baada ya kumkuta akisafiri katika gari hilo.

Njewike alisema tukio hilo lilitokea Mei 25, saa tisa mchana katika Mtaa wa Kemange, Kata ya Nyandoto wakati mtuhumiwa akiendesha gari.

Kamanda huyo alisema bangi hiyo na mbegu hizo zilikutwa kwenye vifurushi vilivyofungwa kwa gundi nyeusi. “Watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili,” alisema kamanda huyo.

MAHAGETI YA LEO YANA HABARI HIZI> MAGUFULI KUJAZA VIJANA SERIKALINI, MRAMBA ASHAURI TANESCO ISIMILIKI MITAMBO IPTL, WAZIRI MBARAWA ASEMA WAZEE HAWATAKIWI TTCL.


SIMU.TV: Timbuka: vigogo wa dawa za kulevya hulishana yamini. Kadi za nauli Udart wiki ijayo. Mrema ataka Maalim Seif atiwe mbaroni; 


SIMU.TV: Magufuli kujaza vijana serikalini. Mramba ashauri Tanesco isimiliki mitambo IPTL. Waziri Mbarawa asema wazee hawatakiwi TTCL. 

Thursday, May 26, 2016

TAKUKURU KUWAFIKIA WANANCHI WOTE ELIMI DHIDI YA RUSHWA KUPITIA "LONGA NASI"


DSC_4229Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi akielezea namna walivyojipanga kusambaza elimu dhidi ya mapambano ya rushwa hapa nchini kupitia Huduma za 113 na LONGA NASI. kushoto kwake ni Afisa mahusiano wa TAKUKU, Bi. Angela Mulanduzi. Wakati wa mkutano huo leo Mei 26.2016, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania imebainisha kuwa, itaendelea kutoa elimu kwa kila mwananchi popote pale alipo atafikiwa ilikunufaika katika mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 26, Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi amesema kuwa baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya ‘LONGA NASI’, alisema kuwa, ni kutoa wigo wa kutoa elimu sahihi ya mapambano hayo ya rushwa na pia kupitia kampeni hiyo, watawafikia watu wote kupitia gari maalum la ‘LONGA NASI’ kwani kutakuwa na faida kubwa.

“Mbali na kuzindua huduma hii ya LONGA NASI, pia tumezindua huduma mpya ya 113 ambayo watu watapiga simu ama kutuma ujumbe mfupi ambao utasaidia kushugulikia matatizo ya vitendo vya rushwa” alisema Bw. Matai Kilumbi.

Aidha, aliongeza kuwa, watu wanaweza kutumia huduma hiyo kwa wakati wowote na watahudumiwa moja kwa moja.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
DSC_4248Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI' Likiwa mitaani wakati wa huduma hiyo ya LONGA NASI kwa kutoa taarifa ya rushwa -simu ya bure ya 113.
DSC_4244Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
DSC_4251Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
Hivyo, kwa kuendesha kampeni ya ‘LONGA NASI’, Mkakati wa Mawasiliano wa TAKUKURU utakuwa umetekelezwa ipasavyo lakini la muhimu ni kwamba jukumu la kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha umma katika kuzuia na kupambana na rushwa litakuwa limetekelezwa.
HUDUMA MPYA YA KURAHISISHA MAWASILIANO NA TAKUKURU
Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI, TAKUKURU tulizindua huduma mpya itakayowasaidia wananchi kutufikia kwa urahisi kupitia namba za dharura “113” au *113# ambazo ni BURE kama ifuatavyo:
  • Ilivyokuwa kabla ni kwamba mwananchi anaweza kupiga namba “113” kupitia simu yake ya kiganjani au mezani na kuongea na Afisa wa TAKUKURU moja kwa moja kumweleza shida yake au kuripoti tukio la rushwa. Utaratibu au huduma hii ni kupitia mitandao ya TTCL, AIRTEL, TIGO, HALOTEL, VODACOM na ZANTEL;
  • Sasa mwananchi anaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yaani “sms” kwenda nambari “113” ili kutoa maoni yake, kuuliza swali au kutoa taarifa.
  • Na pia mwananchi kupitia simu yake ya kiganjani anaweza kutoa taarifa ya rushwa kwa kupiga *113# (USSD) na kufuata maelekezo yatakayofuatia;
OFISI MAALUM YA MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE)
  • Kutokana na kuanzishwa kwa huduma hizo tajwa, tunaamini kutakuwa na mwitikio mkubwa kwa wananchi kuwasiliana nasi. Hivyo ili kuhakikisha kuwa TAKUKURU tunatoa kutoa huduma hii kwa haraka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameanzisha ofisi maalum ya MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE) iliyopo Makao Makuu ambayo itafanya kazi masaa ishirini na manne (24).
  • Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa za wananchi tunazopewa zinashughulikiwa haraka ikiwa ni pamoja na kuanzisha Uchunguzi.
  • Natumia fursa hii kuwahimiza wananchi kuLONGA NASI bila woga lakini si kwa lengo la kumwonea mtu. Tupatieni taarifa sahihi nasi tutakulinda na tutawashughulikia wanaohusika na tuhuma hizo kwa weleni na haki.
Katika huduma ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia mfumo wa USSD - *113# - Mtoa taarifa ana haki ya kutaka atambuliwe au asitambuliwe na TAKUKURU. Iwapo mwananchi hatapenda kutambulika na TAKUKURU basi ahakikishe kuwa taarifa aliyoiwasilisha itakuwa imejitosheleza kwa kiwango Fulani vinginevyo itatuwia vigumu kupata ushirikiano wa mtoa taarifa katika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma husika.

AIRTEL MONEY YAWEZESHA KUBETI NA KULIPA KWA AIRTEL MONEY

Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa (kushoto) akiongea wakati wa kuzindua ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na M-bet utakaowawezesha wapenzi wa kubashiri michezo mbalimbali kubaashiri na kisha Mr. Money kuwawezesha kulipia kupitia huduma ya Airtel Money. pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando  katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa M- bet Dhiresh Kaba
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando  (katikati) akifafanua jambo kwenye huma hizo.\
Mkurugenzi wa M- bet Dhiresh Kaba (kushoto) akipongezana na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (kulia) mara baada ya kuzindua ushirikiano utakaowawezesha wateja watakaobashiri michezo mbalimbali na kisha Mr. Money kuwawezesha  kulipia kwa kutumia huduma ya Airtel Money. akishuhudia ( nyuma kushoto) ni Meneja wa Airtel Money , Asupya Naligingwa
MR MONEY WA AIRTEL AJA NA SULUHISHO LA MALIPO WANAOBET MICHEZO KUWA SALAMA

Mr.  Money awawezesha wateja wa Airtel wanaobet kufanya malipo kwa Airtel Money
Dar es salaam 25 mei 2016 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeshirikiana na kampuni ya M- bet na kuwawezesha wateja wa M-bet kubashiri michezo wa mpira wa miguu ikiwemo ligi E Premier League, Laliga,Bundesliga, Serie A  kisha  kufanya malipo kwa urahisi na usalama kwa kupitia huduma ya Airtel Money

M- Bet ni kampuni inayowawezesha wateja wake kubashiri mshindi katika michezo mbalimbali ya soka duniani kote.

Akiongea wakati wa kutangaza ushirikiano huo Mkurugenzi wa M-Bet Mr. Dhiresh Kaba alisema “Mr Money wa Airtel Money ametupatia suluhisho la kupokea malipo na kulipa wateja wetu ushindi wao kwa usalama zaidi, hili limekuja wakati sahihi kwa kwa kuwa sasa tunaelekea msimu mpya wa ligi za mpira wa miguu hasa ligi ya Uingereza ambapo  wanaobashiri wataweza kubashiriri wakiwa popote na kufanya malipo bila ya kuwa na haja ya kutembelea ofisi za M-Bet kwa urahisi na usalama”

Ili kuweza kufurahia huduma hii unachotakiwa kufanya  tembelea tovuti ya m-bet www.m-bet.co.tz,   pakua  program ya m-bet App.net. Tabiri na ushinde na m-bet.  Mshindi anaweza kushinda hadi shilingi mil 10.  Ili uweze kukamilisha malipo yako huhitaji kubeba pesa tasilimu tena badala yake fanya malipo kwa njia salama ya Airtel Money kwa kupiga  *150*60# kisha chagua namba 5 malipo au(lipia bill) alafu chagua namba 3 weka namba ya kampuni 300300 na kuweka kumbukumbu namba yake. Aliongeza Mr. Dhiresh Kaba wa M-Bet

Kwa upande wake Meneja wa Airtel Money Mr. Asupya B. Nalingigwa alisema”Mr, Money anaendelea kudhihirisha kauli yake ya kwamba yeye ni nafuu na uhakika pale unapotaka kufanya malipo, leo uzinduzi huu wa kulipia tozo za kubashiri/kubet kwa Airtel Money itasaidia kuwaepusha wateja wanaoshiriki mchezo huo wa kubet/kubashiri  majanga ya kutembea na burungutu la pesa taslim kwa kuwa ni salama zaidi.

Nalingigwa alisisitiza kuwa Mr. Money wiki iliyopita alitangaza huduma pekee zinazotolewa na Airtel Money ikiwemo mikopo ya Timiza, nyongeza ya Uniti ukinunua LUKU kwa Airtel Money, nyongeza ya muda wa maongezi au vifurushi kwa Airtel Money bado Mr Money anaendeleza kuweka suluhisho kwa kila mahitaji, bidhaa na huduma mbalimbali”.

“ni uhakika kuwa Mr Money sasa atapokea malipo ya wewe unaebashiri na kisha atakulipa pesa ya ushindi wako wakati wowote mara baada ya kuthibitiishwa kuwa wewe ni mshindi na utaitoa kwa WAKALA  yoyote wa Airtel alisisitiza Bw, Nalingigwa

MPANGO MPYA WA UGAWAJI VYANDARUA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WAZINDULIWA MKOANI MTWARA

Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mganga mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
Mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.
Meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.

JITIHADA za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.

Takwimu hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza au kutokomezwa kabisa.

Takwimu hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.

“Tunataraji kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa wananchi,”alisema Sichalwe

Aidha Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje yani OPD sawa na asilimia 17.5.

Naye Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.

“Hatutumia wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima

Akizungumza mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa manufaa ya baba na mama.

“Nawaomba kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa

Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu